Kuku wa kienyeji hubadilisha chakula kuwa nyama polepole zaidi kuliko kuku wa kisasa (high feed conversion ratio)

Kuku wa kienyeji wakila chakula, pumba
Katika safu yetu ya maswali na majibu leo, (Uliza ujibiwe) nitajibu swali la msomaji wetu mmoja aliyeuliza kama ifuatavyo kupitia email,


Swali kama hili, tofauti ya chakula cha kukuwa kisasa na chakula cha kuku wa kienyeji nilishawahi kulijibu siku za nyuma (bonyeza link ya swali hapo juu kusoma majibu yake)  lakini kwa faida ya msomaji wetu huyo na pengine mtu mwingine yeyote basi nitalijibu tena na kuongezea mambo machache,

Hamna tofauti kubwa sana kwani wote kuku wa kienyeji na kuku wa nyama wanahitaji makundi yote makuu manne ya vyakula, wanga protini, mafuta, madini na vitanimi bila ya kusahau maji. Tofauti yake kubwa hutokana tu na jinsi kila aina ya kuku inavyoweza kupata virutubisho hivyo. Wakati kuku wa kisasa wanatakiwa kupewa kila kitu na wewe mfugaji, wale wa kienyeji wao hata usipowapatia virutubishi hivyo watakwenda kuvitafuta wenyewe kwa kuchakura kwenye michanga/udongo na matakataka mengine.


Kimsingi kuku wa kienyeji unaweza ukawalisha chakula cha kuku wa kisasa bila shida yeyote isipokuwa tu gharama yake itakuwa kubwa kutokana na kuku wa kienyeji kuchukua muda mrefu zaidi kubadilisha chakula kuwa nyama au mayai, hawakui haraka kama walivyo kuku wa kisasa 

Kwa maneno mengine ni kwamba kuku wa kienyeji wana (high feed conversion ratio). Maana yake uwezo wao wa kubadilisha haraka chakula wanachokula kuwa nyama ni mdogo ukilinganisha na wale kuku wa kisasa. Feed conversion ratio ndogo maana yake kuku wanabadilisha haraka chakula kuwa nyama


Food conversio ratio unachukua chakula anachokula kuku unagawa kwa uzito wa kuku. sasa utaona kuku wa kienyeji mpaka uje umchinje anaweza kula hata kilo 6 za chakula wakati wa kisasa anaweza kula kilo 3. Ikiwa wote watachinjwa na uzito wa kilo 2 tuseme, feed cnversion ratio ya kuku wa kienyeji itakuwa 6/2 = 3 wakati kuku wa kisasa ni 3/2 = 1.5, hivyo ya kuku wa kisasa ni nzuri zaidi(low) ingawa wote watachinjwa wakiwa na uzito sawa. Lakini pia ili kuku wa kienyeji afikishe uzito huo atakula chakula kingi zaidi.

Kwa upande wa kuku wa kisasa wao huwezi ukawalisha chakula kwa kutumia mtindo sawa na ule wa kulisha kuku wa kienyeji kutokana na miili yao kutokuweza kuvumilia shida kama wenzao kuku wa kienyeji. Ingawa wanaweza kupata virutubisho lakini hawawezi kujitafutia wenyewe na hivyo kuishia kufa njaa na magojwa.

…………………………………………

Ili kufahamu vizuri faida na gharama za ufugaji wa kuku wa aina zote, nimekuandalia michanganuo/business plans kwa ajili ya kuku wa nyama(boroiler), kuku wa mayai (Layers) na kuku wa kienyeji/asili. Michanganuo hii 3 nimeiita Kifurushi cha MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS

Bei ya kifurushi cha michanganuo hii ni sh. Elfu 10 tu, na ukinunua kabla ya siku ya Jumatatu tarehe 6/7/2020 utapata offa ya vitabu na michanganuo(vipo vitu/items zaidi ya 20) ambavyo unatumiwa kwenye email yako. Mara tu unapomaliza kulipia tuma ujumbe usemao; “NITUMIE KIFURUSHI CHA MKOMBOZI NA OFFA YA VITU 20” katika Whatsapp: 0765553030 au kwa sms namba: 0712202244. Malipo tumia moja kati ya hizo namba 2 na jina ni Peter Augustino Tarimo

Vitu/items hizo ni hizi hapa chini;

1.   KITABU: Tafsiri nzima ya Think & Grow Rich(Fikiri Utajirike)  Ndio kitabu mashuhuri zaidi cha fedha na mafanikio kuwahi kuandikwa duniani –cha  Kiswahili & cha kiingereza

2.   KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI -kwa kiswahili

3.   KITABU: Mifereji 7 ya pesa na siri matajiri wasiyopenda kuitoa-kwa kiswahili

4.   KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa kiingereza

5.   KITABU: Masomo ya fedha yaliyofundishwa watsap Part 1

6.   KITABU: Masomo ya fedha yaliyofundishwa watsap Part 2

7.   KITABU: Michanganuo hatua kwa hatua, watsap,     part 3

8.   Semina ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka - unga wa dona(USADO Milling) )-kwa kiswahili

9.   Kifurushi cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji-zote kwa kiswahili

10.                  Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikiti maji(KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili

11.                  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingereza

12.                  Mchanganuo kamili wa Biashara: Kiwanda cha tofali za sementi(KILUVYA Bricks) -kwa Kiswahili

13.                  Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi(AMANI CHIPS CENTRE) -kwa Kiswahili

14.                  Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako binafsi na kwa biashara yako-kwa kiswahili

15.                  Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. kwa Kiswahili & kiingereza

16.                  Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

17.                  Ukurasa mmoja wa mchanganuo(One page Business plan).(Njia fupi zaidi ya kuandika mchanganuo wa biashara yako kwa nusu saa tu, na mfano)

18.                  Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili

19.                  Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwa kiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika businee plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.

20.                  Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima(michanganuo-online) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla

0 Response to "Kuku wa kienyeji hubadilisha chakula kuwa nyama polepole zaidi kuliko kuku wa kisasa (high feed conversion ratio)"

Post a Comment