MZIMU HATARI UNAOONGOZA KUZIMA NDOTO ZA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI NA NJIA ZA KUUKWEPA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MZIMU HATARI UNAOONGOZA KUZIMA NDOTO ZA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI NA NJIA ZA KUUKWEPA

MZIMU HATARI WA HOFU
Tafadhali kwanza, hebu kabla hatujaenda kuona huo mzimu hatari unaotajwa kuwaaandama asilimia kubwa ya wanadamu, niongelee kidoogo tu juu ya OFFA yangu kubwa ya vitabu, michanganuo na seminars kuelekea uzinduzi wa kitabu, Think and Grow Rich kwa Kiswahili niliyoitoa tangu siku ya tarehe 28/6/2020 na ambayo mwisho wake ni siku ya Jumatatu tarehe 6/7/2020. Nitawalenga zaidi wale ambao hawajachukua hatua ya kuichangamkia offa hiyo mpaka muda huu.

Inawezekana ulipata taarifa juu ya offa hii na bado hujaamua kuchukua hatua, unajua ni sababu ipi kubwa iliyokufanya usichukue hatua licha ya offa yenyewe kuwa ya kipekee na ambayo ikishapita haitarudi tena? Sababu zaweza kuwa ni nyingi na tofauti kulingana na mtu na mtu lakini kusema ule ukweli asilimia kubwa ya watu jambo kama hili wanakuwa na sababu za kushangaza sana ukifanikiwa kuzijua.

SOMA: Download / pakua hapa kitabu Fikiri Utajirike (Think and Grow Rich) kwa Kiswahili, sura zote 15 bure

Simply itakuta ni hofu tu au wasiwasi, na sababu za hofu unaweza kukuta ni kutokana na offa yenyewe kuwa imetangazwa mtandaoni hivyo mtu anahofia kutapeliwa basi, ingawa kweli wapo wenye sababu za msingi kama kukosa pesa kwa muda huo, mwingine anaweza kuogopa tu kuwa labda hatapata faida iliyoahidiwa nk.

Lakini ikiwa una hofu yeyote nikuhakikishie tu kwamba offa hii ni ya kweli(Genuine) na wale wote waliojipatia tayari, kamwe hawawezi kujutia kwani thamani waliyoipata ni kubwa mara 20 kuliko gharama waliyotoa. Nimetoa zaidi ya vitabu na michanganuo 20 kwa sh. Elfu 10 tu, vitu ambavyo mtu angelipia karibu shilingi Laki 2. Nimepata jumbe nyingi watu wakishangaa ni kwa vipi niuze vitu vingi kama hivyo kwa bei ya kutupa namna hiyo

SOMA: Jinsi unavyozuia mafanikio makubwa maishani kwa kuhangaika na vitu vidogovidogo

MZIMU WENYEWE NI HUU HAPA;
Tukiachana na masuala hayo ya offa hebu sasa tuone mada yetu ya leo inazungumzia kitu gani hasa;

1)  Una ndoto kubwa maishani lakini kila ikija fursa kitu fulani kinakuvuta kwa nyuma usiijaribu?

2)  Kila ukitaka kujaribu fursa fulani unahisi watu wengine watakuonaje au ukifeli itakuwaje na kisha unaachana nayo?

3)  Hata ulipojaribu sana kuchukua hatua ukakamilisha baadhi ya malengo uliyojiwekea baadae ulibaini wala hujaridhika moyoni baada ya malengo mengine kuibuka upya?

4)  Kutafuta suluhu ya hali hiyo umejaribu mbinu nyingi za utatuzi kutoka kwa washauri na makocha mbalimbali bila ya mafanikio yeyote?

Tutayajibu maswali hayo baadae kidogo mwishoni mwa hili somo ila kikubwa ninachotaka kukizungumzia hapa leo ni hiki kifuatacho;

Akili zetu wanadamu zina nguvu sana kuliko vile tulivyokuwa tukifikiria na hata wakati mwingine akili yako mwenyewe inaweza kuwa inakuhujumu usiweze kuyafikia mafanikio yale unayostahili. Unaweza kuwa usiwe unalifahamu hili lakini linapokuja suala la kufanya mabadiliko ya kweli katika maisha yako akili yako ndiyo adui yako mkubwa. Na usije ukadhani labda hili hutokea kwako tu hapana, hutokea kwa watu wengine wengi nikiwemo hata na mimi mwenyewe ninayekuandikia huu ujumbe.

Ni watu wangapi umewahi kuwasikia wakipanga hili na lile katika juhudi za kutaka kubadilisha maisha yao? Ukimsimamisha mtu yeyote leo njiani, atakueleza mipango lukuki na malengo aliyojiwekea toka Januari, na hii ni Julai muulize sasa ametekeleza mangapi, nakuambia utashangaa! Si kama nasema ni kila mtu hapana ila ni asilimia kubwa sana ya watu.

SOMA: Maajabu ya kufikiri mambo makubwa na kwanini ujiwekee malengo makuba maishani

Sasa ni kitu gani kinachotokea kwenye akili zetu? hicho hasa ndio mchawi mwenyewe anayeharibu kila kitu na si mwingine bali ni HOFU au WOGA. Hofu ndio mtuhumiwa nambari moja wa mauaji ya ndoto zetu. Woga unazima ndoto za watu wengi duniani na hatimaye kuwafanya waingie makaburini mwao na ndoto zao hizo, ndio maana waswahili husema kuwa Makaburini ndio mahali palipolala mabilionea wengi zaidi hata kuliko duniani penyewe.

Hofu ina tabia ya kujivika tabia ya huruma na kukudanganya kama vile ina nia ya kukukinga na hatari fulani inayokunyemelea hata kama hatari yenyewe siyo hatari ni fursa kubwa kwako. Kazi yote hii hufanywa na akili yako mwenyewe katika harakati ‘feki’ za kutaka kukulinda na madhara mbalimbali, mengine yakiwa wala si madhara asilani. Ni sawa na Mwanamke (Mama) anayehofia kumpeleka bintiye mdogo akaanze shule ya chekechea siku yake ya kwanza kabisa kwa hofu kuwa mwanaye huyo anaweza kudhurika njiani kwa namna moja au nyingine.

SOMA: Kwanini huruma na upendo wa wazazi kwa watoto hupita kiasi?

Wazazi wengi (mimi hii iliwahi kunikuta) hukaribia hata kuahirisha mwaka kuwaanzishia watoto wao chekechea kutokana na sababu hii, mama atahakikisha siku ya kwanza anashinda hata nje ya geti la shule akiogopa tu mwanaye muda wa kutoka anaweza kubakwa, kuibiwa na watu wasiojulikana au hata kugongwa na gari au pikipiki hata kama shule yenyewe ina utaratibu mzuri tu wa kuwapeleka watoto makwao muda wa kutoka.

Lakini ukweli ni kwamba mara nyingi sana vile vitu akili zetu hutudanganya kuwa ni vya hatari tusivifanye, mara nyingi utakuta ndiyo fursa za mafanikio zilipolala. Woga wa mama kumpeleka bintiye akaanze chekechea siku yake ya kwanza kabisa hajui kama kumbe anamyima mtoto fursa ya ‘dhahabu’ ya kujifunza mapema, kukua na kukomaa kiakili. Vipi kama ataendelea kumwacha tu nyumbani mwaka mmoja tena zaidi akaja kukuta watoto wa rika lake wameshafika darasa la kwanza au la pili?

SOMA: Mchanganuo wa biashara: Kuanzisha shule ya chekechea(Day care Centre)

Mara nyingi akili zetu hudhania zinajua kila kitu kinachoendelea katika mazingira yetu na kutufanya tuamini kuwa jambo fulani haliwezekani kabisa hata kama katika jambo hilo hakuna kitu chochote kile kilichoziba mbele yake. Akili zetu hutupofusha tusiweze kuziona fursa sahihi zilizoko mbele yetu.

Hii ndiyo sababu kubwa sana ni kwanini watu wengi tunashindwa kuufikia uwezo wetu wote tuliokuwa nao pale tunapotaka kutimiza malengo tuliyojiwekea ili tuishi maisha yenye mafanikio tunayotamani kila siku na kuendelea tu kubakia kuwa watumwa wa akili zetu wenyewe.

SULUHISHO
Napoleon Hill katika kitabu chake, Think and Grow Rich anafundisha njia sahihi zitakazokuwezesha kuitumia akili yako vizuri na kuondoa kabisa hofu zile zisizokuwa na msingi wowote kwani zipo hofu za kweli na zile za uwongo (fake). Siwezi kukusimulia hapa ni kwa namna gani, ila ukisome mwenyewe kitabu hicho na hata ikiwa ulishakisoma lakini hujakielewa vizuri basi nakushauri ukisome tena na tena kama njia sahihi ya ‘kumaster’ yale yaliyofundishwa humo.

Toka sura ya kwanza mpaka ya kumi na tano kina shuhuda na mifano ya watu wengi waliofanikiwa au kufeli kutokana na jinsi walivyozitumia akili zao kufikiri na katika Sura ya 15 yenyewe imezungumzia mahsusi kabisa jinsi mtu anavyoweza kuondokana na Mzimu wa woga unaotuhumiwa kukatisha ndoto za watu wengi Duniani.

SOMA: Think and Grw Rich kwa ufupi: Mapitio ya vitabu vya mafanikio(Book Review)

Basi ndugu yangu chukua hatua leo usikubali tena kumruhusu adui HOFU kuendelea kukudanganya kila mara kwamba unaibiwa, unadhulumiwa, unahujumiwa, unatapeliwa na ‘kekundu’ na karata tatu nk. kwa kisingizio eti cha kukulinda uwe salama kumbe ndio kwanza inazidi kukudidimiza, hofu zingine kweye maisha yetu ni za ukweli lakini nyingi kwa kweli ndio hizi kama tulizoona hapa.

Wala si kama nakushauri kila fursa uingie kichwakichwa tu bila ya kufanya utafiti wa kina hapana, bali ninachotaka ujue ni kwamba chukua hatua ya zile fursa zinazoonekana bayana kabisa kwako bila kusitasita ndio mafanikio utayaona maishani.

Na mwisho kabisa usisahau hili, kama bado hujajipatia OFFA yangu ya mwisho kwa mwaka huu, basi ufanye hivyo leo kabla ya siku ya Jumatatu tarehe 6, 2020. Zimebakia siku 2 tu toka siku ya leo offa ifungwe rasmi. Ukitaka kujua thamani halisi ya Vitabu, Michanganuo na Seminars nilizokuwekea katika offa hii ya kipekee, tembelea ukurasa huu hapa wa DUKALANGU LA VITABU MTANDAONI kujua kila kitu kinauzwa shilingi gani. Hutaamini! Unaweza ukasema hivi, “Ni mwendawazimu pekee anayeweza kutoa offa kama hii”

“Peter are you Crazy? what kind of that OFFA are you giving to people.” Mimi wala siyo mwendawazimu kama alivyoniuliza rafiki yangu huyo whatsap juzi, bali napenda tu kushea maarifa na wenzangu kwani naamini hata watu wa Magharibi wangelikuwa wachoyo wa maarifa leo hii wala usingelisikia Wachina na Mataifa mengine tukiwemo na sisi huku Afrika tukijivunia Gunduzi za kushangaza kabisa za kisayansi na elimu nyinginezo nyingi kubwakubwa za kistaarabu.

SOMA: Vitabu Chanzo cha maendeleo na mafanikio makubwa ya binadamu duniani

Asili ya elimu na maarifa MWENYEZI MUNGU hajaviwekea mipaka hata kidogo na ndio maana hata uliona pamoja na Wamarekani kuwa watu wa kwanza kabisa duniani kuunda Nyuklia, lakini Urusi haikushindwa nayo kupata teknolojia hiyo ngumu ingawa walikuwa mahasimu wakubwa, halikadhalika Korea ya Kaskazini na sasa Irani. Maarifa hayabagui dini, rangi wala kabila, hayajali unatoka kusini, kaskazini au Mashariki na wala hayaangalii kama wewe ni bepari au mkomunisti

Pia nimalizie na yale Masomo ya kila siku ya fedha na michanganuo kwenye lile group letu la masomo la (MICHANGANUO-ONLINE MASTERMIND GROUP) Yameanza tena na wote wanaochukua offa hii wanaunganishwa moja kwa moja bureee! mwaka mzima, somo letu la leo lina kichwa kisemacho,MBINU ZA KUBAJETI FEDHA KIDOGO KWENYE BIASHARA MPYA INAYOANZA.”….na kesho Jumamosi tutakuwa na Mchanganuo wa biashara ya kuuza mchele wa jumla na rejareja hatua kwa hatua. Hivyo unakaribishwa sana.

OFFA ina vitu vifuatavyo;
   
1.  KITABU: Tafsiri nzima ya Think & Grow Rich (Fikiri Utajirike)  Ndio kitabu mashuhuri zaidi cha fedha na mafanikio kuwahi kuandikwa duniani –cha  Kiswahili & cha kiingereza

2.  KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI - cha kiswahili

3.  KITABU: Mifereji 7 ya pesa na siri matajiri wasiyopenda kuitoa- cha kiswahili

4.  KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.- cha kiingereza

5.  KITABU: Masomo ya fedha yaliyofundishwa watsap Part 1–cha kiswahili

6.  KITABU: Masomo ya fedha yaliyofundishwa watsap Part 2 -cha kiswahili

7.  KITABU: Michanganuo hatua kwa hatua, watsap,     part 3 –cha kiswahili

8.  Semina ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka - unga wa dona (USADO Milling) )-kwa kiswahili

9.  Kifurushi cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku (MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji-zote kwa kiswahili

10.                 Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikiti maji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili

11.                 Mchanganuo wa biashara ya mgahawa (JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingereza

12.                 Mchanganuo kamili wa Biashara: Kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks) -kwa Kiswahili

13.                 Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE) -kwa Kiswahili

14.                 Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako binafsi na kwa biashara yako-kwa kiswahili

15.                 Vielezo (Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. kwa Kiswahili & kiingereza

16.                 Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5–kwa kiswahili

17.                 Ukurasa mmoja wa mchanganuo(One page Business plan).(Njia fupi zaidi ya kuandika mchanganuo wa biashara yako kwa nusu saa tu, na mfano) –kwa kiswahili

18.                 Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili

19.                 Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwa kiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika mwenyewe bila mtaalamu.

20.                 Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima(michanganuo-online mastermind group) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla

Kupata offa mara moja, lipia sh. Elfu 10 kupitia namba zangu; 0712202244 au 0765553030 Tuma pia na ujumbe watsap: 0765553030 au SMS ya kawaida usemao, “NATAKA OFFA YA MWAKA 2020 YA VITU 20” Ikiwa utapenda nikuunge pia na Master Mind Group la MICHANGANUO-ONLINE naomba uniambie tafadhali manake watu wengine haapendelei kuwa kwenye magroup bali wanahitaji tu OFFA yenyewe.

Siyo lazima uwe na Watsap, hata Email peke yake inatosha nitakutumia kila kitu kwa email yako.

Asante sana,


PETER AUGUSTINO TARIMO

0 Response to "MZIMU HATARI UNAOONGOZA KUZIMA NDOTO ZA WATU WENGI ZAIDI DUNIANI NA NJIA ZA KUUKWEPA"

Post a Comment