THINK AND GROW RICH KWA UFUPI: MAPITIO YA VITABU VYA MAFANIKIO(BOOKS-REVIEW) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

THINK AND GROW RICH KWA UFUPI: MAPITIO YA VITABU VYA MAFANIKIO(BOOKS-REVIEW)

Kitabu cha Think and Grow Rich(Fikiri Utajirike) au ‘Msahafuwa mafanikio’ kama kilivyobatizwa na Self Help Books Tanzania Limited, kilianza kutafsiriwa katika lugha ya kiswahili kwa mara ya kwanza kabisa na kampuni hiyo hapo mwaka 2012 kwenye tovuti na blogu yake iliyokuwa ikijulikana kama “KUELEKEAUTAJIRI” na baadaye kuja kuitwa, “JIFUNZEUJASIRIAMALI”.

Lengo letu ni kuhakikisha wapenzi wa kitabu hiki maarufu zaidi duniani na kilichowahi kuuzwa nakala nyingi kuliko kitabu kingine chochote katika tasnia hii, wanaweza wakakisoma katika lugha yao ya mama yaani kiswahili fasaha bila ya bughudha zozote za kuwa na kamusi pembeni, “English-swahili dictionary”, kila mara wanapotaka kukisoma.

Bado kazi ya kuendelea kukichapisha kitabu hiki kidogokidogo katika lugha ya kiswahili inaendelea kwenye blogu ya jifunzeujasiriamali ambapo hadi kufikia sasa tumefika sura ya 4. Pamoja na kukichapisha huko kizima kama kilivyo, pia tumeona ipo haja ya kuweka muhtasari mzima wa kitabu hicho sanjari na mfululizo huo kusudi wasomaji watakaopenda kukisoma kitabu hicho cha Think and Grow Rich kwa ufupi nao waweze kufanya hivyo bila shida.

Hata hivyo muhtasari au ufupisho wa kitabu, kamwe hauwezi ukawa mbadala wa kitabu chenyewe, utamu na maana halisi ya kitabu unaweza ukavipata kwa kusoma kitabu chote na wala siyo ufupisho wake. Kuna “details nyingi” vitu vya ndani ambavyo hauwezi kabisa ukavijumuisha katika uchambuzi wa kitabu na ili uweze kuvipata vitu hivyo kwa ubora wake halisi ni lazima usome kitabu kama kitabu kikiwa kizima.

Hata hivyo, Uchambuzi wa vitabu, mapitio au kitabu kwa ufupi vina faida zake nyingi ikiwa ni pamoja na kumrahisishia msomaji kupata picha ya kitabu kizima katika muda mchache, kupata maudhui ya vitabu vingi katika muda mfupi pamoja na kukwepa kusoma baadhi ya vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa kwake.

Lakini kuna vitabu ambavyo hata kama utasoma ufupisho wake lakini baadaye utahitaji pia kukisoma kitabu kizima. Vitabu vya namna hiyo ni vile vitabu ambavyo kamwe hautaweza kuvisahau maishani mwako. Kitabu kama hiki ‘Think and  Grow Rich’, kitabu kilichowahi kusomwa na karibu watu wote unaowajua wenye mafanikio duniani, wakiwemo kina Barack Obama, Bill Gates, Ophrah Winfrey, Nelson Mandela, Muhammad Ali, John F.Kennedy, Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Eric Shigongo na wengineo wengi,  sidhani kama ungependa ukisome kwa ufupi tu na kisha uachie hapo hapo, ni lazima upange kuja kukisoma chote kizima na hii ndiyo sababu iliyotusukuma sisi SHBPL kukitafsiri kitabu hicho kusudi wasomaji waweze kukisoma kwenye blogu yao ya jifunzeujasiriamali.

Mapitio hayo kwa ufupi tutakuwa tukiyafanya pia kwa vitabu vingine mbalimbali vya elimu ya pesa na mafanikio(vile muhimu zaidi). kumbuka duniani kuna maelfu ya vitabu vya aina hiyo na wala hata useme kwa mfano mtu unataka usome kila kitabu cha mafanikio duniani, utazeeka ungali  bado haujafikisha hata robo yake. Kikubwa na cha msingi ni mtu kuchagua vitabu vyako vya maana ukaamua hivi nitavisoma kikamilifu na kufanyia kazi barabara yale utakayojifunza. Hautaishia hapo kusoma kwani kazi ya kusoma haina mwisho mpaka unaingia kaburini lakini huwezi ukaniambia utasoma bila ratiba na ikiwa utatumia ratiba basi ni lazima tukubaliane ile kanuni ya msingi ya asili isemayo, “Kupanga ni kuchagua, hatuwezi duniani tukafanya kila kitu kilichopo mbele yetu, muda mara zote huwa kikwazo”  .

Ukipenda kufahamu zaidi juu ya falsafa yangu hiyo, nakushauri udownload hapa bure kitabu nilichotunga kiitwacho, Kanui ya kujifunza Elimu ya Pesa naMafanikio kwa Ufanisi mkubwa”. Nimeipa jina kanuni hiyo kuwa (Peter’s Theory of studying Success Books). Wahi mapema kwani kitabu hicho kizuri hivi karibuni kitaingia katika Orodha ya vitabu vinavyouzwa na bei yake itakuwa ni Tsh. 5,000/=.

Kuanza kusoma mapitio au uchambuzi wa kitabu Think and Grow Rich kwa lugha ya kiswahili fasaha, bonyeza maandishi yafuatayo hapo chini; 

MAPITIOYA KITABU THINK AND GROW RICH KWA UFUPI(UCHAMBUZI WA KINA)

                                                                

0 Response to "THINK AND GROW RICH KWA UFUPI: MAPITIO YA VITABU VYA MAFANIKIO(BOOKS-REVIEW)"

Post a Comment