Najua unaweza kuwa unashangaa ni vipi blogu ya
ujasiriamali inaandika tena makala zenye maudhui ya kidini na kujiuliza, “Vipi jamaa wamegeuka kuwa wahubiri nini?”
Mimi kama mwandishi habari napenda sana kuandika ‘facts’ mambo yaliyotokea kweli au
kutokana na vyanzo vya kuaminika na wala siyo riwaya.
UKWELI
hauhitaji mtazamo binafsi wala maoni na ndio maana makala hii juu ya Muhammad
(S.A.W.W.), Mtume Mkubwa wa mwisho
Duniani naiandika kwa kuzingatia muktadha wa kitabu cha Mwandishi Napoleon Hill
kiitwacho Think & Grow Rich (Fikiri & Utajirike) nikiwasilisha ujumbe
kama mwandishi mwenyewe alivyokusudia
Ninapomtaja Mtume Muhammad kuwa Mtume Mkubwa wa Mwisho
sina maana kwamba leo hii hakuna watu wanaojiita Mitume na Manabii hapana,
lakini ni ukweli usiopingika kwamba tokea kuja kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Dunia
haijashuhudia tena Mtume mwingine aliyeacha alama kubwa na ya kudumu sawa na
yeye, na isitoshe nimenukuu maneno sawa na ilivyoandikwa kwenye kitabu hicho
cha Think
and Grow Rich
Lengo kuu la Napoleon Hill la kukiandika kitabu cha Think
& Grow Rich lilikuwa ni kufanya utafiti na kugundua kanuni za mafanikio
ambazo hufanya kazi kwa kila mwanadamu aliyewahi kupata mafanikio makubwa hapa
Duniani na hivyo kanuni hizo kuwa msingi wa wengine wote hata wale watakao taka
kuja kufanikiwa siku zijazo
Bilionea Andrew
Carnegie mtu aliyemuagiza Napoleon Hill kutimiza jukumu hili zito la miaka 20
aliamini katika fikra zake kwamba, ni lazima zitakuwepo kanuni maalumu ambazo
watu wote wanaofikia mafanikio makubwa maishani huzitumia kwa kujua au hata
pasipo wenyewe kujua ikiwa wanazitumia.
Hatimaye Kanuni 13 zilizomo ndani ya Kitabu cha Think
& Grow Rich siyo kwa ajili ya kumpatia mtu utajiri wa kifedha tu peke yake
hapana, bali kanuni hizi pia mtu anaweza akazitumia katika kujipatia mafanikio
kwenye nyanja nyingine zozote zile za kimaisha mfamo kiroho, kiimani,
kifamilia, kiuongozi nk.
Kwahiyo Bwana Napoleon Hill katika kuwachunguza mamia ya
watu mashuhuri waliofanikiwa, hakuishia tu kwa matajiri wa mali na fedha peke
yake, bali pia aliwachunguza viongozi wakubwa wa kisiasa Duniani kama kina Mahatma
Gandhi na Bismark, viongozi na waanzilishi wa Imani na dini mbalimbali kama
vile akina Mtume Muhammad, Budha, Yesu Kristo, Confucius na wengineo.
Leo hapa nimeanza na Mtume Muhammad kiongozi na
mwanzilishi wa Imani ya Kiislamu Duniani aliyeweza kupata mafanikio makubwa
baada ya kupitia vikwazo vingi vya kutisha.
Usiniulize kwanini Uislamu kwenye kitabu hiki kwani dini
nyingine zote kuu pia zimezungumziwa ndani ya kitabu na mwandishi, na ninaahidi
katika kila imani iliyozungumziwa humo bila ubaguzi wowote ule nitaandaa makala
yake maalumu siku zijazo Inshaalah!
Kama nilivyotangulia kusema, kitabu hiki siyo cha Dini
isipokuwa tu mwandishi alitumia dini na imani mbalimbali katika kuelezea kanuni
za mafanikio alizokuwa akizitafiti.
Na bila shaka Napoleon Hill alijitahidi sana
kutokuonyesha upendeleo wa imani au dini yeyote ile (Biasness) na ndio maana hata utagundua kwenye kitabu hiki ikiwa
utakisoma, alikwepa kabisa kutumia majina dini mbalimbali zinayomaanisha “MUNGU”
mfano Allah, Mungu nk. na badala yake alitumia tu jina la, “NGUVU KUU ISIYOKUWA NA MIPAKA” (INFINITE INTELLIGENCE)
Kwa ufupi kabisa nataka utambue ni kanuni zipi ndani ya
kitabu hiki alizotumia Mtume Muhammad kutimiza kazi yake ya Utume aliyoagizwa
kuifanya na Mwenyezi Mungu. Kumbuka kwamba MUNGU (Nguvu Kuu Isiyokuwa na Mipaka
kama anavyoita mwandishi) hufanya kazi na binadamu kupitia njia zinazotambulika
wazi na ambazo zimetajwa bayana kwenye kitabu hiki.
Njia hizo kitu cha kustaajabisha ni kwamba zilifanya kazi
pia kwa Mitume na Manabii wengine wote wakubwa waliokuwa wamemtangulia
Muhammad.
Mwenyezi Mungu anapotaka kuwasilina na mtu huwa hatumii
njia nyingine tofauti na hizo zilizoelezwa humo kwenye hicho kitabu ukisoma
vizuri.
Na wala si kwamba njia hizo zimegunduliwa na Napoleon
Hill hapana, Napoleo Hill yeye alichogundua tu ni kwamba Mitume wote na Manabii
wakubwa Duniani walizitumia kanuni na njia zilezile zinazofanana pasipo hata
wao wenyewe kutambua ikiwa walikuwa wakizitumia.
Nitadokeza japo kidogo baadhi ya kanuni alizotumia Mtume
Muhammad kwa mujibu wa mwandishi lakini kumbuka kitabu kina kanuni 13. Mojawapo
ni ile kanuni ya 8, MSIMAMO, ambayo inapatikana Sura ya 9.
Ukisoma vizuri wasifu
wa Mtume Muhammad utabaini alikuwa ni mtu mwenye msimamo thabiti
usioweza kuyumbishwa kirahisi, mfano ni pale alipokataliwa na jamii yake akaamua
kwenda kuishi Jangwani kwa muda pasipo kusitisha dhamira yake ya kuendelea
kuhubiri ujumbe aliokuwa ameagizwa na Mwenyezi Mungu. MSIMAMO wake ulikuwa ni mmoja tu, watu wote Duniani wamuamini Mungu
mmoja.
Kanuni nyingine ni ile ya 13, MLANGOFAHAMU WA SITA
inayopatikana Sura ya 14. Hii hasa ndiyo kanuni hutumiwa zaidi na Mitume na
Manabii kutokana na uwezo wake wa kutenda Miujiza.
Waarabu ni watu wagumu sana kuamini miujiza lakini
kitendo cha Mtume Muhammad ambaye wala hakuwa anajua kusoma na kuandika kuwa na
uwezo wa kuelezea aya za Quran Tukufu kwa ufasaha na zilizokuwa na maneno
yaliyogusa mno mioyo yao, ulikuwa ni muujiza mkubwa sana kwao usio na kifani.
Ingawa Mtume mwenyewe anakiri kuwa yeye si mtu wa
miujiza, hakuna njia nyingine unayoweza kuelezea kitendo hiki cha Mtume
Muhammad cha kushushiwa Aya za Quran Tukufu akiwa mapangoni kwenye Jangwa zaidi
ya Muujiza ambao ndio mawasiliano ya Akili ya ndani ya mtu na Nguvu Kuu
isiyokuwa na mipaka (MUNGU/ALLAH), mawasiliano yaliyoelezewa ndani ya kitabu
cha Think & Grow Rich
Mtu yeyote yule anaweza akaitumia kanuni hii ya
Mlangofahamu wa sita kufanya mambo makubwa mno maishani ikiwa ataamua, unaweza
usiweze kufanya mambo makubwa sawa na alivyofanya Mtume Muhammad lakini angalao
unaweza kufanya tofauti sana na watu wa kawaida tu wasiozingatia kanuni hii.
Sura hii ya 14 na zile zilizotangulia zinaeleza kwa kina
utaratibu mtu unaoweza kuutumia kanuni hii ikakufanyia mambo ya kushangaza
mfano hata kugundua hatari mbalimbali kabla hazijakupata nk.
Uliwahi nyakati fulani kumsikia mtu au wewe mwenyewe
kuahirisha safari na kisha baadae ukaja kusikia gari uliyoghairi kupanda
ilienda kupata bonge la ajali na watu wakapoteza maisha?
Kuna sauti fulani usiyoijua ilikuja na kukudokeza usisafiri
(wakati mwingine watu huiita hali hii, ‘MACHALE’),
unaweza kusikia mtu akisema machale yalimcheza akaghairisha safari.
Kwahiyo haya machale si kitu kingine bali mawasiliano ya Akili
yako ya ndani na Nguvu kuu isiyo na mipaka. Ni watu wachache huwa na hali hii
kwa kuzaliwa nayo lakini unaweza pia kuipalilia na kuwa nayo ukitaka.
Napoleon Hill anasema kwamba tofauti na zilivyo kanuni
nyingine 12, mtu huwezi kukuza mlango fahamu wako wa sita ambayo ndiyo kanuni
ya mwisho ya 13 pasipo kwanza kujifunza kanuni nyingine zote 12 zilizotangulia,
kuna baadhi ya mafundisho ya kanuni hii yanapatikana pia kwenye hizo kanuni
nyinginezo mfano kanuni ya 1, SHAUKU. ya 2, IMANI na ya 4, KUJISHAURI BINAFSI
Kwa maelezo zaidi kuhusiana na tabia za kipekee za
Muhammad Mtume Mkubwa wa Mwisho usiache kusoma kitabu hiki cha Think & Grow
Rich (Fikiri & Utajirike), wasifu wa Mtume Muhammad kama ulivyoandikwa na
Mwandishi Essad Bey kwenye kitabu
chake cha Wasifu wa Mtume Muhammad.
Uchambuzi huu mfupi wa hicho kitabu alioutumia Napoleon
Hill ndani ya Think & Grow Rich uliandikwa na Thomas Sugrue katika Jarida la Herald Tribune
Ukitumia nakala ya kiingereza ni Sura ya 9, PERSISTENCE ukurasa wa 151 “THE LAST GREAT PROPHET”
Na ikiwa unasoma nakala ya Kiswahili kilichotafsiriwa na
Peter A. Tarimo ni Sura ya 9, MSIMAMO,
ukurasa wa 260 “MTUME MKUBWA WA MWISHO”
.................................
Maoni yangu mimi Binafsi kama Peter:
Kitabu cha Think and Grow Rich nimewahi kukisoma na
kukirudia mara nyingi. Kusema ukweli, binafsi kimenipa faida nyingi mno na hasa
kwenye upande wa kujitambua Binafsi hasahasa kwenye masuala yanayogusa hisia (kufikiri)
na Imani.
Masuala ya kiimani na kihisia dunia ya leo yamekuwa ni
vitu vinavyowahangaisha watu wengi sana hata wakati mwingine kusababisha
maradhi mbalimbali, mitafaruku ya kijamii na hata umasikini wa kutisha
Ukisoma kitabu hiki utagundua kwamba maamuzi mengi
tunayofanya hutokana na imani zilizojichimbia ndani ya akili zetu, hivyo kuna
hatari kubwa sana mtu unapokuwa na imani fulani potofu kwenye akili yako.
Kwa mfano ikiwa utaamini baba/mama yako mzazi anakuloga
uugue itakuwa hivyo kweli hata kama ikiwa wazazi wako hao hawana uchawi wowote
ule
Utaugua magojwa ambayo ni matokeo ya imani uliyokuwa nayo
juu ya hao wazazi wako na mwishowe unaweza hata kuchukua hatua ya kuondoa uhai
wao.
Ukisoma hiki kitabu ukakielewa vizuri hautakaa uyumbishwe
kabisa na masuala yahusuyo Imani kamwe, utabaini kuwa Imani zote Duniani zina
pande kuu 2, UWONGO na UKWELI. Imani yeyote ni ya kweli kwako ikiwa unaiamini
lakini ikiwa huiamini basi imani inakuwa ni ya uwongo kwako
Ukweli huu utakufanya kutokugombana na jirani yako wa
imani tofauti hata siku moja na utadumu na Imani yako huku ukiheshimu imani za
wengine bila chuki yeyote hata kama unaona imani zao ni za uwongo sawasawa tu
na wao pia wanavyoona imani yako ni ya uwongo
Utabaini pia kwamba katika kila Imani, kila dini mtu
unaweza ukafanya miujiza ilimradi tu umezingatia kanuni maalumu ambazo siyo za
siri na zimethibitishwa kisayansi kwamba zinaweza kufanya miujiza.
Kanuni kwa mfano ile ya Kujishauri binafsi (Autosuggestion) mtu unaweza ukaitumia
ukichanganya na baadhi ya nyingine mfano Mlango
fahamu wa 6 na Imani zikakufanyia
maajabu makubwa!
Zaidi ya yote kitabu hiki kwa anayetaka kutajirika
kifedha pia matumizi ya kanuni zilizoko ndani yake kwa usahihi zinaweza
kukupatia kiasi chochote kile cha utajiri uutakao wewe, sawa na wale utakaosoma
mifano yao ndani ya kitabu.
Kundi
la Usomaji wa Kitabu cha Think & Grow Rich
Nimeanzisha Kundi maalumu la usomaji wa kitabu cha Think
& Grow Rich ambapo tutasoma kitabu hiki kuanzia mwanzo mpaka mwisho katika
Lugha zote mbili Kiswahili na Kiingereza
Sifa za mshiriki ni kuwa na nakala ya Kiswahili au ya
Kiingereza ya kitabu hicho kutoka kwangu mwenyewe. Nikikupatia nakala ya kitabu
haijalishi ni ya Kiswahili au ya kiingereza, moja kwa moja unaweza kujiunga na
kundi
Nakala ya kiingereza ni Bure
Nakala ya Kiswahili inapatikana kwa malipo kwa utaratibu
ufuatao;
NAKALA
NGUMU(HARDCOPY) ukiwa Dar es salaa ni Tsh. 25,000/=
unaletewa mpaka ulipo. Na Mikoa mingine ni Tsh. 35,000/= Tunatuma kwa basi au
Boti
NAKALA
LAINI (SOFTCOPY) ukiwa popote pale Duniani ni Tsh. 10,000/= na
kinapatikana kupitia App ya GETVALUE bonyeza kiungo hicho
kununua sasa hivi.
NAFASI
10 TU ZA OFFA!
Kwa watakakubaliwa kuingia kundi hili na kitabu cha
Kiingereza ni watu 10 tu wa mwanzo watakaolipia programu ya 2025 MAKEYOURSELF GREAT
AGAIN Tsh. 10,000/= siku ya kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili. Baada ya
hapo Ofa itafungwa
PROGRAMU
YA 2025 MAKEYOURSELF GREAT AGAIN ni kundi jingine
linaloendelea ambalo washiriki hujifunza kila siku jinsi ya kuandaa mipango ya
biashara, fedha, masoko nje na ndani ya mtandao, mauzo, uwekezaji, ubunifu
kwenye biashara ndogondogo ili kukuza mtaji haraka, Biashara za rejareja na michanganuo
ya biashara zinazolipa upesi.
Kiingilio ni Tsh. 10,000/= na unapatiwa Vitabu na Michanganuo
ya Biashara jumla vitu 10 kwa ajili ya Rejea kikiwemo Kitabu cha kurasa 430 cha
MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI.
Unapata pia mafunzo kamili ya siku 7 ya uandishi wa
mpango wa biashara kwa vitendo
Unaweza kujiunga kwanza group la MAPOKEZI HAPA ambalo pia unapata bure kabisa Basic course on Business planning (masomo 12 ya msingi ya
jinsi ya kuandika mpango wa biashara yeyote ile) wakati ukisubiri kujiunga na
VIP CLASS
Offa ya kesho na keshokutwa kwa Think & Grow Rich
ikiisha, kujiunga na magroup yote mawili lile la usomaji wa Think & Grow
Rich na la MAKEYOURSEL GREAT AGAIN itakuwa jumla ni Tsh. 20,000/= kwa
anayenunua nakala laini na Tsh. 35,000/= kwa 45,000/= kwa wale wa nakala Ngumu
0 Response to "MUHAMMAD, MTUME MKUBWA WA MWISHO DUNIANI"
Post a Comment