NATAKA KUFUNGUA DUKA LA REJAREJA LA MAHITAJI YA KILA SIKU KATIKA JAMII, MBINU GANI NAWEZA KUTUMIA KUFANIKISHA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NATAKA KUFUNGUA DUKA LA REJAREJA LA MAHITAJI YA KILA SIKU KATIKA JAMII, MBINU GANI NAWEZA KUTUMIA KUFANIKISHA?


Leo mmoja wa wadau wetu kwa jina Luca M. (Huwa hatutaji jina kamili bila ridhaa ya muulizaji) ameuliza swali lake katika safu hii na bila ya kuongeza au kupunguza chochote kile swali hilo naliweka hapa chini na majibu yake yatafuata chini yake;

SWALI:
“Nataka kufungua duka la rejareja la mahitaji ya kila siku katika jamii mbinu gani naweza kutumia kufanikisha”

MAJIBU:
Duka la rejareja ni biashara rahisi sana kuanzisha ikiwa tayari unao mtaji na eneo la kuweka duka lako. Yapo mambo muhimu 10 unayopaswa kuyazingatia kabla hujaanzisha biashara yako ya duka la rejareja na mambo hayo niliyaelezea kwa kirefu katika kitabu changu cha SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA katika ukurasa wake wa 7

SOMA: Kuwa Bilionea naweza kutumia mbinu zipi?

Nitaelezea mambo machache lakini mengine kwa kirefu unaweza ukatafuta kitabu hicho kwani sitaweza kuyaeleza hapa yote.

1. Kwanza kabisa kama ilivyo kwa biashara nyingine zozote zile unahitaji kufanya utafiti pamoja na kuandaa mpango wa biashara yako utakavyokuwa. Zoezi hili usiniambie eti hutaliweza au ni mambo ya kitaalamu yanayomhitaji msomi aje akufanyie, la hasha. Utafiti na mchanganuo wa biashara hata mtu ambaye hajakanyaga shule ya vidudu hufanya kabla hajaanzisha biashara yeyote ile. Hapa ndipo maswala kama utapata vipi mtaji, utauza bidhaa zip nk. yanapojibiwa na katika kitabu yameainishwa yote hasa katika shuhuda mbalimbali za watu.

Hivi kuna mtu ambaye katika Ulimwengu wa leo hajawahi kufanya biashara hata ya kuuza karanga hata kama hajasoma? Ni dhahiri kabisa kwamba biashara na ujasiriamali hauchagui kiwango cha elimu ya mtu hivyo na utafiti au mchanganuo nao pia haujalishi umesoma au hujasoma ni lazima mtu afanye kabla hajaanzisha biashara yeyote ile. Kwa kifupi kabisa utafiti na mchanganuo wa biashara ni karibu kitu kimoja hichohicho na ikiwa hujui uanzie wapi basi nikuambie tu si kitu kigeni kwako kwani umeshawahi kufanya pasipo hata wewe kujua kama uliwahi kufanya.

SOMA: Utafiti wa soko la biashara yako/Upembuzi yakinifu

Utafiti au mchanganuo wa biashara kwa kifupi zaidi ni maswala yote unayoyawaza juu ya biashara yako na kutaka kujua yanafanywa vipi kabla hujaanza kuifanya biashara yenyewe na wala siyo sayansi ya kwenda mwezini au sayari ya Mars. Ili uweze kuifanya biashara au shughuli yeyote ile kwa ufanisi wa kutosha ni sharti kwanza uchunguze biashara au shughuli hiyo inafanyikafanyikaje, na huo ndio utafiti au mchanganuo wa biashara yako.

2. Pointi ya pili ni kuirasimisha biashara yako.
Hata ikiwa hautasajili kampuni lakini ni lazima ukitaka biashara yako ya duka isiwe na vikwazo basi angalau uhakikishe unaisajili katika ngazi ya serikali za mitaa kwa kwenda katika manispaa yako wakupe leseni ya biashara. Kuna suala pia la namba ya utambulisho(TIN namba) kwa ajili ya kulipa kodi ya mapato ikiwa biashara yako ni kubwa kidogo nk. Ukipenda unaweza ukasajili Brela jina la biashara yako pia.

3. Pointi ya tatu ni kuchagua eneo la biashara yako,
Watu husema Biashara ya duka la rejareja ni eneo” Eneo
utakalochagua kuweka duka lako, litaathiri kila kitu utakachokifanya katika biashara yako yote. Mafanikio au kuanguka kwa biashara yaduka la rejareja kunategemea kwa asilimia kubwa sana sehemu ulipoiweka biashara hiyo. Usikurupuke wakati wa kufanya uamuzi wa eneo utakaloweka biashara yako ya duka, chukua muda wa kutosha kufanya utafiti
na kuwa mvumilivu.


SOMA: Jinsi gani naweza kutengeneza pesa kwenye mradi wa mashine ya kukamua mafuta ya alizeti?

Ukigundua eneo halifai, basi ni bora ukaahirisha na kuangalia uwezekano wa eneo jingine kuliko baada ya muda mfupi kuja kuanza kuzozana na mwenye nyumba akurudishie kodi au hata biashara yako kufia njiani. Usikubali presha za madalali ambao hutumia ujanja kwa kukuambia eti, eneo/fremu fulani inagombewa na watu zaidi ya watatu na wewe ni wa nne, hivyo ukichelewa kidogo tu hutaikuta.

Katika toleo jipya la kitabu hicho la mwaka 2020 tumeongeza shuhuda mbalimbali za watu jinsi walivyoanzisha maduka yao ya rejareja ukiwemo ushuhuda wake mwenyewe binafsi mwandishi wa kitabu hiki Bwana Peter Augustino Tarimo. Ushuhuda huo upo katika picha za rangi.

SOMA: Tunatuma vitabu vya ujasiriamali mkoa wowote ule Tanzania kwa usalama wa asilimia 100% wa fedha ya mteja

Basi naamini mpaka kufikia hapo ndugu Lukas utakuwa umeshapata mwangaza walau ni mambo gani ya msingi zaidi mtu unayopaswa kuyazingatia ikiwa una ndoto za kuanzisha duka lako la rejareja mtaani.

Tunakaribisha maswali mafupimafupi kama haya na tutayajibu bila ubaguzi wowote ule. Lakini pia ukipenda kuwa karibu zaidi na sisi ili kujifunza mambo mengi zaidi kutoka kwa watu mbalimbali unaweza kujiunga katika magroupu yetu ya Watsap na Telegramu ya MICHANGANUO-ONLINE. Masomo ni kila siku na mada zetu ni Michanganuo ya Biashara mbalimbali pamoja na masomo yenye maudhui ya Pesa yasiyopatikana mahali kwingine kokote.

SIMU/WATSAP: 0765553030
SIMU/SMS:  0712202244

0 Response to "NATAKA KUFUNGUA DUKA LA REJAREJA LA MAHITAJI YA KILA SIKU KATIKA JAMII, MBINU GANI NAWEZA KUTUMIA KUFANIKISHA?"

Post a Comment