Katika hali zote ngumu zilizowahi kutokea
Duniani tangu enzi na enzi kuna vitu ambayo binadamu hakuweza kamwe kuendelea kuishi
bila kuvipata. Ukiachana na majanga yanayohusisha maambukizi ya maradhi mfano wa
hili la Corona(Covid 19) na hata maradhi ‘makongwe’ ya miaka mingi iliyopita
kama vile Tauni na Ukoma katika zama za Mitume kabla na baada ya Yesu Kristo,
na mengine ya karne za hivi karibuni tu
kama vile Kifuakikuu, Malaria, Surua na Ukimwi, majanga mengine makubwa na
yaliyoitikisa Dunia ni Vita, majanga ya asili kama mafuriko, matetemeko,
vimbunga, njaa na majanga ya midororo mikubwa
ya kiuchumi kama ule wa miaka ya 1930(Great Depression) na mwishoni mwa miaka
ya 2000
Majanga yote hayo iwe ni magonjwa na hata
vita mwisho wake husababisha mdororo wa kiuchumi na mdororo wa kiuchumi kwa
mujibu wa wataalamu upo wa aina mbili, (1)Recession – Huu ni mdororo wa
kiuchumi usiokuwa mkubwa sana na unaochukua miezi kadhaa tu au pengine hata
mwaka nk.(2) Depression – Mdororo huu ni mkubwa zaidi na huchukua hata muongo mzima
ambapo madhara yake ni makubwa zaidi yanayoweza kuenea Dunia nzima.
Tukiacha Midororo mikubwa karne nyingi huko
nyuma, katika historia ya Dunia ya hivi karibuni Mdororo mkubwa zaidi wa
kiuchumi, Great Depression umewahi kutokea mara moja tu mwaka 1930 mpaka baada
ya Vita kuu ya II ya Dunia, lakini midororo midogo midogo ya kiuchumi
(recessions) imewahi kutokea mara nyingi tu ukiwemo ule wa mwaka 2017 mpaka
2019 ulioanzia huko Marekani na baadhi ya nchi nyingine Duniani.
Majanga yote hayo iwe ni magonjwa na hata
vita mwisho wake husababisha mdororo wa kiuchumi na mdororo wa kiuchumi kwa
mujibu wa wataalamu upo wa aina mbili, (1)Recession – Huu ni mdororo wa
kiuchumi usiokuwa mkubwa sana na unaochukua miezi kadhaa tu au pengine hata
mwaka nk.(2) Depression – Mdororo huu ni mkubwa zaidi na huchukua hata muongo mzima
ambapo madhara yake ni makubwa zaidi yanayoweza kuenea Dunia nzima.
Tukiacha Midororo mikubwa karne nyingi huko
nyuma, katika historia ya Dunia ya hivi karibuni Mdororo mkubwa zaidi wa
kiuchumi, Great Depression umewahi kutokea mara moja tu mwaka 1930 mpaka baada
ya Vita kuu ya II ya Dunia, lakini midororo midogo midogo ya kiuchumi
(recessions) imewahi kutokea mara nyingi tu ukiwemo ule wa mwaka 2017 mpaka
2019 ulioanzia huko Marekani na baadhi ya nchi nyingine Duniani.
Kwa kifupi tu ni kwamba Mdororo wa Kiuchumi
maana yake hasa ni ile hali ya kushuka kwa shughuli za kiuchumi za nchi au
Dunia katika kipindi fulani ambapo hali hiyo husababisha vipato vya watu
kuporomoka vibaya, ukosefu mkubwa wa ajira, kushuka kwa uzalishaji viwandani,
biashara kufungwa, watu kushindwa kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma
mbalimbali pamoja na kushuka kwa pato la ndani la Taifa (GDP)
Kama nilivyotangulia kusema pale mwanzoni
kabisa katika mazingira magumu kama hayo niliyoyataja bado kuna biashara au
shughuli za kiuchumi ambazo piga ua zitaendelea kustawi hata kama ungekuja
mdororo mkubwa wa kiuchumi kiasi gani. Na sababu kubwa nitaitaja hapo baadae
kidogo baada ya kuelezea kidogo kuhusiana na janga kuu linalotunyemelea sasa
hivi la Covid 19 na ambalo hamna mwenye uhakika ikiwa Dunia itasalimika kuingia
katika Mdororo mkuu(Great Depression) kama ule wa wakati wa Vita kuu ya 2 ya
Dunia- World War II au utakuwa tu mdororo wa kawaida kama mingine mingi
iliyowahi kutokea Duniani katika karne ya 20 na 21. Ila tu uhakika ni kwamba
mdororo wa kiuchumi baada ya Corona ni lazima utokee uwe mkubwa au mdogo
Janga la Corona maarufu kama Covid 19
lililoanzia huko jijini Wuhan nchini Uchina limeyashitua Mataifa mengi yakiwemo
yale Mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza, Italy, Urusi, Ufaranza, Iran,
Uhispania na Korea ya Kusini. Mataifa haya kwa kweli hayakufikiria hata kidogo
ikiwa Corona ingeliweza kugeuka kuwa mwiba mkali hivi kwao, badala yake wakati corona
ikianza huko China, wao walidhani labda ingeliweza kuwa hatari tu kwa zile nchi
masikini zilizo na mifumo dhaifu ya kiafya kama nchi nyingi za Kiafrika au
baadhi ya nchi masikini za Asia na Amerika ya Kusini.
Virusi vya Covid 19 ni dada wa virusi wengine
wawili maarufu wa Corona, SARS na MERS, wote wakisababisha maambukizi ya homa
kali za mapafu. Virusi hawa wote ndugu vyanzo vyao ni mnyama mwenye mabawa kama
ndege au kwa jina la kawaida POPO. Inasemekana na Wanasayansi kuwa Sars
iliyoanzia pia nchini China virusi wake walihamia kwa binadamu kutoka kwa Popo
kupitia aina fulani ya Paka wafugwao, wakati Virusi wa Mers wao walimuingia binadamu
kutoka kwa popo kupitia Ngamia huko nchinni Jordan. Kwa upande wa Covid 19
inasemekana virusi hawa walimuingia binadamu wa kwanza huko Wuhan kupitia nyama
zilizokuwa zikiuzwa katika soko moja na chanzo chake pia inasadikiwa kuwa ni
haohao Popo.
Si kama Wachina wanakula nyama na supu ya Popo kama
watu wengi wanavyokazia hapana, bali inasemekana soko hili la nyama lilikuwa
likiuza kiholela pia ndege na wanyama wengine hai kama vile kuku, bata, mbuzi
nk. hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa popo waliweza kuwaambukiza ndege hao
virusi na binadamu alipowachinja na kuwala basi naye akaambukizwa Covid 19.
Unaweza ukastaajabu pia kwamba Dunia miaka ya
nyuma iiliwahi kushuhudia Magonjwa ya virusi yaliyoua watu wengi zaidi na pengine
hata yaliyokuwa hatari zaidi kuliko haya ya Corona. Katika zama tunazoishi sasa
mlipuko wa homa ya virusi uliotisha zaidi na kuangamiza roho za watu wengi
kupita mwingine wowote ule hata huu wa Corona ni ule wa virusi vijulikanavyo
kama H1N1 maarufu kama SPAIN INFUENZA. Spain Infuenza ulienea dunia nzima hapo
mwaka 1918 wakati wa vita kuu ya I ya Dunia na kuua watu wapatao milioni 50 mpaka milioni 100 duniani kote.
Mlipuko
mwingine wa ugojwa unaosababishwa na virusi uitwao ASIAN FLU hapo mwaka
1957 uliangamiza watu milioni 2. Miaka 10 baadae ugojwa mwingine unaofanana na
huo, HONG KONG FLU pia ukaua watu milioni moja. Mwaka 2009 yalizuka Mafua ya
Nguruwe, SWINE FLU nao ni wa virusi
ukaua watu 575,400. Ugojwa wa ZIKA 2015 wenyewe hauna madhara makubwa sana kwa
watu wazima lakini umeacha maelfu ya watoto waliozaliwa na mama wenye virusi
hivyo wakiwa na ulemavu wa kudumu wa viungo hususani kichwa na ubongo.
SASA
NI KIPI CHA KUFANYA?
TUSIPANIKI WALA KUPUUZIA! Janga
la Corona litapita kama yalivyopita hayo majanga mengine yote yaliyotajwa hapo
juu, lakini haliwezi kupita hivihivi tu, kila mtu ni lazima alipe gharama
fulani katika kuhakikisha tunapunguza madhara yake. Kuna watakaolipa gharama
kubwa zaidi mfano wale watakaolazimika kukatisha uhai wao kutokana na ugonjwa
huu lakini pia wengi watalipa gharama japo kidogo kama tunavyosisitiziwa na mamlaka
mbalimbali likiwemo Shirika la Afya Duniani WHO, Serikali zetu na viongozi
wengine wa wizara ya Afya na hata wale wa Dini.
Gharama kubwa tunayopaswa sote kuilipa kwa
mujibu wa Mamlaka hizo ni kuhakikisha mara kwa mara tunaosha mikono yetu kwa
sabuni au vitakatishi(sanitizers), kuepuka kukaribiana na mtu yeyote zaidi ya
wale tunaoishi nao ndani, kukwepa mikusanyiko yeyote ile na kumripoti mgeni
yeyote unayehisi katoka nchi nyingine kinyemela bila kufuata taratibu
zilizowekwa ili awekwe karantini mara moja.
Basi baada ya kuangazia Virusi vya ugojwa wa
Corona kwa ujumla na maambukizi mengine ya virusi, sasa moja kwa moja hebu
twende tukazione zile biashara ambazo huwa zina tabia ya kuvumilia hali yeyote ile
ngumu ukiwamo hata ugonjwa huu wa Corona.
AINA
KUU NNE (4) ZA BIASHARA ZILIZO NA UWEZO WA KUJIKINGA DHIDI YA HATARI ZA MAJANGA
KAMA CORONA NA MENGINEYO
Kunapotokea janga kubwa kama la Corona,
biashara nyingi huathirika kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi lakini
kubwa zaidi ikiwa ni matatizo ya mzunguko mdogo wa pesa kwa biashara au kampuni
zile zisizokuwa na kinga dhidi ya majanga. Mara nyingi biashara hizo hulazimika
kupunguza matumizi kama vile idadi ya wafanyakazi, mishahara, ikiwa ni pamoja
na kukopa ili ziendelee kuwepo. Kwa upande wa wateja wao nao pia hupunguza kwa
kiasi kikubwa manunuzi ya vitu visivyokuwa na ulazima hali inayozidisha hali
mbaya zaidi kwa kampuni/biashara hizo.
Kwa upande wa zile biashara zenye kinga dhidi
ya majanga, zenyewe huendelea kuwa imara kutokana na mzunguko wake wa fedha
kutokutetereka sana na hii haijalishi ikiwa uchumi umedorora sana ama la. Sisemi kwamba biashara hizo haziathiriwi kabisa hapana, bali ukizilinganisha na nyingine huwa zinakuwa na unafuu mkubwa zaidi. Aina
ya biashara hizo ni hizi hapa chini;
(1)
Biashara zote za mahitaji yale ya msingi.
Hizi ni zile biashara zote zinazohusisha
bidhaa za msingi kabisa kwa uhai wa binadamu na ambazo kamwe haziwezi kuepukika
kwa hali yeyote ile. Mfano wake ni biashara za vyakula na biashara ya madawa na
vifaa tiba, vifaa vya usafi kama vile sabuni, vitakatishi(sanitizers), dawa za
mswaki nk. Umuhimu wa chakula kwa
binadamu hauna kifani, kuna hatua inaweza kufikia pande mbili mahasimu katika
vita wakaamua kusitisha vita au hata kuamua kupatana kisa tu njaa au mlipuko wa
janga kubwa mfano wa hili la Covid 19. Mfano mzuri tumeshuhudia kwenye Janga
hili sasa hivi ambapo Mataifa mengi baada ya kufunga kila kitu maduka ya
chakula na dawa hayajaguswa hata kidogo.
Tuchukulie mfano tu labda mtu unamiliki
kiwanda chako cha unga wa dona au hata unga wa sembe katikati ya janga kama
hili, tuseme hata ikiwa hauna mtaji wa kutosha kuendeshea kiwanda chako,
serikali inaweza hata kuwa tayari kukukopesha fedha ilimradi tu uendelee
kuzalisha unga wa kutosha kwa ajili ya wananchi waliojifungia majumbani mwao
kujikinga na virusi.
(2)
Biashara za utoaji huduma muhimu za msingi.
Kama ilivyo kwa bidhaa muhimu, kuna huduma
pia ambazo katu haziwezi kuepukika katika hali yeyote ile ya kiuchumi. Huduma
kama vile za afya: zahanati, hospitali na vituo vya afya ni lazima ziwepo. Kuna
biashara nyingine kwa mfano utoaji wa huduma za kusafirisha abiria haziwezi
kuathirika sana isipokuwa tu zitawekewa taratibu fulani fulani huku zikiendelea
kufanya kazi.
Usafirishaji wa mizigo ndio kabisa hauguswi
na hata tumeshuhudia nchi nyingi zikiruhusu mizigo kuingizwa licha ya mipaka
kufungwa abiria wasiingie. Biashara nyingine zinazoshamiri kipindi kama hiki ni
zile za utoaji huduma kama vile usafirishaji na uuzaji wa mafuta ya magari na
mitambo(sheli), umeme na nishati za kupikia majumbani.
(3)
Biashara ya kurepea vitu vilivyoharibika pamoja na uuzaji wa vipuri
Katika hali yeyote ile ngumu ya kiuchumi iwe
imesababishwa na Ugonjwa, Mdororo wa kiuchumi au hata Majanga mengine ya asili,
ni kawaida watu kutokupenda kabisa kununua vitu vipya. Badala yake utakuta kila
mtu akitaka kukifanyia marekebisho kifaa au kitu chake cha zamani
anachokimiliki ili kupunguza gharama za manunuzi ya vitu vipya. Wataripea vitu
vya zamani mpaka mwisho vitakapokuwa havirekebiki tena, iwe ni gari, redio au
hata sufuria. Hii huenda sambamba na biashara ya vipuri vile vinavyobadilishwa
mara kwa mara na visivyokuwa na mbadala wake.
(4)
Biashara za huduma zinazosaidia watu kujikwamua na janga lililosababisha
mdororo wa kiuchumi.
Ikiwa utafanya biashara yeyote ile
inayohusisha huduma au bidhaa zinazosaidia watu kuondokana na tatizo
lililopelekea hali kuwa ngumu, biashara hiyo haitaathirika kutokana na sababu
kwamba kila mtu atataka kupata hiyo huduma ili hatimaye aweze kujinasua. Tumeshuhudia
biashara kwa mfano za vifaa vya kujikinga na Corona kama vitakatishi na
barakoa(masks) wafanyabiashara wakipandisha bei kama fursa kwao ya kutengeneza
kiasi kikubwa cha faida. Huduma za ushauri na uhasibu huendelea kufanya vizuri
hata yanapotokea majanga kwa sababu makampuni mengi bado yanakuwa yakihitaji
watu wa namna hiyo kwa ajili ya kufufua uchumi wa biashara zao uliozorota.
…………mwisho……………
*TANGAZO MUHIMU*
SEMINA YA MCHANGANUO WA BIASHARA BUNIFU
YA KIWANDA CHA UNGA SAFI NA SALAMA WA DONA
(USADO MILLING)
Mpendwa msomaji na mjasiriamali unayependa
kusoma Makala katika blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali napenda
kukujulisha kwamba zile huduma zetu zote zimerudi tena kama kawaida baada ya
kipindi kama cha miezi 2 hivi. Kwa wale tuliokuwa pamoja mwaka mzima wa 2019 mtakumbuka ahadi yangu ya
Uzinduzi wa kiwanda changu mwenyewe kipya nilichoahidi kwamba utakuwa ni wa
kihistoria, kwa takribani miezi 2 nilikuwa nikitengeneza documentary kwa ajili ya shughuli hiyo muhimu na kwa bahati mbaya
kabla sijamalizia likazuka janga hili la Corona.
Kwa kuwa mikusanyiko imekatazwa shughuli hiyo
imekuwa ngumu kidogo kumalizia kutokana na maeneo yenyewe niliyokuwa nikichukua
baadhi ya video kuhusisha mkusanyiko wa watu. Hata hivyo naamini baada ya janga
kwisha kazi itaendelea na Mungu akipenda basi Aprili mwishoni itakuwa ndiyo
shughuli yenyewe rasmi.
Basi hapo tarehe 2 Aprili mpaka tarehe 4
katika magroup mawili ya MICHANGANUO-ONLINE tutakuwa na SEMINA juu ya jinsi ya
kuandaa Mpango wa biashara(MCHANGANUO) wa Kiwanda kidogo cha Usagishaji unga
safi na salama wa Dona(USADO MILLING)
Semina itafanyika katika Group la whatsapp la zamani na jipya linaloanzishwa
leo hii kwa jina MICHANGANUO-ONLINE-2.
Hakuna tofauti kubwa baina ya magroup haya mawili isipokuwa tu muda mtu
aliojiunga na OFFA zilizotolewa.
FAIDA
ZA KUJIUNGA NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE-2 2020 NI HIZI ZIFUATAZO.
Kwanza nitangaze rasmi kwamba ile OFFA ya mwaka jana ya vitu zaidi ya 15
haipo tena mwaka huu, badala yake tumeleta offa nyingine mpya. Manufaa hayo ni pamoja
na kushiriki semina zote kwa mwaka huu wa 2020 tukianza na ile ya Aprili ya
Kiwanda cha Unga wa Dona(USADO MILLING), kuwa member wa group kwa mwaka wote wa
2020, kupata masomo(somo moja kila siku)
linalohusiana na elimu ya fedha(Financia literacy), kutoa mchango
wowote uutakao kwenye group, kuuliza chochote, fursa ya kutangaza bidhaa au
huduma zako ilimradi tu huvunji sheria za nchi pamoja na Upendeleo maalumu(Special
privilledge) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda changu bunifu hapo
Aprili mwishoni.
Manufaa hayo yanaambatana na OFFA ya vitu hivi 5 vifuatavyo
utakavyotumiwa pindi tu umalizapo kulipia ada ya mwaka shilingi 10,000/= ;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO-ONLINE katika lugha ya Kiswahili.
2. Kitabu
cha Michanganuo katika lugha ya kiingereza, kinachotumiwa na vyuo vikuu vingi
Duniani-English
3. Michanganuo
3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3 PACKS)-Swahili
4. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT BUSINESS PLAN)-English & swahili
5. Mchanganuo
wa Matikiti maji(KIBADA WATERMELON-BUSINESS PLAN)-Swahili.
Kiingilio/Ada katika Semina hii ni shilingi elfu 10 tu
ambayo inalipwa kupitia namba zetu zifuatazo,
0765553030 au
0712202244 na
Jina ni Peter Augustino Tarimo
Baada ya malipo, tuma ujumbe wa watsap au SMS usemao,
NIUNGANISHE GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE PAMOJA NA OFFA YA VITU 6
Mwisho wa kulipa kwa ajili ya semina ni tarehe 30/3/2020.
Baada ya tarehe hii ukilipia utaweza kupata hizo offa na kuungwa katika group
lakini semina ya USADO MILLS utakuwa umeikosa.
Asante na Karibu sana !
Peter Tarimo
Mhamasishaji na Mwanaviwanda mwenzako 2020
WHATSAPP: 0765553030
SOMA PIA MAKALA ZIFUATAZO;
1. Wanasayansi wagundua dawa mpya ya kuua virusi vya Ukimwi vilivyojificha
2. Hatimaye ile nyama ya kutengeneza maabara yaanza kuliwa.
3. Wanasayansi wagundua mnyama wa ajabu !
4. Dengue ni kama Tauni na Ukoma zama za Yesu Kristo, ukiupata hamna dawa-unawekwa karantini
5. EBOLA: Tuachane na dawa za kizungu turudi kwenye asili, vikombe vya babu na muarobaini?
naweza kupata msaada wa kufungua blog na website account.
ReplyDelete