Duniani kuna mawazo mengi sana ya biashara
yanayovutia, Watu wengi hasa katika mitandao hii ya kijamii huhamasika sana
pale wanapokutana na Makala au video kuhusiana na biashara zenye kulipa kiasi
kikubwa cha faida, biashara zinazolipa haraka na hata zile biashara
ndogondogo zinazoweza kufanywakwa mtaji mdogo ama hata bila ya mtaji kabisa.
Lakini ukweli wa mambo upo hivi, hakuna biashara yeyote isiyolipa, katika kila
biashara unayoiona au kuisikia inalipa kutegemeana na mahitaji yake katika
jamii yapoje na isitoshe, wewe mwenyewe unaweza ukayatengeneza mahitaji hayo
hata ikiwa hayapo au wateja hawayaoni, hili nitalielezea vizuri karibu na
mwisho wa Makala hii.
Ikiwa jamii(Wateja) wana uhitaji na bidhaa
ama huduma fulani basi ujue wazi hapo kuna biashara na unaweza ukatengeneza
wazo lako zuri la biashara inayolipa faida. Pamoja na ukweli huu bado kuna
mawazo ya biashara yanayovutia watu zaidi au kuonekana kuwa ni yenye kuleta
faida chapchap kushinda mengine ila cha kusikitisha ni kwamba wajasiriamali
wengi kila wanaposema “ngoja nikamate wazo hili bora la biashara
nipate pesa”, njiani wanakuja kubaini kumbe wazo hilo lina ushindani
mkali kupindukia na haiwezekani kirahisi mtu akapata faida aliyotarajia
angeliipata haraka.
Miongoni mwa mawazo bora kabisa ya biashara
yanayowavutia watu wengi mara kwa mara kuanzisha yapo mengi lakini katika Makala
haya nitataja mawazo mawili tu kama mifano ya kuwakilisha yale mengine, nayo ni
hii ifuatayo;
1. Miradi
au Biashara za ufugaji wa kuku.
Hii ni miradi maarufu sana kote duniani na
kila mjasiriamali mdogo anapoisikia tu ikitajwa mahali moyo hulipuka akifikiria
namna biashara hii ya ufugaji wa kuku inavyoweza kumtajirisha au kumtoa kimaisha
haraka. Kwa mara ya kwanza mimi binafsi kusoma katika vyombo mbalimbali vya
habari ukiwemo mtandao wa intaneti na majarida jinsi biashara ya ufugaji wa
kuku inavyolipa upesi, mara moja nilikumbuka enzi zile nasoma shule ya msingi
kijijini nilpokuwa nafuga kuku wachache wa kienyeji.
Nilipojaribu kuvuta picha ni lini niliwahi
hata kujilipia ada kwa faida ya wale kuku nikakuta hakuna hata siku moja zaidi
ya pesa za wazazi wangu. Sasa nikajiuliza tena ikiwa kuku wana uwezo wa kulipa
kimaajabu namna ile ni vipi sikuweza hata kujilipia ada kutokana na faida
niliyokuwa nikiipata?
Nakumbuka changamoto yangu kubwa ilikuwa ni uwekezaji
mdogo kwenye mradi ule kwani kuku walikuwa wachache na hivyo kupata faida kubwa
ya kutosha halikuwa jambo rahisi ukitegemea majirani walionizunguka nao walikuwa
wakifuga kuku huku bei ya kuku na mayai ikibakia kuwa ni ileile huwezi
kupandisha kirahisi kuwazidi hao washindani. Nilihitaji uwekezaji(Mtaji) mkubwa
zaidi kuniwezesha kupata faida au mafanikio makubwa na ya haraka jambo ambalo
halikuwa rahisi kwangu kipindi hicho.
Hata baada ya kipindi hicho kupita(sasa hivi)
bado nimeendelea kuwa mfugaji mzuri wa kuku na siku moja nikaamua kukaa chini
na kufanya tathmini ya kina juu ya miradi hii ya ufugaji wa kuku aina zote
kujua kama nilikuwa nakosea wapi muda wote huo nisiwe milionea. Nilifanya utafiti
wa kina na kuandaa michanganuo mitatu ya biashara za ufugaji wa kuku, kuku wa mayai, kuku wa nyama na
kuku wa kienyeji(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS).
Katika michanganuo hii 3 kitu kikubwa
nilichogundua ni kwamba, ni kweli kabisa biashara ya ufugaji wa kuku iwe ni wa
mayai, nyama au wale wa kienyeji yote ina faida lakini ni faida ya kawaida
ambayo huwa inaweza ikapatikana katika kipindi kifupi mfano wiki tano tu hadi 8
kwa kuku wa nyama. Miradi hii haina tofauti kubwa na miradi mingine ya
kibiashara na ikiwa basi mtu atapenda kupata mafanikio makubwa upesi basi hana
budi kufuata kanuni zote za biashara sawa tu na mmiliki wa biashara ya nguo au
duka la rejareja afanyavyo.
Kitakachokufanya ufaulu kwenye biashara ya
ufugaji wa kuku ni kuwa na mtaji wa kutosha pamoja na utekelezaji mzuri wa
mipango na mikakati yako ya kimasoko utakayojiwekea na wala siyo wazo lenyewe
tu kama watu wengi tulivyokuwa tukifkiria hapo kabla. Na haijalishi kama mtaji wa
kutosha unao tayari au utafuga kuku wawili na kusubiria mpaka wafike mia, elfu
nk., mafanikio makubwa utayaona tu pale kuku wako watakapofikia idadi kubwa hata
kama itakuchukua miaka 10 kufikisha idadi hiyo, vinginevyo utaishia tu kufuga
kuku wawili, watatu kwa ajili ya mayai ya kunywea chai asubuhi na kitoweo siku
moja moja.
2. Biashara
ya Viwanda vidogovidogo
Wazo la kumiliki kiwanda kidogo pia linawavutia
watu wengi sana kutokana na ukweli kwamba wapo matajiri wengi leo hii hapa
Tanzania na Duniani walioanzia kwenye biashara hizi. Kiwanda ni biashara ya
uhakika sana kushinda biashara nyingine za kawaida endapo tu kitatimiza vizuri
na kwa ufanisi mahitaji fulani ya kundi fulani la wateja na siyo kila kiwanda
tu ilimradi kinaitwa kiwanda kinaweza kumletea faida haraka mmiliki wake.
Katika mfano huu wa kiwanda na nimeutoa kwa makusudi kabisa kutokana na maswali
mengi ya wajasiriamali ninayokutana nayo wakitaka taarifa mbalimbali jinsi
kiwanda kinavyoweza kuwatoa kimaisha, ndio nitajibu swali la ni mbinu zipi
utumie katika kiwanda chako kupata faida licha ya ushindani mkali uliopo.
Kama ilivyokuwa kwa biashara nyingine zote
kiwanda chako kinatakiwa lazima kizalishe bidhaa itakayotatua tatizo la aina
fulani la wateja kwenye jamii. Haiwezekani watu wote wakawa na hilo tatizo
ingawa pia wakati mwingine kuna bidhaa zinazoweza kuwa zinahitajika na kila mtu
lakini kwa nyakati tofauti. Lakini bado tu hata ikiwa mahitaji yapo ushindani
mkali hauepukiki kirahisi, hii ni sababu kubwa inayozifanya biashara zinazovutia sana mwishowe watu wengi wazione ni ngumu kwao kuzifanya na haziwezi kuwaletea mafanikio ya haraka.
SASA
BASI UTUMIE MBINU ZIPI KUSUDI BIASHARA YAKO YENYE USHINDANI MKALI IWEZE KUPATA WATEJA WENGI NA WA KUDUMU?
Biashara ya kuuza chakula kwa mfano ni wazo
jingine zuri la biashara inayopendwa na watu wengi lakini ubaya wake mmoja tu ni kwamba lina ushindani mkubwa sana kutokana na watu wengi kutamani kuifanya kwa kuwa wanafahamu
fika watu kila siku wanahitaji kula, iwe masika au kiangazi, kuwe na vita au amani,
kuwe na janga la Corona au kusiwe nalo nk. Halikadhalika pia na biashara ya utengenezaji na uuzaji wa sabuni aina zote
Kulijibu swali hili kwa ufasaha kabisa,
nimelazimika kuandika Mchanganuo/Mpango wa biashara ya kiwanda kidogo cha Unga
wa Dona(USADO MILLING). Niliona kwa maneno matupu tu kama ilivyozoeleka wengi
hawatanielewa. Kumbuka mchanganuo au mpango wa biashara maana yake ni maelezo
ya kila kitu utakachokifanya katika biashara uliyokusudia kuifanya, ni hatua
zote bila kujali hayo uliyoyaandika au kuyawaza utayatekeleza kama yalivyo au
tofauti.
Wapo watu wengine hupotosha kwa makusudi
kwamba mpango wa biashara si muhimu na kuuandaa ni kupoteza tu muda. Hii si
kweli hata kidogo kwasababu kila anayeanzisha biashara ni maono kwanza huanzia
kichwani mwake na maono hayo ndiyo mpango wenyewe wa biashara. Ikiwa kama
hautatabiri biashara inaweza kukulipa utaingiaje tu kichwakichwa kuifanya?
Hivyo ni kusema kwamba kila mjasirimali awe
mdogo au mkubwa huanza na mpango wa biashara kwanza kichwani mwake kabla hata
ya kufanya kitu chochote kile. Na sasa utakapoamua uuandike mpango huo kwenye
karatasi hilo ni jambo jingine lakini mpango ni mpango tu, iwe umeuandika
mahali ama umeufikiria na kuuacha kichwani mwako.
Tukirudi kwenye mbinu zenyewe maanake sasa
naona nimezama mno kwenye business plan, mbinu hizo ni hizi
hapa chini; Katika kuhakikisha kiwanda hiki cha USADO unga wake unapata wateja
wa uhakika na wakudumu licha ya ushindani mkali uliopo, mambo kadhaa yalifanyika;
Kuamua
kuwa tofauti
Kwanza kabisa wamiliki wake ambao ni madada
wawili(kina mama) baada ya kuunganisha nguvu zao kimtaji walikaa chini na
kutengeneza mkakati wao wa masoko utakaowawezesha kuwa tofauti kabisa na
wazalishaji wengine wa unga wa DONA sokoni. Mkakati huo naweza kuuita, MKAKATI WA KUFA MTU(The
Killer Marketing Plan) Je, unajua ni mikakati gani hiyo waliyokuja
nayo? Soma mpango huo mzima.
Bidhaa
za kipekee
Unga wa dona umezoeleka sana na hamna mtu
asiyeujua, ukienda dukani na kusema nipe dona utachotewa kwenye kiroba na
kupimiwa mara moja bila maswali zaidi kutoka kwa muuzaji. Sasa ni mbinu zipi
walizozitumia ili kuhakikisha ‘dona lao’
linakuwa tofauti kabisa na Dona wanayozalisha watu wengine wote katika soko
wanalolilenga? Mchanganuo huu unajibu kila kitu katika Sura yake ya Mkakati
maalumu kabisa wa Masoko wa USADO MILLING. Na kumbuka mkakati wa soko
hauhusishi matangazo ya biashara tu peke yake bali ni vitu vingi kuanzia ubora
wa bidhaa yenyewe, jinsi unavyoifungasha, bei, wateja, washindani nk.
Kujiposition
vizuri katika soko/Kujipanga katika soko/Kujibrandi
Hizi ni kaulimbiu, alama au maandishi mbalimbali
watakayoyatumia kwenye matangazo yao mbalimbali katika kujitofautisha kabisa na
washindani wao sokoni, ni jinsi wanavyotaka wateja wao wawaone au kuwafikiria.
Siyo kila kauli mbiu tu itawahamasisha wateja wazipende bidhaa zako, ni lazima
uchague kauli yenye maneno yatakayogusa hisia za watu mpaka muda wote wakiziona
bidhaa hizo mahali wazikumbuke hisia hizo. USADO MILLING wameibuka na kauli
mbiu ya kipekee sana ambayo wateja wao watarajiwa wataipenda na moja kwa moja
kuupenda unga wao kwa kuwa inawagusa mioyoni moja kwa moja.
Kutatua
matatizo ya wateja.
Unga kazi yake kbwa ni kupikia ugali kwa ajili ya
kumpatia mtu shibe ili kutatua tatizo la njaa, hili hamna asiyelifahamu hata
mtoto wa chekechea analijua. Sasa unaweza ukaniuliza hivi, “Bwana
pita ni tatizo gani la kipekee hapa USADO MILLING watalitatua ili kuwashawishi
watu waachane na unga wa dona unaouzwa madukani bei chee?” Sasa hapa
ndio penye kazi pevu, pale mwanzoni niliahidi kuja kuelezea dhana ya
kutengeneza mahitaji ya bidhaa hata kama wateja wenyewe hawayaoni. Usipoweza
kubaini matatizo mengine ya kipekee bidhaa yako inayoweza kuyatatua utaishia
kulia kiwanda chako hakilipi.
Hapa sasa ni lazima ufanye kitu kinachoitwa
Mchanganyiko wa mbinu za kimasoko(Market
Mix) ili uweze kuchuja na kupata kundi fulani tu la wateja wako miongoni
mwa wateja wote wanaohitaji zile bidhaa, kundi ambalo limesahaulika na
washindani wako bado hawajalishitukia. Watakapokuja kushtuka watakuta wewe upo
mbali sana, hukamatiki tena, ni kama unavyowaona kina Moo na Bakhresa sasa, unaweza
kuanza biashara ukashindana nao kirahisi sasa hivi? USADO MILLING kwa kutumia
unga wao wa Dona wanatatua matatizo mengine tofauti kabisa na yale
yaliyozoeleka kila siku. Ni yapi hayo?
Kuacha
Wateja wenyewe ndio wakutangazie bidhaa zako.
Mbinu hii ni nzuri na haikugharimu pesa
nyingi kwa ajili ya kuzitangaza bidhaa zako, wateja wenyewe ndio watakaochukua
jukumu la kukutangaza popote pale kwa wateja wengine watarajiwa. Kazi yako
inakuwa ni ndogo tu, kuanzisha mjadala mithili ya vile uwashapo jiko la mkaa
kwa tutumia vipande viwili tu vya mkaa wa moto na baada ya muda mchache jiko
zima kukolea moto.
Hizo ni baadhi tu ya mbinu za kimasoko
unazoweza ukazitumia katika kuhakikisha bidhaa za kiwanda chako zinapata wateja
miongoni mwa viwanda vingine vingi vinavyozalisha bidhaa sawa na za kwako na
wala siyo sayansi ya kuunda rocketi au kwenda mwezini inayotumika ili kiwanda
chako kiweze kuuza kama ‘njugu’ Kujibrandi ni lazima kuoane kweli na uzuri na ubora wa
bidhaa zako na siyo kwenye matangazo unadai unga wako ni bora kumbe mtu
akiupika anakutana na mabuje au wadudu kibao, hiyo itakufukuzia wateja na kuanza
kumtafuta mchawi bure.
Katka mchanganuo huu kuna vitu wamiliki wa
USADO MILLING watavitekeleza katika kuhakikisha kweli unga wao unakuwa na ubora
brandi au jina lao linaoupigia debe na siyo blaa blaa tu. Kuna mikakati mahsusi
itakayotekelezwa kwa lengo la kuwathibitishia wateja kuwa ni kweli ubora huo
upo na wala siyo matangazo matupu ya biashara. Yote haya yameainishwa katika
mkakati huo wa ‘kufa mtu’ ndani ya Mpango wa biashara ya USADO MILLING.
Nimekudondolea kiasi kidogo sana kuhusiana na
Mkakati wa masoko wa biashara hii ya kiwanda cha USADO MILLING, mengi zaidi
unaweza kuyapata tu kwa kuusoma mpango huo mwenyewe ukiwa umetulia. Si lazima
uandike wa kwako ili uweze kufungua biashara ya kiwanda kama hicho au
kinachoshabihiana nacho, bali kwa kuusoma tu unapata madini ambayo
yatakuwezesha na wewe kuweka mikakati yako hata ikiwa unaiweka kichwani tu kama
watu wengi wanavyofanya kabla ya kuanzisha miradi yao.
SOMA: Sababu kuu (5) kwanini uandike mpango wa biashara yako kwanza kabla hujaianzisha biashara yenyewe.
Ikiwa utapenda kuupata mpango huu kabambe wa
biashara ya USADO MILLING na kuusoma kwa kituo, karibu sana siku ya Alhamisi ya
tarehe 2 mwezi wa 4, 2020 katika mafunzo ya siku 3. Pamoja na kupata mpango huo
kamili katika lugha ya Kiswahili lakini tutajifunza hatua kwa hatua jinsi
mchanganuo huo ulivyotengenezwa tangu Muhtasari wake mpaka Makisio ya ripoti za
fedha zote kama faida na hasara nk. pamoja na vielelezo mbalimbali. Mafunzo
yatafanyika kwenye magroup ya whatsap ya MICHANGANUO-ONLINE
sambamba na Channel yetu mpya ya Telegramu maalumu kwa ajili hiyo.
Kwa ambaye hatumii Whatsap wala Telegramu
hamna shida kwani tunatuma pia kila kitu kupitia Baruapepe(E-mail)
Kila mshiriki mara tu atakapomaliza kulipia
kiingilio chake sh. Elfu 10 atapata papo hapo OFFA ya vitu vingine 5 vifuatavyo na offa hii ni ya muda mfupi
sana, haitakaa tena muda mrefu kama ile ya mwaka jana ya vitu 15. Vitu hivyo ni
Kitabu chetu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pamoja na michanganuo
mbalimbali kama ifuatavyo;
1. Kitabu
cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI -kwa
kiswahili
2. Kitabu
mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza,
ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa
kiingereza
3. Kifurushi
maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)-kwa kiswahili
4. Mchanganuo
kamili wa kilimo cha Matikiti maji(KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili
5. Mchanganuo
wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT BUSINESS PLAN) -kwa Kiswahili & kiingereza
Pia kwa wale watakaopenda kubakia kwenye
group hili baada ya mafunzo hayo ya siku 3 (Kwani
kuna wasiopenda kuwa ktk magroup) wataruhusiwa kubaki mpaka mwaka huu wa
2020 utakapomalizika. Katika magroup ya MICHANGANUO-ONLINE huwa tunajifunza
kila siku masomo yenye maudhui ya pesa(Financial Literacy) pamoja na
kufanya michanganuo rahisi ya biashara ndogondogo zinazolipa. Kutakuwa pia na
michanganuo kamili(Mirefu) mfano wa huu wa USADO MILLING au ile iliyotajwa
kwenye OFFA katika vipindi maalumu.
NAOMBA
NIRUDIE TENA KWA HERUFI KUBWA KABISA KWAMBA, ADA YA MWAKA MZIMA NI SH. ELFU 10
TU ZA KITANZANIA NA HATUNA MALIPO YALIYOJIFICHA MBELE YA SAFARI. UTA ENJOY
MASOMO NA VITU MBALIMBALI KWA ELFU 10 HIYOHIYO BILA KUTIMULIWA KWENYE GROUP AU
CHANELI YETU KISA ADA.
Lipia sasa hivi kupitia namba zetu hizi hapa;
0765553030 au 0712202244 kunufaika na OFFA hiyo ya vile
vitu 6 papo hapo huku ukisubiria Mkakati
wa masoko wa kufa mtu(The killer Marketing Plan of USADO Milling Plant)
siku ya Alhamisi tarehe 2 Aprili.
Jina M-pesa au Tigo-pesa litakuja, Peter Augustino Tarimo
Baada ya kulipa shilingi 10,000/= yako kama ada ya mwaka huu wote, tuma ujumbe kupitia watsap
0765553030 au SMS ya kawaida usemao;
“NITUMIE
OFFA YA VITU 6 NA KUNIUNGANISHA NA GROUP LA MASOMO YA MICHANGANUO 2020”
Si lazima uwe na Watsap au Telegramu, E-mail pia inatosha. Ingawa ukiwa navyo
ni vizuri tu.
ASANTE SANA NA UNAKARIBISHWA
PETER
A. TARIMO
Writer and Tanzanian Industrialist 2020
I am
playing my part, how about you?
0 Response to "KWANINI WAZO ZURI LA BIASHARA NDIO LENYE USHINDANI MKALI & MBINU ZA KUFANYA LIWEZE KUKUPA FAIDA KULIKO WASHINDANI WAKO"
Post a Comment