WAZO BORA LA BIASHARA INAYOLIPA SIYO LAZIMA LIWE JIPYA SANA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

WAZO BORA LA BIASHARA INAYOLIPA SIYO LAZIMA LIWE JIPYA SANA

Wazungu husema “you can’t re-invent the wheel” wakimaanisha kwamba huwezi ukagundua upya matairi ya gari. Usemi huu maana yake ni kwamba ili kufanikiwa katika jambo fulani haulazimiki kufanya kitu au jambo jipya kabisa duniani na badala yake inakupasa ufanye yaleyale waliyofanya watu wengine kwa ubunifu na ustadi zaidi pengine hata kuwashinda.

Biashara zipo nyingi na za kila aina, ili uweze kuwa mjasiriamali mzuri unatakiwa aidha ubuni kitu kipya kabisa, au ubuni njia mpya ya kufanya biashara, masoko mapya, njia mpya za usimamiaji biashara, namna mpya na bora zaidi ya kuwahudumia wateja nk.


Kinachohitajika wakati wa kutafuta wazo bora la biashara ni mbinu za kupata wazo hilo ambazo ndizo zitakazolifanya liweze kufaa au kuwa bora na wala siyo upya au upekee wa wazo la biashara, ingawa pia upya au upekee ni moja kati ya njia nyingi zinazoweza kutumiwa kupata wazo linalofaa la biashara na wajasiriamali au wafanyabiashara.

Mbinu au njia mbalimbali za kutumia wakati wa kutafuta wazo bora linalofaa la biashara inayolipa.

1. Taaluma ama ujuzi uliopata
Ujuzi au taaluma uliyo nayo ndiyo mbinu ya kwanza kabisa unayoweza kuitumia katika mchakato wako wa kupata wazo mwanana la biashara itakayokupa faida. Madhalani unaweza ukawa wewe umeajiriwa kama mtaalamu wa maabara katika zahanati fulani. Unaweza ukaamua baada ya kupata mtaji wa kutosha na wewe kwenda kufungua kituo chako kwa ajili ya kuhudumia afya za watu aidha kwa kufanya vipimo mbalimbali vya magojwa au hata kwa kufungua zahanati yako mwenyewe huku na wewe ukiajiri wataalamu ambao wewe huna utaalamu wa kazi zao kama manesi au madaktari.

Utakuta wajasiriamali wengi duniani wenye mafanikio makubwa ni watu ambao zamani walikuwa wameajiriwa mahali fulani kutokana na ujuzi waliokuwa nao na kisha baadae kuja na wao kufungua biashara zao zinazohusiana na ujuzi waliokuwa nao.

2. Hobby uliyokuwa nayo unaweza ukaigeuza kuwa biashara.
Kile kitu unachopendelea maishani mwako unaweza badala tu ya kukifanya kama burudani basi ukaamua kukifanya kibiashara na kikakulipa vizuri sana. Tuseme labda wewe hobby yako ni kutazama mpira wa miguu pamoja na kushabikia timu za hapa na ulaya kama vile Manchester United, Liverpool, Simba, Yanga na hata Azam FC.

Unaweza ukaamua kuwa mchambuzi wa soka katika maredio au Tv, kazi itakayokuingizia kipato badala ya kubakia kuwa mshabiki tu peke yake. Au hata ikiwa wewe unapendelea mchezo huo unaweza ukaanzisha banda kwa ajili ya kuonyesha mipira mbalimbali ya nje kupitia decoda au TV na kwa kuwa watu wengi wanapenda sana mchezo wa soka watajaa kuja kutazama kila siku kama utawawekea chaneli nzuri za mpira wa miguu.

3. Kununua biashara iliyokwisha anzishwa tayari
Njia ya tatu, unaweza kupata wazo lako la biashara kwa njia ya kununua biashara ya mtu mwingine aliyekwisha ianzisha tayari lakini akaamua kuiuza. Watu huuza biashara zao kutokana na sababu mbalimbali.

4. Mahitaji ya watu eneo unakoishi au kufanya kazi.
Hebu jiulize maswali haya,
·       Ni kitu gani hapo unapoishi au kazini kwako kinachokupa usumbufu mkubwa kukipata aidha kwa kuwa mbali au bei kubwa?
·       Ni bidhaa zipi au huduma ambazo katika maeneo yako hazipo kabisa lakini watu wanazihitaji?
·       Ni vitu gani wewe na watu wengine waliokuzunguka mnavyolalamikia sana kwenye biashara za hapo mtaani/kazini?

7. Utalii ama kutembelea maeneo mbalimbali.
Unapotembelea sehemu nyingine ngeni kwako, ukiwa njiani kwenye gari au hata baada ya kuwasili sehemu husika utaona na kukutana na vitu vingi vigeni kwako ambavyo vinaweza vikawa ni fursa ya kibiashara katika sehemu ulikotoka. Kwa mfano umeenda kutembelea mbuga za wanyama za  Ngoro ngoro ukakuta kule nyama pori zikiuzwa bei rahisi sana. Unaweza baada ya kufuatilia taratibu za vibali vya serikali na ruksa ukaamua kuanzisha biashara ya kuuza nyama pori za swala, nyumbu na hata pundamilia maeneo kama ya Dar ambako vitoweo vitamu kama hivyo ni adimu sana.

8. Teknolojia inaweza ikakupa wazo la biashara.
Chunguza ni teknolojia ipi inayoenda na wakati uliopo kwa mfano sasa hivi kuna teknolojia ya huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu za mkononi kama Maxmalipo, tigo pesa, mpesa, airtelmoney, halopesa, ezy pesa na nyinginezo. Kutokana na teknolojia hizo unaweza ukaanzisha biashara nzuri tu kama wakala wa kampuni hizo kuuza miamala, muda wa maongezi, pamoja na bandle za intaneti.

9. Haiba, urembo na utanashati wako.
Haiba yako inaweza ikatumika kama wazo la biashara. Tumeshuhudia hata hapa Tanzania achilia mbali nchi za nje wasichana wengi wakitengeneza pesa kupitia tasnia ya urembo, basi tu kwasababu ni warembo, wanapata mikataba minono ya pesa nyingi kwenye matangazo ya biashara na hata katika mashindano ya urembo. Wanaume watanashati nao hupata pesa kupitia mashindano ya watunisha misuli pamoja na kuingia katika mikataba minono kama walivyokuwa wenzao wasichana.

10. Mahitaji katika makampuni makubwa na taasisi mbalimbali
Kuna makampuni na taasisi nyingi kama mashule, mahospitali, mahoteli, vyuo, viwanda, taasisi za dini, serikali nk. wote hawa wana mahitaji mbalimbali yanayosubiri kutimizwa kama vile kusambaziwa bidhaa au huduma mbalimbali.

11. Kununua haki ya kufanya biashara ya kampuni nyingine(FRANCHISE)
Njia hii mtu unanunua haki ya kutumia jina (BRAND) la kampuni au biashara ya mtu mwingine ambaye tayari anajulikana na wewe ukafanya biashara kwa masharti ya kutoa huduma au bidhaa zinazofanana na kwa ubora wa kiwango kilekile cha mmiliki wa hilo jina. Kuna mifano hata hapa ya biashara kama hizo kama vile makampuni ya soda za cocacola na pepsi, migahawa kama ya mackdonald iliyosambaa duniani kote nk.

12. Kuangalia na kusikiliza vyombo vya habari.
Magazeti, televisheni, redio, kusika kutoka mazungumzo ya watu ya mdomoni, majarida na siku hizi mtandao wa intaneti ni njia nzuri sana za mtu kuweza kupata wazo la biashara kwa kusikiliza au kuona ni fursa zipi zilizopo mahali fulani zinazohitaji kutimizwa.

13. Ugunduzi.
Kama unaweza kugundua ama kuvumbua kitu fulani nayo ni fursa nzuri ya kibiashara. Kuna watu waliokuwa na uwezo wa kugundua dawa za asili au hata dawa za kisasa, kugundua mitambo au mashine ya kurahisisha jambo fulani, kugundua mbinu mbalimbali zinazoweza kuleta unafuu wa maisha ya binadamu nk. ni moja kati ya njia za kupata mawazo bora ya biashara itakayokupatia pesa.

14. Kuiga mawazo ya biashara za watu wengine waliofanikiwa.
Hii japo unaweza kuiona siyo njia nzuri sana lakini ndiyo moja kati ya njia zinazotumiwa zaidi na watu wengi ijapokuwa baadhi yao huwa hawawezi kufanikiwa kwa kiwango kile waanzilishi wa mawazo hayo walivyofanikiwa.

…………………………………………………………………….

Ndugu msomaji wa blogu hii, kwa elimu ya kina zaidi kuhusiana na Ujasiriamali, kuanzisha biashara za aina mbalimbali, kuziendeleza, kuzisimamia na hata njia wanazotumia matajiri kutajirika, jipatie vitabu vyako kutoka Self Help Books Tanzania ltd.

Unaweza kununua kitabu kimoja kimoja lakini pia ukitaka kifurushi(bundle) la vitabu vyote vitatu(3pack) unapata.
Kifurushi cha vitabu halisi vya karatasi hardcopy ni Tsh. 35,000/=

Na kifurushi cha vitabupepe kwa njia ya e-mail softcopy ni Tsh. 18,000/=

Kwa bei ya kitabu kimoja kimoja bonyeza maandishi yafuatayo, PATA VITABU VYA UJASIRIAMALI PDF NA HARSCOPY HAPA



Usisahau pia lile DARASA LA SEMINA YA MICHANGANUO YA BIASHARA linaendelea. 

0 Response to "WAZO BORA LA BIASHARA INAYOLIPA SIYO LAZIMA LIWE JIPYA SANA "

Post a Comment