NJIA 3 ZA UHAKIKA NA ZILIZOTHIBITISHWA ZA KUWAPIKU WASHINDANI WAKO KIBIASHARA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

NJIA 3 ZA UHAKIKA NA ZILIZOTHIBITISHWA ZA KUWAPIKU WASHINDANI WAKO KIBIASHARA

Siyo rahisi uanzishe biashara mahali pakosekane biashara nyingine au hata biashara zinazouza bidhaa sawa na za kwako katika eneo hilo. Ingawa hauwezi  ukawazuia kuuza kile wakitakacho wao, lakini hapa kuna mbinu  ambazo ukizitumia, utakuwa kileleni juu zaidi kuliko wao. Ni mbinu 3 rahisi zilizothibitishwa za kuwapiku washindani wako kibiashara katika biashara yeyote ile unayoifanya.

1. Punguza gharama.
Katika jedwali lako la mapato na matumizi hakikisha unaorodhesha gharama zote unazotumia, jiulize ni gharama ipi kati ya hizo unayoweza ukaipunguza lakini angalia zipo gharama nyingine  ambazo hauwezi kamwe kuzipunguza kwani zitaleta athari mbaya zaidi katika biashara yako kwa ujumla.

Kwa mfano gharama kama mshahara wa mfanyakazi,  manunuzi ya bidhaa za kuuza ikiwa ni biashara inayohusisha bidhaa, na gharama za matangazo au masoko kwa ujumla wake siyo vitu vya kupunguza hata kidogo.

2 .Kuwa mbunifu
Biashara yeyote ile, inahiaji mtu kuwa mbunifu katika mambo mbalimbali katika kuwafikia wateja wako walengwa. Baada ya kufanya tathmini ya soko lako na kugundua siri yako ya ushindi, fahamu ni mbinu gani za kipee utakazozitumia kuwavutia wateja tofauti na wanavyofanya washindani wako. Unaweza hata ukabaini eneo ambalo utaweka biashara yako lisilokuwa na ushindani mkubwa mathalani maeneo kama miji mipya nk.


     3. Toa huduma kwa wateja zinazopita matarajio yao.
Kwa  kuwapa wateja wako huduma nzuri za kipekee na kuwajali utakuwa juu kushinda washindani wako  kwani watarudi tena na tena huku wakigeuka kuwa mabalozi wako wazuri kwa wateja wengine wapya. Wateja hupenda kununua mahali ambapo hujiskia vizuri, na kumuona mmiliki/muuzaji kuwa ni mtu anayejali maslahi na mahitaji yao kutoka moyoni.

..............................................................

Ndugu msomaji wa makala hii, ile semina yetu kwa mwaka huu ya biashara na mbinu mbalimbali za kuongeza mtiririko wa fedha katika biashara zetu, inaendelea katika group letu la Whatsapp, email na blogu ya private ya darasa la michanganuo. Leo sikutoa taarifa mapema shauri ya kukatika kwa umeme lakini somo lipo palepale saa 3 usiku na leo nitafundisha, mada isemayo, KATI YA VITU HIVI 3, USIMAMIZI, MASOKO, NA UZALISHAJI  NI KIPI MUHIMU ZAIDI KATIKA KULETA MAFANIKIO YA BIASHARA?

Chonde chonde mtu wangu usipange kukosa! pamoja na makala za nguvu kutoka kwa wadau wengine kwenye group kama vile wataalamu wa kuku kina FRANK MAPUNDA na wengineo.

UKITAKA VITABU PIA TEMBELEA, SMART BOOKS TANZANIA


0 Response to "NJIA 3 ZA UHAKIKA NA ZILIZOTHIBITISHWA ZA KUWAPIKU WASHINDANI WAKO KIBIASHARA"

Post a Comment