JE, ULIKOSA ILE SEMINA YETU YA KUANDIKA MCHANGANUO WA MRADI WA KUSAGA NA KUUZA UNGA WA DONA (USADO)? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, ULIKOSA ILE SEMINA YETU YA KUANDIKA MCHANGANUO WA MRADI WA KUSAGA NA KUUZA UNGA WA DONA (USADO)?

Kama hukuweza kuipata ile course kuhusiana na uandaaji wa mpango wa biashara ya usagishaji na uuzaji wa unga safi na salama wa dona (USADO), leo hii kuna habari njema nataka nikujulishe .

Semina hiyo ilikuwa imeandaliwa mahsusi kwa ajili tu ya wale waliojiunga na Magroup ya Whatsap & Telegramu ya MICHANGNUO-ONLINE, lakini sasa hivi tumeona ni vyema kuitoa bure kwa wasomaji na wafuasi wetu wote katika blogu ya JIFUNZEUJASIRIAMALI pamoja na mitandao yake ya kijamii.

Mafunzo hayo yataanza kutolewa hapa katika mtandao huu wa jifunzeujasiriamali BLOG kuanzia siku ya Jumamosi ya tarehe 18/4/2020 saa 4 asubuhi na saa 10 jioni kila siku kwa muda wa siku 7 na vipengele muhimu vitakavyofundishwa ni Utangulizi pamoja na Sura zote 9 za Mchanganuo huo wa biashara ya USADO Mlilling

Ifuatayo ni ratiba ya kila siku na masomo/vipengele vitakavyofundishwa;

SIKU YA KWANZA I, JUMAMOSI: 18/4/2020
1)  Utangulizi
2)  Maana hasa ya mpango wa biashara
3)  Mambo makubwa 3 ambayo kila mtu humu duniani anayeanzisha biashara huyafanya hata pasipo kujua kama anayafanya.
4)  Utafiti / upembuzi wa biashara ya USADO Milling
5)  Njia kuu 3 za kuandika mpango wa biashara yeyote ile
6)  Sura kuu zinazounda mpango wa biashara  

SIKU YA PILI 2, JUMAPILI:  19/4/2020
1)  Kuanza rasmi hatua kwa hatua kuandika Mchanganuo wa biashara ya USADO Milling
2)  Muhtasari.
3)  Maelezo ya Biashara

4)  Maelezo ya Bidhaa

SIKU YA TATU 3, JUMATATU: 20/4/2020
1)  Tathmini ya Soko

SIKU YA NNE 4, JUMANNE:   21/4/2020
2)  Mikakati na Utekelezaji

SIKU YA TANO 5, JUMATANO: 22/4/2020
3)  Mpango wa Uendeshaji
4)  Uongozi na Nguvukazi

SIKU YA SITA 6, ALHAMISI:     23/4/2020
1)  Mpango wa Fedha / Financials

SIKU YA SABA 7, IJUMAA:       24/4/2020
2)  Vielelezo / Viambatanisho muhimu

Na huo ndio utakaokuwa mwisho wa Semina yetu hii, Ukipenda kuifuatilia kwenye mtandao huu wa jifunzeujasiriamali basi ingia kwenye mtandao huu kuanzia tarehe 18/4/2020 kisha tazama post ya kwanza au ya pili utakutana na mfululizo huo kuanzia mwanzo mpaka semina itakapomalizika siku ya tarehe 24/4/2020

UNAKARIBISHWA SANA!

Peter Augustino Tarimo

Whatsapp/call: 0765553030
SMS/Call:  0712202244

ASANTE.

0 Response to "JE, ULIKOSA ILE SEMINA YETU YA KUANDIKA MCHANGANUO WA MRADI WA KUSAGA NA KUUZA UNGA WA DONA (USADO)?"

Post a Comment