AINA 4 ZA BIASHARA ZENYE KINGA YA MAJANGA VIKIWEMO VIRUSI VYA CORONA(COVID 19) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

AINA 4 ZA BIASHARA ZENYE KINGA YA MAJANGA VIKIWEMO VIRUSI VYA CORONA(COVID 19)

Katika hali zote ngumu zilizowahi kutokea Duniani tangu enzi na enzi kuna vitu ambayo binadamu hakuweza kamwe kuendelea kuishi bila kuvipata. Ukiachana na majanga yanayohusisha maambukizi ya maradhi mfano wa hili la Corona(Covid 19) na hata maradhi ‘makongwe’ ya miaka mingi iliyopita kama vile Tauni na Ukoma katika zama za Mitume kabla na baada ya Yesu Kristo, na mengine ya karne za hivi  karibuni tu kama vile Kifuakikuu, Malaria, Surua na Ukimwi, majanga mengine makubwa na yaliyoitikisa Dunia ni Vita, majanga ya asili kama mafuriko, matetemeko, vimbunga, njaa  na majanga ya midororo mikubwa ya kiuchumi kama ule wa miaka ya 1930(Great Depression) na mwishoni mwa miaka ya 2000

Majanga yote hayo iwe ni magonjwa na hata vita mwisho wake husababisha mdororo wa kiuchumi na mdororo wa kiuchumi kwa mujibu wa wataalamu upo wa aina mbili, (1)Recession – Huu ni mdororo wa kiuchumi usiokuwa mkubwa sana na unaochukua miezi kadhaa tu au pengine hata mwaka nk.(2) Depression – Mdororo huu ni mkubwa zaidi na huchukua hata muongo mzima ambapo madhara yake ni makubwa zaidi yanayoweza kuenea Dunia nzima.

Tukiacha Midororo mikubwa karne nyingi huko nyuma, katika historia ya Dunia ya hivi karibuni Mdororo mkubwa zaidi wa kiuchumi, Great Depression umewahi kutokea mara moja tu mwaka 1930 mpaka baada ya Vita kuu ya II ya Dunia, lakini midororo midogo midogo ya kiuchumi (recessions) imewahi kutokea mara nyingi tu ukiwemo ule wa mwaka 2017 mpaka 2019 ulioanzia huko Marekani na baadhi ya nchi nyingine Duniani.


Majanga yote hayo iwe ni magonjwa na hata vita mwisho wake husababisha mdororo wa kiuchumi na mdororo wa kiuchumi kwa mujibu wa wataalamu upo wa aina mbili, (1)Recession – Huu ni mdororo wa kiuchumi usiokuwa mkubwa sana na unaochukua miezi kadhaa tu au pengine hata mwaka nk.(2) Depression – Mdororo huu ni mkubwa zaidi na huchukua hata muongo mzima ambapo madhara yake ni makubwa zaidi yanayoweza kuenea Dunia nzima.

Tukiacha Midororo mikubwa karne nyingi huko nyuma, katika historia ya Dunia ya hivi karibuni Mdororo mkubwa zaidi wa kiuchumi, Great Depression umewahi kutokea mara moja tu mwaka 1930 mpaka baada ya Vita kuu ya II ya Dunia, lakini midororo midogo midogo ya kiuchumi (recessions) imewahi kutokea mara nyingi tu ukiwemo ule wa mwaka 2017 mpaka 2019 ulioanzia huko Marekani na baadhi ya nchi nyingine Duniani.

Kwa kifupi tu ni kwamba Mdororo wa Kiuchumi maana yake hasa ni ile hali ya kushuka kwa shughuli za kiuchumi za nchi au Dunia katika kipindi fulani ambapo hali hiyo husababisha vipato vya watu kuporomoka vibaya, ukosefu mkubwa wa ajira, kushuka kwa uzalishaji viwandani, biashara kufungwa, watu kushindwa kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma mbalimbali pamoja na kushuka kwa pato la ndani la Taifa (GDP)

Kama nilivyotangulia kusema pale mwanzoni kabisa katika mazingira magumu kama hayo niliyoyataja bado kuna biashara au shughuli za kiuchumi ambazo piga ua zitaendelea kustawi hata kama ungekuja mdororo mkubwa wa kiuchumi kiasi gani. Na sababu kubwa nitaitaja hapo baadae kidogo baada ya kuelezea kidogo kuhusiana na janga kuu linalotunyemelea sasa hivi la Covid 19 na ambalo hamna mwenye uhakika ikiwa Dunia itasalimika kuingia katika Mdororo mkuu(Great Depression) kama ule wa wakati wa Vita kuu ya 2 ya Dunia- World War II au utakuwa tu mdororo wa kawaida kama mingine mingi iliyowahi kutokea Duniani katika karne ya 20 na 21. Ila tu uhakika ni kwamba mdororo wa kiuchumi baada ya Corona ni lazima utokee uwe mkubwa au mdogo
Kirusi hatari cha covid 19

Kirusi hatari cha Covid 19 (corona)

Janga la Corona maarufu kama Covid 19 lililoanzia huko jijini Wuhan nchini Uchina limeyashitua Mataifa mengi yakiwemo yale Mataifa makubwa kama Marekani, Uingereza, Italy, Urusi, Ufaranza, Iran, Uhispania na Korea ya Kusini. Mataifa haya kwa kweli hayakufikiria hata kidogo ikiwa Corona ingeliweza kugeuka kuwa mwiba mkali hivi kwao, badala yake wakati corona ikianza huko China, wao walidhani labda ingeliweza kuwa hatari tu kwa zile nchi masikini zilizo na mifumo dhaifu ya kiafya kama nchi nyingi za Kiafrika au baadhi ya nchi masikini za Asia na Amerika ya Kusini. 

Virusi vya Covid 19 ni dada wa virusi wengine wawili maarufu wa Corona, SARS na MERS, wote wakisababisha maambukizi ya homa kali za mapafu. Virusi hawa wote ndugu vyanzo vyao ni mnyama mwenye mabawa kama ndege au kwa jina la kawaida POPO. Inasemekana na Wanasayansi kuwa Sars iliyoanzia pia nchini China virusi wake walihamia kwa binadamu kutoka kwa Popo kupitia aina fulani ya Paka wafugwao, wakati Virusi wa Mers wao walimuingia binadamu kutoka kwa popo kupitia Ngamia huko nchinni Jordan. Kwa upande wa Covid 19 inasemekana virusi hawa walimuingia binadamu wa kwanza huko Wuhan kupitia nyama zilizokuwa zikiuzwa katika soko moja na chanzo chake pia inasadikiwa kuwa ni haohao Popo.
popo
Popo
Si kama Wachina wanakula nyama na supu ya Popo kama watu wengi wanavyokazia hapana, bali inasemekana soko hili la nyama lilikuwa likiuza kiholela pia ndege na wanyama wengine hai kama vile kuku, bata, mbuzi nk. hivyo kuna uwezekano mkubwa kuwa popo waliweza kuwaambukiza ndege hao virusi na binadamu alipowachinja na kuwala basi naye akaambukizwa Covid 19.

Unaweza ukastaajabu pia kwamba Dunia miaka ya nyuma iiliwahi kushuhudia Magonjwa ya virusi yaliyoua watu wengi zaidi na pengine hata yaliyokuwa hatari zaidi kuliko haya ya Corona. Katika zama tunazoishi sasa mlipuko wa homa ya virusi uliotisha zaidi na kuangamiza roho za watu wengi kupita mwingine wowote ule hata huu wa Corona ni ule wa virusi vijulikanavyo kama H1N1 maarufu kama SPAIN INFUENZA. Spain Infuenza ulienea dunia nzima hapo mwaka 1918 wakati wa vita kuu ya I ya Dunia na kuua watu wapatao milioni  50 mpaka milioni 100 duniani kote.

Mlipuko  mwingine wa ugojwa unaosababishwa na virusi uitwao ASIAN FLU hapo mwaka 1957 uliangamiza watu milioni 2. Miaka 10 baadae ugojwa mwingine unaofanana na huo, HONG KONG FLU pia ukaua watu milioni moja. Mwaka 2009 yalizuka Mafua ya Nguruwe, SWINE FLU nao ni  wa virusi ukaua watu 575,400. Ugojwa wa ZIKA 2015 wenyewe hauna madhara makubwa sana kwa watu wazima lakini umeacha maelfu ya watoto waliozaliwa na mama wenye virusi hivyo wakiwa na ulemavu wa kudumu wa viungo hususani kichwa na ubongo.

SASA NI KIPI CHA KUFANYA?

TUSIPANIKI WALA KUPUUZIA! Janga la Corona litapita kama yalivyopita hayo majanga mengine yote yaliyotajwa hapo juu, lakini haliwezi kupita hivihivi tu, kila mtu ni lazima alipe gharama fulani katika kuhakikisha tunapunguza madhara yake. Kuna watakaolipa gharama kubwa zaidi mfano wale watakaolazimika kukatisha uhai wao kutokana na ugonjwa huu lakini pia wengi watalipa gharama japo kidogo kama tunavyosisitiziwa na mamlaka mbalimbali likiwemo Shirika la Afya Duniani WHO, Serikali zetu na viongozi wengine wa wizara ya Afya na hata wale wa Dini.

Gharama kubwa tunayopaswa sote kuilipa kwa mujibu wa Mamlaka hizo ni kuhakikisha mara kwa mara tunaosha mikono yetu kwa sabuni au vitakatishi(sanitizers), kuepuka kukaribiana na mtu yeyote zaidi ya wale tunaoishi nao ndani, kukwepa mikusanyiko yeyote ile na kumripoti mgeni yeyote unayehisi katoka nchi nyingine kinyemela bila kufuata taratibu zilizowekwa ili awekwe karantini mara moja.

Basi baada ya kuangazia Virusi vya ugojwa wa Corona kwa ujumla na maambukizi mengine ya virusi, sasa moja kwa moja hebu twende tukazione zile biashara ambazo huwa zina tabia ya kuvumilia hali yeyote ile ngumu ukiwamo hata ugonjwa huu wa Corona.

AINA KUU NNE (4) ZA BIASHARA ZILIZO NA UWEZO WA KUJIKINGA DHIDI YA HATARI ZA MAJANGA KAMA CORONA NA MENGINEYO
Kunapotokea janga kubwa kama la Corona, biashara nyingi huathirika kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi lakini kubwa zaidi ikiwa ni matatizo ya mzunguko mdogo wa pesa kwa biashara au kampuni zile zisizokuwa na kinga dhidi ya majanga. Mara nyingi biashara hizo hulazimika kupunguza matumizi kama vile idadi ya wafanyakazi, mishahara, ikiwa ni pamoja na kukopa ili ziendelee kuwepo. Kwa upande wa wateja wao nao pia hupunguza kwa kiasi kikubwa manunuzi ya vitu visivyokuwa na ulazima hali inayozidisha hali mbaya zaidi kwa kampuni/biashara hizo.

Kwa upande wa zile biashara zenye kinga dhidi ya majanga, zenyewe huendelea kuwa imara kutokana na mzunguko wake wa fedha kutokutetereka sana na hii haijalishi ikiwa uchumi umedorora sana ama la. Sisemi kwamba biashara hizo haziathiriwi kabisa hapana, bali ukizilinganisha na nyingine huwa zinakuwa na unafuu mkubwa zaidi. Aina ya biashara hizo ni hizi hapa chini;

(1) Biashara zote za mahitaji yale ya msingi.
Hizi ni zile biashara zote zinazohusisha bidhaa za msingi kabisa kwa uhai wa binadamu na ambazo kamwe haziwezi kuepukika kwa hali yeyote ile. Mfano wake ni biashara za vyakula na biashara ya madawa na vifaa tiba, vifaa vya usafi kama vile sabuni, vitakatishi(sanitizers), dawa za mswaki nk. Umuhimu wa chakula kwa binadamu hauna kifani, kuna hatua inaweza kufikia pande mbili mahasimu katika vita wakaamua kusitisha vita au hata kuamua kupatana kisa tu njaa au mlipuko wa janga kubwa mfano wa hili la Covid 19. Mfano mzuri tumeshuhudia kwenye Janga hili sasa hivi ambapo Mataifa mengi baada ya kufunga kila kitu maduka ya chakula na dawa hayajaguswa hata kidogo.

Tuchukulie mfano tu labda mtu unamiliki kiwanda chako cha unga wa dona au hata unga wa sembe katikati ya janga kama hili, tuseme hata ikiwa hauna mtaji wa kutosha kuendeshea kiwanda chako, serikali inaweza hata kuwa tayari kukukopesha fedha ilimradi tu uendelee kuzalisha unga wa kutosha kwa ajili ya wananchi waliojifungia majumbani mwao kujikinga na virusi.

(2) Biashara za utoaji huduma muhimu za msingi.
Kama ilivyo kwa bidhaa muhimu, kuna huduma pia ambazo katu haziwezi kuepukika katika hali yeyote ile ya kiuchumi. Huduma kama vile za afya: zahanati, hospitali na vituo vya afya ni lazima ziwepo. Kuna biashara nyingine kwa mfano utoaji wa huduma za kusafirisha abiria haziwezi kuathirika sana isipokuwa tu zitawekewa taratibu fulani fulani huku zikiendelea kufanya kazi.

Usafirishaji wa mizigo ndio kabisa hauguswi na hata tumeshuhudia nchi nyingi zikiruhusu mizigo kuingizwa licha ya mipaka kufungwa abiria wasiingie. Biashara nyingine zinazoshamiri kipindi kama hiki ni zile za utoaji huduma kama vile usafirishaji na uuzaji wa mafuta ya magari na mitambo(sheli), umeme na nishati za kupikia majumbani.


(3) Biashara ya kurepea vitu vilivyoharibika pamoja na uuzaji wa vipuri
Katika hali yeyote ile ngumu ya kiuchumi iwe imesababishwa na Ugonjwa, Mdororo wa kiuchumi au hata Majanga mengine ya asili, ni kawaida watu kutokupenda kabisa kununua vitu vipya. Badala yake utakuta kila mtu akitaka kukifanyia marekebisho kifaa au kitu chake cha zamani anachokimiliki ili kupunguza gharama za manunuzi ya vitu vipya. Wataripea vitu vya zamani mpaka mwisho vitakapokuwa havirekebiki tena, iwe ni gari, redio au hata sufuria. Hii huenda sambamba na biashara ya vipuri vile vinavyobadilishwa mara kwa mara na visivyokuwa na mbadala wake.

(4) Biashara za huduma zinazosaidia watu kujikwamua na janga lililosababisha mdororo wa kiuchumi.
Ikiwa utafanya biashara yeyote ile inayohusisha huduma au bidhaa zinazosaidia watu kuondokana na tatizo lililopelekea hali kuwa ngumu, biashara hiyo haitaathirika kutokana na sababu kwamba kila mtu atataka kupata hiyo huduma ili hatimaye aweze kujinasua. Tumeshuhudia biashara kwa mfano za vifaa vya kujikinga na Corona kama vitakatishi na barakoa(masks) wafanyabiashara wakipandisha bei kama fursa kwao ya kutengeneza kiasi kikubwa cha faida. Huduma za ushauri na uhasibu huendelea kufanya vizuri hata yanapotokea majanga kwa sababu makampuni mengi bado yanakuwa yakihitaji watu wa namna hiyo kwa ajili ya kufufua uchumi wa biashara zao uliozorota.

…………mwisho……………


*TANGAZO MUHIMU*
SEMINA YA MCHANGANUO WA BIASHARA BUNIFU YA KIWANDA CHA UNGA SAFI NA SALAMA WA DONA
(USADO MILLING)

Mpendwa msomaji na mjasiriamali unayependa kusoma Makala katika blogu yako hii ya jifunzeujasiriamali napenda kukujulisha kwamba zile huduma zetu zote zimerudi tena kama kawaida baada ya kipindi kama cha miezi 2 hivi. Kwa wale tuliokuwa pamoja  mwaka mzima wa 2019 mtakumbuka ahadi yangu ya Uzinduzi wa kiwanda changu mwenyewe kipya nilichoahidi kwamba utakuwa ni wa kihistoria, kwa takribani miezi 2 nilikuwa nikitengeneza documentary kwa ajili ya shughuli hiyo muhimu na kwa bahati mbaya kabla sijamalizia likazuka janga hili la Corona.

Kwa kuwa mikusanyiko imekatazwa shughuli hiyo imekuwa ngumu kidogo kumalizia kutokana na maeneo yenyewe niliyokuwa nikichukua baadhi ya video kuhusisha mkusanyiko wa watu. Hata hivyo naamini baada ya janga kwisha kazi itaendelea na Mungu akipenda basi Aprili mwishoni itakuwa ndiyo shughuli yenyewe rasmi.

Basi hapo tarehe 2 Aprili mpaka tarehe 4 katika magroup mawili ya MICHANGANUO-ONLINE tutakuwa na SEMINA juu ya jinsi ya kuandaa Mpango wa biashara(MCHANGANUO) wa Kiwanda kidogo cha Usagishaji unga safi na salama wa Dona(USADO MILLING) Semina itafanyika katika Group la whatsapp la zamani na jipya linaloanzishwa leo hii kwa jina MICHANGANUO-ONLINE-2. Hakuna tofauti kubwa baina ya magroup haya mawili isipokuwa tu muda mtu aliojiunga na OFFA zilizotolewa.

FAIDA ZA KUJIUNGA NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE-2  2020 NI HIZI ZIFUATAZO.

Kwanza nitangaze rasmi kwamba ile OFFA ya mwaka jana ya vitu zaidi ya 15 haipo tena mwaka huu, badala yake tumeleta offa nyingine mpya. Manufaa hayo ni pamoja na kushiriki semina zote kwa mwaka huu wa 2020 tukianza na ile ya Aprili ya Kiwanda cha Unga wa Dona(USADO MILLING), kuwa member wa group kwa mwaka wote wa 2020, kupata masomo(somo moja kila siku) linalohusiana na elimu ya fedha(Financia literacy), kutoa mchango wowote uutakao kwenye group, kuuliza chochote, fursa ya kutangaza bidhaa au huduma zako ilimradi tu huvunji sheria za nchi pamoja na Upendeleo maalumu(Special privilledge) wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda changu bunifu hapo Aprili mwishoni.

Manufaa hayo yanaambatana na OFFA ya vitu hivi 5 vifuatavyo utakavyotumiwa pindi tu umalizapo kulipia ada ya mwaka shilingi 10,000/= ;
1.   Kitabu cha MICHANGANUO-ONLINE katika lugha ya Kiswahili.

2.   Kitabu cha Michanganuo katika lugha ya kiingereza, kinachotumiwa na vyuo vikuu vingi Duniani-English

3.   Michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3 PACKS)-Swahili

4.   Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT BUSINESS PLAN)-English & swahili

5.   Mchanganuo wa Matikiti maji(KIBADA WATERMELON-BUSINESS PLAN)-Swahili.

Kiingilio/Ada katika Semina hii ni shilingi elfu 10 tu ambayo inalipwa kupitia namba zetu zifuatazo,

0765553030 au
0712202244 na

Jina ni Peter Augustino Tarimo

Baada ya malipo, tuma ujumbe wa watsap au SMS usemao, NIUNGANISHE GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE PAMOJA NA OFFA YA VITU 6

Mwisho wa kulipa kwa ajili ya semina ni tarehe 30/3/2020. Baada ya tarehe hii ukilipia utaweza kupata hizo offa na kuungwa katika group lakini semina ya USADO MILLS utakuwa umeikosa.

Asante na Karibu sana !
Peter Tarimo
Mhamasishaji na Mwanaviwanda mwenzako 2020
WHATSAPP: 0765553030


1 Response to "AINA 4 ZA BIASHARA ZENYE KINGA YA MAJANGA VIKIWEMO VIRUSI VYA CORONA(COVID 19)"