KUWA BILIONEA NAWEZA KUTUMIA NJIA ZIPI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUWA BILIONEA NAWEZA KUTUMIA NJIA ZIPI?

KUWA BILIONEA NIFANYEJE
Kwenye safu yetu ya maswali na majibu au Ongea na mshauri wako leo, tuna Swali kutoka kwa kijana mmoja aliyejitambulisha kwamba ndiyo kwanza ametoka kumaliza shule na hivyo angependa kufahamu hatua ambazo anaweza akazifuata ili kuwa bilionea haraka iwezekanvyo.(Safu hii hatutaji jina la muuliza swali labda kwa ridhaa yake mwenyewe)

Swali huyu kijana alilonitumia Whatsap lilikuwa kama hivi, bila kuongeza wala kupunguza nukta;

Kak, naomba msaada ako mimi ni mchanga katika biashara naomba unikochi vizuri nmetok shule si zamani sana bado sielew kitu.
Ata kwa mazungumzo mwanzo itakuwa vizur
Naitaj kuwa Billionaire

Wakati mwingine maswali wanayouliza vijana hasa wale walio katika umri wa kumaliza masomo yao ya vyuo au mashuleni yanaweza kukuchekesha au hata wakati mwingine ukafikiria pengine wanatania au ni “wendawazimu” lakini ikiwa na wewe uliwahi kupitia umri wa ujana na kukutana na changamoto hizi huwezi kamwe kuwabeza au kuona ni wendawazimu.

SOMA: Kuanzisha biashara nikiwa chuoni nasoma, naomba ushauri, nina wakati mgumu.

Vijana hasa wanaomaliza shule na vyuo mbalimbali hupendelea sana kujua siri ya kuwa tajiri ni nini, kanuni za kuwa tajiri na hata jinsi ya kupata pesa haraka. Kwa ujumla wanakuwa na hamu kubwa ya kupata mafanikio katika maisha yao. Huu ndio umri sahihi binadamu anaotamani kujua jinsi ya kufanikiwa biashara ama chochote kile atakachokifanya kwa haraka(kwa spidi ya umeme).

Kwa hiyo maswali kama haya ikiwa wewe ni mtu unayedili na maswala ya ushauri kwa vijana yategemee kwa asilimia kubwa sana na ni haki yao ya msingi kupatiwa majibu sahihi na wale tuliowatangulia ama yeyote mwenye uwezo wa kutoa majibu sahihi hata ikiwa mtoa majibu siyo Bilionea, kwani siyo jambo rahisi kila kijana aweze kumfuata Bilionea au tajiri na kumuomba amfundishe njia alizopitia mpaka akatajirika, ingawa pia ni vizuri zaidi kijana akamuuliza bilionea moja kwa moja kama itawezekana.

MAJIBU KWA SWALI LA KIJANA WETU NI HAYA HAPA
Nisingependa nirudie kuandika tena upya makala(post) za zamani, lakini kwakuwa swali hili linanitaka hivyo,basi nitaandika kwa ufupi kabisa dondoo muhimu tu zinazopatikana katika makala moja isemayo, UNAPENDA KUWA KAMA BAKHRESA, MENGI, DEWJ NA ROSTAM?, Makala hii ina maelezo ambayo yanatosha kabisa kujibu swali la kijana wetu huyu na dondoo hizo ni hizi hapa;
1.  Anza na Ndoto au Maono.


2.  Jijengee akilini mtazamo wa mafanikio.


3.  Ongeza ufahamu wako juu ya biashara unayoifanya.


4.  Buni wazo la biashara lenye uwezo wa kulipa haraka.


5.  Tafuta mtu wako wa mfano(Mentor)


6.  Anzisha biashara.


7.  Unda timu imara kwenye biashara yako.


8.  Tafuta mtaji wa kuendeshea biashara yako.


9.  Endesha biashara yako katika mfumo wa kampuni.


10.      Wekeza katika biashara(vitegauchumi) vingine.

Ukitaka uwe Bilionea ni lazima ufuate kanuni au njia hizo walizopitia mabilionea wengine wote duniani wakiwemo hata na wale wanaopatikana hapa Tanzania. Mabillionea wote duniani wana vitu fulani vinavyofanana ambavyo hujikuta wamevifanya iwe walikuwa wanajua au hata hawajui. Kwa undani zaidi unaweza ukasoma makala hiyo.

Na siyo hivyo tu peke yake, ili mtu kuwa tajiri(Bilionea) wa ‘kutupa’ ni lazima kwanza kabla ya yote uwe na SABABU(KWANINI) unataka kuwa Bilionea. Niliwahi kuandika pia katika makala nyingine isemayo, KWANINI KUFANIKIWA KIFEDHA SI DHAMBI NA KILA MTU ANASTAHILI AFANIKIWE? nikazitaja sababu kadhaa za watu kutaka kutajirika au kumiliki fedha nyingi ambazo kwa kifupi nilisema ni hizi hapa;

1.  Kuondokana na mnyororo wa umasikini uliotesa kizazi chao tangu mababu.

2.  Kugusa maisha ya watu wengine(Kusaidia)

3.  Kuwaridhisha wapenzi wao-mtu anaamua ‘kufight’ kufa na kupona atajirike kisa tu mridhishe mpenzi wake au kutaka kuoa katika familia fulani.

4.  Kuwa na uwezo wa kusikilizwa na karibu kila mtu hata serikali.

Kwa ujumla unahitaji NGUVU ITAKAYOKUSUKUMA KATIKA KUUTAFUTA HUO UBILIONEA. Njia za mtu kuwa bilionea au kutajirika siyo siri tena wala siyo lazima mtu umfuate Bill Gates, au Bilionea mwingine yeyote akakufundishe. Ugumu upo tu kwenye utekelezaji wake. Ukiweza kutekeleza kwa vitendo njia hizo, Ubilionea ni haki yako kama tu zilivyokuwa haki nyinginezo zile za binadamu na hakuna kiumbe chini ya jua atakayeweza kukuzuia kuupata.
.......................................................................

Kama bado hukuwa umesoma kitabu mashuhuri cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI pata nakala yako(softcopy) kwa shilingi elfu 10 tu. Au Hardcopy kwa shilingi elfu 22 Ukiwa Dar es salaam. Mikoani tunatuma kwa sh. elfu 30 katika basi. 

SIMU:       0712202244, 
WASAPP: 0765553030




0 Response to "KUWA BILIONEA NAWEZA KUTUMIA NJIA ZIPI?"

Post a Comment