FURSA ZA MAFANIKIO KAMWE HAZITAKAA ZIISHE LAKINI PIA HAZICHUMWI MTINI KAMA EMBE

JIWE LA DHAHABU-MFANO WA FURSA KWENYE MIGODI
Jinsi ya kuyafikia malengo fulani muhimu kabisa maishani, kila binadamu hapa Duniani huanza kuwaza kitu hiki mapema kabisa tangu akiwa mtoto mdogo pale akili inapoanza kupata ufahamu. Lakini kwa bahati mbaya sana siyo kila ndoto za mtu huja kutokea kuwa kweli kama alivyoota utotoni. Kwanini….?  Wengi watakujibu ni kwasababu hawakuweza kupata njia au namna ya kutimiza ndoto hizo, hawakuwa na fedha za mtaji, walikosa mbinu sahihi za kufanikiwa kibiashara, walikosa hiki, walikosa kile na blaa blaa chungu nzima! Ilimradi tu hazikosekani sababu.

Lakini ikiwa ingewezekana kurudisha muda nyuma na kuchunguza mazingira ya watu hawa kwa umakini, ungeweza kugundua kuwa sababu wanazozitoa hazina mashiko yeyote na fursa zilikuwepo tele ila tatizo tu ni kwamba hawakuweza kuziona. Kwanini hawakuweza kuziona…..?, tuendelee tutajua hapahapa…..

SOMA: Je upo kwenye kazi au fani uliyotamani kuwa tangu ulipokuwa mtoto mdogo?

Ujue, Duniani na Tanzanaia ikiwemo wapo watu wengi tu tunaowachukulia kama ni watu wenye “BAHATI” kwasababu wameweza kufanikisha kila lengo walilojiwekea maishani, wana biashara nzuri za ndoto zao zinazowaingizia mamilioni ya pesa, wana kazi nzuri zinazowapa mshahara mzuri, wanamiliki magari ya kifahari, wana majumba na vitu vizuri kibao. Lakini watu hao siri ya utajiri wao ni nini? na hii BAHATI iliwaangukia vipi?, Ni kwa njia ya kuweza kuziona fursa mapema na huo ndio ukawa mwanzo wa wao kufanikisha mipango iliyotimiza ndoto zao hizo, hakuna uchawi hapo wala sijui kitu gani.

Kuna watu hudhani eti kwamba ili mtu ahesabike kwamba ana bahati basi ni lazima awe ameshinda bahati na asibu au apate jiwe kubwa katika mgodi wa madini wanakochimba mamia ya watu. Lakini hebu nikuulize swali moja, zile shamrashamra unazozionaga pale wimbi la la michezo ya kubahatisha inapoibuka(Bingo nk.) huwa zinakoishia ni wapi? Si watu baada ya kucheza weee….na  kuchoka hushitukia hapo hamna bahati na kuamua kupotezea wenyewe huku wahusika wakija kuibuka tena upya na shamrashamra zingine baada ya watu kusahau?

SOMA: Maisha ya mafanikio? Soma vitabu hivi vya biashara na ujasiriamali kwa kiswahili.

Kwahiyo utakubaliana na mimi kwamba bahati za ukweli hupatikana tu katika vitu vile unavyoweza kuvitabiri ama kuvifikiria mwenyewe kwenye akili yako pasi na shaka kwamba unaweza kuvipata. Wajasiriamali, Mawakili, Madaktari, Wagunduzi, Wanamichezo, Wanamuziki, Waalimu, Waandishi, na wengine wote walio na fani mbalimbali, wote hao unaweza ukasema ni watu walioona fursa mbalimbali na kwa kutumia akili zao wanaweza wakazigeuza fursa hizo kuwa BAHATI kubwa kwao maishani.

SOMA:Ukweli uliofichwa juu ya pesa: Watu hawatafuti kazi bali hutafuta pesa.

Fursa ni nyingi mno unazoweza kuzitaja na kila binadamu ana nafasi sawa ya kuzipata isipokuwa tu huwa zenyewe hazijianiki barabarani wala kujitangaza bali huja zikiwa zimejificha ndani ya koti la matatizo na magumu mbalimbali ya kimaisha kusudi ili wale waoga wasiokuwa na subira wazikimbie na kusema, fursa duniani hamna tena siku hizi zimekwisha. Kwa wale wajanja waliokuwa na subira huu huwa ndio mwanzo wa kutoboa na kuwa mabilonea.
Ni kanuni ya asili iliyojijenga yenyewe kwamba, fursa hujitokeza pale ambapo haitegemewi kabisa kuibukia na usije ukategemea kamwe kwamba kuna siku moja mtu atakuja na kukuonyesha fursa ilipo, ila uwezekano wa fursa hauna mwisho na kila mtu anaweza kuziona endapo tu ataamua mwenyewe. Ili kulithibitisha hili nisemalo nakuomba ufanye jaribio lifuatalo;

Tafuta zawadi nzuri zipatazo 5 hivi tofautitofauti, kisha chagua yule mtu umpendaye, yeyote tu yule na si lazima awe ni mpenzi wako, halafu zifiche zawadi hizo ndani maeneo tofautitofauti akiwa hayupo. Sasa mwambie azitafute mpaka azipate ila usimwambie kama zipo ngapi wala ni zawadi za aina gani, wewe mwambie tu zipo zaidi ya moja. Atazitafuta na akifanikiwa kuzipata 2 au 3 tu utamuona amesitisha zoezi la kutafuta kwa sababu, kwanza hajui ni zawadi ngapi ulizoficha, wala zawadi hizo ni zipi. Lakini kama ungelikuwa umemtajia idadi na aina ya zawadi  zote bila shaka asingesita kuzisaka mpaka ahakikishe amezipata zote 5.

Hapo zamani za kale Binadamu aliishi katika Dunia isiyokuwa na mwanga wa umeme, magari, simu za mkononi, kompyuta, Intaneti, Tv wala redio. Lakini muda ulivyozidi kwenda Wabunifu na Wagunduzi mbalimbali waliweza kubuni vitu vyote hivyo na sasa kila mmoja wetu anavifurahia. Na bado katika karne zijazo kutakuwa na vitu vya kustaajabisha zaidi ya hivi tuonavyo leo. Haya yote ni maajabu ya jinsi fursa zilivyotapakaa na namna watu mbailmbali wanavyoziona na kuzitendea kazi.

SOMA: Njia mpya za kufanya mambo: Dunia, Biashara, Ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu

Leo hii unaweza kulalamika fursa hakuna lakini cha kustaajabisha ni kwamba mtoto ambaye hata hajazaliwa atakuja kuzaliwa na atakuwa bilionea miaka ijayo sisi tumeshakufa kitambo, sasa hizo fursa unafikiria atazitoa wapi ilihali leo hii sisi tunalalamika fursa hamna?

HITIMISHO.
Dunia imejaa fursa tele kwa watu wa rika zote, jinsia na makabila yote, kila mtu anaweza akatimiza malengo yake yote aliyojiwekea maishani. Kinachotakiwa tu ni mtu kujifunza jinsi ya kuitumia akili yake vizuri katika kupata mbinu za kufanikiwa kibiashara. Inaweza ikachukua muda mtu kujitayarisha kiakili lakini mwishowe inalipa. Katika maandalizi hayo iaminishe akili yako kabisa kwamba mafanikio ni kitu kinachowezekana na hiyo ndiyo siri kubwa ya mafanikio.

Jaribu kuwa mbunifu, kwenye kitabu changu kiitwacho, MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, chenye kila kitu mjasiriamali anachohitaji kufanya biashara ya kisasa, dhana ya UBUNIFU na UJASIRIAMALI nilizielezea kwa undani sana kwamba ndiyo injini kuu ya wafanyabiashara kuibua mambo mapya na bila ubunifu basi duniani hakuna maendeleo ya aina yeyote yale.

SOMA: Ujasiriamali: Ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria.

Mfano mdogo tu ni kwamba ikiwa wewe ni mfanyabisahara mdogo, unaweza ukashughulika kwanza na eneo dogo ambalo bado watu wengi hawajaanza kulifanyia kazi sana, simaanishi eneo tu kama sehemu ya nchi hapana, bali namaanisha eneo hata kisoko, aina fulani ya bidhaa, kwa kimombo wanaita a ‘niche’  fanya hayo huku ukiamini fursa zipo. Fursa zenyewe hazitakaa hata siku moja zisubiri mahali mtu aje na kuzichukua tu kirahisirahisi kama embe au machungwa mtini.

………………………………………

HII NI KWA YULE TU AMBAYE BADO HAJAJIUNGA NA GROUP YETU YA MASOMO YA FEDHA YA KILA SIKU(MICHANGANUO-ONLINE)

Ikiwa tayari umeshajiunga, tafadhali usipoteze muda wako kusoma kwani muda ni pesa.

Ni wajibu wangu kukukumbusha kila mara kwani najua inawezekana hujui mambo mengine mazuri yanayoendelea kila siku nyuma ya pazia mbali na makala hizi ninazoandika hapa.

Unapolipia ada ya kujiunga na Group unapata vitu vifuatavyo;

A. MAMBO MAPYA NA YANAYOKUJA HIVI PUNDE(new & Coming soon)
1.  Masomo ya fedha kila siku usiku saa 3 mpaka saa 4

2.  Kuna Kitabu kipya chenye masomo mazuri sana ya fedha kitatoka siku ya Jumanne tarehe 3 Septemba

3.  Semina ya mpango wa kuanzisha kiwanda kidogo cha usagishaji nafaka. Tofauti na michanganuo mingine yote tuliyowahi kufanya huu utakuwa na ubunifu wa kipekee mno! na mtu ataweza kuutumia ubunifu huo kuuza unga wa mahindi kama njugu.(A Unique marketing strategy)


B. OFFA YA ZAMANI (VITU 14) NA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA MCHACHE UJAO, BADO KIDOGO SANA TUTAIONDOA !
   
1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Semina na mchanganuo wa Biashara: Kiwanda cha tofali za saruji Kiluvya.

12.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

13.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

14.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Nirudie tena, vitu vyoote hivi unavipata kwa shilingi Elfu 10 tu! Unaweza ikiwa utawahi kabla offa hii maalumu haijafungwa. Thamani ya masomo na vitabu unavyoona hapo juu ni zaidi ya shilingi elfu 90 kwa bei ya kawaida. Nilitamani sana wewe msomaji wangu upate masomo haya yote kwani ni dhamira yangu kuu wewe kutumia vizuri kila fursa iliyokuwepo katika kufanikisha ndoto zako.

Namba za malipo ni, 0765553030 au 0712202244 jina, Peter Augustino Tarimo, na baada ya kulipia, nitumie ujumbe wasap au meseji ya kawaida kwa namba 0765553030 isemayo; “NIUNGANISHE  MASOMO YA KILA SIKU NA OFFA INAYOISHIA

Asante na Karibu sana…

Peter A. Tarimo

0 Response to "FURSA ZA MAFANIKIO KAMWE HAZITAKAA ZIISHE LAKINI PIA HAZICHUMWI MTINI KAMA EMBE"

Post a Comment