Kuna wanaodai kwamba hii ndio sababu kubwa
inayozifanya serikali zote duniani ikiwemo hata ile ya Marekani kutoruhusu
elimu ya kupata pesa ifundishwe mashuleni moja kwa moja. Watu tangia utotoni
huaminishwa tu kwamba kitu muhimu zaidi maishani ni kazi. Pengine inawezekana
sababu kubwa za kuficha ukweli huu ni hofu kuwa endapo watu wengi wataujua basi
dunia itageuka balaa tupu kwani watu watatumia njia zozote zile zikiwemo hata
njia haramu ilimradi tu wajipatie pesa, mimi sijui, hebu fuatilia somo hili
mpaka tamati.
SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka.
SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka.
Tukiacha ajira katika migahawa, hebu niambie unapofanya kazi
mahali au au biashara katika jengo fulani, ukifika muda wa chakula cha
mchana(lunch) unaweza ukamega kipande cha jengo, mashine au fenicha ukakitia
mdomoni na kukitafuna mithili ya chakula? Bila shaka haiwezekani, badala yake
utachukua pesa unazolipwa au faida ya biashara
na kwenda mgahawani kununulia chakula ili uweze kula. Hivyo hapo
hukwenda kutafuta kazi bali pesa.
Lakini mamilioni ya watu kote Duniani wamekuwa wakifanya kosa
hili kubwa la kufikiria kwamba wanatafuta kazi, kweli wengi huwa wanapata kazi
lakini hatimaye kazi hizo baadae hugeuka kuwa kitu kisichowasisimua kabisa huku
zikiwalipa mishahara midogo wasiyoweza kukidhi mahitaji yao yote ya kimaisha.
Kinyume chake ni kwamba unapoamua kutafuta pesa badala ya kazi, unapata vyote
viwili, pesa pamoja na kazi nzuri. Unajua ni kwanini?...
Idadi kubwa ya wafanyabiashara hujiingiza katika biashara pasipo
kuwa na malengo ya kutengeneza pesa. Makampuni nayo huajiri watu na kujiwekea
malengo ya mauzo bila ya kujishughulisha kulenga katika lengo kuu la kuingiza
pesa.
Ukitaka kuthibitisha ukweli kwamba watu wanachotafuta ni pesa na
wala siyo kazi, hebu fanya jaribio lifuatalo; Nenda katika kampuni yenye wafanyakazi
wengi kisha wajulishe kila mmoja kwa siri pasipo bosi wao kujua kwamba kuna
kampuni nyingine inayofanana na ile ya kwao inatafuta wafanyakazi kwa mshahara
mara 2 ya ule wanaolipwa pale.
Kama atabaki mfanyakazi hata mmoja kwenye hiyo kampuni basi ujue
kwamba labda huyo atakuwa alikuwa anamiliki hisa katika hiyo kampuni, kama siyo
hivyo basi kampuni ni mali ya baba yake na yeye huenda ndiye wa kuja kuirithi.
Kila mtu atatamani kwenda kulipwa mara 2 ya mshahara anaolipwa sasa na hilo
halina ubishi.
Sasa ni nini kifanyike?
Ingawa
si viongozi wa kiserikali wala jamii........inaendelea......
Ndugu msomaji wa somo hili, huu siyo mwisho wa hili somo, bado
litaendelea katika group la Whatsapp la Michanganuo-online leo februari 25
usiku saa 3. Masomo mengine mengi kama haya ni kila siku, pia unapojiunga na
group tunakupatia masomo na semina zote zilizopita tangu mwaka uliopita, ni
masomo mengi utakayochagua ni yapi yanakufaa zaidi.
Kujiunga kiingilio ni shilingi elfu 10 mwaka mzima na namba zetu
za malipo ni, 0712202244 au 0765553030 jina, Peter Augustino Tarimo. Baada ya
malipo tuma ujumbe wa wasap au wa kawaida ukisema, “NIUNGE NA GROUP LA MASOMO”
Muda huohuo nitakuunganisha na kukutumia kila kitu.
Ikiwa hutumii wasap usijali kwani vitu vyote pia tunatuma katika
email yako na updates zote muhimu tutakuwa tukikuforwadia kila siku, iwe ni
masomo mapya, michanganuo, vitabu au semina.
Vitabu vya ujasiriamali na biashara kwa kiswahili pia vinapatikana, Softcopy na Hardcopy kwa bei nzuri, kama unahitaji fungua ukurasa huu, SMART BOOKS TZ
0 Response to "UKWELI ULIOFICHWA JUU YA PESA: WATU HAWATAFUTI KAZI BALI HUTAFUTA PESA"
Post a Comment