SHAMBA DARASA: TOMATO-SUPER MASTER CLASS ELNINO & MASIKA SEHEMU YA 1-UTANGULIZI | Jifunzeujasiriamali

SHAMBA DARASA: TOMATO-SUPER MASTER CLASS ELNINO & MASIKA SEHEMU YA 1-UTANGULIZI

Shamba darasa la nyanya elnino na masika 2026/2027

1.0 Utangulizi

Mafunzo haya yamejikita katika mbinu bora za kuzalisha zao la nyanya na kupata mavuno endedelevu. Yanatoa maelezo ya kivitendo kuanzia maandalizi ya shamba na mbegu, usiaji wa mbegu, utunzaji wa miche, udhibiti wa wadudu na magonjwa, utiaji mbolea, uvunaji, uhifadhi, usindikaji, masoko ya nyanya, pamoja na utunzaji wa kumbukumbu za shamba

Ni matumaini yangu kwamba maelezo haya yatakuwa na msaada mkubwa kwa wakulima wa nyanya wakubwa kwa wadogo lakini pia kwa wadau wengine wote wa sekta hii nyeti wakiwemo walaji/wateja wa mwisho ambao kipaumbele chao kikubwa hasa ni usalama wa mbogamboga na matunda kwa afya zao (Wakulima tuna wajibu wa kulinda afya za wateja wetu)

Maelezo mafupi kuhusu sekta ya nyanya nchini Tanzania

Nyanya (Lycopersicon esculentum Mill) ni moja ya mboga mboga muhimu zaidi duniani. Ni sekta ndogo miongoni mwa sekta kubwa ya mbogamboga na inakua kwa kasi sana nchini Tanzania karibu asilimia 5% kwa mwaka na uzalishaji kitaifa wa tani 800,000. Ina uzalsihaji mkubwa lakini pia soko lenye uhitaji wa kila siku

Nyanya nchini Tanzania hulimwa zaidi maeneo ya mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Tanga, Morogoro, Pwani na Singida huku masoko makubwa yakiwa ni Dar es salaam, miji mingine mikubwa mbalimbali na nchi za jirani ikiwemo Kenya, Burundi na Rwanda

Changamoto kubwa zinazoikabili sekta hii ni pamoja na kuyumba na kuporomoka kwa bei msimu wa mavuno hasa msimu wakulima wengi wanapokuwa wamelima nyanya, bei hufika mpaka shilingi elfu 8 kwa tenga kutoka shilingi elfu 80 msimu wa uhaba wa nyanya (off season)

Changamoto nyingine ni kuharibika kwa nyanya kabla ya kufikishwa sokoni, uhaba wa viwanda vya usindikaji nyanya na gharama kubwa za pembejeo hasa dawa na mbolea

Fursa kubwa zilizopo ni uongezaji wa thamani, uwekezaji kwenye teknolojia za uhifadhi wa nyanya, uwekezaji kwenye teknolojia za kuongeza uzalishaji mfano Green house za gharama nafuu, umwagiliaji wa matone (Drip irrigation) na ufikiaji wa masoko ya kikanda mfano Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Comoro na Sudani ya Kusini

Chimbuko la Nyanya Duniani

Nyanya ipo katika kundi / familia ya mimea ya Solanaceae Familia hii pia inajumuisha mimea mingine kama vile viazi mbatata, tumbaku, pilipili na bilingani

Chimbuko la nyanya ni katika Milima ya Andes huko Amerika ya Kusini. Nyanya zilizolimwa huko zilipelekwa Ulaya na wavumbuzi wa Kihispania katika karne ya kumi na sita na baadaye kusambazwa kutoka Ulaya kwenda Kusini na Mashariki mwa Asia, Afrika, na Mashariki ya Kati. Hivi karibuni, zipo pia nyanya pori au wengine huziita nyanya za kienyeji maeneo mengi duniani

Nyanya zina wingi wa madini, vitamini, asidi za amino, sukari, na nyuzi nyuzi. Pia zina kiwango kikubwa cha Vitamini B na C, madini ya chuma na fosforasi. Matunda ya nyanya huliwa yakiwa mabichi kwenye kachumbari au yakipikwa kwenye chakula, mchuzi, supu nk. Zinaweza kusindikwa na kuwekwa kwenye chupa au makopo kama sosi nzito au unga wa nyanya

Nyanya pia zina kiasili cha lycopene kinachosaidia kuondoa sumu mwilini (anti-oxidant) na kulinda mwili dhidi ya vichocheo hatari vya saratani

Mmea wa nyanya ni zao la msimu mmoja ambalo linaweza kukua na kufikia urefu wa zaidi ya mita mbili. Hata hivyo, huko Amerika ya Kusini mimea hiyo hiyo inaweza kuvunwa kwa miaka kadhaa mfululizo kabla haijakauka.

Mavuno ya kwanza huanza kati ya siku 45-75 baada ya kuhamishwa kitalun au siku 90-120 baada ya kusia mbegu, umbo la tunda hutofautiana kulingana na aina ya mbegu

Aina kuu tatu za nyanya kulingana na ukuaji wake

●     Nyanya fupi/kichaka (Determinate type)

●     Nyanya za kati (Semi-Determinate type)

●     Nyanya ndefu zinazotambaa (Indeterminate type)

Nyanya ndefu na zile fupi (kichaka) ni aina mbili za nyanya zinazotofautiana kabisa

Nyanya ndefu (indeterminate) ndiyo chaguo bora zaidi kwa ajili ya msimu mrefu wa kuvuna kwani huendelea kurefuka hata baada ya kutoa maua. Tabia hii inaitwa indeterminate, hata hivyo katika mazingira ya joto mfano hapa kwetu Tanzania magonjwa na wadudu husitisha ukuaji huo

Nyanya fupi (determinate) kwa kawaida hujitegemea yenyewe na mara nyingi huwa haihitaji kuwekewa miti wala kamba. Hata hivyo, chini ya hali mbaya ya hewa kama vile mvua na upepo mkali kuweka miti /nguzo hakukwepeki

Aina hii huacha kurefuka baada tu ya kutoa maua, zinahitaji nguvu kazi kidogo hivyo ni maarufu sana kwa kilimo cha biashara. Zina tabia ya kutoa matunda mengi kwa pamoja yanayoiva ndani ya wiki mbili au tatu tu na matunda yake huiva haraka sana kuliko yale ya aina ndefu (indeterminate)

Nyanya za kati (Semideterminate), zenyewe sifa zake zipo katikati ya fupi na ndefu, hazirefuki sana wala kuwa fupi sana na uzaaji wake ni miezi 2 mpaka 4

Faida ya zao la Nyanya:

●     Ni moja ya mazao ya mbogamboga yanayochukua muda mfupi zaidi shambani

●     Lina msimu mfupi au mrefu wa uzalishaji (kulingana na aina ya mbegu).

●     Nyanya zinaweza  kulimwa eneo la wazi (open field) au kwenye greenhouse

●     Ni rahisi kufanya kilimo cha mzunguko na mazao mengine (crop rotation)

●     Zao la nyanya lina thamani kubwa ya kiuchumi (soko zuri)

●     Nyanya zina kiwango kikubwa cha virutubisho vidogo mwilini (micronutrients)

●     Matunda yake yanaweza kusindikwa, kukaushwa na kuwekwa kwenye makopo (kufungashwa)

Maelezo ya Kisayanzi juu ya mmea wa nyanya

●     Mizizi: Ina mfumo thabiti wa mzizi mkuu (tap root) unaokwenda chini kwa kina cha sentimita 50 au zaidi. Mzizi mkuu hutoa mizizi mingi ya pembeni na mizizi ya juu

●     Shina: Tabia ya ukuaji huanzia kusimama hadi kutambaa chini. Inakua hadi urefu wa mita 2-4. Shina ni gumu kiasi, lina vinyweleo na tezi

●     Majani: Yamejipanga kwa mzunguko yenye urefu wa sm 15-50 na upana wa sm 10-30. Vijani vidogo vina umbo la yai hadi mstatili ulioviringishwa vikiwa vimefunikwa na vinyweleo na vijani vidogo sana hujitokeza kati ya majani makubwa. Kikundi cha maua (inflorescence) huwa kwenye makundi na hutoa maua 6-12. Kikonyo cha jani kina urefu wa sm 3-6

●     Ua: Lina jinsia zote mbili (dume na jike kwenye ua moja) umbo la kawaida na kipenyo cha sm 1.5 - 2. Huota mkabala au kati ya majani. Kikombe cha ua (calyx tube) ni kifupi chenye vinyweleo na majani ya kikombe (sepals) hudumu

Kawaida lina petali 6 zenye urefu wa hadi sm 1, rangi ya njano na hujipinda kuelekea nyuma yanapokomaa. Lina dume (stamens) 6, na sehemu za poleni (anthers) zina rangi ya njano inayong'aa zikiwa zimezunguka sehemu ya kike (style) yenye ncha ndefu isiyo na uzazi. Ovari huwa juu na ina vyumba 2-9. Nyanya nyingi hujichavusha zenyewe (self-pollinated), lakini wakati mwingine huchavushwa na wadudu au upepo (cross-pollinated). Nyuki wakubwa ndio wachavushaji wakubwa zaidi

●     Tunda: Ni tunda lenye nyama (fleshy berry) lililo na umbo la duara au duara lililobonyea kidogo ncha zake na kipenyo cha sm 2-15. Tunda ambalo halijakomaa ni la kijani na lina vinyweleo. Matunda yaliyoiva huanzia rangi ya njano, machungwa hadi nyekundu. Kwa kawaida huwa ya duara, laini au yenye mifereji/mishororo (furrowed)

●     Mbegu: Ni nyingi, zenye umbo la figo au pea. Zina vinyweleo, rangi ya kahawia, urefu wa mm 3-5 na upana wa mm 2-4. Kiinitete (embryo) kimevingirika ndani ya tishu ya chakula (endosperm). Uzito wa wastani wa mbegu 1,000 ni gramu 2.5 – 3.5


.........................................................


Masomo haya ya kinadharia ya msingi (BASIC) katika blogu hii ya Jifunzeujasiriamali ni mbinu za kilimo cha nyanya kwa ujumla wake iwe unalima masika au kiangazi, eneo la wazi au kwenye green house, unalima mbegu ndefu au mbegu fupi

Katika Shamba darsa letu la nyanya TOMATO SUPER-MASTERCLASS ELNINO & MASIKA 26/27 tuna masomo mengine kwa undani zaidi na ya kivitendo kwa yule anayehitaji tu, tukizingatia zaidi kilimo cha nyanya msimu wa mvua nyingi ambao ndio soko la “DHAHABU” la nyanya lilipo

Masomo hayo yanazingatia mada kubwa 16 zifuatazo kwa kina;

                1)      Siri kuu ya kupata faida kubwa kwenye kilimo cha nyanya ndani ya kipindi kifupi cha miezi 3-5 (siyo mbolea, dawa wala mbegu)

                2)      Msimu na muda mzuri zaidi wa kulima nyanya ukutane na soko la “DHAHABU” la nyanya (tarehe kamili ya kusia mbegu)

                3)      Jinsi ya kukinga mbegu na miche yako dhidi ya magonjwa na wadudu kabla hata ya kuisia kitaluni (nitaonyesha kwa vitendo)

                4)      Mbinu na mikakati mahsusi ya kuzuia magonjwa na wadudu wakati wa mvua nyingi za El-nino & masika

                5)      Jinsi ya kuchagua aina ya dawa za ukungu, bacteria, na minyoo wa ardhini kwa usahihi mkubwa pasipo kusababisha usugu

                6)      Ratiba kamili ya dawa na mbolea (misimu yote 2 masika na kiangazi)

                7)      Jinsi ya kudhibiti magojwa hatari ya virusi wa nyanya kwa urahisi bila kutumia dawa yeyote

                8)      Aina bora zaidi ya mbegu za kulima msimu wa mvua nyingi za el-nino na masika

                9)      Njia rahisi zaidi ya kukinga magonjwa ya mnyauko kabla hayajashambulia nyanya zako shambani

              10)    Mdudu mdogo hatari zaidi wa nyanya kuliko hata Kantangaze na mbinu za kupambana naye, hufanya uharibifu mkubwa kwa mda mfupi na akishaingia ni vigumu mno kumdhibiti)

              11)    Mbali na Ukungu, Wadudu, Virusi na Minyoo wa ardhini, je unajua kitu kingine hatari zaidi kwa nyanya ambacho watu wengi hukidharau na mwishowe kinawaumiza vibaya?

              12)    Mbinu za kufanya nyanya zako kuwa ngumu na zidumu muda mrefu sokoni hata zaidi ya mwezi mmoja bila kuharibika (Wakenye huzitumia sana nsio maana nyanya zao Tanzania hugombaniwa kama njugu)

              13)    Mbinu na mikakati ya kuwalinda walaji na sumu za viuatilifu & kemikali za viwandani ili kundelea kulinda soko la nyanya (hii ni kwa wakulima kibiashara tu)

              14)    Kilimo cha nyanya miche 7(Family size)-hii siyo kibiashara ni kwa mtu mmoja mmoja tu nyumbani kwake anayejali zaidi ulaji wa mboga hai (Organic)

              15)    Mbinu za kiubunifu za kulima nyanya msimu wa masika kwa kutumia GREENHOUSE YA GHARAMA NAFUU, (Ni teknolojia mpyaTanzania bado haijafika ), ufanisi wake hautofautiani na greenhouse za gharama kubwa na material za kutengeneza hupatikana kirahisi maeneo tunamoishi

              16)    Hatua kwa hatua darasa la ujenzi wa greenhouse hiyo ya bei nafuu ukiwa wewe mwenyewe na fundi wako mmoja tu wa mtaani, huhitaji wataalamu waliobobea kutoka mbali

Darasa pia lina ubunifu wa aina tofautitofauti wa kibiashara hasa kwa vijana na wajasiriamali ambao bado mitaji yao ni midogo au wanajitafuta.

Kipekee zaidi ni kwa wajasiriamali waishio vijijini au nje kidogo ya miji na wanaofanya biashara zao au kilimo kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya mitandao ya kijamii hasa kutafuta masoko kupitia utengenezaji wa maudhui (Content creation). Nina habari njema sana kwao darasani!

Kujiunga na TOMATO SUPER MASTECLASS nitumie ujumbe usemao “Supermasterclass” kupitia whatsap: 0761002125

Baada ya kujiunga pia kuna OFFA ya michanganuo 9 ya kilimo cha nyanya nakutumia inbox muda huohuo kabla hata hujaingia darasani;

                 1.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya ndani ya Greenhouse ya gharama nafuu miche 600 (sqm 160)

                 2.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Heka 1miche 8,000 masika eneo la wazi

                 3.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Heka 1 miche 8,000 kiangazi eneo la wazi

                 4.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Miche 500 masika eneo la wazi

                 5.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Miche 500 kiangazi eneo la wazi

                 6.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Miche 50 Masika eneo la wazi

                 7.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Miche 50 Kiangazi eneo la wazi

                 8.       Mchanganuo wa kilimo cha nyanya Miche 7 (Familly size) ORGANIC)

                 9.       Mchanganuo kilimo cha nyanya Miche 7 (Familly size) mbolea za viwandani

Bei ya kawaida ya mchanganuo mmoja OFFA ikimalizika ni shilingi 10,000/= michanganuo yote 8 ya eneo la wazi, na elfu 30 ule wa Greenhouse ya bei nafuu

Gharama ya kujiunga na TOMATO SUPERMASTER CLASS 2026/27 ni shilingi 10,000/= tu kwa muda wote mpaka mavuno ya nyanya za shambadarasa yaishe (Msimu mzima wa masika na elnino 2026/27)

Aidha offa zote mwisho wake ni tarehe 30/11/2026

Wanachama wanaojiunga mwezi huu wote wa Novemba wanapata ufikiaji/ ‘access’ ya masomo yote kuanzia somo la kwanza na kuendelea pale wenzao walipoishia isipokuwa ufikiaji huo utakoma rasmi tarehe ya mwisho wa OFFA, 30/11/2026. Hii ni kutoa muda zaidi kwa wanachama waliowahi darasani kuendelea na elimu ya vitendo shambani (Practicals)



SOMA NA HIZI PIA;

                 1.       Mbinu za kufanikiwa kufikia malengo katika uwekezaji wowote utakaofanya

                 2.       Kwanini ulime nyanya msimu wa mvua za masika? zijue faida zake nyingi na changamoto kidogo

                 3.       Siri ya kupata mtaji wa biashara kirahisi kwa mjasiriamali mdogo asiye na dhamana mjini na kijijini

                 4.       Kama una biashara ndogo ya mtaji mdogo, hizi hapa njia 11 za kuibusti

                 5.       Biashara ndogo zilizosahaulika: bustani ndogo ya miwa jijini dar es salaam

                 6.       Namna bora zaidi ya kubuni wazo la biashara itakayolipa haraka bila msaada wa mtu mwingine

                 7.       Wazo la biashara ipi yenye hatari kidogo naweza kufanya kwa mtaji wa milioni 5?: mwajiriwa serikalini

                 8.       Changamkia fursa hii mpya ya mazao ya tikiti mahindi, maharage nyanya na mbogamboga

                 9.       Soko la sungura tanzania linakua kwa kasi kuliko uzalishaji wenyewe

               10.     Mawazo ya biashara zitakazovuma miaka ijayo 2018 na kuendelea mpaka 2030

      


0 Response to "SHAMBA DARASA: TOMATO-SUPER MASTER CLASS ELNINO & MASIKA SEHEMU YA 1-UTANGULIZI"

Post a Comment