Hakuna Jinsi Mjasiriamali mdogo masikini anavyoweza
kupata mtaji wa uhakika wa biashara ya ndoto yake zaidi ya kutumia Akili,
Ubunifu na Nguvu zake mwenyewe kwanza kwenye hatua za awali za biashara
Kuna dhana ya siku nyingi kwamba tatizo la wajasiriamali
wengi masikini siyo mtaji bali ni ukosefu wa mawazo bora ya biashara zinazolipa
jambo linalowafanya washindwe kupata mafanikio ya kiuchumi wanayotamani
Lakini hata pale wanapojitahidi kutafuta mawazo mazuri ya
biashara zinazolipa bado wanashindwa kutoboa kwa urahisi na wengi wanaendelea
tu kubakia kwenye mzunguko uleule wa umasikini miaka nenda miaka rudi
Ukweli ni kwamba mtaji wa kwanza kabisa katika biashara
yeyote ile duniani siyo pesa bali ni akili ya mtu kichwani mwake kwa kuona
matatizo na fursa mbalimbali kisha kufikiria mbinu na mikakati sahihi ya
kuyatatua kwa njia itakayomletea faida kiuchumi
Hata hivyo kufikiria kichwani tu peke yake hakutoshi bado,
kunamhitaji mjasiriamali kuchukua hatua ya kuwekeza nguvu, muda na rasilimali
nyingine alizokuwa nazo ili wazo lake liweze kumletea faida
Katika hatua hizo za mwanzo haiwezekani mtu kutajirika au
kupata mafanikio ya maana, zinahitajika bado juhudi nyingi, ubunifu, mbinu na
mikakati mbalimbali
Kitu wajasiriamali wengi wanacholalamika kuwa kimekuwa
kikwazo kikubwa kwao licha ya kuwa na mawazo mazuri mno ya biashara vichwani ni
MTAJI, na mtaji si ule wa kuanza tu bali ni mtaji wa kuendeleza au ‘kuboost’ biashara zao pindi zinapotaka
kutoka katika ile hatua ya unyonge ya awali
Unakuta mtu anaanzisha biashara vizuri tu yenye faida
lakini kabla hata haijaanza kuleta matunda inakufa shauri ya kukosa mzunguko chanya+ wa
kutosha wa fedha. Kinachoua biashara nyingi siyo ukosefu wa wateja bali
mzunguko mdogo wa fedha
Wachache wanaofanikiwa aidha wana bahati ya kupata mitaji
mahali pengine ya kuongezea au hutumia mbinu ya kujibana sana na kurudisha
faida wanayoipata kwenye mitaji yao
Mbinu hii ya kujibana na kurudisha faida kwenye mtaji
ingawa ni nzuri sana na ya uhakika lakini ina changamoto zake kubwa kwani
wajasiriamali wengi masikini hutegemea moja kwa moja vipato vyao vidogo katika
matumizi ya kawaida ya kujikimu kimaisha na hawana kabisa njia ya kulikwepa
hili
Na mbaya zaidi ni pale kunapojitokeza dharura za kimaisha
zisizoweza kuepukika kirahisi mfano magonjwa, vifo na majanga mengine
mbalimbali ya kimaisha na kukuta hakuna njia nyingine ya kuyatatua zaidi ya
kutumia fedha kidogo zilizokuwepo kwenye mzunguko wa biashara
Katika hali ngumu kama hizo ni vigumu sana kumwambia
mjasiriamali mdogo atenganishe fedha za biashara na zile za matumizi yake
binafsi – kanuni muhimu sana kwenye
biashara
Kumbuka faida anayoipata kwenye biashara bado ni kidogo
kutokana na mtaji pia nao kuwa ni mdogo mno halafu anahitaji kutumia mtaji
huohuo kutatulia shida za kila siku za maisha zinazomkabili
Suluhisho la tatizo hili ikiwa biashara ina uwezo wa
kutengeneza faida kubwa ingeliweza kuwa ni kukopa mahali licha ya hatari za
riba na kushindwa marejesho lakini bado kwa mjasiriamali mdogo masikini
anakabiliwa na kikwazo kingine kikubwa zaidi cha DHAMANA, masikini hakopesheki
kirahisi iwe ni katika taasisi rasmi za kifedha au kwa ndugu, jamaa na marafiki
Unaijua
siri ya Mikopo?
Wakopeshaji wakishagundua tayari umesimamisha biashara
yenye mifumo yote muhimu kwa kutumia nguvu zako mwenyewe hujileta wenyewe kwako
kirahisi wala huhitaji juhudi za kuwatafua
Sasa
ni nini hasa suluhisho la vikwazo vyoote hivi na kukataliwa kila kona kwa
mjasiriamali masikini asiye na dhamana za uhakika?
Jibu ni kutumia mbinu, mikakati na ubunifu kwenye
biashara hizohizo ndogo zizalishe faida kubwa kwa haraka zaidi kuliko vile
ambavyo mjasiriamali anatumia faida hiyo kwenye matumizi yake ya kujikimu
kimaisha (kujilipa gawio) maana ndio njia yake kuu ya kupata mahitaji ya kila siku
vinginevyo hataweza kuishi
Mahitaji ya msingi sana kwa binadamu ni chakula, malazi
na mavazi. Vitu hivi ni lazima avipate piga ua, iwe ni kwa kutumia fedha za
mshahara, ruzuku au faida ya biashara anayoifanya
Kumzuia asiyapate kabisa mahitaji hayo biashara au kazi
anayofanya haina maana yeyote kwake na ndiyo sababu wajasiriamali wengi
masikini hawawezi kamwe kukuelewa unapowaambia juu ya kuweka akiba wakati
hawana kipato cha kujikimu na mahitaji hayo ya kila siku – kanuni nyingine tena muhimu zaidi kwenye biashara
Kuna
njia kuu mbili (2) za kuifanya miradi / biashara ndogo zizalishe faida/mapato
makubwa haraka kuliko matumizi ya mjasiriamali ya msingi
1. Kuchagua
biashara / miradi ambayo moja kwa moja ina sifa za kutengeneza faida kubwa kwa
muda mfupi
2. Kutumia
mbinu na mikakati ya kiubunifu kuufanya mradi wowote ule wa kawaida kuwa ni
wenye faida kubwa na ya haraka
Kumbuka ninaposema FAIDA KUBWA NA YA HARAKA simaanishi miradi ile ya kitapeli (Pyramid schemes) hapana, namaaanisha miradi hii hii ya ukweli ya kawaida tunayoifanya kila siku
Na pia simaanishi kwamba miradi hii unaifanya leo ukilala
usiku mmoja tu kesho yake unaamka tajiri hapana, inahitaji muda kamili mfano
ikiwa kama mchicha unahitaji siku 21 ukomae ndipo uuze, unahitaji kweli kusubiria
siku hizo 21 na siyo blaa blaa za kudanganyana eti mchicha siku 10 tu unavuna!
hiyo hapana
Inawezekana mtu akachagua mbinu moja kati ya hizo mbili
nilizozitaja hapo juu au akachanganya mbinu zote 2 kwa mara moja kupata matokeo
makubwa na ya uhakika zaidi
Lakini bado mjasiriamali anaweza akajiuliza hivi;- “hizo
mbinu zipoje na zinatumika-tumika vipi ili kumpatia mtu faida kubwa haraka
kuliko matumizi yake ya kawaida?
Kulijibu swali hili sitatumia maneno ya nadharia bali
mifano hai ya biashara ambazo mimi binafsi nazifanya/nimezifanya na watu
wengine pia wanazifanya, na uzuri zaidi ni kwamba nimeanzisha madarasa halisi
ya mfano kama Mashamba darasa mtu yeyote anaweza kukopi na kupaste mbinu halisi
zinazotumika bila kufanya majaribio tena (Trial
& error)
Biashara/Miradi michache nitakayoitaja hapa inawakilisha
biashara na miradi mingine mingi mtu yeyote anaweza akaanzisha, kikubwa tu ni
ubunifu, mbinu na mikakati inayotumika kuifanikisha
Kwa
wajasiriamali wa Mijini na Majiji makubwa
Simaanishi biashara hizi mtu wa kijijini hawezi kuzifanya
hapana bali namaanisha hufanywa zaidi na watu waishio mijini kuliko vijijini.
Hii ni biashara ya REJAREJA aina yeyote ijapokuwa mimi nimetumia Duka la
rejareja maalumu kuwakilisha biashara nyingine zote za rejareja
Mjasiriamali yeyote yule mdogo wa mjini mara nyingi
kimbilio lake la kwanza ni biashara ya rejareja kutokana na asili/nature ya
mtaji wake mdogo, ni dadra sana kufikiria biashara ya jumla
Biashara ya Duka la Rejarja yenyewe kama biashara huwezi
ukasema ni biashara yenye ile sifa niliyoitaja pale juu ya kuzalisha faida
haraka ndani ya kipindi kifupi hapana, inategemea eneo na vigezo vingine vingi kama
mtaji nk, lakini mimi kwa kesi yangu hapa utaona nilitumia ubunifu, mbinu na
mikakati ya kipekee kuifanya biashara hii kutoa matokeo yale niliyokusudia
kuyapata yaani faida kubwa ndani ya kipindi kifupi kwa kadiri ilivyowezekana
Kwa kutumia mfano hai wakwangu mwenyewe nimeeleza na
kuonyesha jisi nilivyofanikiwa kuanzisha biashara ya duka la rejareja lenye
wasaidizi 2 nikiwa sina hata mia mfukoni ndani ya kipindi cha miezi 12 tu
Kariakoo. Mbinu, ubunifu na mikakati niliyoitumia mtu mwingine yeyote yule
anaweza akaikopi na kuitumia kama ilivyo mahali pengine popote pale hata kama
ikiwa siyo Kariakoo
Wajasiriamali wadogo waishio mijini na majiji makubwa
tayari nimemalizana nao kwenye kitabu changu chenye kurasa 334 kiitwacho “MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA-
NEW TECH EDITON”. Najua wengi wanafahamu kile cha kurasa 176 toleo la zamani ambacho kinakosa mambo
mengi mapya
Gharama ya kitabu hiki softcopy ni sh. 15,000/= lakini
kuna offa ya muda mfupi ya sh. 10,000/= Kukipata muda huu huu popote kwenye
simu au kompyuta yako kwa bei ya offa ya sh. elfu 10 malipo ni kupitia namba,
0761002125 jina Peter Augusino Tarimo, kisha nitakutumia kiungo cha kupakua
kitabu chako na coupon ya offa muda
huohuo
Lakini pia ukitaka kukinunua moja kwa moja mtandao wa
Selar kwa bei ya kawaida ya sh. elfu 15 bofya kiungo kifuatacho; SIRI YA MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA -NEWTECH EDITION 2026
Kwa
wajasiriamali wa Vijijini na Nje kidogo ya Miji & Majiji
Miradi hii simaanishi ni ya watu wa vijijini tu hapana,
bali ni miradi ambayo hufanywa zaidi na watu waishio vijijini kulingana na
asili/nature yake lakini hata waishio mijini na nje kidogo ya majiji makubwa pia
wanaweza wakaifanya kukuza mitaji ya biashara za ndoto zao
Nimefanya tafiti kwa ajili ya miradi mingi ya kilimo na
ufugaji ndani ya kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja (tangu Agosti mwaka jana
mpaka sasa) na tayari ninayo miradi/biashara 3 za mfano ambazo nipo tayari
kuzishea kwa yeyote anayehitaji kuiga/kukopi ubunifu, mbinu na mikakati
niliyoitumia kuzifanya biashara hizo ziweze kutengeneza mtaji haraka
Kuthibitisha ukweli na uhalali wa mbinu hizi yeyote
anayetaka kujifunza hatajifunza kwa nadharia zilizozoeleka bali kupitia darasa
maalumu la vitendo ambalo mimi mwenyewe kama mwezeshaji tayari ninayo miradi
yangu inayoendelea na mingine mipya itakayokwenda sambamba na ile ya wanafunzi
kusudi waweze kujifunza katika wakati halisi (real time)
Nikimaanisha kama shamba la mwalimu nyanya ina mwezi
mmoja halikadhalika na shamba la mwanafunzi nalo nyanya ina mwezi mmoja huohuo
kusudi aweze kuona ‘live’ mbinu,
mikakati na ubunifu unaofanyika na hatimaye faida inavyopatikana
Nimeamua kuanza na shamba-darasa la nyanya, mkakati wangu
ni kumfanya mjasiriamali mdogo asiyekuwa na mtaji kabisa au mwenye mtaji kidogo
sana aweze kufanya kilimo cha nyanya kipindi cha masika ijayo kuanzia mwezi wa
Desemba mwaka huu 2026 mpaka Mei mwakani kutengeneza Mtaji wa biashara ya ndoto
yake
Umekaa miaka mingi ukiwaza utapata vipi mtaji kwa ajili
ya biashara yako pengine ya kuagiza mzigo kutoka China, kufungua saluni, kufuga
kuku kisasa nk. lakini matumaini yanazidi kufifia na wala huoni taasisi / mtu
yeyote anayeonyesha dalili za kukukopesha mtaji?. Basi acha kulia suluhisho
limepatikana
Zao la nyanya huchukua miezi mitatu tu tangu kuhamishwa
kitaluni mpaka mavuno ya kwanza na soko lake ingawa hubadilikabadilika
kulingana na msimu lakini ni zao lenye uhakika mkubwa wa soko kwani hakuna
binadamu asiyetumia tunda hili kwenye chakula
Kwa kutumia ubunifu, mbinu na mikakati sahihi hasa “timing” ya soko na msimu mkulima anaweza
akajitengenezea kiasi kikubwa sana cha fedha ambazo hawezi kuamini kama anaweza
kuzipata ndani ya kipindi kifupi hivyo kisichozidi miezi 5
Tayari ninayo mashamba ya nyanya za majaribio niliyokuwa
nikifanya na pia kuna mengine naanzisha hivi karibuni kwa ajii ya madarasa,
sitaki kujaza nadharia hapa tukutane shambani ikiwa upo tayari kuanza
Kwenye ‘propject’
hii sitaki kabisa mtu anifuatilie kinadharia akisoma post zangu bila vitendo na
nimeshasema miradi yangu hii niliyofanyia tafiti zaidi ya mwaka 1 sasa
nikitumia gharama kubwa nisingependa iishie hivihivi tu kinadharia, napenda
iwanufaishe wajasiriamali masikini nione wakiinuka na kutengeneza biashara za
mamilioni waache kusemwa kuwa ni wavivu kisa tu wamekosa mitaji
Hivyo basi ikiwa huna kabisa mtaji au una mtaji kidogo
sana ili kwenda sambamba na mimi kwa vitendo kwenye hii project nakuomba ufanye
jambo lifuatalo mara baada tu ya kumaliza kusoma hapa;-
Nenda sokoni au gengeni kwa muuzaji wa nyanya muombe
MASALO kidogo au nunua hata nyanya za buku ukiweza zilete nyumbani unakoishi,
si huna kabisa mtaji wa kununua hata mbegu ya nyanya dukani ya shilingi elfu 5?
Sasa hapa ndio utanielewa kwa wewe unayesema huna hata mia ya mtaji wa kuanzia
Kisha kwenye madarasa yangu yatakayofuata huko mbele
nitakueleza cha kufanya na hayo masalo au nyanya za buku ulizonunua gengeni
Ninachohitaji hapa ni kukupatia “crash program”-mafunzo maalunu ya haraka maana msimu wa masika
tayari unakaribia. Miezi hii kuanzia huu wa Agosti mpaka Desemba nataka tufanye
shamba darasa la nyanya live litakalokupa tu uzoefu wa kilimo cha nyanya huku
nikikupa na mbinu za kulima nyanya msimu wa masika wenye soko la ‘dhahabu’ kwa
zao la nyanya
Hakuna biashara yeyote ile ulimwengu wa leo inayowezekana
pasipo kuwekeza mtaji hata kidogo wa nguvu, maarifa na fedha. Miradi hii tangu
mwanzo nimetangulia kusema si kwamba hutawekeza chochote hapana, Bali uwekezaji
wake ni mdogo lakini mapato ni makubwa sana ukiweza kutumia ubunifu, mbinu na
mikakati sahihi iliyofanyiwa majaribio na kuthibitika kufanya kazi
Kwahiyo chochote kile ufanyacho sasa hivi kama shughuli
ya kiuchumi inayokuingizia pesa hata ikiwa unapata ruzuku/msaada mahali fulani,
rai yangu kwako ni hii- mega hapo kiasi kidogokidogo jiwekee akiba kwa ajili ya
mradi wetu huu wa kihistoria wa kimkakati kuanzia Desemaba wa kutengeneza mtaji
wa biashara ya ndoto yako, usiniambie eti huingizi chochote, kwani unaishije?
Hata kama wewe ni ombaomba mjini bado kuna kipato cha
namna fulani unaingiza na hichohicho ndio ukimege kwa ajili ya maandalizi ya
pembejeo za kulima nyanya za msimu wa masika, asikudanganye mtu hakuna mradi
usiokuwa na mtaji hata kidogo, nitakuwa nikikupa mbinu na mikakati ya
kulifanikisha hili hapa kila siku nifuatilie
Haijalishi upo kijijini au mjini, midhali una ndoto ya
kutengeneza mtaji wako mwenyewe wa uhakika inawezekana tu. Kwani hapo mjini
ulipo pana umbali gani na maeneo ya nje ya mji unayoweza kufanya kilimo cha
nyanya?
Nafahamu majiji yote kuanzia Dar, Arudha, Mwanza na hata
Mbeya ukitoka nje kidogo tu ya miji hii kuna maeneo kibao unaweza kukodi shamba
au hata kuomba kwa muda ufanye kilimo cha bustani, Panga kuondoka kwa muda hapo
unapofanya biashara yako ndogo bila mtaji wa uhakika lakini ukijua kabisa
utarudi baada ya miezi michache ukiwa na mtaji wa maana wa kukusongesha mbele
haraka zaidi
Ikishindikana basi kwanini usirudi hata kijijini kwako kabisa
ulikozaliwa ambapo mashamba ni ya bure kabisa wala hulipi chochote?
Kuendelea kujifariji eti itatokea siku moja upate mtaji
wa maana kimiujiza hapo mjini hiyo ni ndoto ya mchana labda tu ikiwa utatumia
mbinu na ubunifu niliotumia Kariakoo,
ni lazima ukubali kufanya maamuzi magumu leo kwa faida na maslahi ya kizazi
chako baadae. Kata huu mnyororo wa umasikini wajukuu zako na vitukuu
wasijeteseka kama wewe
Kampeni hii ndio inaanza, kadiri siku zitakavyosonga
mbele tutaendelea kujuzana mengine mengi zaidi hapahapa bure bila malipo yeyote
lakini ikiwa upo ‘serious’ zaidi
unaweza ukajiunga na Shambadarasa langu live
kwa uwekezaji wa shilingi elfu 10 kwa msimu wote mpaka mavuno ya nyanya.
Kulipia uungwe kwenye kundi muda huu huu namba yangu ni 0761002125 jina Peter
Augustino Tarimo
Zipo huduma nyinginezo pia kwa anayehitaji kama vile
Michanganuo ya kilimo cha nyanya za masika, kilimo cha nyanya msimu wa kawaida
na Muongozo wa Ujenzi wa Greenhouse ya gharama nafuu kwa ajili ya kilimo cha
nyanya nyakati za masika na mchanganuo wake
Kwa wajasiriamali waishio mijini au maeneo yenye ufinyu
wa ardhi ya kulima hata bustani ndogo tu ya majaribio kuna mbinu maalumu
nitawapatia wakati huu wa shamba darasa la majaribio, kipindi kabla ya mvua za
masika wakijitayarisha kuhama kwa muda kutoka maeneo yao ya faraja (partial migration from their places of
comfort zone) waliyoyazoea
Kumbuka nimetangulia kusema kwamba mjasiriamali hulazimiki
kuachana moja kwa moja na biashara yako uhamie jumla kwenye kilimo cha nyanya
hapana, bali mradi huu ni wa kimkakati unapaswa kuufanya ukupatie mtaji wa
maana kwa ajili ya hiyohiyo biashara yako inayokutesa hapo mjini miaka na miaka
pasipo kukua kisa mtaji mdogo
Niamini wewe huna mkosi wala si kweli kwamba hujui biashara
bali tatizo lako kubwa ni mtaji finyu, haiwezekani mtaji huohuo ndio uutumie
kupanua biashara yako wakati huohuo ukiutumia kwa ajili ya mahitaji yako ya
kila siku na mbaya zaidi kama una familia inakutegemea huku ukiwa huna sifa
yeyote ile ya kukopesheka, mwishowe ni lazima tu utakufa masikini wala huna
haja ya kwenda kwa nabii au mganga kupiga ramli ya kumtafuta mchawi
Mbali na mradi huu wa nyanya za masika, ninayo miradi
mingine 3 ya kimkakati mmoja wa kilimo na miwili ya ufugaji ambayo yote
nimeshakamilisha utafiti wake wa kina nasubiri tu kuitambulisha kwa wahitaji.
Yote ni miradi bunifu iliyo na sifa ama uwezo wa kuzalisha faida kubwa haraka
ukitumia mbinu na mikakati sahihi
Hayo ndiyo majibu ya Safari yangu ya mwaka 1+ kijijini
kwa wasomaji wa blogu yangu ya Jifunzeujasiriamali mliokuwa mkiniuliza kila
mara ikiwa nimeacha kuandika ama la

0 Response to "SIRI YA KUPATA MTAJI WA BIASHARA KIRAHISI KWA MJASIRIAMALI MDOGO ASIYE NA DHAMANA MJINI NA KIJIJINI"
Post a Comment