KWANINI ULIME NYANYA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA? ZIJUE FAIDA ZAKE NYINGI NA CHANGAMOTO KIDOGO | Jifunzeujasiriamali

KWANINI ULIME NYANYA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA? ZIJUE FAIDA ZAKE NYINGI NA CHANGAMOTO KIDOGO

Nyanya za msimu wa masika

Unaweza kushangaa ni kwanini nimetaja changamoto za nyanya kidogo msimu wa masika wakati inafahamika wazi kwamba kipindi hicho kilimo cha nyanya ndiyo wakulima wengi huacha kulima kutokana na changamoto lukuki za magonjwa hasa yale ya ukungu na bacteria pia kudondoka kwa maua na kupasuka kwa matunda ya nyanya kunakosababisha hasara kubwa

Lakini pamoja na changamoto hizo za kilimo cha nyanya msimu wa masika au mvua nyingi kama hizi za El-nino bado kulima nyanya na kupata mavuno mazuri ni jambo linalowezekana na ndiyo maana utakuta kipindi hicho sokoni nyanya zipo lakini bei yake ni ya juu sana nyanya moja rejareja hufika mpaka sh. 300. Hebu jiulize kwani hao wanaovuna nyanya kipindi cha masika na mvua nyingi nyanya zao hulima Sayari nyingine?

Ikiwa jibu ni hapana wanalima hapahapa sayari yetu ya Dunia, basi jiulize tena swali la pili, kwani wao hutumia mbinu gani wakulima wengine wengi wanashindwa kuzitumia na kubwaga “manyanga”?

Kwanini sasa mimi niseme hizo changamoto ni kidogo kuliko faida zake?

Katika biashara yeyote ile duniani mjasiriamali anachopaswa kuangalia kwanza kabla ya vitu vyote ni SOKO. Ikiwa soko lipo la uhakika kwa bidhaa ama huduma fulani ni juu yako wewe mjasiriamali kuhakikisha unatumia kila njia inayowezekana kulisambazia bidhaa/huduma hiyo, wala haijalishi ni changamoto kiasi gani utakazokumbana nazo

Kitu kikubwa kinachohitajika hapa ni UBNIFU wa kukabiliana na changamoto hizo na siyo kuogopa na kurudi nyuma. Ikiwa kuna wateja wa kutosha na faida nono mimi hapo sioni changamoto bali naiona fursa kubwa ya kuingiza fedha nyingi kwani kila ugunduzi wa jambo duniani ulianza kwanza baada ya watu wachache kuona changamoto zilizokuwa zikiwatesa binadamu kwenye maisha yao ya kila siku ndipo wakaamua kubuni suluhisho la tatizo huku wengine wengi wakiona tatizo lile kamwe isingeliwezekana kulitatua

Hebu fikiria Mtu akiyefariki mwaka 1995 leo hii ingeliwezekana akafufuka ukamwambia unachati ‘live’ whatsapp na mtu alieko Songea wewe ukiwa Kagera tena muda huohuo unamtumia na pesa kwa simu hawezi kukuelewa kabisa kwani kipindi hicho alihitaji wiki nzima kutuma barua na Money Order iliyochukua pia wiki nzima kumfikia, hata hivyo watu wachache waliliona lile tatizo ndio maana leo hii tuna ‘enjoy’ teknolojia hizi mpya za mawasiliano, kompyuta na intaneti

Vivyo hivyo na ugumu wa kulima nyanya za masika nao ni changamoto kwa watu wengi lakini watu wachache wabunifu haziwezi kuwazuia kulima nyanya       

Sasa nisikupotezee muda wako mwingi twende tukazione hizo pande mbili za sarafu, faida na changamoto za nyanya kipindi cha mvua nyingi za masika au hata elnino ukipenda kwani mwaka huu pia mamlaka za hali ya hewa duniani zimetabiri uwepo wa mvua kubwa za El nino (2026–2027)

FAIDA ZA KILIMO CHA NYANYA WAKATI WA MVUA NYINGI (MASIKA/El-nino)

                 1.      Bei Kubwa na Faida Nono Sokoni (Super Profits): Huu ndio mkosi na baraka ya msimu huu. Wakulima wengi wanaogopa kulima masika kwa sababu ya magonjwa, hivyo nyanya inakuwa adimu sana sokoni. Ukifanikiwa kuvuna nyanya zako vizuri, utauza kwa bei ya juu mara mbili au tatu ya bei ya kawaida ya kiangazi

                 2.      Soko la Uhakika na Haraka: Hauhitaji kutafuta wateja; wao ndio watakaokusaka hadi shambani kwako. Nyanya inagombaniwa kwa sababu ugavi/supply unakuwa mdogo wakati mahitaji/demand yanakuwa vilevile au kuongezeka

                 3.      Kupungua kwa Gharama za Umwagiliaji (Zero Irrigation Cost): Hutatumia gharama yeyote ya mafuta ya pampu, umeme, au nguvu kazi kwa ajili ya kumwagilia shamba. Mvua inafanya kazi hiyo bure, jambo linalookoa muda na pesa nyingi za uendeshaji. Ule muda, nguvu na rasilimali za kumwagilia shamba wewe unazielekeza kwenye huduma nyingine kwa ajili ya nyanya zako

                 4.      Kutoweka kwa Wadudu Wanaopenda Ukame: Wadudu hatari kama Utitiri Mwekundu (Red Spider Mites), Nzi weupe(White flies), Vidukari / Wadudu mafuta (Aphids) na Chawa wa Mimea (Thrips) ambao husumbua sana kiangazi na kukausha nyanya, wanapotea kabisa msimu wa mvua kubwa na masika kwa sababu hawapendi unyevu na wanaoshwa na mvua hiyo

                 5.      Ukuaji wa Haraka wa Mimea: Udongo ukiwa na unyevu wa kutosha na kukiwa na joto la wastani, nyanya hukua kwa kasi kubwa, kutoa matawi mengi (vegetative), na kuwa na majani yenye afya na rangi ya kijani iliyokolea haraka kuliko kiangazi

CHANGAMOTO ZA KILIMO CHA NYANYA WAKATI WA MVUA NYINGI

Gharama kubwa za kemikali (Dawa za kuzuia ukungu): Utalazimika kununua dawa nyingi za ukungu za kimfumo (Systemic Fungicides) kama Ridomil, Master kutu au Amistar, ambazo ni za bei ghali. Pia unalazimika kupiga dawa mara kwa mara jambo linaloongeza gharama ya uzalishaji

                 1.   Mlipuko wa Magonjwa Hatari ya Fangasi na Bakteria mfano:

                                              ·       Bakajani Tangulia (Early Blight):Unasababishwa na fangasi Alternaria solani. Huweka madoa ya mviringo kwenye majani ya chini na mashina. Majani hugeuka manjano na kudondoka

                                              ·       Baka Jani Chelewa (Late Blight): Ugonjwa huu pia unaosababishwa na fangasi unaweza kuangamiza shamba zima ndani ya muda mfupi tu kukiwa na baridi na mvua

                                              ·       Mnyauko wa Bakteria (Bacterial Wilt): Bakteria walio kwenye udongo hushambulia mizizi na kukausha mmea ukiwa kijani na hauna tiba

                 2.      Kupukutika kwa Maua (Flower Drop): Vishindo vya matone ya mvua yanapiga na kukatisha maua machanga. Pia unyevu unagandisha chavua, na kuzuia uchavushaji, hivyo mmea unatoa maua lakini hayatoi matunda

                 3.      Matunda Kupasuka (Fruit Cracking): Nyanya inapofyonza maji mengi ghafla kutoka kwenye udongo uliolowa, nyama ya ndani inatanuka kwa kasi kuliko ngozi ya nje, na kusababisha nyanya kupasuka zikiwa mbichi na kuanza kuoza

                 4.      Kuoza kwa Mizizi na Kukwama kwa Lishe (Waterlogging): Udongo ukijaa maji mfululizo unakosa hewa. Mizizi inalegea (suffocate), inaoza, na mmea unashindwa kufyonza mbolea uliyoweka chini, hivyo unaanza kugeuka njano na kudumaa

                 5.      Uharibifu wa Miundombinu na Mazao: Mvua kubwa za masika au El-nino zinaweza kusababisha mafuriko yanayosomba miche au mmomonoko wa udongo unaosafisha mbolea na virutubisho vyote vya juu vya udongo

HITIMISHO:

Kilimo cha masika na el-nino ni "High Risk, High Return" (Hatari ni kubwa, lakini Faida ni kubwa mno). Wakulima wanaofeli ni wale waoga ama wanaolima kienyeji bila ya kutumia ubunifu wowote wala teknolojia zinazoweza kupunguza au kuondoa kabisa changamoto zilizopo

Kama mjasiriamali mbunifu una nafasi kubwa sana ya kuwa mmoja wa washindi watakaomiliki soko msimu huu ujao wa masika na el-nino !

Nimeandaa darasa la vitendo kwa ajili ya nyanya za msimu wa mvua kubwa hususani mwaka huu 2026-2027 wenye mvua za El nino kwani tunatarajia vuli kuwa ndefu kidogo kwani itaungana na masika, badala ya kuona majanga sisi tunaona fursa kubwa! Ni wakati wa wasio na mitaji na wenye mitaji kidogo kuongeza mitaji yao kirahisi kupitia kilimo cha nyanya. Kama mtaji wako ni kidogo mno hama mjini kwa muda, hamia kijijini au pembezoni kidogo mwa mji na mtaji wako huo kidogo, ukipata mtaji wa uhakika utarudi mjini upya

Mkakati wangu siyo wa kawaida hivyo darasa langu hili halitafanana kabisa na darasa jingine lolote lile ulilowahi kuliona. Natambua madarasa ya nyanya yapo mengi mitandaoni, kwenye magroup ya watsap, facebook, telegram, Google meet, community mbalimbali nk. lakini hili tofauti yake kubwa ni VITENDO

Mbegu za nyanya za kukamua kienyeji

Sitafundisha mwanafunzi asiye na bustani au shamba la nyanya, hata miche kuanzia 5 -15 tu inatosha kwa ajili ya shamba darasa hili ndio maana hapo mezani pichani umeona nimeweka hili bakuli la nyanya, nitakueleza nini cha kufanya ukitoka hapa ila tu ni kama unahitaji darasa lakini, ikiwa huhitaji usifanye chochote

Toka nimeanza utafiti wa zao hili kikamilifu nina mwaka sasa na zaidi kijijini, namimi nilihama mjini kwa muda , nimeotesha nyanya za majaribio hii vuli (el-nino) ni msimu wangu wa tatu na masika utakuwa msimu wa nne. Kila nikivuna nyanya nasia nyanya, zote kwa ajili tu ya majaribio ili niweze kupata fomula nzuri kwa wanafunzi wangu ya kuotesha nyanya kwa ajili ya kupata faida kubwa ili kukuza mitaji yao na sio tu kuuza kujikimu kimaisha

Mimi mkakati wangu mkubwa siyo kufundisha “jinsi ya kulima nyanya” bali nafundisha JINSI MJASIRIAMALI MWENYE MTAJI KIDOGO AU ASIYE NA MTAJI ANAVYOWEZA KUPATA MTAJI KUPITIA KILIMO CHA NYANYA ZA MSIMU WA MVUA KUBWA MASIKA & EL-NINO

Maana kama ni kujifunza jinsi ya kufanya kilimo cha nyanya watu wengi wameanza kujifunza tangia wakiwa shule za msingi / sekondari na sasa kwenye mitandao na vitabu mbalimbali, sasa mimi nitakuja na jipya gani?

Nakusihi ikiwa umevutiwa na darasa hili basi usikose hata siku moja kujipatia elimu hii ya bure kabisa hapa kwenye blogu yako hii ya Jifunzeujasiriamali pamoja na mitandao yetu mingine ya kijamii kama facebook, Insta, Whatsapp group na You tube

Na ikiwa upo serious zaidi unaweza ukajiunga na darasa letu maalumu la VIP ambalo utapata nyenzo muhimu kwa ajili ya kilimo cha nyanya za Masika/El nino kama vile Mchanganuo kamili na halisi wa kilimo cha nyanya za masika ndani ya Green house ya gharama nafuu, pia Muongozo kamili wa kutengeneza Greenhouse hiyo  ya kipekee kwa wenye mitaji kidogo (Teknolojia hii Haijafika bado Tanzania, ni China, Israel, Pakistan na Marekani tu mpaka sasa imewahi kutumika)

 

HUDUMA ZA MALIPO

         (1)         Gharama ya VIP class ni TZS 15,000/= msimu mzima kuanzia hizi mvua za Vuli, El-nino mpaka masika zinamalizika mwakani, Utapewa na mchanganuo/Business Plan ya Kilimo cha nyanya msimu wa mvua nyingi za masika/elnino ndani ya Green-house ya gharama nafuu. Unapata bure pia Muongozo kamili wa kutengeneza Greenhouse hiyo hatua kwa hatua na darasa live 

         (2)          Kwa wanafunzi 10 watakaowahi darasani kutakuwa na OFFA ya muda mfupi ya kulipia shilingi 10,000/= tu badala ya sh. 15,000/= bei ya kawaida 

Mwisho wa kupokea wanafunzi ni muda wa kuhamisha miche ya nyanya tutakazosia mwezi Desemba kwa ajili ya mvua za masika, andaa mbolea iliyo poa ya kuku, ngombe au samadi kwa ajili ya kitalu nitafundisha karibuni namna ya kuandaa kitalu cha nyanya kwa vitendo

Namba ya Malipo ni; 0761002125 Jina: Peter Augustino Tarimo

         (3)          Ikiwa bado upo mjini  hujaamua kuhama kwa muda na unahangaika kupata mtaji wa biashara ya ndoto yako bila mafanikio, pakua kitabu hiki hapa cha>>> MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION ujue siri nilizotumia mimi mwenyewe Kariakoo kumiliki duka lenye wasaidizi 2 ndani ya mwaka 1 tu nikianza na bidhaa chache ‘kibarazani’ nje ya duka la mtu  

 

 

SOMA NA HIZI HAPA;

                 1.      Maana kamili ya ujasiriamali: ulikotoka, ulipo na unakoelekea duniani

                 2.      Biashara 7 nzuri mwaka 2019: chagua 1 uingize faida na kipato cha ziada kwa urahisi

                 3.       Ujasiriamali: ubunifu ndiyo msingi wake mkuu na injini ya uchumi katika soko huria

                 4.      Biashara yenye mtaji mdogo isiyojulikana na watu wengi bado-1

                 5.      Kuku wa nyama broilers: kwanini faida na gharama za ufugaji zinavunja moyo?

                 6.      Mafunzo matano (5) ya jinsi ya kuanzisha biashara toka mwanzo mpaka mafanikio

                 7.      Changamkia fursa hii mpya ya mazao ya tikiti mahindi, maharage nyanya na mbogamboga

                 8.      Mchanganuo wa biashara ya genge la kisasa la matunda, mbogamboga na vyakula

                 9.      Mchanganuo wa biashara ya kuuza chipsi, je, unajua gharama ya sahani moja mpaka inafika mezani ni sh. ngapi?

              10.    Siri ya kupata mtaji wa biashara kirahisi kwa mjasiriamali mdogo asiye na dhamana mjini na kijijini

 

0 Response to "KWANINI ULIME NYANYA MSIMU WA MVUA ZA MASIKA? ZIJUE FAIDA ZAKE NYINGI NA CHANGAMOTO KIDOGO"

Post a Comment