ORODHA YA BIASHARA ZA VIJIJINI UNAZOWEZA KUANZA NA MTAJI WA SH. LAKI 3 (300,000/=)

Biashara ya kijijini inayolipa

Katika safu yetu ya maswali na majibu leo kutokea Mkoani Dodoma (Makao makuu ya nchi), msomaji wetu mmoja kwa jina Janeth, ameuliza kama ifuatavyo; 

 

“Habari! Naomba ushauri wako, Nina mtaji wa laki tatu nitafanya biashara gani itakayoniingizia hela? Nipo kijijini siyo mjini.”

 SOMA: Unajua biashara yenye faida kubwa na ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

Na hii hapa ni ‘Screenshot’ ya swali hilo alilonitumia kwa SMS ya kawaida.

swali la msomaji wetu

 

Nilimjibu kama ifuatavyo:

Mimi siwezi kuzijua fursa zilizoko hapo kijijini kwenu kwakuwa sijafanya utafiti. Mimi naweza tu kukutajia kwa ujumla fursa zinazoweza kupatikana katika vijiji vyote  siyo kimoja tu

 

Majibu ya swali la msomaji wetu

Unatakiwa utafiti ni fursa za biashara zipi zilizoko hapo  kulingana na mazingira yaliyopo. Lakini pia ni  lazima ujitathmini wewe mwenyewe binafsi ikiwa una uwezo au nguvu katika aina gani ya biashara.

 SOMA: Nina mtaji wa milioni moja ya mkopo, nifanye biashara gani inayolipa?

Nguvu ninazozizungumzia hapa namaanisha vile vitu ambavyo una uwezo navyo kwa mfano ikiwa wewe umewahi kusomea kozi fulani labda tuseme ‘course’ ya matumizi ya compyuta, basi wewe biashara unayoweza kuanza kuifikiria ni biashara ya steshenari au biashara ya graphic designing. Ikiwa wewe uliwahi kuajiriwa katika duka fulani la rejareja lakini baadae ukaacha, wazo lako la biashara utakalolipa kipaumbele ni kufungua duka la rejareja.

 

Kitu kingine kinachoweza kukupa wazo la biashara ni hobi au mapenzi na biashara fulani. Jiulize mwenyewe je, ni biashara gani  unayoihusudu Sana? Kile unachokiwaza mara kwa mara akilini kwako kina uwezekano mkubwa wa  kugeuka kuwa wazo lako la biashara.

 SOMA: Namna bora zaidi ya kubuni wazo la biashara itakayolipa haraka bila msaada wa mtu mwingine

Kitu kingine ni mahitaji au shida  za watu. Jiulize hapo hapo kijijini watu wanahangaika sana kutafuta bidhaa/huduma gani. Au hata wewe mwenyewe ni kitu gani ukikihitaji unazunguka mwendo mrefu kukipata? Basi ujue ikiwa utaanzisha biashara ya bidhaa ama huduma hiyo utakuwa umetatua shida za watu wengine wengi na hivyo watu hao watakupa fedha kama malipo. Na hii itageuka biashara inayolipa hapo kijijini kwenu

 

Biashara za vijijini zipo nyingi kutegemeana na mahitaji ya kijiji husika lakini kwa ujumla orodha ya biashara nyingi zinazofanyika vijijini na kuwalipa watu vizuri ni hizi zifuatazo;

 

Biashara za kununua na kuuza mazao ya vyakula yanayotokana na kilimo au ufugaji. Biashara hii italipa vizuri zaidi ikiwa unanunua mazao na kuyapeleka maeneo ya mjini. Unaweza pia kununua mazao hayo msimu wa mavuno kwa bei ya chini kisha kuyahifadhi ukaja kuyauza kipindi cha uhaba wa chakula kwa bei ya juu.

 SOMA: Mtaji wangu ni mdogo sana lakini nahitaji kufanya biashara na sina ajira, naomba ushauri wako

Biashara nyingine unayoweza kufanya kijijini ni biashara ya kuuza bidhaa zitokazo mijini. Ukifungua duka la rejareja au hata duka la jumla kijijini na kisha bidhaa zako ukawa unazifuata mjini unao uwezekano wa kupata faida mara mbili ya mfanyabiashara anayenunua kwa jumla hapohapo kijijini.

 

Biashara hizi kubwakubwa nilizozitaja hapo juu zinataka uwe na mtaji mkubwa wa kutosha lakini nakumbuka wewe umeniambia mtaji wako ni lakini tatu tu. Biashara ndogondogo unazoweza kufanya kijijini na zikakupatia faida zipo pia ingawa haziwezi kufanana na biashara nyingi ndogondogo zinazoingiza fedha nyingi mjini.

 

Biashara kama za kuuza vitafunwa na biashara za vyakula kwa ujumla zinalipa sana mijini lakini biashara hizi vijijini haziwezi kutamba sana kutokana na watu wengi kutegemea milo inayopikwa majumbani mwao zaidi.

SOMA: Wazo la biashara ipi yenye hatari kidogo naweza kufanya kwa mtaji wa milioni 5 tano? Mwajiriwa serikalini 

Biashara ya kuuza vyombo nayo inalipa kijijini. Lenga vile vyombo vinavyopatikana kwa shida na vilivyo na uhitaji mkubwa mfano, mapipa, ndoo, mifuko ya kuhifadhia mazao, madumu ya maji, kamba za manila na mashine ndogondogo za kurahisishia kazi za shamba kama vile mabomba ya kunyunyizia madawa,  mitego na sumu za kuulia wadudu/wanyama waharibifu nk.

 

Kuna biashara nyingine ndogo yenye faida kubwa ambayo malighafi zake wala hununui unapata bure ardhini, hii ni biashara ya kutengeneza majiko sanifu na vifaa vya ufinyanzi kwa kutumia udongo wa mfinyanzi. Kama kijiji chenu kimebarikiwa kuwa na aina hiyo ya udongo basi kumbuka mnaukalia utajiri pasipo kujua. Maeneo ya mijini wanahitaji sana majiko sanifu ya kutumia mkaa kidogo, ukijifunza kuyatengeneza na kuyatafutia soko maeneo ya mijini umeula!

 

Ikiwa kijijini kwenu mikate ni ya shida pia unaweza kuanzisha biashara ya kuoka na kuuza mikate kwa kutumia oven rahisi za mkaa.

Kwa mtaji wa laki 3 pia kijijini unaweza ukaanzisha biashara ya kununua na kuuza matunda. Lakini pia biashara hii unatakiwa ukishanunua matunda yako kijijini basi soko lako liwe ni mjini. Tafuta mji uliokuwa karibu na wewe au hata ikiwa ni mji wa mbali basi pawe na usafiri was uhakika. Matunda mijini yana soko kubwa ukiwa na mahali pa uhakika pa kushushia matunda yako kisha wateja wakaja kuyachukulia pale isijekuwa tena ukishayafikisha mjini unawaita madalali wanakuja kukuupangia bei. Matunda na mbogamboga ni aina ya mazao ya biashara yenye faida kubwa nje na ndani ya nchi.

 SOMA: Mchanganuo wa biashara ya genge la kisasa la matunda, mbogamboga na vyakula

Mwisho Janeth nakushauri fikiria wazo la biashara unayoona utaimudu, ifanyie utafiti kuijua nje ndani na baada ya hapo sasa ianze taratibu kwa kutumia kiasi kidogo kwanza cha huo mtaji wako(300,000/=) unaweza kutumia hapo laki na nusu kisha ukiona biashara inakupa matumaini kwa kuingiza faida basi ndipo uongeze taratibu kiasi kingine cha mtaji uliobakia.

 

…………………………………………………………

 

Ndugu msomaji wa makala hizi, ikiwa ungependelea kujifunza zaidi kwa makala nzuri kila siku zinazohusu fedha na ujasiriamali basi nakukaribisha katika darasa letu ndani ya group la Whatsap la MICHANGANUO-ONLINE. Ada ni sh. Elfu 10 tu kwa mwaka mzima na tayari sasa hivi masomo yakiwa yameshaanza tunaendelea na usajili wa wanachama wapya kwa ajili ya mwaka 2021

 

FAIDA UTAKAZOZIPATA

1.  OFFA ya vitabu na michanganuo, ni items zipatazo 20

 

2.  Kuwa member wa group kwa mwaka mzima bila malipo ya ziada.

 

3.  Semina za jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara zinazolipa

 

4.  Fursa ya kuuliza swali lolote lile kuhusiana na Mpango wa biashara na Ujasiriamali na kujibiwa kwa kina

 

5.  Fursa ya kutangaza bure katika group

 

6.  Fursa ya kuchangia chochote, kutoa somo au semina nk.

Offa ya kupata hivyo vitu 20 kikiwamo kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI mwisho wake ni tarehe 10 Desemba 2020 siku ya Alhamisi usiku. Baada ya hapo kama nafasi zitakuwepo bado utaweza kulipia kujiunga na group lakini offa hii haitakuwepo tena.

 

Kulipia tumia namba zetu; 0765553030  au  0712202244 jina ni Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe kwa meseji au watsap usemao;

 

NATAKA OFFA YA MWISHO 2020 NA KUUNGWA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE”

 

Baada ya hapo nitakutumia offa zote na kukuunganisha na group la masomo uanze kujifunza siku hiyohiyo.

 

Ikiwa hutumii WATSAP hamna shida kwani tunatuma kila kitu pia kwa njia ya E-mail.

 

NA IFUATAYO NDIO ORODHA YA OFFA NITAKAZOKUTUMIA!


              1.      KITABU cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI (New special edition 2021) –cha kiswahili

 

              2.      KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-cha kiingereza

 

              3.      KITABU: MIFEREJI 7 YA FEDHA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA –cha kiswahili

 

              4.      Semina nzima ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwa kiswahili

 

              5.      Kifurushi cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS) kuku wa mayai, kuku wa nyama na kuku wa kienyeji-zote kwa kiswahili

 

              6.      Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN)-kwa kiswahili

 

              7.      Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa Kiswahili & kiingereza

 

              8.      Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks) -Kiswahili

 

              9.      Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE)-Kiswahili

 

             10.    Somo maalumu la Mzunguko chanya wa fedha kwako binafsi na kwa biashara yako-kwa kiswahili

 

             11.    Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi. - Kiswahili & kiingereza

 

 

             12.    Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili

 

             13.    Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwa kiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.

 

             14.    Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2021 (MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla

0 Response to "ORODHA YA BIASHARA ZA VIJIJINI UNAZOWEZA KUANZA NA MTAJI WA SH. LAKI 3 (300,000/=)"

Post a Comment