MFUMO MPYA WA BURE WA KUSIMAMIA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA (Forever Free POS & CRM) | Jifunzeujasiriamali

MFUMO MPYA WA BURE WA KUSIMAMIA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA (Forever Free POS & CRM)

Mfumo wa kusimamia biashara za rejareja (ForeverFree POS & CRM)

Forever free POS & CRM ni mfumo maalumu wa bure kwa asilimia 100% kwa matumizi ya msingi ya biashara za rejareja.

Inafanya kazi vizuri sana kwenye simu za mkononi, tablets (Android/iOS) na hata katika kivinjari cha kompyuta za kawaida za mezani. Inakusaidia kurekodi mauzo, kusimamia bidhaa, na kuona ripoti za faida & hasara

Ingawa mfumo huu unafanya kazi vizuri sana kwenye biashara ya duka la rejareja maarufu kama “Maduka ya Mangi” lakini pia unaweza kutumiwa na biashara nyingine zote za rejareja mfano, Genge la matunda na mbogamboga, kioski, baba na mama lishe, migahawa, saluni, uuzaji wa nguo, vifaa vya kielektroniki, hardware, maduka ya dawa, mabucha, biashara ndogondogo za sokoni na hata biashara za kuuza bidhaa za rejareja mtandaoni

Sifa na Faida kubwa za Mfumo huu kwa biashara za Rejareja

                ·          Usimamizi wa Mauzo (POS): Unabadilisha simu au tablet yako kuwa mashine ya kusajili mauzo, risiti, na kupokea malipo mbalimbali

                ·          Uwezekano wa kutumia kotekote, kwenye simu ya mkononi, tablet na kompyuta ya kawaida ya mezani

                ·          Udhibiti kikamilifu wa bidhaa (Stoku): Unafuatilia kiwango cha bidhaa zilizobaki dukani kwa muda halisi (real-time) na unapokea taarifa bidhaa zikiwa zinakaribia kuisha (alert) ili uagize nyingine

                ·          Kudhibiti Wafanyakazi: Unaweza kuona nani ameuza nini, kwa muda gani, muda wa kuingia na kutoka pamoja na ni kiasi gani cha fedha kilichopo kwenye droo

                ·          Ripoti za Biashara: Unatoa ripoti za kina kuhusu faida, bidhaa zinazouza zaidi, na mwenendo wa mauzo ya kila siku au kila mwezi

                ·          Uwezo wa kurekodi Matumizi (Expenses) ya kila siku kwa ajili ya kujua Faida halisi inayopatikana au Hasara katika kipindi chochote utakacho mfano lisaa au siku

                ·          Kutunza Kumbukumbu za Wateja: Inarekodi namba zao za simu na madeni yao kwa urahisi

                ·          Huduma ya Wateja (Loyalty): Inakuruhusu kusajili wateja na kuwapa pointi za zawadi ili kuwahimiza kurudi tena

                ·          Ni wa bure daima: Tofauti na mifumo mingi ya nje na ndani ya Tanzania ambayo hukupa kipindi kifupi tu cha majaribio labda siku 10 mpaka 40, ForeverFree POS & CRM hauna kabisa kipindi cha majaribio na ni bure daima!

Hatua na Jinsi ya kuanza kuutumia mfumo wa ForeverFree POS & CRM

               (1)     Pakua app/programu ya ForeverFree POS & CRM

               (2)     Jisajili kwa akaunti ya bure kwenye tovuti au moja kwa moja kupitia app yako

               (3)     Ingiza orodha ya bidhaa zako (Inventory), bei zake, na picha za bidhaa

               (4)     Anza kufanya mauzo na kufuatilia biashara yako kupitia simu au kompyuta/laptop yako

Mafunzo hatua kwa hatua ya jinsi ya kutumia mfumo huu yameanza rasmi leo katika kundi la whatsapp & Telegram  la Tanzania Retailers Whatsapp Premium Group (TRPG)

Ikiwa unahitaji kutumia mfumo huu kwenye biashara yako pasipo kuwa na malipo yeyote ya mwezi wala ya mwaka na kutimiza mahitaji yote ya msingi kwa biashara ndogo au ya kati, unaweza kuwasiliana na mimi nikupe utaratibu wa kujiunga na mafunzo hayo rahisi mara moja

Mafunzo yote utayakuta ndani ya group kuanzia somo la kwanza mara tu uingiapo

Mafunzo hayachoshi, si marefu na wala huhitaji kuwa mtaalamu wa IT ndipo uelewe, unaweza kuchukua siku 1 mpaka 2 tu kujua kuutumia mfumo kikamilifu

Mawasilinao tumia kiungo kifuatacho au unaweza kunitumia ujumbe wa “ForeverFree” kwa namba 0761002125


Jiunge na group la mafunzo hapa


0 Response to "MFUMO MPYA WA BURE WA KUSIMAMIA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA (Forever Free POS & CRM)"

Post a Comment