BIASHARA BUNIFU ZA MTAJI MDOGO ZINAVVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA MWAKA 2022 | JIFUNZE UJASIRIAMALI

BIASHARA BUNIFU ZA MTAJI MDOGO ZINAVVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA MWAKA 2022

Biashara bunifu ya uzalishaji

Bila shaka umewahi kusikia maajabu mengi ya watu waliofanikiwa kimaisha haraka au ndani ya muda mfupi kiasi kwamba mpaka hivi leo hujaamini bado ikiwa mafanikio hayo yalitokana na juhudi za kawaida. Ni desturi kwa Waafrika tulio wengi na pengine Binadamu wote wa Dunia ya Tatu kuwa na imani mbalimbali zisizokuwa na uthibitisho kwamba mafanikio kimaisha kama hayo lazima nyuma yake kuna nguvu za giza. 

Sasa basi ikiwa siyo nguvu za giza ni nguvu gani hiyo inayowezesha baadhi ya binadamu wenzetu kupata mafanikio ya haraka kimaajabu namna hiyo?  Utasikia mara huyu alianza na genge tu, mara yule alianza na ufundi viatu nk. lakini sasa hivi ni matajiri “wakutupa”

SOMA: Jinsi kiwanda kidogo kinavyoweza kukutoa kimaisha nakuwa tajiri wa kutupa

Kuna siri moja kubwa watu wengi hawajaigundua au wakati mwingine hata wanapoigundua basi hawaitilii maanani kabisa. Kuna hatua katika biashara mtu kamwe huwezi kulazimisha ikuletee mafanikio haraka. Nasema hivyo kwani ni leo tu msomaji wangu mmoja alinipigia simu kutaka nimshauri afanyeje baada ya biashara yake ya duka kuifunga mwezi mmoja tu baada ya kuifungua.

Maelezo yake kwa kina nitayaelezea hapa siku nyingine lakini ninachotaka kusema tu ni kwamba, hatua ya awali ya biashara yeyote ile inataka subira, kujitoa na ubunifu wa hali ya juu pasipo kujali ‘factors’ nyinginezo kama vile washindani, mtaji wa kutosha na eneo ulipo. Una washindani wengi, usikimbie kiholela wewe huna rasilimali za kutangatanga tafuta njia za kukabiliana nao, mtaji ni kidogo- zipo mbinu, eneo ni bovu lakini tayari umeshalivaa, utakimbia? Na ukikimbia je una pesa za pango kwenda kulipia kwingine haraka?. Niliwahi kuandika makala moja hii… Huna mtaji wa kutosha, hukopesheki?, jaribu njia ya kufunga mkanda (bootstrapping). ukiisoma unaweza kujua nasema kitu gani. 

Bootstrapping ni dhana ya mtu kujipatia mtaji kwa njia fupi lakini ngumu na inayohitaji ubunifu. Kwanini tunaona wanaofanikiwa haraka wanafanya maajabu fulani pengine hata kudhania wanatumia nguvu za giza? ni kwa sababu Bootstrapping ni ngumu na isiyoweza kuvumiliwa na kila mtu isipokuwa tu wachache walioamua kujitoa kwelikweli wakisaidiwa na UBUNIFU.

SOMA: Maana kamili ya Ujasiriamali, ulikotoka, Ulipo na Unakoelekea Duniani

Ukweli ni kwamba hatua ya biashara mtu anapokuwa na mtaji wa kutosha ni rahisi sana kuendesha na haiumizi tena kichwa ndio maana kila anayefikia hatua hiyo wengine wote humchukulia kama mtu mjanja au mwenye akili nyingi lakini ukweli ni mtu wa kawaida tu aliyefikia hatua ya biashara isiyokuwa ngumu.

Pesa ni ngumu kupatikana hivihivi na bila ya mtaji-pesa tusidanganyane  dunia ya leo kufanikiwa biashara kwa kiwango kikubwa ni ndoto za alinacha. Kuna mengi hapa ya kufafanua pamoja na zile dhana kwamba, pesa si ishu bali ishu ni mawazo nk. lakini yote hayo tutayapa muda wa kutosha siku nyingine au kwenye MASTERMIND GROUP letu Watsap na Telegram(MICHANGANUO-ONLINE-2022)

SOMA: Elimu ya fedha na umuhimu wake 2022 njoo tuunganishe nguvu tuhamishe milima!

Tunaweza kwa kutumia biashara zilezile tulizonazo na tunazoona hazitulipi kihivyo, kutafuta mtaji wa kutosha kufanya mambo makubwa zadi. Ikiwa mtego mkubwa wa mafanikio upo katika MTAJI basi hatuna budi kutumia kila njia zinazoweza kutupatia mitaji ya kutosha ili nasisi tuweze kufanya biashara za kijanja zenye mafanikio makubwa yanayoeleweka.

Mwezi ule wa 11 nilifanya semina ya kuandika mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku watu wengi wakaniona kama mwehu, “kutoka na biashara za kuku? huyu jamaa ana wazimu, kuku nafuga toka utotoni  na sijaona mafanikio yeyote” alicomment msomaji katika forum moja nilikokuwa natangaza ile semina.

Lakini msomaji yule hajui ni nini kilichomkwamisha katika ufugaji wake miaka yote hiyo tokea utotoni, ndio maana nikafanya semina ya kuandika mchanganuo wa biashara ya kuku wa KUOMBEA MKOPO BENKI. Utafanikiwaje kwa kufuga kuku majike 5 na jogoo 1 ukitumaini watotoe mpaka wafike kuku 1000, si utaota mvi kabla lengo lako hilo halijatimia?

SOMA: Kuendesha biashara bila mtaji wa kutosha ni sawa na kulima kwa jembe lisilokuwa na mpini

Tufike mahali Watanzania tufikirie nje ya maboksi, bila ya ubunifu na kutafuta mitaji ya uhakika mafanikio kibiashara tutaendelea kuyasikia kwenye media. Ndio maana mwaka huu 2022 katika MASTERMIND GROUP LANGU nimeandaa biashara ndogondogo Bunifu nyingi tutakazochanganua kila siku kwa lengo la kujijengea uwezo mkubwa kimtaji. Hakuna jipya chini ya jua, biashara hizo ni zile zile tulizozizowea lakini KIPYA hapo ni UBUNIFU na njia mpya za kuzifanya zitakazowezesha mzunguko wa fedha kwenda chapchap.

Nakukaribisha sana kwenye GROUP LANGU, mwaka huu litakuwa tofaui sana na miaka mingine.

Katika kipindi chote cha uandishi wangu nimeandika vitabu 4 na kutafsiri kimoja. Vitabu hivi vina utajiri mkubwa wa Maarifa ya ujasiriamali ninayoweza kusema ukivipata vyote hautahangaika kutafuta maarifa kwingine labda tu utake mwenyewe.

Kwa siku 5 kuanzia leo tarehe 19/12/2021 mpaka 25/12/2021 nimetoa OFFA kwa mtu yeyote kujipatia vitabu vyangu hivyo vyote pamoja na michanganuo ya biashara kama nitakavyoorodhesha hapo chini kwa Shlingi elfu 11 tu ! Gharama ya vitu vyote hivyo inafika shilingi laki moja siku za kawaida.

 

JINSI YA KULIPIA OFFA HII

Unalipa shilingi elfu 10 kupitia namba 0765553030 au 0712202244  na jina ni Peter Augustino Tarimo

Punde tu baada ya malipo hayo, nitakutumia kwa njia ya Email au Watsap vitabu na michanganuo yote kasoro kitu kimoja tu, KITABU CHA THINK AND GROW RICH CHA KISWAHILI

Kwa kutumia ile sh. Elfu moja iliyobakia nitakutumia COUPON maalumu itakayokuwezesha kukinunua kitabu hicho kutoka katika Mtandao wa GETVALUE kwa shilingi elfu moja tu badala ya shilingi elfu 15 bei ya kawaida. Aidha ni lazima uwe na simu ya Smartphone kupata kitanu hiki.

 NB: Unaweza kujipatia offa ya vitabu na michanganuo tu peke yake au pamoja na nafasi ya kujiunga na MASTERMIND GROUP 

1.  Kupata vyote viwili tuma kwa sms au wasap maneno, “NATAKA OFFA NA KUUNGWA GROUP

 

2.  Kupata offa peke yake group hutaki tuma neno, “NATAKA OFFA TU”


*Ukiwa na akaunti ya telegram unapata pia fursa ya kusoma masomo yetu yote ya fedha tuliyojifunza siku za nyuma zaidi ya 70.

 

*Ikiwa huna watsap wala telegramu, bado tunaweza kukutumia vitabu, michanganuo na masomo kupitia e-mail yako

 

 

ORODHA YA VITU (ITEMS) PAPO KWA HAPO VYA OFFA YENYEWE NI HIVI HAPA CHINI;

 

             1.     KITABU: THINK & GROW RICH – SWAHILI EDITIONkiswahili

 

             2.     KITABU: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIANALI (New special Edition 2021) - kiswahili

 

             3.     KITABU: MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA - Kiswahili

 

              4.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOAkiswahili

 

             5.     KITABU: SIRI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO KWA UFANISIkiswahili

 

             6.     KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.- kiingereza

 

             7.     Semina nzima ya siku 4 na Mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku wa Mayai kuomba mkopo benki. -kiswahili

 

             8.     Semina nzima ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwa kiswahili

 

             9.     Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kiswahili

 

           10.   Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT)kwa Kiswahili & kiingereza

 

           11.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

           12.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE) -kwaKiswahili

 

           13.   Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.- Kiswahili & kiingereza

 

           14.   Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili

 

           15.   Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.

 

           16.   Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2022 (MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla

0 Response to "BIASHARA BUNIFU ZA MTAJI MDOGO ZINAVVYOWEZA KUKUTOA KIMAISHA MWAKA 2022"

Post a Comment