HATUA KWA HATUA JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUKU WA NYAMA 2000 KUOMBA MKOPO TAASISI ZA FEDHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HATUA KWA HATUA JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUKU WA NYAMA 2000 KUOMBA MKOPO TAASISI ZA FEDHA

SEMINA YA KUKU WA NYAMA HATUA KWA HATUA SIKU YA 3

Baada ya kumaliza kazi ya kufanya utafiti wetu kuhusiana na biashara ya ufugaji wa kuku wa nyama na kupata taarifa mbalimbali, sasa tunaweza tukaanza kuandika mchanganuo wetu hatua kwa hatua. Zipo njia tano mtu unazoweza ukazitumia katika kuandika mpango wa biashara yeyote ile kama ifuatavyo;

1.    Njia ya kutumia vipengele vya mpango wa biashata(Outlines) ambapo unaorodhesha vipengele vyote kisha unaanza kuandika kwa undani kimoja baada ya kingine hadi unamaliza mpango wako mzima

2.    Kwa kutumia Vielezo(Templates); Njia hii unafuatisha maelezo yaliyokwishawekwa kwenye kurasa kwa kuondoa au kubadilisha yale yaliyokuwepo na kuweka yakwako kulingana na biashara yako

3.    Kwa kutumia Michanganuo ya biashara nyingine iliyokwisha kuandikwa tayari(Business plan samples); Hii unasoma michanganuo mbalimbali inayofanana na wakwako unaotaka kuandika kisha unaandika wa kwako.

4.    Kwa kutumia Programu maalumu za kompyuta za kuandika mpango wa biashara(Business plan softwares); Hizi ni applications maalumu unazojaza taarifa za biashara yako na kisha zenyewe zinakutengenezea mchanganuo wako yakiwamo na makisio ya taarifa zote za mahesabu.

5.    Kutumia mchanganyiko wa njia zaidi ya moja au zote zilizotajwa hapo juu.

Katika mchanganuo wetu huu wa kuku wa nyama wa kuombea mkopo tutatumia njia ya vipengele vya mpango wa biashara (Business plan outlines). Ingawa vifuatavyo ndiyo vipengele vinavyounda mpango mzima wa biashara lakini siyo sheria kwamba ni lazima kila kipengele ukiweke katika mpango wako hata kama kipengele hakifanyi kazi katika biashara husika.

Weka tu vile vipengele unavyoona vitafanya kazi au vitafaa kwenye aina ya biashara unayotarajia kuifanya. Kumbuka lengo hasa la mpango wa biashara siyo kujaza kurasa maneno matupu bali ni MATOKEO(results) mpango huo utakayoyaleta.

Hata hivyo kulingana na hadhira au walengwa wa mchanganuo wako inawezekana wakawa wanahitaji baadhi ya vipengele lazima viwekwe hivyo hauna budi kuviweka mfano benki au taasisi unayoomba fedha inaweza kukuwekea sharti la kujumuisha vipengele fulani katika mchanganuo wako.

 

VIPENGELE RASMI VYA MCHANGANUO WA BIASHARA

 1.0 MUHTASARI

 

2.0 MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA

2.1 Dhamira kuu

2.2 Malengo

2.3 Siri za mafanikio

2.4 Umiliki wa Biashara

2.5 Kianzio (kwa biashara mpya au historia kwa kampuni iliyokwishaanza zamani)

2.6 Eneo la biashara na vitu vilivyopo

 

3.0 MAELEZO YA BIDHAA / HUDUMA au VYOTE

3.1 Maelezo ya bidhaa/huduma

3.2 Sifa za kiushundani au Utofauti wa bidhaa/huduma na za washindani wako

3.3 Vyanzo vya malighafi/bidhaa

3.4 Kopi za matangazo

3.5 Teknolojia

3.6 Bidhaa au Huduma za baadae


4.0 TATHMINI  YA  SOKO

4.1 Mgawanyo wa soko

4.2 Soko lengwa

4.2.1 Mahitaji ya soko

4.2.2 Mwelekeo wa soko

4.2.3 Ukuaji wa soko

4.3 Tathmini ya sekta

4.3.1 Washiriki katika sekta

4.3.2 Usambazaji

4.3.3 Ushindani

4.3.4 Washindani wako wakubwa

 

5.0 MIKAKATI NA UTEKELEZAJI

5.1 Nguvu za kiushindani

5.2 Mkakati wa soko

5.2.1 Kauli ya kujipanga katika soko

5.2.2 Mkakati wa bei

5.2.3 Mkakati wa matangazo/promosheni

5.2.4 Programu za masoko

5.3  Mkakati wa mauzo

5.3.1 Makisio ya mauzo

5.3.2 Programu za mauzo

5.4 Mkakati wa ushirikiano

5.5 Vitendo na utekelezaji

5.5.1 Uendeshaji

 

6.0 MAELEZO YA UONGOZI NA WAFANYAKAZI

6.1 Mfumo wa uongozi

6.2 Timu ya uongozi na wafanyakazi

6.3 Mpango wa mishahara

 

7.0 MPANGO WA FEDHA

7.1 Dhana/makisio muhimu

7.2 Tathmini ya mauzo ya kurudisha gharama (Break Even Analysis)

7.3 Makisio ya faida na hasara

7.4 Makisio ya mtiririko wa fedha

7.5 Makisio ya mali na madeni (mizania ya  biashara)

7.6 Sehemu muhimu za biashara


8.0 VIELELEZO / VIAMBATANISHO

·       Taarifa za mahesabu ya fedha kwa undani

·       Mahesabu yako ya nyuma

·       Leseni, vibali, ripoti za kodi, hatimiliki na alama za biashara

·       Mikataba mbalimbali

·       Orodha ya mali na vifaa mbalimbali(Dhamana)

·       CV za viongozi na wafanyakazi muhimu

·       Kopi za matangazo ya biashara

Ingawa Muhtasari ndiyo sura au kipengele cha kwanza kabisa katika mlolongo wa vipengele kama tulivyoona hapo juu, kwenye kuandika siyo lazima tuanze na kipengele cha kwanza, tunaweza tukaanza na kipengele kingine chochote kile kati ya hivyo vinane. Sisi katika mchanganuo wetu huu tutaanza na kipengele cha pili cha MAELEZO YA BIASHARA / KAMPUNI.

Unapoanza kuandika sura au kipengele chochote kile acha nafasi ya kuandika muhtasari wa sura hiyo kisha ukishamaliza kuandika sura nzima ndipo unakuja kumalizia na muhtasari huo. Jumla ya mihutasari yote 8 katika kila kipengele/sura ndiyo inayokuja kuunda Muhtasari mkuu wa mchanganuo wako wote ambao ndio unaoanza pale mwanzoni kabisa mwa mchanganuo wako.

Kwa kawaida wawekezaji, taasisi za fedha na wakopeshaji wengine huwa wana kawaida ya kutaka kusoma muhtasari tu wa mpango mzima wa biashara na watahitaji kusoma mpango mzima mara chache sana hivyo unatakiwa muhtasari wako uuandike kwa umakini ili uweze kubeba picha halisi ya mchanganuo wako mzima ikiwa ni pamoja na kuonyesha kwa kifupi vile vipengele muhimu vinavyogusa mkopo au vinavyohitajika zaidi na wawekezaji / taasisi au benki.

Benki

Ikiwa unaandika mchanganuo wako kwa ajili ya kuomba mkopo benki au taasisi nyingine yeyote ile ya kifedha ni lazima utambue kuwa benki au taasisi yeyote ya mkopo hawawekezi kwenye biashara yako bali wanakukopesha na mwishowe urejeshe fedha zao zote iwe biashara itafanikiwa au itafeli. Kwa hiyo watataka maelezo yanayojitosheleza kwenye vipengele vinavyogusa biashara hasa umiliki, maombi ya mkopo, matumizi ya mkopo, dhamana na jinsi utakavyorejesha fedha zao. Pia watalenga kwenye kipengele cha makisio ya fedha hasa mtiririko wa fedha utakavyokuwa.

Wabia/Wawekezaji

Kama unalenga kuwavutia wawekezaji au wabia basi ni lazima uweke msisitizo kwenye kipengele kinachoonyesha wewe ushiriki wako katika hiyo biashara ni kiasi gani na pia mbia atapata asilimia ngapi ya umiliki. Wawekezaji na wabia pia wanapenda kupata maelezo ya kutosha katika kipengee cha Uongozi na timu nzima itakayohusika katika uendeshaji wa biashara, sifa, wasifu wao na uzoefu waliokuwa nao kufanikisha biashara husika.

Baada ya maelezo hayo machache hebu sasa tuanze kuandika vipengele vya mchanganuo wetu;

 

2.0 MAELEZO YA KAMPUNI / BIASHARA

 

Sehemu hii ni kwa ajili ya muhtasari mdogo wa Sura hii mara baada ya kumaliza kuandika sura yetu nzima

 

2.1 Dhamira kuu (Mission statement)

Kwenye dhamira kuu tutaandika, shughuli ile biashara inayokwenda kutekeleza ambayo ni;

Kuzalisha na kusambaza bidhaa bora za kuku zilizojaa virutubisho na protini ya kutosha kwa wateja wetu katika eneo la Bagamoyo na maeneo mengine ya karibu

2.2 Malengo.(Objectives)

Hapa tutayataja malengo ya muda mfupi na yale ya muda mrefu ya biashara hii ambayo ni haya yafuatayo; 

1.    Kuomba mkopo benki wa shilingi 5,000,000/=

2.    Kufuga kuku 2000 katika msimu mmoja na kuku elfu 16 Kwa mwaka

3.    Kutengeneza ajira ya kudumu kwa watu wawili

4.    Kutengeneza jina zuri la kampuni kwa wateja wetu kwa kuwauzia kuku walio na afya kwa bei nafuu.

 2.3 Siri ya Mafanikio (Keys to success)

Katika siri za mafanikio tutataja vile vitu ambavyo biashara inatarajia kuvipa kipaumbele kusudi iweze kufanikiwa, vyaweza kuwa ni kitu chochote kile na hapa sisi tutataja;

·       Kununua chakula cha kuku kwa bei nafuu ya jumla kutoka kiwandani moja kwa moja

·       Banda la kuku kubwa na lililojengwa kwa uimara linalotosha kuku 2000

·       Uuzaji wa kuku kwa wakati katika wiki ya 4 – 5

·       Kutembelewa na afisa wa mifugo mara kwa mara

·       Kuzingatia kikamilifu kanuni za ulinzi wa kuku dhidi ya maambukizi ya magonjwa (Strictly biosecurity measures)

2.4 Historia ya Kampuni

Kampuni ya Tumaini Poultry ilianza rasmi shughuli za ufugaji wa kuku kwa ajili ya nyama mnamo mwezi Desemba mwaka 2020 kwa kuanza na vifaranga 1000 wa siku moja. Kampuni kwa mwaka 2022 imelenga kufuga kuku 2000 katika mzunguko mmoja wa siku 44  ambapo kwa mwaka mmoja kutakuwa na mizunguko/misimu 8.  Kampuni inamilikiwa na Bwana Tumaini Masanja kwa asilimia zote 100% za hisa na imelenga kuomba mkopo benki wa shilingi 5,000,000/= mwanzoni mwa mwaka 2022 utakaolindwa kwa dhamana za kampuni na zile za mmiliki mwenyewe binafsi. Mradi huu upo katika eneo la Kiromo karibu na barabara ya Bagamoyo kilomita 50 kutoka katikati ya jiji la Dar es salaam.

2.5 Mahesabu ya kipindi kilichopita (Past performance)

Kipengele hiki chote  kipo kwenye somo hili zima katika group la masomo la mastermind Michanganuo-ONLINE

 

2.6 Maombi ya Mkopo.(Fund request)

Kipengele hiki pia utakipata chote kwenye somo hili zima katika mastermind group la michanganuo-ONLINE

2.7  Mahitaji ya Mradi

Kwenye kipengele hiki tutachora jedwali linaloonyesha mahitaji yote ya mradi huu kwa mwaka 2022 ili biashara iweze kutekeleza malengo iliyojiwekea kikamilifu. Hapa tutaorodhesha mahitaji yote, kiasi cha fedha kitakachohitajika kugharamia mahitaji hayo pamoja na chanzo cha fedha kwa ajili ya mahitaji hayo. Kujua undani wa jedwali hilo pata semina hii nzima.

Vifaranga

Vitahitajika vifaranga 2000 wa siku moja kutoka kwa  wakala anayeaminika wa kampuni ya kutotolesha vifaranga wa nyama. Kila kifaranga kitagharimu shilingi 2,000/=  sawa na shilingi 4,000,000/= kwa vifaranga vyote 2000

Chakula

Kitahitajika chakula starter mifuko 35 na finisher mifuko 45, chakula hiki kitaagizwa moja kwa moja kutoka katika kiwanda cha kutengeneza chakula cha kuku kwa bei ya kiwandani ya wastani wa shilingi 70,000/= starter na sh. 65,000/= finisher  Kwa kila mfuko wa kilo 50.

Kwa mujibu wa taarifa za utafiti wetu tulioufanya kule mwanzoni wakati tunaanza semina hii ambapo kuku mmoja anakadiriwa kula kiasi cha chakula kilo mbili kwa muda wote wa wiki 4-5, Jumla ya gharama zote za chakula pamoja na usafirishaji wake tangu siku ya kwanza mpaka kuku wanauzwa wote zinakadiriwa kuwa shilingi 5,375,000/=

Maji

Kulingana na utafiti tuliofanya kuku mmoja wa nyama kwa wiki zote 4 mpaka 5 anakadiriwa kunywa kiasi cha maji lita 2, x kuku 2000 jumla ni lita 4000 za maji ambazo ni sawa na madumu 200 ya lita 20. Bei ya dumu moja la maji inakadiriwa kuwa shilingi 100, hivyo kwa muda wote gharama za maji ni shiingi 20,000/=

Mabanda:

Kuku 2000 kwa mujibu wa utafiti wetu kama unafuatilia semina hii toka mwanzo tuliona wanahitaji mita za mraba 200, hili ni eneo lenye ukubwa sawa na nusu ya kiwanja cha mita 20 kwa 20. Katika mradi huu mmiliki wake hatajenga mabanda yake binafsi bali atakodisha mabanda yaliyokuwa tayari kwa shilingi 100,000 katika mzungiko mmoja wa siku 44    

Wafanyakazi

Watahitajika wafanyakazi 2 wa kuhudumia mradi wa kuku na kila mmoja atalipwa shilingi 100,000/= kwa wiki zote 5 za mzunguko mmoja Jumla wote wawili watalipwa sh. 200,000/=

Madawa na chanjo:

Katika mzunguko mmoja gharama za chanjo, madawa na vitamini kwa kuku wote 2000 zinakadiriwa kufikia shilingi 300,000/=

Viota

Kutakuwa na viota 20 kila kimoja vifaranga 100. Gharama ya kutengeneza kiota kimoja inakadiriwa kuwa ni shilingi 10,000 sawa na shilingi 200,000/= kwa viota vyote 20

Joto na mwanga

Vifaranga wakiwa kwenye viota kwa siku 7 za mwanzo watahitaji taa wastani wa saa zote 24. Taa 20 za watts 100  zitawaka kwa saa 24, Taa 20 x 100w = 2000w / 2kW (Kilowat 1 = Watts 1000)

Hivyo Kilowatt 2 x saa 24 x Siku 7 = 336kWh

Kilowatt- Hour 1(1kWh) = Unit moja ya umeme, hivyo 336kWh = Units 336

Unit 1 = shilingi 300, hivyo 336unit x 300 = Tsh. 100,800

Hivyo kwa siku 7 gharama za umeme zitakuwa ni shilingi 100,800/=

Kwa siku 7 zinazofuata taa kwa ajili ya joto zitahitajika kwa wastani wa saa 12 tu kwa siku ambapo ni sawa na nusu ya gharama iliyopatikana hapo juu = 50,400

Kuanzia wiki ya 3 na kuendelea kuku watahitaji taa kwa ajili ya mwanga tu masaa ya usiku na zitawashwa taa 10 tu katika banda zima kwa wastani wa masaa 10. = taa 10 za watts 100 x saa 10 x siku 18 = 180kWh x 300 = 54,000

Jumla ya gharama zote za mwanga na joto ni shilingi 205,200

Matandazo

Wastani wa viroba 30 vya maranda ya mbao vitahitajika katika mzunguko mmoja wa ufugaji na kila kiroba kimoja kinagharimu shilingi 2000 x 30 = 60,000/=

Vyombo vya kulia chakula

Kila kuku 100 watahitaji kutumia wastani wa vilishio 2 mpaka 3 vya chakula, tukitumia vilishio 3, kuku 2000 watahitaji jumla ya vilishio 60

Kilishio kimoja huuzwa kwa bei kati ya shilingi 7,000 – 12,000 tunakadiria bei ya shiilingi 9,000 kwa kila kilishio sawa na shilingi 540,000 kwa vilishio vyote 60

Vyombo vya kunywea maji

Kwa kila kuku 100 watatumia wastani wa vinyweo 2 sawa na vinyweo 40 kwa kuku wote 2000. Kinyweo kimoja ni kati ya shilingi 5,000 – 12,000, tukitumia shilingi 7,500 x 40 = 300,000/=

Kipimajoto (Thermometer)

Kitatumika kipimajoto kimoja sh. 35,000/=

Gum boots

Pea mbili za viatu vya kufanyia kazi bandani jumla shilingi 50,000/=

Jedwali la mahitaji (Gharama)


Jedwali hili kamili unaweza ukaliona kwenye semina nzima iliyowekwa katika channel ya group la Michanganuo-online

 

Chanzo cha mahitaji

Mtaji wa mmiliki

7,125,200

Mkopo wa Benki

5,000,000

JUMLA YA VYANZO VYOTE

12,125,200

 

Mpaka hapo tumemaliza kujadili Sura au kipengele cha 2.0 cha BIASHARA/KAMPUNI, Kwahiyo tunaweza kuhamia katika kipengele kingine chochote kile kati ya vile 8. Hapa sisi kwa mfano tumeamua tuendelee tu na kipengele cha 3.0 cha BIDHAA/HUDUMA ambapo kama uonavyo kwenye mchanganuo wetu tumetaja bidhaa yetu kuu kuwa ni kuku wa nyama lakini pia tuna bidhaa nyingine ambayo ni mbolea ya kuku……

 

Kupata semina hii ikiwa kamili pamoja na mchanganuo wake wote katika lugha 2, kiswahili na kiingereza karibu kwenye mastermind group, mahali unapoweza kupata kila kitu unachohitaji kama mjasiriamali.

Wahi pia offa yetu hapo chini ya kupata vitabu vyetu vyote na michanganuo kabla haijamalizika. 


ORODHA YA VITU (ITEMS) PAPO KWA HAPO VYA OFFA KUBWA NA YA MWISHO KWA MWAKA 2021;

 

             1.     KITABU: THINK & GROW RICH – SWAHILI EDITION –kiswahili

 

             2.     KITABU: MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIANALI (New special Edition 2021) - kiswahili

 

             3.     KITABU: MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA - Kiswahili

 

              4.      KITABU: MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIYOPENDA KUITOA – kiswahili

 

             5.     KITABU: SIRI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO KWA UFANISI– kiswahili

 

             6.     KITABU mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.- kiingereza

 

             7.     Semina nzima ya siku 4 na Mchanganuo wa biashara ya ufugaji wa kuku wa Mayai kuomba mkopo benki. -kiswahili

 

             8.     Semina nzima ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji nafaka –unga wa dona(USADO Milling))-kwa kiswahili

 

             9.     Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikitimaji (KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kiswahili

 

           10.   Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) –kwa Kiswahili & kiingereza

 

           11.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya kiwanda cha tofali za sementi (KILUVYA Bricks)-kwa Kiswahili

 

           12.   Mchanganuo kamili wa Biashara ya Chipsi (AMANI CHIPS CENTRE) -kwaKiswahili

 

           13.   Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara vinayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.- Kiswahili & kiingereza

 

           14.   Mchanganuo mfupi wa biashara ya Steshenari (One page Business plan) (NEEMA STESHENARY) -kwa Kiswahili

 

           15.   Vipengele / (Outlines) vya Mpango wowote ule wa Biashara kwa kiswahili na kwakiingereza. Hata ikiwa hujui kabisa kuandika business plan unaweza kuvifuatisha ukaandika.

 

           16.   Kuungwa group la Michanganuo la mentorship mwaka mzima 2022 (MICHANGANUO-ONLINE) unaweza kuuliza swali lolote lile muda wowote kuhusu michanganuo na ujasiramali kwa ujumla

SOMA PIA NA HIZI:

0 Response to "HATUA KWA HATUA JINSI YA KUANDIKA MCHANGANUO WA BIASHARA YA KUKU WA NYAMA 2000 KUOMBA MKOPO TAASISI ZA FEDHA"

Post a Comment