CHANJO YA COVID-19 ALIYOCHANJA RAIS SAMIA SULUHU ETI SIYO YA KWELI ILIKUWA FEKI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

CHANJO YA COVID-19 ALIYOCHANJA RAIS SAMIA SULUHU ETI SIYO YA KWELI ILIKUWA FEKI?

Rais wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akichanjwa kinga ya ugonjwa wa Covid-19

..Ilikuwa ni maji siyo chanjo…

..Mbona kipindi cha Rais Magufuli tena bila hata ya chanjo Korona ilipungua haraka na haikusambaa kama sasa hivi…?

 

Kiukweli kabisa makala hii unayosoma sasa niseme wazi kabisa kwamba nimeiandika kiupendeleo (biased) kinyume kabisa na vile nilivyofundishwa katika uandishi wa habari na sababu nitaielezea.

Nimeegemea upande ule wa wanaohitaji kuchanjwa Korona kwa udi na uvumba na hata ingeliwezekana kuchanjwa mara tu baada ya Mama samia jana kuchanjwa basi ningechanjwa. Waswahili husema aisifuye mvua imemnyea, kama alivyosema Rais Mama Samia Suluhu Hassan jana wakati akifanya uzinduzi wa chanjo dhidi ya covid-19 ya Johnson & Johnson chini ya mpango wa chanjo wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wa Covax kuwa kama hujaguswa na hili janga kwenye ukoo au familia yako unaweza ukasema lolote, lakini likikugusa unajua hatari ya hili janga.

SOMA: Jinsi ya kutumia maajabu yaliyopunguza korona Tanzania kubusti uchumi wako unaosambaratika.

Binafsi mimi janga la corona limenigusa, ndugu yangu kaugua ijapokuwa amepona lakini najua wasiwasi na hekaheka ndugu na jamaa tulizopitia kwa takriban wiki zaidi ya 2 alizoumwa achilia mbali yeye mwenyewe maumivu na hali aliyopitia. Inatosha na wala sihitaji kuwa Tomaso kwa suala hili.

Ushahidi pia wa watu ninaowajua kufa kwa korona ninao lakini sina ushahidi wa mtu hata mmoja aliyefariki kwa athari za chanjo yeyote iwe ya corona au hata ya magojwa yale mengine kama polio na surua ijapokuwa tangu nikiwa shule ya chekechea uvumi wa hatari za chanjo nimekuwa nikiusikia tu mitaani na miaka yote tumekuwa tukitumia chanjo mbalimbali kutoka kwa hawahawa wazungu, iweje sumu waje watutilie kwenye hii ya corona tu? Chanjo ya korona Kenya na Uganda zimetangulia kabla yaTanzania lakini hatujasikia bado madhara ya kutisha yaliyotokea mpaka sasa hivi zaidi ya faida za chanjo ya corona zenyewe, hivyo usalama wa chanjo hii kwa kiasi kikubwa hauna mashaka kama Wizara ya Afya na shirika la afya Duniani WHO wanavyosisitiza.

Mimi siyo daktari wala sina taaluma yeyote ile ya uuguzi, lakini kama muelimishaji ninao wajibu wa kuhakikisha natoa taarifa zilizokuwa sahihi kwa jamii yangu kuhusiana na jambo lolote lile likiwemo na hili la kiafya kwa malengo ya kuwafanya watu wachukue maamuzi sahihi yanayohusu usalama na ubora wa maisha yao. Siwezi kuhubiri mafanikio ya kifedha tu peke yake huku watu wakiangamia kwa korona au magonjwa mengine yanayoweza kuzuilika kwa urahisi kabisa kisayansi.

SOMA: Aina (4) za biashara zenye kinga ya majanga vikiwemo virusi vya corona(covid-19)

Wakati Rais Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye uzinduzi wa chanjo ya covid-19 nikiwa na kisimu changu kidogo chenye redio, kama kawaida yangu nilipita mitaani nikitaka kujua kilichokuwa kikisemwa juu ya zoezi lile. Nilichogundua ni kwamba, wananchi wengi mitaani wala hawakuwa na habari, wengi walikuwa wakiendelea tu na mishemishe zao, wengine wakipiga story mitaani na kwenye vijiwe.

Watanzania tumezowea kushabikia mno habari na taarifa feki(potofu) kuliko taarifa rasmi za ukweli, tumekuwa wavivu hata kusikiliza tu taarifa ya habari redioni. Kwa hali hiyo unakuta jambo la uzushi ndilo hubebewa bango na kila mtu hata kama watu hao hawajajiridhisha kutoka katika vyanzo vya habari vya uhakika. Taarifa kama chanjo ya corona kuongeza maumbile ya kiume hata ‘ugoogle’ mitandao ya Kimataifa huwezi kukuta kitu kama hicho kutoka kwa vyanzo makini zaidi ya wazushi(Conspiracy theorists)

Katika kijiwe kimoja maeneo ya stendi ya Mbezi mwisho nilikuta kina dada fulani  wakinunua samaki mahali huku mjadala mkali ukiendelea juu ya suala la chanjo ya corona baina yao na muuza samaki. Dada mmoja alikuwa akipinga kabisa chanjo na kusema,

mimi hata waniwekee panga shingoni sichanjwi ng’o! mbona Rais Magufuli enzi zake alikataa hayo machanjo na hatukuona korona ikisambaa kama sasa hivi? Hayo machanjo Wazungu wawetuwekea humo virusi vya corona”

Sikuweza kuvumilia ikabidi nisogee karibu nijiunge na mjadala ule kwa lengo la kusahihisha kauli ile potofu.

Muuza samaki naye akadakia,

 Unafikiri Mama Samia pale amechanjwa dawa yenyewe wanayosema…...yale yalikuwa ni maji matupu, amezuga tu ili wananchi tukubali kiurahisi kuingia mtegoni…..hawezi kukubali kitu cha kumuua taratibu…….

Kifupi pale mtetezi wa chanjo nilijikuta ni mimi peke yangu, nikapata picha jinsi serikali ilivyo na kibarua kigumu kuwaelimisha wananchi wake kusafisha uwongo waliopandikiziwa vichwani mwao na wapinga chanjo. Kauli ya Hayati Rais Magufuli juu ya chanjo ya korona nakumbuka hata makala zangu za nyuma kwenye lile wimbi la pili niliwahi kuandika; TULIKOSEA WAPI TANZANIA CORONA IKARUDI TENA KWA KASI HII? Mimi sikusikia mahali Magufuli alipokataza chanjo isipokuwa serikali kujiridhisha kwanza na usalama wake jambo ambalo leo kweli limetekelezwa, rejea makala hiyo utafahamu ukweli wa mambo ulivyo.

Siku hizi kutokana na karibu kila mtu mwenye simu ya mkononi na akaunti ya mtandao wa kijamii kuwa “mwandishi wa habari”, kutofautisha taarifa potofu na zile za ukweli limekuwa ni jambo gumu hasa kwa watu wa kawaida wasiokuwa na taaluma ya uanahabari.

Na taarifa potofu zisizokuwa na uthibitisho wowote huwa zinazidi kupata nguvu kwa wananchi wa kawaida pale zinaposhadidiwa na baadhi ya watu kwenye jamii ambao kutokana na dhamana au nyadhifa fulani walizonazo, wanaaminika kirahisi na kwa kiasi kikubwa na makundi makubwa ya watu. Watu hao wanaweza wakawa Wanasiasa wenye ushawishi, viongozi wa dini(dini zote kuu, Uislamu, Ukristo, na Dini za kienyeji), Wasanii na Wanamichezo.

Watu hao maarufu wanaweza wakapotosha jambo si kama hawajui kuwa wanapotosha hapana, wanajua fika lakini wanafanya hivyo kutokana na maslahi fulani ambayo wanajua kabisa wafuasi wao au wale wanaowashabikia wakiujua ukweli basi kwa namna moja ama nyingine wanaweza wakapunguza ufuasi au kiwango cha kuwaamini kutokana na sababu kwamba msingi mkuu wa ufuasi wao umesimama katika taarifa au mambo potofu waliyowahi kuwaaminisha hapo kabla.

SOMA: Puuza Imani na dhana hizi potofu ufanikiwe katika biashara yako ya duka la vyakula

Kwa mfano kiongozi wa dini ambaye wafuasi wake wengi amewapata kwa njia za kuwahadaa na miujiza mbalimbali feki mfano uwezo wa kutibu, kufufua wafu, misukule nk. kiongozi kama huyo katu hawezi kukubali wafuasi wake waambiwe ukweli katika jambo lolote ambalo ameshawaaminisha kuwa yeye ana uwezo wa kulitatua.

Baadhi ya viongozi wa dini kwenye janga kama hili la korona hutafuta kila aina ya fursa ya kunufaika nalo, na kwa sababu korona ni ugonjwa hatari unaoua haraka hamna namna mhubiri au mganga wa jadi anaweza akapata nafasi ya kuwahadaa waumini wake kuwa ana uwezo wowote wa kusaidia, kinachobakia sasa unakuta mtu anaanza kutapatapa, mara ..ooo… chancho haifai, …..chanjo ya corona ina madhara makubwa…, masuala sijui ya namba 666…, sijui vinasaba vya mwili kubadilika….. na mambo kibao yanayofanana na hayo yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

Ndio maana utakuta sasa hivi kuna wimbi kubwa la watu kama hao wanaojitangaza kuponyesha ukimwi na magojwa hatari kama kansa na kisukari kwa kuwa wanajua fika magojwa haya kwanza mgojwa hawezi kufa mara moja na kuna dawa za kufubaza nk. Wewe subiri korona chanjo ifanye kazi vizuri, utawaona tu wajanja hawa wakiibuka na kuanza kujitangaza kuwa hata korona wanatibu wakitumia mgongo na fursa ya ugonjwa huo kupunguzwa makali na chanjo, utasikia tu shuhuda kibao watu wakidai oo…, “mimi niliugua korona lakini baada ya kuja kwa nabii/mtaalamu/ustaath/mganga/mtume/ Askofu fulani. sasa nimepona kabisa

SOMA: Jinsi ya kutambua na kuacha fikra hasi ulizonazo juu ya pesa zinazokurudisha nyuma usifanikiwe

Kwa hiyo ukiona kiongozi au mtu mwenye ushawishi katika jamii akitumia nguvu nyingi sana kupinga jambo la kisayansi kama hili la chanjo ya korona bila ya kuonyesha njia yeyote ile mbadala ya kukabiliana nalo zaidi ya kudai watu wamtegemee Mungu peke yake, malimao na kufukiza wakati Mungu mwenyewe ndiye aliyeweka wataalamu ili wawatibu watu wake, basi ujue kiongozi au mtu huyo anacho hofia ni hatima yake(legitimacy) Anajua fika watu aliozowea kuwaaminisha kuwa yeye ndiye dawa ya matatizo yao yote sasa watamdharau baada ya kuona kwenye korona hawezi kuwakinga wala hawezi tena kutengeneza shuhuda za uwongo kuwahadaa.

Ni nani atakayekubali tena kuwa Nabii/Askofu/Mganga/Shehe/Padre au Mtume anaweza kuondoa korona ilihali chanjo tayari imeshakubalika ndiyo suluhisho la korona? Baadhi yao hata wamefikia hatua ya kuchukua nafasi ya ukuu wa Mungu kwa mfano utasikia baadhi ya waumini au wafuasi wakitaja maneno kama vile, “Mungu wa Nabii/Mtume/Askofu fulani” wakiwa na maana kwamba kiongozi wao huyo anaye Mungu wake spesho tofauti na Mungu yule wa watu wote aliyeumba kila kitu.

SOMA: Dhana potofu ya ushirikina ni hatari kushinda ushirikina wenyewe

Kwa hali kama hii utagundua kabisa kwamba kiasi kiongozi huyu alivyowakamata wafuasi wake(brainwash) kwa kauli mbalimbali za kizushi hawawezi kuchomoka hata kidogo pindi atakapowaagiza jambo lolote lile hata kama liwe ni la hatari na la kuwaangamiza kama alivyofanya Kibwetere kule Uganda.

Umefika wakati sasa watu makini kuwaeleza ukweli watu hawa ambao wengine wanajificha kwenye koti la Dini au Utumishi wa Mungu huku wakiwatisha wale wanaowaeleza ukweli eti watapata laana ya Mungu kwani wanakufuru. Na Wafuasi wengi kweli wanakubaliana nao kwa kuwa Imani huwa hazina kawaida ya kuhojiwa. Ukihoji unaambiwa wewe utaishia motoni, utapata laana, utakufa, nk. Hebu jiulize mbona hao viongozi na wao pia huwa wanakufa na kupata matatizo sawa tu na watu wengine wa kawaida?

Uvumi na taarifa zenye utata(Conspiracies) nchi hii, nyingi huwa zinaanzia kwenye imani mbalimbali,  za kidini na hata za kijadi pia. Simaanishi ni imani hizo kwa ujumla wake hapana bali baadhi tu ya vikundi au madhehebu machache. Kwa mfano madhehebu mengi ya dini wanaendesha mambo yao kwa kuzingatia ukweli pasipo mambo ya kuhadaa hadaa waumini. Kinachofanya baadhi watumie mbinu chafu za udanganyifu ni suala zima la kutaka wafuasi wengi. Hakuna tofauti na biashara, ili dhehebu, kikundi, au mganga apate wafuasi, kunahitajika mbinu mbalimbali za kimasoko zikiwemo na hizo mbinu feki.

Mbinu kubwa inayotumika 

Motivational Speeches(Kauli za kushawishi), hapa ieleweke sipigi vita motivational Speakers kwani na mimi pia nimo katika kundi hilohilo kama Motivational writer(mwandishi mshawishi). Kushawishi siyo jambo baya hata kidogo lakini jambo hili linapotumiwa vibaya kama vile kwenye masuala ya kitaaluma kama vile utabibu, sheria na uandishi habari, linaweza likaleta madhara makubwa na ndio maana utakuta katika taaluma nyingi wamezuia sana maswala haya ya kushawishishawishi ovyo au kujitangaza kwa kuwa wanafahamu fika madhara yake.

SOMA: Je, biashara ya kilimo cha matikitimaji ni hadithi zilezile za mayai ya kware, sungura na kuku?

Kwa mfano hata kwenye uandishi wa habari ni tofauti sana na uandishi wa kawaida wa kushawishi, wenyewe msingi wake upo katika ukweli zaidi(facts) kuliko utiaji chumvi na ushawishi.

Sasa wahubiri wengi na watu wenye ushawishi kwenye jamii hupata wafuasi wao kwa njia hii ya ushawishi pasipo kuzingatia kile wanachoshawishi kama kina ukweli kiasi gani. Imani iwe na ukweli au isiwe haijalishi, ilimradi imeshaitwa ni imani na haina madhara ya moja kwa moja kwa watu.

Mambo yahusuyo imani mtu usipokuwa makini unaweza ukajikuta unayumbishwa kama kishada, badala ya kumwabudu na kumsujudia Mungu asiyekuwa na mfano utajikuta ukiwasujudia binadamu wenzako waliozaliwa kama wewe, wenye shida kama za kwako na watakaokufa kama wewe, kisa tu wenzako hao ni motivational speakers wanaojua kushawishi na kutumia mbimu mbalimbali za kimasoko kukuhadaa na kukuchota kisaikolojia kwa maslahi yao wenyewe binafsi ya kiuchumi, kijamii  au kisiasa.

Chanjo ya corona Uingereza, Marekani na nchi nyingine mbalimbali imeonyesha mafanikio makubwa, wanaokufa kwa korona katika Mataifa hayo sasa hivi ni wale tu ambao bado hawajachanja aidha kwa ukaidi kama huu tunaoushuhudia hapa Tanzania au tu pengine kwa kutokufikiwa na vyombo husika vinavyohusika na chanjo hizo.

SOMA: Kwanini chanjo ya malaria imekuwa ngumu hivyokupatikana?

Akikuhubiria mtu yeyote eti chanjo ya covid-19 haifai inaua naomba umfungulie habari ya muumini huyu wa dhehebu fulani la dini aliyekuwa akipinga sana chanjo ya korona lakini akaja kujutia ukaidi wake dakika za mwisho alipokuwa akipigania uhai wake kwenye mtungi wa gesi ya oksijeni dakika chache kabla hajakata roho kwa covid-19 huku akiwaomba wafuasi wake kumuombea apone bila mafanikio.

Tanzania imepokea chanjo zipatazo milioni moja aina ya Johnson, taarifa kuhusu korona duniani zinasema kwamba kuna aina nyinginezo za chanjo mbali na Johnson Jansen kama vile chanjo za Pfizer, Moderna, Novavax, Sinovac,  AstraZenecaSputnik ya urusi na nyingine zilizo kwenye majaribio.

Wataalamu wanapendekeza chanjo hizi kwa mtu yeyote wa umri juu ya miaka 12 na wanasisitiza kwamba aina bora zaidi ya chanjo kwa mtu ni ile inayopatikana kwake kwa wakati muafaka, usije eti ukakaa ukisubiria aina fulani ya chanjo ambayo bado haijafika ulipo kwani aina zote zilizoidhinishwa na Shirika la WHO zote ni salama, zilizo na ufanisi wa kukabiliana na aina mpya ya virusi vya corona (Delta variant) na zinazopunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuugua corona ile kali inayoweza kuondoa uhai wako.

"Chanjo" yangu binafsi, haikupendekezwa na WHO wala Wizara ya Afya lakini inafanya kazi pia  

Leo hii Kuna dawa moja kubwa sana nitakayoipendekeza kwako kama kinga ya kukuzuia usiyumbishwe wala kubabaishwa na wajanja wanaotumia vivuli vya imani mbalimbali ziwe za kidini au zile za kijadi. Dawa hiyo ni maarifa sahihi ya kujitambua, Kujitambuni ni kinga ya magojwa mengi hata zaidi ya corona, na maarifa sahihi unaweza ukayapata mahali popote na kwa mtu yeyote lakini napendekeza kuyapata kutoka katika kitabu kimoja mashuhuri kiitwacho THINK AND GROW RICH (FIKIRI NA UTAJIRIKE)

SOMA: Jinsi ya kununua kitabu cha Think & Grow Rich-swahili edition katika mtandao wa Getvalue

Kitabu hiki kina sura maalumu ya IMANI, hapa utajifunza jinsi imani mbalimbali duniani zinavyofanya kazi kuanzia dini zote kubwa mpaka zile za kienyeji, athari zake na namna mtu unatakiwa kuzichukulia. Imani hasa za dini zile rasmi zina mambo mazuri sana zikitumika vizuri kama waanzilishi wake walivyokusudia, lakini zinapotumiwa kinyume chake hazina tofauti na bomu la nyuklia.

……………………….

 

JINSI YA KUKIPATA KITABU HIKI KATIKA LUGHA YA KISWAHILI

NAKALA YA KITABU HALISI CHA KARATASI (HARDCOPY)

Kinapatikana FUTURE BRIGHT BOOKS AND STATIONERY iliyopo Mbezi ya Kimara. Barabara ya Morogoro ukipita njia ya Kibanda cha mkaa kwa bajaji shuka kituoni kwa MOTA. Ukipita njia ya Temboni shuka Kanisa la KKKT Mji mpya au Sekondari ya St. Augustine(TAGASTE) uliza kituo cha kwa MOTA kilipo. Bei ya kitabu dukani ni sh. 20,000/=

Tuna huduma ya kukuletea ulipo(Delivery) ikiwa upo Dar es salaam ila gharama ya daladala sh. Elfu mbili huongezeka.

Mikoani, mkoa wowote Tanzania Bara na Zanzibar tunatuma kwa njia ya basi au boti lakini pia gharama za usafiri zitaongezeka na hutegemea aina ya basi lakini mara nyingi huwa ni sh. Elfu 10.   

 

NAKALA YA KITABU PEPE(SOFTCOPY)

Unaweza kukinunua kitabu hiki mara moja(instantly) kwenye simu-janja yako kupitia mtandao uitwao GETVALUE kwa kupitia kiungo/link ifuatayo hapo chini, lakini kabla hujanunua ni vizuri kwanza ukapitia kidogo video hii inayoelezea jinsi ya kununua kitabu kutoka mtandao wa Getvalue.   

THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION 2021(TAFSIRI ORIJINO YA MWAKA 1937 NA NAPOLEON HILL)

Bei ya nakala tete ni shilingi elfu kumi na tano (15,000/=)

 

KWA MAWASILIANO  YA SIMU AU WATSAP TUMIA NAMBA HIZI: 0765553030 au 0712202244

0 Response to "CHANJO YA COVID-19 ALIYOCHANJA RAIS SAMIA SULUHU ETI SIYO YA KWELI ILIKUWA FEKI?"

Post a Comment