JINSI YA KUTAMBUA NA KUACHA FIKRA HASI ULIZONAZO JUU YA PESA ZINAZOKURUDISHA NYUMA USIFANIKIWE. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JINSI YA KUTAMBUA NA KUACHA FIKRA HASI ULIZONAZO JUU YA PESA ZINAZOKURUDISHA NYUMA USIFANIKIWE.


PAKA ANAYEDHANIWA CHUMA ULETE
Katika jamii zetu nyingi za kiafrika suala la pesa limewekewa miiko na imani nyingi hasi(mbaya) kuliko hata ilivyo kwa suala la mapenzi na kujamiiana. Wakati huohuo mada ya pesa ndiyo inayoongoza kujadiliwa kwa hisia na mihemko. Unaonekana mtu wa ajabu sana au hata mwanga kisa tu umetaka kujua mshahara mtu anaopata au faida anayoingiza kwenye biashara yake.

Mihemko hasi ya pesa ni mibaya kiasi hata cha kukosanisha ndugu wa damu, ukimkopa ndugu yako halafu usimlipe mnaweza msiongee tena maisha yenu yote nk. Kutokana na tabia hiyo ya pesa basi watu na jamii nyingi zimejijengea fikra mbalimbali juu ya pesa na nyingi zikiwa ni hasi zisizokuwa na tija yeyote ile zaidi ya maumivu na umasikini mkubwa.

SOMA: Puuza imani hizi na dhana potofu ulizokuwa nazo ufanikiwe katika biashara yako ya duka la vyakula.

Pesa huhusishwa na hisia nyingi nzuri na mbaya kama vile hisia za chuki, wivu, ushirikina, mapenzi na kujitoa sadaka. Kwa waliokuwa wengi fedha na kila kitu kinachohusiana nazo huchochea hisia kali za ndani kabisa.

Hisia hizo chanzo chake ni nini?
Mara nyingi imani/fikra hizi wala siyo za kwetu, zimepandikizwa ndani yetu na jamii tunamoishi kwa kujifunza kutoka kwa wazazi, walezi na wale tunaoishi nao na kwa kupitia hata mifumo rasmi ya elimu iliyopo tokea mtoto anapozaliwa mpaka utu uzima.

SOMA: Imani ndoto na kujiamini.

Imani hizo au fikra kama nilivyotangulia kusema zipo nyingi sana na kuna zile zilizokuwa mbaya(hasi) na nyingine pia zipo chanya(nzuri). Lakini kwa muktadha wa makala hii napenda nitilie mkazo zaidi zile fikra na imani hasi  juu ya pesa. Imani hizi watu wanapozitaja huona kama wanazungumzia tu mambo ya kawaida lakini kisaikolojia zina athari kubwa sana kwa mustakabali wa watu hao kifedha na maisha yao kwa ujumla.

Unaweza kumsikia mtu katika mazungumzo ya kawaida tu akisema, “Haiwezekani mtu kufanikiwa kwenye kazi ya ajira bila kumwibia mwajiri wake” Kauli kama hii mtoto kwa mfano anapoiingiza akilini, maisha yake yote atakua akiwa na imani hiyo na hata atakapokuja kuajiriwa hataamini kabisa kufanikiwa bila kuiba. Sasa mtoto huyo asipokuja kuifuta fikra hiyo akilini kwake kwa kutumia njia tunayokwenda kuonyesha hapa hataweza kamwe kuja kupata maendeleo angali katika ajira.

SOMA: Fedha zako hupotelea wapi kila siku? fahamu uchukue hatua haraka.

Usishangae sana vitendo vingi unavyosikia kila siku watu wakisema ni imani za kishirikina mfano mauaji ya watoto wadogo, vikongwe na walemavu wa ngozi(Albino), haya ni matokeo ya imani na fikra za watu na jamii mbalimbali juu ya pesa na wala ushirikina au uchawi hapo hauna lolote la kufanya, husingiziwa tu.

Imani kwa mfano matajiri wengi hufanikiwa baada ya kwenda kwa waganga wa jadi na stori kibao zinazofanana na hizo, vyanzo vyake utakuta ni masimulizi tu ya vijiweni, majumbani, mashuleni, vyuoni na hadithi zinazorithishwa kutoka vizazi hata vizazi. Wengine hata huona kwenye michezo ya kuigiza katika video na TV na kutokana na upeo mdogo wao huchukulia kuwa ni kweli.




Kwa mfano tu umkamate mtu anayesimulia mambo hayo umwambie sasa hebu nipeleke kwa mganga anayetoa dawa hizo za utajiri, atababaika na kuishia kukuambia, ooo.. nilisikia….  sijui niliambiwa na fulani, lakini ukweli hawezi kukuonyesha dhahiri zaidi ya kuwa na imani hiyo katika akili yake ambapo naye atamrithisha kama si mwanawe basi mtu mwingine yeyote yule katika jamii anayoishi.

Mfano mwingine ni imani za chuma ulete, kutokana na ugumu wa maisha na pesa kupatikana kwa shida, mtu anashindwa kuamini kama mapato yake ni madogo anaishia kutafuta visingizio rahisi kama vile chuma ulete. Imani hii humfanya mfanyabiashara kuishi kwa wasiwasi mkubwa huku akiwatuhumu karibu kila mteja anayemhisi anaweza kuwa chuma ulete. Ataonyesha tabia za ajabuajabu kama vile kuweka pesa ya mtu anayemtuhumu pembeni mbali na droo aliyozoea kuweka pesa, kuzisalia pesa hizo au kuzifukizia vitu kama udi au maji ya upako(Baraka) kwa imani ya kuvunja roho ya chumaulete nk.

SOMA: Njia 7 halali na nzuri za kupata mafanikio na utajiri wa haraka.

Tabia na fikra hizi hasi hazitokani tu na imani za kienyeji peke yake, bali nyingine pia chanzo chake ni imani za dini tunazoabudu, kwa mfano kuna watu katika dini hizihizi kuu wanaoamini kwamba Mungu hapendezwi na watu kupata utajiri na mafanikio makubwa, imani hii huwafanya watu hao kushindwa kusonga mbele kiuchumi bila ya kujijua.

Hata kuna kauli yingine kama hizi, Huwezi ukanunua furaha kwa pesaNi rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia peponi nk.” hizi si fikra nzuri hata kidogo kwani muda wote utakuwa ukiichukia fedha kwa madai kuwa hazina uwezo wa kukuletea furaha. Sasa hebu jiulize umasikini au kutokuwa na fedha ndiko kutakupa furaha?

UTAZITAMBUA VIPI IMANI NA FIKRA HASI ULIZOKUWA NAZO NDANI YA AKILI YAKO YA NDANI?

Usipokuwa makini hutaweza kuzitambua kabisa kwani ni vitu vinavyojichimbia ndani ya ufahamu wa mtu wa ndani kabisa(subconscious mind). Na kumbuka ndizo zinazoamua hali ya baadae ya kifedha ya mtu, awe masikini au tajiri. Bila ya kujali kama mtu anaingiza pesa  kiasi gani kwa sasa, hata ziwe nyingi vipi lakini ikiwa anazo fikra hasi ndani yake mwisho wake ni umasikini kwa kuwa muda wote yeye fikra na imani zake zinakinzana na mafanikio anayoyatafuta na tayari anayo sababu ya kutokupata pesa.

SOMA: Imani, mapenzi na ngono ndiyo vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa.

Hii ndiyo sababu ni muhimu sana mtu kutambua mapema vile vitu vinavyokufanya ujione una hatia juu ya pesa, jinsi vitu hivyo vinavyoathiri maamuzi yako kwenye kutafuta pesa na katika maisha kwa ujumla halafu uchukue hatua mara moja.

Sasa naomba uchukue kalamu na karatasi.
1.  Andika imani na fikra zako zote juu ya pesa na utajiri.

2.  Andika fikra a mitazamo yote uliyofundishwa na wazazi wako au walezi ulipokuwa mtoto mdogo kuhusiana na pesa na watu matajiri au waliofanikiwa kifedha.

3.  Hebu jiulize, mazingira uliyokulia, nyumbani, shuleni, chuoni, marafiki, watu, jamii nk. yanahusiana vipi na pesa na watu matajiri?

4.  Hebu jiulize, mazingira unayoishi sasa hivi yanahusiana vipi na pesa na watu matajiri au waliofanikiwa kifedha?

Katika hayo mambo manne andika chochote kile kinachokuja akilini kuhusiana navyo. Baada ya kumaliza orodha hiyo utakuta kuna kauli nyingine hata zinakinzana wewe usijali, zitafakari kwa umakini na ikiwezekana mshirikishe mtu mwingine wa karibu. Ukiichunguza orodha hiyo kwa umakini utagundua vitu vingi na utakuwa na uwezo sasa wa kuamua kwa hiyari yako mwenyewe kubadilisha fikra na mitazamo hiyo hasi juu ya pesa iliyokuwa ikikurudisha nyuma kiuchumi.

....................................................................... 


Ndugu msomaji wa blogu hii ya jifunzeujasiriamali, napenda kukutaarifu kwamba vitabu vyetu 3 vifuatavyo  vinapatikana katika mtindo wa Hardcopy na pia softcopy Ukihitaji hardcopy kama upo Dar tunakuletea ulipo, mikoani tunatuma kwa mabasi lakini gharama kidogo ya basi huongezeka. 

Kwa upande wa softcopy tunatuma kwa njia ya email katika simu au kompyuta yako.
Hardcopy sh.22,000  Dar
        Softcopy sh.10,000 popote



Hardcopy sh.12,000
Softcopy sh. 5,000


Hardcopy sh.5,000
Softcopy sh. 3,000

Ukinunua vyote 3 softcopy au hicho cha kwanza na kimoja kati ya hivyo 2 unapata offa yetu kubwa ya masomo na vitabu vifuatavyo pamoja na kujiunga na group la masomo ya kila siku la michanganuo-online kama ukipenda;


1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.      Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.      Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.      Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.


0 Response to "JINSI YA KUTAMBUA NA KUACHA FIKRA HASI ULIZONAZO JUU YA PESA ZINAZOKURUDISHA NYUMA USIFANIKIWE."

Post a Comment