Sura ya 3.
Hatua ya 2 Kuelekea mafanikio.
Akili ya binadamu (mind) imegawanyika katika sehemu mbili, upande mmoja
unahusika na mawazo au hisia za ndani (Subconcious mind) na wa pili (conscious
mind) eneo linalohusika na hisia za kawaida zinazotokana na ile milango mitano
ya fahamu yaani, masikio, pua, macho, ngozi na ulimi. Mawazo ya
ndani kazi yake ni kupokea
taarifa kutoka mawazo ya nje na kuzifanyia kazi. Taarifa hizo zinapokaa muda mrefu ndani ya mawazo ya ndani ndipo hutafsiriwa
kuwa kitu halisi, kwa mfano ukiwaza kupata kitu fulani, ukanuwia kwa muda mrefu
matokeo yake mawazo ya ndani yatakufanya kila unachokifanya uelekeze nguvu
katika kutimiza lengo hilo na hatima
yake jambo hilo hutokea kuwa kweli. Ukinuwia kuumwa ugonjwa fulani, hutokea
kuwa kweli, ukinuwia kuwa iko siku utaua, uwezekano wa kuja kuua mtu kweli huwa
mkubwa nk.
Na hiki ndicho hutokea katika
imani zote duniani, iwe ni za dini au mila hata uchawi. Kuna nguvu isiyoshikika
yenye uwezo wa kuwasiliana na akili ya
ndani kwa kila mwanadamu, nguvu hiyo kuu
wengi husema ndiyo Mungu na wengine
hudai ni nguvu tu isiyokuwa ya kawaida.(Super Natural Force)
Kwa hiyo katika akili zetu haijalishi ni mawazo ya aina gani, mazuri au
mabaya tunayofikiri, yanaporudiwa rudiwa na kukaa muda
mrefu akilini matokeo yake hutengeneza kitu halisi. Hivyo unaweza ukanufaika
kwa kuingiza akilini mwako mawazo mazuri
kama ya kujipatia utajiri na mwishowe ukatajirika kweli. Ndiyo mana katika sura hii mwandishi anashauri kuwa unapokuwa na wazo lolote la kupata utajiri au
mpango, basi andika mahali na kisha uwe unafanya
marudio kila mara kwa sauti mpaka mawimbi ya sauti hiyo yatakapofikia katika
akili yako ya ndani.
Ushahidi wa suala hili la imani unaweza ukaupata kutoka maeneo
mengi, kwa mfano watu mashuhuri
kama Mahatna Ghandi wa India,
hakuwa na chochote zaidi ya imani ambayo
mwishowe ilimfanya kuwa rais wa Taifa hilo, Yesu Kristo kwa imani aliamuru maji
ya bahari kupisha watu wakatembea juu yake. Mtume Muhamad aliweza, kwa imani kuwaunganisha
mamilioni ya watu kumfuata na inasema kama pia huko Mashariki ya mbali wapo watu wenye imani ya Kibudha walio na
uwezo wa kupasua vitu vigumu ajabu kwa kutumia vichwa vyao. Hii yote ni kutokana
na Imani.
0 Response to "SURA YA TATU, THINK AND GROW RICH KWA UFUPI, IMANI NDOTO NA KUJIAMINI."
Post a Comment