THINK & GROW RICH: MAPITIO NA UCHAMBUZI SAHIHI SURA YA NNE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

THINK & GROW RICH: MAPITIO NA UCHAMBUZI SAHIHI SURA YA NNE


SURA  YA  4.
KUJISHAURI (Njia  ya kusisimua mawazo ya ndani.)
Hatua ya 3 kuufikia utajiri.

Kujishauri binafsi (Autosuggestion) ni neno linalomaanisha ushauri, mawazo  au pendekezo lolote mtu  analojipa mwenyewe ndani ya akili yake. Akili ya kila mtu  inao uwezo wa kudhibiti kile kinachoingia katika mawazo/akili ya ndani kupitia akili ya nje (milango  5 ya fahamu) ni kama vile lilivyokuwa shamba, ikiwa utaotesha mbegu za mazao mazuri, pia utavuna mazoa mazuri na ukiamua kuacha vitu vijiotee vyenyewe tu utavuna magugu na miiba. Hali kadhalika na akili yako ya ndani(Subconscious mind). Kwa kutumia utaalamu huu wa kujishauri mwenyewe mambo yaliyokuwa mema au chanya, ukichanganya na viungo vinginevyo vilivyokwishatajwa hapo awali, shauku, imani na uvumilivu, ni lazima utafanikiwa katika lengo lolote unalojiwekea.




>>>Geuka nyuma sura iliyopita<<<<<                            


0 Response to "THINK & GROW RICH: MAPITIO NA UCHAMBUZI SAHIHI SURA YA NNE"

Post a Comment