JE, IPO KANUNI YA MAFANIKIO YA KIFEDHA?: MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

JE, IPO KANUNI YA MAFANIKIO YA KIFEDHA?: MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA

Kanuni ya mafanikio ya kifedha

Bila shaka duniani hakuna mtu ambaye hajawahi kukumbana na tatizo la kifedha  angalau mara moja. Lakini unafikiria ingelikuwaje ikiwa matatizo hayo yasingelikuwa na mwisho na hata ujaribu vipi kuyatatua huwezi kurekebisha chochote? Basi leo katika somo letu hili tunakwenda kupata majibu ya maswali hayo lakini katika mtizamo wa kisaikolojia zaidi.

Saikolojia ya pesa ni moja kati ya matawi ya saikolojia inayoshughulika na tabia za watu kwenye fedha pamoja na athari za fedha kwenye haiba ya mtu. Tawi hili lina uhusiano wa karibu na uchumi.

SOMA: Kuvalia vizuri huongeza kipato

Saikolojia ya pesa itadumu katika maisha yetu muda wote ilimradi tu kuna mzunguko wa fedha miongoni mwa jamii inayozunguka na pia kuna kipimo cha fedha katika kila huduma na bidhaa zinazozalishwa. Fedha na binadamu ni vitu viwili vinavyotegemeana na hakuna kimoja kati yake kinachoweza kujidai kuishi bila mwenzake. Pesa bila ya binadamu ni makaratasi matupu yasiyo na thamani yeyote ile na binadamu naye bila pesa hawezi kujenga mahusiano yake ya kawaida ya kibiashara na binadamu wenzake.

Je, inawezekana kwa kiasi fulani kufahamu chanzo cha matatizo ya kifedha na kwa kiasi fulani kuweza kuyatatua?

Kitu kikubwa tunachojifunza kwenye saikolojia ya pesa ni tabia ya binadamu kwenye fedha, kila mtu huichukulia pesa tofauti na mwenzake na kila mtu anaweza akaielezea pesa kwa namna tofauti anavyoichukulia mwenyewe. Mzunguko wa fedha kwa mtu yeyote yule unategemea uwepo kwa kiasi fulani cha uwajibikaji hasahasa katika eneo la elimu ya fedha. Pasipo kujifunza vizuri jinsi ya kusimamia mtiririko wa fedha na mali zako ni vigumu sana kuviondoa vyanzo vya matatizo ya kifedha. Pesa zinahitaji uwajibikaji, utulivu, usimamizi na uthibiti. Lakini mambo hayo yote mtu huwezi kuyatekeleza ikiwa kama hujajijengea aina fulanifulani ya tabia.

Ni tabia zipi unazozihitaji ili kutokomeza matatizo ya kifedha na uwe mtu uliyefanikiwa?

Unahitaji kuishi tabia za kitajiri lakini pia usije ukasahau, kila mtu anao uelewa wake mwenyewe kwenye dhana nzima ya Mafanikio sawasawa na kama ilivyokuwa kwenye dhana ya pesa kama tulivyoona hapo juu. Kwa baadhi ya watu kuwa na milioni kadhaa kwenye akaunti ya benki kwao ndio kilele chao cha mafanikio, Wengine kilele  cha mafanikio kipo katika maendeleo yao ya kiroho.

SOMA: Jinsi ya kupanga malengo ya biashara au maisha yanayotimizika kwa ufanisi

Hivyo usijilinganishe na watu wengine  linapokuja suala la mafanikio. Isitoshe wala hatuwezi kujua kwa yakini ni njia ipi ya maisha  mtu aliyopitia  katika kufanikisha hili au lile maishani. Fuata ndoto zako, malengo yako na katu usiige malengo na ndoto za mtu mwingine huku ukidumisha tabia zote za kitajiri tunazokwenda kujifunza leo kwa matokeo bora zaidi. Iga tabia zao lakini siyo njia walizotumia kutajirika utapotea. Tabia ndiyo kila kitu kwenye mafanikio ya jambo lolote lile maishani.

Kuna ukweli watu waliofanikiwa kifedha wana fikra tofauti – zile zijulikanazo kama tabia za kitajiri?

Ukweli upo asilimia 100%, ingawa mitazamo ya watu kwenye pesa na namna wanavyofikiri juu yake ni tofauti sana. Na mara nyingi fikra na tabia hizi zinaweza kurithishwa katika familia kutoka kizazi kimoja hadi kingine, Ni muhimu kutambua kwamba kila mtu yuko peke yake na kile kinachofanya kazi vizuri kwa mtu mmoja kinaweza kisifanye vizuri kwa mwingine. Ni ukweli kuna tabia za kitajiri ambazo mtu yeyote yule akiamua kuziishi na kuziweka katika vitendo hamna shaka yeyote kwamba siku moja atapata utajiri, mafanikio na furaha maishani. Mtu unapofanikiwa kuzifahamu tabia za kitajirii ni nusu ya kuigundua kanuni kuu ya kupata mafanikio ya kifedha.

SOMA: Hatua 6 + kanuni ya kuingiza kiasi chochote cha pesa unazotaka maishani 

Baba wa vitabu vyote vya mafanikio duniani, THINK & GROW RICH katika sehemu mbalimbali za kitabu hicho mashuhuri zaidi mwandishi wake Napoleon hill amezitaja tabia zote za kitajiri na katika makala hii ya leo pamoja na kwamba nitakutajia baadhi ya tabia za kitajiri(kama 12  zile muhimu zaidi) lakini pia nitakutajia kurasa ambazo unaweza kujifunza kwa kina zaidi tabia nyinginezo. Nitatumia kitabu hicho katika toleo la Kiswahili sanifu la mwaka 2021 lakini kikiwa ni tafsiri orijino ya lile toleo mama la mwaka 1937 lililoandikwa na Napoleon Hill mwenyewe.

Ingawa tabia za kitajiri zipo, lakini kwa kweli ni lazima tabia hizo ziende sambamba na mpango mzuri na usimamizi thabiti wa fedha zako. Tabia hizo mtu yeyote yule anaweza akajifunza na kuzifanyia kazi kama nilivyotangulia kusema pia kwamba zinaweza zikarithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kama wafanyavyo baadhi ya makabila.

SOMA: Ili ufanikiwe kuwa tajiri mkubwa jiepushe kabisa na kauli hizi nne (4)

Watu wengi tunaposikia kuna tabia za kitajiri ambazo mtu ukiziishi kila siku  hatimaye unapata utajiri, mafanikio na furaha tunaweza tukadhani labda ni tabia ngeni kabisa ambazo sisi ndio mara yetu ya kwanza kabisa kuzisikia masikioni. Mimi kwa mfano ni mpaka baada ya kukisoma vizuri kitabu cha Think and Grow Rich(Fikiri na Utajirike) ndipo nilipogundua kumbe tabia zenyewe ni zilezile za kawaida tunazohimizwa hata katika maisha tu ya kawaida tuziishi.

Tabia na mienendo yote inayosaidia mtu kupata pesa, kuzisimamia fedha zake vizuri hasa katika upande wa matumizi, kuweka akiba na uwekezaji kwenye miradi ya faida zinaingia katika kundi la tabia za kitajiri. Tabia tunazozizungumzia hapa ni tabia zote nzuri zinazosaidia mtu kupata epesa, kuzisimamia na hatimaye kumfikisha kwenye uhuru kamili wa kifedha.

SOMA: Utajuaje kama umeufikia uhuru kamili wa kifedha? Kanuni hii hapa

Kuingia kwenye matatizo ya kifedha siyo mwisho wa dunia na wala usikatishe uhai wako bure, ipo njia unaweza kutoka kwa kubadili tabia kutoka zile zinazokuzuia usipate pesa kwenda zile zinazokupeleka kwenye kupata pesa kama hizi tutakazoelezea hapa

Sitapoteza muda mwingi zaidi hebu kwanza nizitaje moja baada ya nyingine;

1. Haiba nzuri

Utaniambia haiba inahusiana vipi na kupata pesa?

Haiba nzuri(muonekano nadhifu )-kama tabia niliyochagua ya kwanza kabisa miongoni mwa nyinginezo nyingi, ndiyo inayoamua mwajiriwa alipwe kiasi gani, mfanyabiashara alipwe kiasi gani nk. Haiba njema maana yake ni pana na inajumuisha vitu vingi ndani yake na wala siyo muonekano tu, hata vaa yako, namna unavyowasiliana na watu, ongea yako, ‘body language’ nk. vyote huingia katika haiba yako.

Motivational speakers na writers wengi wanatilia sana mkazo tabia hii kwamba ndio msingi mkubwa wa mtu kufanikiwa. Huwezi kumuuzia mtu kitu kirahisi ikiwa huna haiba nzuri kama wasemavyo wazungu, “First impression matters!” Ndani ya Fikiri na Utajirike haiba imezungumziwa mahali pengi ikiwemo uk. 96 sura ya Tatu “IMANI”........................................

...................

Somo hili kamili unaweza kulidownload ndani ya Channel ya MASTERMIND GROUP la MICHANGANUO-ONLINE pamoja na masomo mengine adimu ya fedha zaidi ya 70 yasiyopatikana mahali kwingine kokote. Kujiunga na group, lipia kiingilio cha mwaka mzima(miezi 12 tokea siku ya kujiunga) sh. 10,000/= tu kisha tuma ujumbe ukisema; niunganishe na mastermind group-2021" Nitakuunganisha na group na channel pia kukutumia vitabu na michanganuo huku ukipata masomo mapya na semina kwa miezi yote 12 bila ya gharama za ziada au zilizojificha. 

0 Response to "JE, IPO KANUNI YA MAFANIKIO YA KIFEDHA?: MTAZAMO WA KISAIKOLOJIA"

Post a Comment