KUVALIA VIZURI HUONGEZA KIPATO. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUVALIA VIZURI HUONGEZA KIPATO.

Muonekano mzuri kimavazi na haiba, kwa Kiswahili kisichokuwa rasmi siku hizi maarufu kama ‘Kutokelezea’  kunaweza kukuongezea kipato chako. Kwa mujibu wa makala moja kutoka Jarida la Forbes (isome yote hapa ukitaka) Mwandishi David K. Williams anasimulia……………

Mwanamitindo Lindsey Shores akiwa na mumewe Jared Shores, producer ktk TV ya BYU
































Watu watanashati na  waliofanikiwa  huonyesha umaridadi wao katika kila jambo wanalolifanya. Hata hivyo siyo kila siku mtu unahitaji muda, pesa na umakini katika shughuli rasmi za kikazi, utamaduni wa makampuni hutofautiana. Kwa mfano sisi kwenye kampuni yetu tunavaa Jeans na Tshirt. Tunajisikia vizuri tu, tunaweka kipaumbele  katika afya na mazoezi na uvaaji usiokuwa rasmi hutusaidia katika kupangilia mambo yetu vizuri, kuuza vizuri nk.

Kila mtu anaweza kunufaika kutokana na kujifunza kidogo kuhusu namna ya kujiweka vizuri mwenyewe katika ulimwengu wa mafanikio. Mtaalamu wa mitindo na mavazi Lindsay Shores anaweka wazi njia za kutumia katika kuongeza mafanikio kwenye kazi na biashara kwa kuzingatia muonekano wetu mbele za watu.

“Yeyote anayesema  ‘Ni kile kilichomo ndani ndicho kinacho’matter’ (muhimu)’, hayuko sahihi” anasema Lindsey. “Lakini kile kilichokuwa nje kinaweza kikawa muhimu zaidi. Mitindo siku hizi inasonga mbele kila kona”


Mbali na kubainika kwamba kuvaa vizuri kunaweza kuongeza kipato, pia ni muhimu  katika kuongeza heshima ya mtu binafsi na haiba yake. Mwandishi mwingine mashuhuri, M.Mafiso anasema, kuna njia 7 za kupata heshima. Ya kwanza anasema, “Pasipokujali zamani ulifanya kitu gani, wewe ni tajiri kiasi gani, umaarufu wako au hata umbile lako kama ni mnene au mwembamba, lakini ukiwa umevalia vizuri mara zote utatendewa vizuri kuliko yule aliyevalia kawaida.

Mwanamitindo Lindsey Shores siku ya harusi yake.

Mantiki yake inafanya kazi katika nyanja zote za biashara, iwe ni kwa mwanamuziki, mpokea wageni, na hata mcheza golf. “Valia vizuri kwenye pati, pasipokujali ni pati ya namna gani kwani ni muhimu katika kufikisha ujumbe kwamba,wewe ni nani na unataka kuwa nani. Na jambo hili linatakiwa liwe ndiyo kitu cha kwanza katika akili yako kila asubuhi unapoamka” anasema Lindsey. “Kuvalia vizuri mahali pa kazi , kunakuongezea tabia za uchangamfu pamoja na kuzidisha kujiamini”.

Katika biashara ni ukweli usiopingika  kuwa, “kamwe huwezi kupata tena kwa mara ya pili nafasi ya kuonyesha muonekano wako mzuri wa kwanza” 

0 Response to "KUVALIA VIZURI HUONGEZA KIPATO."

Post a Comment