THINK AND GROW RICH KWA KISWAHILI(FIKIRI NA UTAJIRIKE) | JIFUNZE UJASIRIAMALI

THINK AND GROW RICH KWA KISWAHILI(FIKIRI NA UTAJIRIKE)

KITABU KIPYA-FIKIRI NA UTAJIRIKE(THINK &GROW RICH-SWAHILI EDITION)

Fikiri na Utajirike(Think and Grow Rich) ndiyo babu wa vitabu vingine vyote vya hamasa na mafanikio duniani. Ndio kitabu cha kwanza kueleza kiini cha mafanikio na utajiri wa watu ni nini kwa namna ambayo watu wengine wanaweza wakaiga na wao kufanikiwa.  

Kwa muda wa miaka 20 Napoleon Hill alifanya utafiti kwa kuwahoji watu matajiri na waliokuwa na mafanikio makubwa kipindi chake wapatao 500. Miongoni mwao alikuwemo Andrew Carnegie, Henry Ford, Charles Schwab, King Gillete, Alexander Graham Bell na wengineo. 

Kwa muda wa miaka 20 Napoleon Hill alifanya utafiti kwa kuwahoji watu matajiri na waliokuwa na mafanikio makubwa kipindi chake wapatao 500. Miongoni mwao alikuwemo Andrew Carnegie, Henry Ford, Charles Schwab, King Gillete, Alexander Graham Bell na wengineo.

Kitabu hiki kimethibitisha pasi na shaka kuwa mtu yeyote anaweza akafanikiwa maishani bila kujali rangi yake, kabila, jinsia, dini, umri, elimu, hali ya kifedha, au kilema kingine chochote alichonacho.

 “Binadamu anaweza kufanya au kuwa chochote kile atakacho, ilimradi tu kitu hicho anaweza kukifikiria akilini”

Mafanikio Napoleon amemaanisha ni kitu chochote kile unachokitaka maishani na wala siyo lazima iwe ni fedha tu peke yake.

Kwa mara ya kwanza kabisa Think & Grow Rich kimetafsiriwa katika lugha adhimu ya Kiswahili na mtu yeyote yule anaweza kujifunza Siri za mafanikio kupitia kanuni 13 zilizogunduliwa na Napoleon Hill katika mahojiano yake na watu hao mashuhuri 500. Kitabu hiki kwa takriban miaka zaidi ya 80 hakijapoteza maana wala kuchuja maudhui yake yaliyokusudiwa na mwandishi.

Ni kwa njia ya kukisoma tu ndipo mtu anaweza akagundua siri ni kwanini kitabu hiki kimeweza muda wote kuendelea kubakia kuwa bora duniani miongoni mwa vitabu vingine vyote vya fedha na mafanikio ya mtu binafsi.

 

JINSI YA KUKIPATA KITABU CHA FIKIRI NA UTAJIRIKE NA BEI YAKE

HARDCOPY-Kitabu halisi cha karatasi;-

1.  Kwa Dar es salaam tunakuletea ulipo kwa sh. 21,000/=  au ukifuata mwenyewe Kwa wakala wetu Mbezi-Kimara ni sh. 20,000/=tu

2.  Mikoa mingine tunatuma kwa njia ya mabasi na gharama inategemea ni basi lipi na mkoa ulipo, lakini mara nyingi huwa ni kuanzia sh. elfu 5 mpaka 10 mikoa ya mbali. Hivyo mteja atalipia gharama ya kitabu pamoja na kiasi kitakachotozwa na basi tu

SOFTCOPY-Kitabu-nakalatete kwa njia ya simu-janja;-

1.  Kupakua kitabu kwenye Smartphone yako bonyeza link(kiungo) kifuatacho kisha baada ya malipo utaweza kudownload kitabu chako muda huohuo. Bei yake ni sh. 15,000/=

FIKIRI NA UTAJIRIKE(THINK AND GROW RICH-SWAHILI) E-BOOK


0 Response to "THINK AND GROW RICH KWA KISWAHILI(FIKIRI NA UTAJIRIKE)"

Post a Comment