SAIKOLOJIA YA UMASIKINI: SABABU (9) KWANINI HUPATI PESA ZA KUTOSHA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

SAIKOLOJIA YA UMASIKINI: SABABU (9) KWANINI HUPATI PESA ZA KUTOSHA

Msichana akicheza kamari mtaani

Kuna vitabu vingi, makala na maandiko mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii yanayohusiana na mada ya pesa au hali za watu kifedha. Katika somo letu hili la leo tutakwenda kuona ni aina gani za fikra na tabia zinazompeleka mtu kwenye umasikini na wala siyo kumpeleka kwenye kumiliki utajiri ambako ndio kila mtu hapa duniani anatamani kuelekea.

Siku hizi kwa kila mtu siyo siri tena kwamba fedha ni sawa na kama ilivyo nishati ya umeme iendeshayo karibu kila kitu. Nguvu ya umeme inapokatika nadhani sote tunafahamu ni taharuki kiasi gani watu huwa tunaipata, hali kadhalika na pesa nayo ndiyo hivyo hivyo ilivyo. Watu wanapoikosa au kuwa nayo kidogo sana huibua taharuki sawa na ilivyokuwa kukatika kwa nguvu ya umeme.

SOMA: Usilaumu kukosa pesa, bali laumu njia iliyokufikisha pale ulipo(Parti & ii)

Ikiwa mtu hana pesa kuna uwezekano mkubwa kwamba ni mawazo na vitendo vyake vinavyochangia yeye kukimbiwa na nguvu hii muhimu, PESA. Hebu sasa pasipo kupoteza muda wako mwingi, tukaone ni kwa jinsi gani vitendo na fikra za mtu(saikolojia) inavyoweza kumnyima hela hata akadhania labda ameshalogwa tayari.

1. Pesa siyo furaha, haiwezio kununua kila kitu bwana!

Wakati upande mmoja ukiwa umejijengea akilini mtazamo kwamba pesa haiwezi ikanunua furaha, upande mwingine wa pili unatamani ule vizuri na familia yako, ununue simu nzuri ya gharama, ujenge nyumba, ununue kiwanja, uende matembezini na wale uwapendao kustarehe nk. Hivyo unapokuwa na pande mbili zinazokinzana juu ya jambo moja, ni dhahiri kabisa jambo hilo umeshaliwekea vizingiti na kamwe hautaweza kufaulu na hivi ndivyo tunavyokosa pesa pasipo wenyewe kujua.

2. Sihitaji Pesa!

Ni kauli nyingine ya kimasikini iliyo rahisi kutamka mdomoni lakini inayoweza kugeuka na kuwa chanzo kizuri cha mtu kutokupata pesa inavyotakiwa. Kuridhika na kile kidogo unachokipata huku akilini ukiwaza tu juu ya kupunguziwa bei na kuweka akiba ya kile kidogo unachokipata wakati mwingine siyo sahihi na ni hatari pia kwani kunaweza kupunguza au kukatisha kabisa mzunguko wako wa fedha taslimu.

SOMA: Njia 6 za kuondoa woga na stress za fedha katika maisha yako

Fikra hii inamfanya mtu aishie tu kulenga katika kumiliki fedha kidogo(uhaba/ukata) badala ya kulenga katika kumiliki fedha nyingi(Ukwasi/Utajiri) hali ambayo hatimaye humlazimisha kutawanya rasilimali chache alizokuwa nazo badala ya kulenga katika kuzikuza na kuzizalisha zaidi.

3. Kushindwa kutumia Pesa

Pesa kama zilivyo nguvu za aina nyingine huwa haina tabia ya kustahimili udumavu, pesa haipendi kukaa tu bure bila ya kufanya kazi yeyote, na hii ndiyo sababu utawasikia watu wengi wakisema wanapata pesa zaidi na kwa urahisi pale wanapoamua kutumia pesa lakini wanapozibanabana zinapotea hawazioni (*Angalizo: lakini siyo matumizi holela, hapa namaanisha matumizi yale ya busara tu na yenye kuleta faida siyo utapanyaji)

SOMA: Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaisha.

Tafiti zimebainisha pia kwamba majanga mbalimbali kama vile magonjwa, wezi na majanga mengine ya asili huwa na kawaida ya kuwanyemelea zaidi watu walio na tabia ya kubana sana pesa zao wakihofia zisiishe au kupotea ilihali walizipata kwa jasho. Cha ajabu sasa inakuwa ni kinyume chake kwani pesa hizohizo wanazochelea kuzitumia hatimaye zinakuja kutoka kirahisi kupitia kukabiliana na majanga hayo au nguvu za asili ambazo wanakuwa hawana uwezo mwingine wa kuzizuia zaidi ya kutumia kile walicho nacho.

SOMO: Unahitaji pesa kiasi gani kwa siku ili uweze kuwa na furaha maishani?

Sasa unaweza kujiuliza ni kwanini tu wasingeamua mapema kufanya matumizi ya pesa zao kupitia njia nzuri ya kuzizalisha kama vile uwekezaji katika miradi na biashara mbalimbali kuliko kuziweka kabatini wakisubiria majanga?

4. Peponi (Mbinguni) Hakuna Pesa !

Mawazo ya masikini wengi ni kwamba, hata ukitafuta pesa vipi lakini mwisho wa siku utaziacha hapahapa Duniani, hutaenda nazo peponi. Dhana hii inakufanya usione umuhimu wa ‘kufight’ kufa na kupona na mwishowe ni umasikini hadi unaingia kaburini kweli kama mawazo yako hayo yanavyokudanganya. Midhali unaishi na kupumua, tafuta pesa uishi maisha mazuri hapa Duniani, achana na dhana hizo za “kiboya’………………….

....…Somo litaendelea jioni MASTERMIND-CLASS-2021…….

 

ü Saikolojia ya Umasikini ina mambo mengi watu wala hatuyadhanii hata kidogo kama ndiyo chanzo cha sisi kukosa pesa. Ungana na sisi leo hii tarehe 23/7/2021 kujifunza sababu nyingine 5 nilizokuandalia kwenye hili somo.

 

ü MASTERMINDO-GROUP-2021 tunakutana kila siku usiku saa 3 katika group la Watsap na Channel ya Telegram ya MICHANGANUO-ONLINE kujifunza masomo haya adimu kabisa ya fedha.

 

ü Tunakuwa pia na semina za mara kwa mara juu ya Michanganuo ya biashara zinazolipa Tanzania. Unakaribishwa ujiunge leo kwa ada ya sh. 10,000/= tu kwa mwaka mzima(Miezi 12 toka siku ya kujiunga)

 

ü Unapewa access ya masomo mengine yote ya siku zilizopita katika channel yetu.(zaidi ya masomo 70)

 

ü Unatakiwa uwe na APP za Watsap na Telegram kwenye simu yako lakini pia kwa ambaye hana tuna utaratibu mwingine mzuri tu wa kutuma kila kitu kwa njia ya E-mail hivyo ikiwa unataka njia hii nijulishe nikupe utaratibu huo.

 

ü Malipo ni kupitia namba, 0765553030 au 0712202244  jina Peter Augustino Tarimo. Na baada ya kulipa tuma ujumbe wa, “NIUNGANISHE NA MASTERMIND GROUP-2021

0 Response to "SAIKOLOJIA YA UMASIKINI: SABABU (9) KWANINI HUPATI PESA ZA KUTOSHA"

Post a Comment