UNAHITAJI KUPATA PESA KIASI GANI KWA SIKU ILI UWEZE KUWA NA FURAHA MAISHANI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

UNAHITAJI KUPATA PESA KIASI GANI KWA SIKU ILI UWEZE KUWA NA FURAHA MAISHANI?

PESA NA FURAHA
Jana na leo nimeona ni vizuri nizungumzie PESA NA FURAHA tu ili kuweka wazi umuhimu wa pesa, swala ikiwa pesa ni chanzo cha furaha au siyo hili itategemea zaidi mtazamo wa mtu mwenyewe. Pesa tuache unafiki ni kitu kizuri na siku hizi pesa siyo kwamba ni nzuri tu, bali zina umuhimu mkubwa. Ukiacha Mungu aliyetuumba na hewa tunayovuta, pengine pesa ndiyo kitu kinachofuata kwa umuhimu

Bila shaka afya, mapenzi, mahusiano na furaha ni vitu muhimu lakini hatuwezi kupata mlo wa siku au dawa za homa au kulipia vitu mbalimbali maishani bila kwanza ya kuwa na pesa. Na mpaka pale ambapo mwanadamu atakapobadilika labda karne nyingi zijazo, pesa itaendelea kubakia kuwa na umuhimu uleule iliyokuwa nao sasa.

SOMA: Saikolojia ya pesa na kanuni 10 za kufuata ili uwe mtu uliyefanikiwa kimaosha.

Hii haimaanishi kwamba pesa ndiyo iwe lengo kuu la mtu la kuishi hapa duniani hapana, Ili binadamu tuweze kuwa na furaha tunahitaji kiasi fulani tu cha fedha kwa siku, mwezi au mwaka. Pesa zote juu ya kiasi hicho, hazihitajiki na umuhimu wake ni mdogo kushinda afya, familia, marafiki na hata mapenzi. Pia ikiwa pesa zitakua chini ya kiwango hicho kinachotokea kwa mtuni hali ya mapambano ili mtu aweze kuishi(Struggle for survival), na hali hii ndiyo ambayo kila mtu anapaswa kuiepuka kwa gharama zote.

Pesa siyo chanzo cha maovu yote duniani
Watu wengi sana tokea utotoni wamejijengea mitazamo mbalimbali katika akili zao juu ya pesa. Kwa bahati mbaya sana hivyo ndivyo imani nyingi potofu kuhusiana na pesa zilivyoanza katika maisha yetu. Moja kati ya imani hizo potofu ni hii inayosema, eti pesa ndiyo chanzo cha maovu yote duniani na ndiyo hutusababishia matatizo yetu yote. Imani hii potofu ingeliweza kuondoka vichwani mwa watu endapo wazazi, waalimu na jamii kwa ujumla wangeungana kuikomesha tangu watoto wangali wadogo.

SOMA: Ujanja matajiri wanaoutumia ili kupata pesa  kutoka nyanzo vingi vya mapato 

Ndiyo, ni ukweli kwamba pesa hushiriki katika matatizo mengi sana yanayomwandama binadamu lakini matatizo hayo kiukweli husababishwa na sisi wenyewe na pesa hutumika tu kama kifaa au zana ya kuleta machafuko. Wapo watu wengi waliokuwa tayari hata kufa ama kuua kwa sababu tu ya pesa. Sasa utasema pesa ndiyo zilizo ndani ya akili zao? Kwa upande mwingine pia wa shilingi kuna watu wengi tu walio tayari kutumia pesa zao kwa ajili ya kulisha masikini na kuponya wagojwa. Hivyo watu wazuri hutumia pesa katika mambo mazuri yanayojenga wakati watu wabaya hutumia pesa kwa ajili ya mambo maovu yanayobomoa.

Unaweza ukainunua furaha kwa pesa
Huu ni msemo mwingine unaohusu pesa. Kwa kiasi kikubwa huu nao ni uzushi(upotofu) ingawa kuna chembechembe kidogo za ukweli. Inawezekana mtu kuwa na pesa kidogo na ukaishi maisha yenye furaha na kujitosheleza. Lakini pia ikiwa utakuwa na fedha kidogo kupindukia, kiasi kwamba watoto wako au familia inashinda na kulala na njaa huku wadeni wako wakikugongea mlango kila siku asubuhi, utakuwa na furaha kweli?

SOMA: Vitu hivi 5 vitakupa mafanikio, furaha moyoni na amani ya nafsi maishani

Ukweli wa mambo ni kwamba pesa inaweza tu kuongezea furaha tuliyokuwa nayo. Kwa mfano kumiliki nyumba yako mwenyewe, kuwa na uwezo wa kula vyakula bora vyenye afya na kuvaa mavazi ya kupendeza huongeza kiwango cha mtu cha furaha. Kwa matajiri wakubwa wengi wao furaha huongezeka pale wanapowasaidia watu wengine au kutatua matatizo makubwa yanayowasumbua binadamu duniani.


Ongeza pesa zako
Hata kama unafikiria kwamba pesa ni shetani, na haziwezi zikaleta furaha, lakini ni vigumu pia kukataa kwamba ongezeko kidogo la pesa zako litasababisha maisha yako kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa. Ipo njia ya kuongeza kiasi cha fedha(kipato) ambayo watu wengi huidharau kwa kufikiria ili kupata pesa nyingi mtu anahitaji atumie nguvu nyingi sana. Unachohitaji ni  kujinyima  kidogo kile unachotumia sasa na kuwa na subira kama inavyoelezwa hapa chini.

SOMA: Stadi moja ya maisha itakayokuwezesha kuingiza pesa bila kuwekeza chochote

Weka asilimia 10% tu au zaidi ukipenda ya kipato chako unachopata sasa.
Njia ya kuelekea kwenye utajiri huanza na kujiwekea akiba ya kile upatacho kila siku kidogokidogo. Pesa hizi za akiba si kwa ajili ya kuja kununulia nguo wala kufanyia sherehe hapana, bali ni kwa ajili ya kununulia asseti mbalimbali zitakazokuingizia pesa baadae au ambazo thamani yake itapanda kidogokidogo mfano ardhi. Na wala haijalishi umeanza lini ingawa ukianza mapema zaidi ungali kijana ndiyo vizuri. Masomo yanayohusiana na kujinunulia asseti nadhani tulishasoma mengi tu siku za nyuma. 


Sasa basi ni kiasi gani hasa cha  pesa unachohitaji kwa siku ili uweze kuwa na furaha maishani?

…………………………………..

Somo hili linaendelea katika group la MICHANGANUO-ONLINE
HII NI KWA YULE TU AMBAYE BADO HAJAJIUNGA NA GROUP HILI.


Ni wajibu wangu kukukumbusha kila mara kwani najua inawezekana hujui mambo mengine mazuri yanayoendelea kila siku nyuma ya pazia mbali na makala hizi ninazoandika hapa.

Unapolipia ada ya kujiunga na Group SH. Elfu 10 unapata vitu vifuatavyo;

A. MAMBO MAPYA NA YANAYOKUJA HIVI PUNDE(new & Coming soon)
1.  Masomo ya fedha kila siku usiku saa 3 mpaka saa 4

2.  Kuna Kitabu kipya chenye masomo mazuri sana ya fedha kitatoka siku ya Jumanne tarehe 3 Septemba

3.  Semina ya mpango wa kuanzisha kiwanda kidogo cha usagishaji nafaka. Tofauti na michanganuo mingine yote tuliyowahi kufanya huu utakuwa na ubunifu wa kipekee mno! na mtu ataweza kuutumia ubunifu huo kuuza unga wa mahindi kama njugu.(Unique marketing strategy)


B. OFFA YA ZAMANI (VITU 14) NA INAYOKARIBIA KUISHA MUDA MCHACHE UJAO, BADO KIDOGO SANA TUTAIONDOA !
   
1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Semina na mchanganuo wa Biashara: Kiwanda cha tofali za saruji Kiluvya.

12.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

13.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

14.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Nirudie tena, vitu vyoote hivi unavipata kwa shilingi Elfu 10 tu! Unaweza ikiwa utawahi kabla offa hii maalumu haijafungwa. Thamani ya masomo na vitabu unavyoona hapo juu ni zaidi ya shilingi elfu 90 kwa bei ya kawaida. Nilitamani sana wewe msomaji wangu upate masomo haya yote kwani ni dhamira yangu kuu wewe kutumia vizuri kila fursa iliyokuwepo katika kufanikisha ndoto zako.

Namba za malipo ni, 0765553030 au 0712202244 jina, Peter Augustino Tarimo, na baada ya kulipia, nitumie ujumbe wasap au meseji ya kawaida kwa namba 0765553030 isemayo; “NIUNGANISHE  MASOMO YA KILA SIKU NA OFFA INAYOISHIA

Asante na Karibu sana…

Peter A. Tarimo

0 Response to "UNAHITAJI KUPATA PESA KIASI GANI KWA SIKU ILI UWEZE KUWA NA FURAHA MAISHANI?"

Post a Comment