UTAJUAJE KAMA UMEUFIKIA UHURU KAMILI WA KIFEDHA? KANUNI HII HAPA

KINADADA WAJASIRIAMALI WALIOHURU KIFEDHA
Kabla hatujaenda kuona ni jinsi gani mtu unavyoweza kutambua ikiwa sasa umeshakuwa huru kifedha au la, hebu kwanza tuone maana ya dhana hizi mbili zinazoshabihiana sana, ‘Kipato cha ziada.’ na ‘Uhuru wa kifedha’.

Tunapozungumzia kipato cha ziada (Passive income) maana yake hasa ni kipato mtu anachoingiza pasipo kufanya kazi au kufanya kazi kidogo sana. ni kipato kile mtu anachoweza kuingiza hata ikiwa yeye menyewe hayupo pale katika eneo la tukio, labda anaweza kuwa yupo kazini kwake au ana mishemishe zingine mahali. Mara nyingi kipato cha ziada huhusishwa na uhuru wa kifedha ingawa siyo lazima mtu unapoingiza kipato cha ziada basi pia uwe huru kifedha.

Kwa upande mwingine uhuru wa kifedha unaweza kuwa na maana moja kati ya hizi zifuatazo kulingana na mazingira na kipato cha mhusika.

1.  Maana ya kwanza mtu anajihesabu kuwa huru kifedha pale anapokuwa na kipato cha ziada kinachomtosha kugharamia mahitaji yake yote ya msingi.

2.  Maana ya pili ni pale mtu anapokuwa na kipato cha ziada cha kumuwezesha kulipia chochote kile akitakacho maishani ikiwa ni pamoja na vitu vyote visivyokuwa muhimu kama anasa nk.

Mtu aliyekuwa huru kifedha pia yeye afanye kazi asifanye kipato huingia kama kawaida, lakini ikumbukwe kwamba kuwa na kipato cha ziada tu peke yake hakutoshi kukuhakikishia uhuru wa kifedha mpaka pale utakapohakikisha kipato hicho kinatosha kugharamia mahitaji yako yako yote ya msingi na kubaki, wakati huohuo ukiwa haulazimiki kufanya kazi yeyote labda tu ufanye kwa mapenzi yako au kama hobi.Unahitaji kipato cha shilingi ngapi kuwa huru kifedha?
Unaweza ukajiuliza, upate kipato cha ziada kiasi gani kusudi ujue sasa umeshakuwa huru kifedha?” hupaswi wala kuumiza kichwa kwani jibu lake ni rahisi sana.
Tumesema awali kwamba, kuwa huru kifedha kunaweza kutafsiriwa katika maana 2, ya kwanza ni pale mtu utakapoweza kuyamudu mahitaji yako yote ya msingi pasipo kubabaika na ya pili ni pale utakapoweza kuingiza kipato cha ziada kinachotosha kugharamia mahitaji yako yote ya msingi na hata yale yasiyokuwa ya msingi mfano anasa huku ukiwa huna haja ya kuuza muda wako ndipo uweze kulipia gharama hizo.

Sasa kanuni au hesabu rahisi ya kujua kama umeingia kwenye uhuru kamili wa kifedha ni hii hapa chini............

....................................

Ndugu msomaji wa masomo haya, Hili ndilo somo tulilojifunza leo siku ya tarehe 29/4/ 2020 katika group la MICHANGANUO-ONLINE.

Kila siku masomo kama haya yahusuyo fedha hufundishwa pamoja na masomo yahusuyo jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara bunifu zinazolipa.

Ili uweze kuyapata masomo hayo yote yaliyopita na yatakayotolewa kwa mwaka wote huu wa 2020 unatakiwa kujiunga na group hilo. Ada kwa mwaka mzima ni sh. elfu 10 tu na tunakutumia pia na offa ya vitabu na michanganuo mbalimbali mara baada ya kujiunga.

Malipo ni kupitia namba zetu, 0765553030  au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo kisha tuma ujumbe usemao, "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO NA OFFA YA VITU 6"

0 Response to "UTAJUAJE KAMA UMEUFIKIA UHURU KAMILI WA KIFEDHA? KANUNI HII HAPA"

Post a Comment