SHUGHULI HIZI HUWEZI KUZIDHANIA KABISA KAMA ZINA MCHANGO MKUBWA WEWE KUFANIKIWA KIFEDHA

Mwanamke akifanya biashara nyumbani kwake

Ni shughuli zinazoonekana kuwa za kawaida sana lakini siri yake wanaijua matajiri na watu wote waliofanikiwa kichumi, wao huzijali sana ndiyo maana wamefanikiwa kufika pale walipo huku watu wa kawaida wakihangaika kusaka usiku na mchana siri za mafanikio na utajiri ni kitu gani.Nyumbani ni mahali ambapo, binadamu tunatumia muda wetu mwingi kuliko sehemu nyingine yeyote ile katika maisha yetu. Unaweza ukasema sasa mbona unashinda kazini masaa mengi kuliko vile unavyoshinda nyumbani lakini nikukumbushe tu kwamba ule muda wa usiku, likizo na yale masaa ya kila asubuhi na jioni unapotoka kazini ukiyajumlisha yote ni zaidi ya muda unaoshinda kazini, isitoshe pia kuna kustaafu ni lazima urudi home na pale utakaa muda mrefu. Hivyo nyumbani ni nyumbani panatakiwa upajengee misingi inayostahili.


Mada yangu leo hasa siyo ya kuonyesha wingi wa masaa tunayoishi nyumbani hapana, bali ninachotaka kusema leo ni juu ya shughuli za kuingiza pesa zinazoweza kufanyika mazingira ya nyumbani na zikaweza kuongeza mzunguko wa mtu wa fedha. Uzuri wa nyumbani ni kuwa hata wakati wewe mwenyewe haupo lakini kunabaki mtu aidha msaidizi wa kazi au yeyote yule ambaye ikiwa kuna shughuli zozote zile ndogondogo anaweza akazisimamia bila shida.

Kwahiyo nyumbani iwe umepanga au unaishi kwako ni jambo jema sana endapo utapafanya kuwa mahali panapoingiza pesa badala ya kutoa tu. Matumizi mbalimbali ya nyumbani hutegemea kipato ulichokuwa nacho kama ajira au biashara unayoifanya. Kazi na biashara zinatofautiana baina ya mtu na mtu mwingine. Kwa mfano kuna ajira na biashara kubwa zilizokuwa na uhakika na pia zipo ajira na biashara ndogondgo ambazo haziwezi zikatabirika sana kwani wakati wowote tuchukulie mfano kipindi hiki cha janga la corona, zinaweza zikatetereka au kusimama ghafla halafu yule anayezitegemea akajikuta njia panda asijue la kufanya.


Lakini tayari ukiwa na uzoefu na miradi kama hii inaweza ikakuokoa katika nyakati ngumu na za kuvunja moyo namna hii. Vilevile shughuli hizi zina uwezo mkubwa wa kuongeza mzunguko wa fedha nyumbani na hata kwenye biashara kwani ikiwa unafanya biashara hautachukua tena kiasi kikubwa cha fedha kama gawio kutoka katika biashara na hivyo kuwa na mzunguko chanya wa fedha.


Shughuli au miradi midogomidogo maarufu ya nyumbani mtu anayoweza akaanzisha ni hii ifuatayo, nitaitolea na maelezo.......Somo bado litaendelea.......

............................................

Somo hili ndilo nitakalofundisha leo hii tarehe 1 Mei. 2020 siku kuu ya Wafanyakazi katika darasa la WHATSAPP, EMAIL NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM, saa 3 mpaka saa4 usiku.

Ikiwa umechelewa na kusoma ujumbe huu somo limeshapita, usijali, kwani unapojiunga masomo yote yaliyopita unayakuta katika channel yetu ya telegramu au pia tunaweza kukutumia kwa email/wasap

Kiingilio katika semina hizi ni shilingi Elfu 10 tu unapata uanachama wa mwaka wote huu wa 2020 pamoja na masomo yote ya semina zilizopita, offa ya vitabu, michanganuo na templates(vielezo) vya kuandika mpango wowote ule wa biashara kwa urahisi. 

Hii offa ni ya muda tu, idadi fulani ya watu ikitimia itamalizika na kila kitu kuuzwa chenyewe. Siyo lazima uwe unatumia WHATSAPP na TELEGRAM kwani masomo tunatuma pia kwa njia ya email 


Kujiunga na masomo haya lipia shilingi elfu 10 kupitia namba zetu za simu, 0712202244  au  0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo. 

Kisha tuma ujumbe huu, NIUNGANISHE NA GROUP LA WHATSAP PAMOJA NA OFFA YA VITU 6". Utaunganishwa mara moja na kutumiwa kila kitu. 

0 Response to "SHUGHULI HIZI HUWEZI KUZIDHANIA KABISA KAMA ZINA MCHANGO MKUBWA WEWE KUFANIKIWA KIFEDHA"

Post a Comment