NJIA (7) ZA KUJENGA UKARIBU NA WAJASIRIAMALI WALIOFANIKIWA UINUKE KIFEDHA

Wajasiriamali waliofanikiwa kifedha
Miongoni mwa njia mtu unazoweza kutumia ili kufanikiwa kifedha ni kwa kuwa karibu na kufanya kazi na watu ambao tayari wameshafanikiwa au kuwa na uzoefu mkubwa kwenye eneo unalotaka kufanikiwa. Haitoshi tu kuwa karibu au kufanya kazi pamoja lakini pia inatakiwa watu hao wakubali na wawe tayari kukusaidia.


Kutengeneza mtandao au mahusiano mazuri na watu unaotaka kuiga mfano wao kuna faida nyingi mbali na fedha. Unaweza kupata maarifa, siri, kanuni, mbinu mbalimbali na hata mitazamo ya kimaisha itakayokuwezesha katika safari yako ya kuelekea uhuru kifedha. Zifuatazo ni njia unazoweza kuzitumia katika kujenga daraja kati yako wewe na watu mbalimbali waliofanikiwa, wataalamu, washauri na hata wabia kwenye sekta ya biashara au shughuli uliyoamua kuifanya maishani;

(1) Amua ni biashara au shughuli ipi utakayofanya.
Hiki ni kama chombo utakachokitumia kuwafikia wale unaotamani wakupe msaada unaohitaji. Kujenga tu ukaribu peke yake hakutoshi ni lazima uhakikishe unakuwa na biashara hata kama ni ndogo.

Inawezekana hata mtaji wa kuanzisha biashara yenyewe bado huna, utakachopaswa kufanya ni kuchukua hatua ambayo mwishowe itakupeleka kwenye biashara unayotamani kuja kuifanya. Unaweza hata kutafuta ajira inayohusiana nayo.


Biashara zipo za aina mbalimbali mfano, uuzaji bidhaa, utoaji huduma, ardhi na majengo, udalali, biashara za mtandao (multilevel marketting), biashara za hisa, kuanzisha kiwanda nk. Lengo ni kuwa mahiri katika lile eneo unalotaka kufanikiwa na hatua hii ni muhimu hata kabla hujaanza kutafuta watu waliofanikiwa au wenye uzoefu mkubwa watakaokupa msaada.


(2) Watambue watu wanaoweza kukusaidia kuyafikia malengo yako.
Baada ya kuchagua biashara, hatua ya pili ni kubaini ni watu gani unaoweza kujenga nao uhusiano watakaoweza kukupa msaada unaohitaji. Watu hao wanaweza wakawa ni kati ya hawa wafuatao.
·      Watu waliobobea katika biashara hiyo kama wamiliki, nk.
·      Wataalamu mfano,washauri, wanasheria nk
Tuchukulie mfano umechagua kufanikiwa katika biashara ya vyombo vya habari(media), kumiliki vituo vya redio, televisheni labda na magazeti. Katika upande wa biashara za media, wamiliki wanaweza wakawa ni wenye vituo vya redio TV na magazeti. Wataalamu ni kama vile, wahariri na waandishi wa habari nguli waliodumu katika tasnia hiyo kwa muda mrefu, watangazaji, vyuo vya uandishi habari nk.


Watu waliobobea na wataalamu katika eneo ulilochagua wanaweza wakawa chanzo kizuri sana cha taarifa zitakazokusaida. Kusanya orodha ya watu hao na wanaweza kuwa ni wa hapa hapa nchini au hata kutoka nje ya nchi. Tumia njia mbalimbali kupata mawasiliano nao hasa unaweza ukatumia mtandao wa intaneti(google) kwani siku hizi watu wengi walio katika biashara makini wapo pia kwenye mitandao. Chukua namba zao za simu na hata anuani za email.

3. Toa kabla hujapokea.
Usifikiri ni rahisi tu mtu kukubali kukupatia ushirikiano hivihivi unapokuwa ukitafuta washauri au watu wa kujenga nao mtandao. Ni lazima ukubali kutoa kwanza kabla hujapokea, hapa namaanisha kwamba, wafanyabiashara wengi wakubwa au watu waliobobea katika fani zao, hawafanyi kazi za hisani, wapo kwenye biashara hivyo huwezi ukawapotezea muda wao hivihivi tu ukitegemea huruma, haitawezekana na wala hawawezi kukubali.

Ndiyo maana ukitaka kuonana na watu wengi maarufu, huwezi kwenda kienyeji tu ni lazima upitie kwanza  kwa mtu atakayehakikisha kama kinachokupeleka kwake kweli kina tija vinginevyo unarudishwa mlangoni. Si kama hawapendi kuonana na watu wa kawaida hapana, bali wana watu wengi mno wenye shida zinazofanana na za kwako wanaohitaji kuwaona. Sasa ni lazima ubuni ni mbinu gani utakayotumia kumshawishi ili akubali kukusikiliza na kuacha hao wengine. Baadhi ya mbinu unazoweza ukazitumia kama “hongo” kusudi akusikilize ni hizi hapa;
·      Fanya kila linalowezekana upate ajira katika kampuni yake.
·      Mnunulie chakula mahali
·      Waandike katika blogu yako, kitabu au hata kwenye kurasa za kijamii.
·      Kuwa mteja wa biashara/kazi zake mfano unaweza ukanunua hata kitabu chake nk
·      Watumie zawadi ya thamani.
·      Wasaidie kupata wateja zaidi katika biashara zao.
·      Unapowasiliana nao kwa email epuka maneno kama, “Msaada” “Haraka” nk. anaweza akafikiria ni matapeli kama wale wa Kinaijeria, badala yake tumia maneno kama, “Nipo tayari kufanya kazi kwa kujitolea” nk.
Utakachotoa ni kidogo sana ukilinganisha na kile unachotazamia kukipata.

4. Hudhuria matukio na shughuli mbalimbali.
Hakikisha hukosi zile shughuli ambazo unafahamu watu unaotaka kutengeneza nao mtandao hawakosekani. Kwa mfano watu kwenye biashara ya vyombo vya habari, unaweza kuhudhuria sherehe mbalimbali za wanahabari, jukwaa la wahariri, mikutano ya wamiliki wa vyombo vya habari, uzinduzi wa vyombo mbalimbali nk. Shughuli nyingine zinaweza zisihusiane moja kwa moja na malengo yako lakini unaweza kukutana pale na mtu muhimu anayehusiana nayo akakusaidia...........somo linaendelea...


.....................................................

Ndugu msomaji wa blog hii; 
Hili ni somo letu la leo tarehe 28/4/2020 katika Group la Wasap la MICHANGANUO ONLINE, CHANNEL YETU YA TELEGRAM na pia kwa njia ya EMAIL ikiwa hutumii wasap au telegramu, masomo haya ni kila siku usiku saa 3 - mpaka saa 4. Kiingilio ni  sh. elfu 10 ambayo ni ada ya mwaka wote huu wa 2020. 

Masomo mengine yote yaliyokwisha pia utayapata yote kwenye group au katika channel yetu ya telegramu


Mbali na masomo haya ya kila siku yenye maudhui ya pesa pia tunakutumia, vitabu, michanganuo na vitu vyote hapa chini pindi tu unapojiunga hivi.

Ili kujiunga lipa kiingilio sh. elfu 10 kupitia namba zetu, 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe unaosema, "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE PAMOJA NA OFFA YA VITU 6"

Ikiwa hutumii wasap au telegram tunakutumia kila kitu kupitia E-mail yako.

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI -kwa kiswahili

2.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa kiingereza

3.  Semina ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji unga wa dona(USADO Milling) )-kwa kiswahili

4.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)-kwa kiswahili

5.  Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikiti maji(KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili

6.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingerezaWhatsapp:  0765553030
SIMU:         0765553030 au 0712202244


Kujipatia vitabu vyetu au Michanganuo mbalimbali ya biashara tembelea duka letu la mtandaoni hapa la SMART BOOKS TZ

Kupata toleo jipya 2020 la kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA bofya hayo maandishi.

Kufuatilia Semina hatua kwa hatua jinsi ya kuandika MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA KIDOGO CHA USAGAJI UNGA WA DONA bonyeza hiyo link0 Response to "NJIA (7) ZA KUJENGA UKARIBU NA WAJASIRIAMALI WALIOFANIKIWA UINUKE KIFEDHA"

Post a Comment