MAUZO KWA MKOPO NI KWA AJILI YA BIASHARA KUBWA, SIYO BIASHARA NDOGONDOGO


BIASHARA YA KUUZA MADELA
Katika mada hii nitaegemea zaidi kwenye biashara ndogo.

Uhai wa biashara yeyote ile unategemea mzunguko chanya wa fedha nikiwa namaanisha fedha zinazoingia ziwe nyingi kuliko fedha zinazotoka nje ya biashara. Ingawa biashara inaweza kuwa na faida nzuri tu lakini mzunguko hasi wa fedha taslimu unaweza ukaifanya kuwa ni biashara isiyofaa kabisa wala kuwezekana kufanyika.

Moja ya makosa makubwa baadhi ya wajasiriamali wadogo wanayoyafanya ni kuuza bidhaa zao kwa mkopo bila kuzingatia vigezo muhimu kwa umakini. Kuna ambao hata huthubutu kuanzisha “BIASHARA ZA KUKOPESHA MITAANI”. Hapa mtu anakwenda Manzese, Tandika au Kariakoo, ananunua viatu, nguo au bidhaa zozote zile za jumla kwa fedha taslimu halafu akifika mtaani anaanza kupita nyumba hadi nyumba akiwahimiza wateja wakope  na kisha kuja kulipa baadae.

SOMA: Ajabu la nane(8) la dunia, nguvu ya kushangaza inayoweza kumtajirisha mtu bila ya kutoa jasho

Mtindo huu siyo mbaya ila tu ubaya huja pale biashara yenyewe inapokuwa ndogo, na bila ya mtaji wa kutosha. Hata ikiwa wateja wako wote watakuja kukulipa lakini je, watakulipa wote kwa wakati muafaka? Wateja kutokulipa kwa wakati kunaleta athari kubwa na mbaya sana katika mzunguko wako wa fedha kwenye biashara ndogo. Kwa kawaida imezoeleka sehemu nyingi duniani kuuza kwa mkopo kunafanywa na biashara kubwakubwa tu au makampuni na siyo biashara ndogondogo.

Wakopaji nao ni binadamu, inaweza ikafika siku ya kulipa deni anakuambia  amefiwa, amesafiri, anaumwa, amelazwa au  anauguliwa na mtu wa karibu kama mtoto nk. Utampeleka polisi? Anaweza akaahidi kulipa mwezi unaofuata, vipi kuhusu mzunguko wa biashara yako wa pesa? Kwa hizo siku 30 za ziada utapata wapi fedha taslimu za kuziba pengo na wakati huo mtaji wenyewe pengine ni wa kukopa? Mzunguko wako wa fedha tayari kwa mwezi huo utakuwa hasi, hautakuwa na fedha taslimu za kwenda kufuatilia mzigo mwingine na matokeo yake hata fedha kidogo ulizolipwa na baadhi ya wateja unaamua kuzifanyia majukumu mengine.

Hii ndiyo sababu kubwa ni kwanini biashara nyingi za kukopesha vitu mitaani hazipigi hatua. Kuna gharama pia za kufuatilia madeni, muda nk. ukija kujumlisha vyote unakuta biashara ya namna hiyo haina tija zaidi ya kuumiza kichwa.

Sisemi katika biashara ndogo mtu hauwezi ukakopesha kabisa hapana, ila kama utaamua kukopesha na ni jambo lisiloepukika kwa asilimia 100, basi uhakikishe yule unayemkopesha unafahamu historia yake vizuri, unapajua na anakoishi, tena isitoshe weka idadi maalumu ya wateja utakaoruhusu wakope ikiwa utalazimika kukopesha.

Kwa mfano unaweza ukajiwekea malengo hivi, mzigo wako hebu tuchukulie labda ni mzigo wa madela ya kina mama pisi 100, kati ya hayo madela 100 amua ukisha kopesha hapo madela 15 au 20 tu basi, hayo mengine yanayobakia 85 au 80, piga ua hata aje nani hautamruhusu akope. Hii itasaidia sana kuwa na uhakika wa fedha taslimu ya madela yako 80.

Hebu fikiria kwa mfano madela yako uliyanunua mwezi wa pili mwanzoni na ulitegemea mwishoni mwa mwezi wa pili kabla hata ya kuanza kwa mfungo wa ramadhani utafuata tena mzingo mwingine kusudi uje kuwahi msimu wa sikukuu za Pasaka na Idi. Lakini mwishoni mwa mwezi wa pili unajikuta ulikopesha zaidi ya robotatu ya madela yote na wateja wote kila unayemfuata anakupa sababu lukuki huku akiahidi kulipa mwezi wa tatu mwishoni. Hebu fikiria hizi siku 30 hapo katikati biashara yako na pengine wewe mwenyewe utaishije?.

Hata kama madela yako yana faida kubwa kisi gani........................... somo hili linaendelea...........................................................

Mpenzi msomaji wangu; 
Hili ni somo letu la leo tarehe 27/4/2020 katika Group la Wasap la MICHANGANUO ONLINE, CHANNEL YETU YA TELEGRAM na pia kwa njia ya EMAIL ikiwa hutumii wasap au telegramu, masomo haya ni kila siku usiku saa 3 - mpaka saa 4. Kiingilio ni  sh. elfu 10 ambayo ni ada ya mwaka wote huu wa 2020. 

Masomo mengine yote yaliyokwisha pia utayapata yote kwenye group au katika channel yetu ya telegramu


Mbali na masomo haya ya kila siku yenye maudhui ya pesa pia tunakutumia, vitabu, michanganuo na vitu vyote hapa chini pindi tu unapojiunga hivi.

Ili kujiunga lipa kiingilio sh. elfu 10 kupitia namba zetu, 0765553030 au 0712202244 jina Peter Augustino Tarimo. Kisha tuma ujumbe unaosema, "NIUNGANISHE NA GROUP LA MICHANGANUO-ONLINE PAMOJA NA OFFA YA VITU 6"

Ikiwa hutumii wasap au telegram tunakutumia kila kitu kupitia E-mail yako.

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI -kwa kiswahili

2.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.-kwa kiingereza

3.  Semina ya siku 7 na mpango kamili wa biashara ya usagishaji unga wa dona(USADO Milling) )-kwa kiswahili

4.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)-kwa kiswahili

5.  Mchanganuo kamili wa kilimo cha Matikiti maji(KIBADA WATERMELON BUSINESS PLAN) -kwa kiswahili

6.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) -kwa Kiswahili & kiingerezaWhatsapp:  0765553030
SIMU:         0765553030 au 0712202244


Kujipatia vitabu vyetu au Michanganuo mbalimbali ya biashara tembelea duka letu la mtandaoni hapa la SMART BOOKS TZ

Kupata toleo jipya 2020 la kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA bofya hayo maandishi.

Kufuatilia Semina hatua kwa hatua jinsi ya kuandika MCHANGANUO WA BIASHARA YA KIWANDA KIDOGO CHA USAGAJI UNGA WA DONA bonyeza hiyo link

0 Response to "MAUZO KWA MKOPO NI KWA AJILI YA BIASHARA KUBWA, SIYO BIASHARA NDOGONDOGO"

Post a Comment