KWANINI CHANJO YA MALARIA IMEKUWA NGUMU HIVYO KUPATIKANA? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KWANINI CHANJO YA MALARIA IMEKUWA NGUMU HIVYO KUPATIKANA?

Vimelea wanaosababisha ugonjwa wa Malaria waitwao Plasmodium waligunduliwa kwa mara ya kwanza hapo mwaka 1888, na kujulikana kwamba mbu ndiyo wahusika wakuu katika kueneza vimelea hao ilikuja kugunduliwa hapo mwaka 1898. Tangu kipindi hicho magonjwa mengi mfano wa surua na polio yaliyokuja kugunduliwa nyuma yake yamepatiwa chanjo lakini Malaria bado haijaweza kupatiwa chanjo mpaka hivi karibuni kabisa ambapo kumekuwa na matumaini kidogo ya kupatikana kwa chanjo hiyo.

Kwanini?
Malaria husababishwa na vimelea jamii ya Protozoa, ni wakubwa na tata kuliko  virusi. Wawapo katika mwili wa binadamu kabla hawajachukuliwa na mbu jike aina ya Anofeles, mfumo wake wa maisha ni tata na usiotabirika kama ilivyokuwa kwa bacteria na virusi.

Ni wajanja sana kwani wanao uwezo wa kukwepa mfumo wa asili wa kinga ya mwili(Natural immune system) ambao pamoja na kuwa na nguvu sana lakini hauwezi kufua dafu kwa vimelea hawa. Wanachokifanya ili kujikinga wasiuwawe ni kujificha ndani ya seli za mwili, hupenyeza humo haraka na kujikinga na mfumo wa kinga ya mwili.

Wana mbinu nyingine tena  ambapo wakiwa ndani ya seli hujijengea kitu mfano wa ‘koti’ la protini linalowazuguka , na ingawa chanjo inaweza ikatengenezwa kubaini hili koti, wadudu hawa wa malaria mara moja hujibadilisha na kutengeneza koti lingine lisilotambuliwa na chanjo husika. Kwa hiyo hali hiyo imefanya chanjo ya malaria kuwa kitu kigumu na ghali sana kutengeneza. 

0 Response to "KWANINI CHANJO YA MALARIA IMEKUWA NGUMU HIVYO KUPATIKANA?"

Post a Comment