KUHUSU USHOGA, NDOA ZA JINSIA MOJA NA UFISADI, OBAMA HATOMUNGUNYA MANENO. | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KUHUSU USHOGA, NDOA ZA JINSIA MOJA NA UFISADI, OBAMA HATOMUNGUNYA MANENO.

Rais Barack Obama ameweka wazi kwamba ataongea waziwazi pasipo kumungunya maneno juu ya maswala yote yanayohusiana na haki za mashoga, pamoja na ubaguzi wa aina yeyote ile kwa binadamu. Alisema hayo alipokuwa akihojiwa na Shirika la habari la auaingereza BBC muda mfupi kabla hajaondoka kuelekea Nairobi.

“Mimi siyo mshabiki wa ubaguzi na ukandamizaji kwa mtu yeyote kwa kigezo cha ukabila, dini, ushoga au jinsia” alisema  na kuendelea kwamba “Kama  mtu aliyekuwa na familia nchini Kenya na anajua historia ya jinsi nchi inavyorudishwa nyuma mara nyingi kutokana na wanawake na wasichana kutokutendewa haki, nafikiri  hali ni hiyohiyo pia linapokuja suala la mapenzi ya jinsia moja”

Kenya kwa upande mwingine imekataa katakata kuruhusu ndoa za jinsia moja na Rais Kenyatta mwenyewe ni miongoni mwa watu wasiotaka jambo hilo kutendeka nchini Kenya.

0 Response to "KUHUSU USHOGA, NDOA ZA JINSIA MOJA NA UFISADI, OBAMA HATOMUNGUNYA MANENO."

Post a Comment