OBAMA ATUA RASMI KENYA, SIMU, MAWASILIANO VYAKATIKA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

OBAMA ATUA RASMI KENYA, SIMU, MAWASILIANO VYAKATIKA


Hatimaye Dege la Rais Barack Obama wa Marekani  Air Force One limetua rasmi katika uwanja wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi hapo majira ya saa mbili na nusu 8:30pm hivi usiku saa za Afrika ya Mashariki baada ya safari ya karibu saa 15.


Alilakiwa na mwenyeji wake Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na baada ya muda mfupi alisaini kitabu cha wageni kisha wakapanda magari na kuondoka uwanjani hapo. Kwa mujibu wa Shirika la habari la Uingereza BBC, wakati ndege hiyo ikitua mawasiliano ya simu za mkononi yalikatika kwa muda na baadaye kurudi tena. 

Usalama ulikuwa ni wa hali ya juu mno! huku maafisa usalama wa Marekani wenyewe wakiwa ndiyo wahusika wakuu. Hata mkuu  wa usalama nchini Kenya mwenyewe alikaguliwa na maofisa hao. Kuna askari polisi wapatao elfu 10 waliosambazwa kote jijini Nairobi na angani kulikuwa na helikopta za usalama za Marekani zikizunguka kuhakikisha hakuna kitu chochote cha hatari kitakachosogea.


Baada ya kuondoka uwanjani hapo, haijulikani atakwenda kulala wapi, kwani zipo Hoteli zaidi ya mbili zilizolipiwa na maofisa wa Marekani na njia zote zinazoelekea katika hoteli hizo zilikuwa zimefungwa.Lakini kuna tetesi zingine kwamba huenda akaenda kulala katika moja ya vyumba vya hoteli ya The Villa Rosa Kempinski iliyokuwa na vyumba zaidi ya 200 au katika Hoteli ya Serena


Rais Barak Obama akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Msafara wa Rais Obama ukiondoka uwanja wa Jommo Kenyatta airport. 
Hoteli ya Villa Rosa Kempinski inayosadikiwa kwamba Barak Obama huenda atakwenda kupumzika.



0 Response to "OBAMA ATUA RASMI KENYA, SIMU, MAWASILIANO VYAKATIKA"

Post a Comment