HOTUBA YA RAIS BARACK OBAMA KENYA AKIFUNGUA KONGAMANO LA DUNIA LA UJASIRIAMALI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HOTUBA YA RAIS BARACK OBAMA KENYA AKIFUNGUA KONGAMANO LA DUNIA LA UJASIRIAMALI


Rais wa Marekani Barack Obama ameisifu Afrika kwa maendeleo yake ya kiuchumi, akiita, “Moja  kati ya maeneo Duniani yanayoku a kwa kasi” Aliyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa Ujasiriamali wa Dunia pamoja na mwenyekiti mwenzake Rais wa Kenya  Uhuru Kenyatta jijini Nairobi.


Katika mkutano wake wa kwanza rasmi tangu alipowasili jijini Nairobi jana  amesema kwamba; “Afrika inasonga mbele” “Watu wanaondokana na umasikini, vipato vinapanda, daraja la kati linakua, na vijana kama ninyi wanaitumia teknolojia kwa manufaa kubadilisha  mtindo ambao Afrika inafanya biashara.” Aliuambia mkutano.

Akichangia jukwaa na Obama, Kenyatta pia alionyesha matumaini kuelekea mustakabali mwema wa Bara hilo.

“Simulizi za kuvunja moyo kuhusu Afrika ni za uwongo, na kwa kweli hazijawahi kuwa kweli” Kenyatta alisema. “Waache wajue kwamba, Afrika ipo wazi na tayari kwa biashara.”

Angalia na kusikiliza hotuba hiyo ya Obama hapa (full speech)

Kongamano hilo linalenga kuchochea biashara itakayowainua Waafrika wengi zaidi kutoka kwenye umasikini na kusaidia kuzikinga  jamii dhidi ya wenye misimamo mikali.

Obama mara tu alipotua Kenya nyumbani alikozaliwa baba yake mzazi, umati mkubwa wa watu ulikuwa umejipanga mtsari  kusindikiza msafara wa magari na pikipiki, wakishangilia kwa vifijo na kupunga mikono huku helikopta ikizunguka angani.

Ripota mmoja wa Aljazeera akiwa mjini Nairobi alisema;  “Ni furaha isiyo kifani” Obama alipowasili, akaongeza kuwa Rais wa Marekani ndiyo kiongozi wa kisiasa “mashuhuri zaidi” nchini Kenya.

Siku ya Ijumaa jioni, Obama aliungana na ndugu zake wote upande wa baba. Amewahi kusema kuwa hamkumbuki vizuri baba yake  aliyemuona angali bado mdogo sana.

Baba yake alizaliwa Magharibi kabisa mwa Kenya katika kijiji kiitwacho Kogelo, pwani ya ziwa Victoria. Alikuwa mchumi na aliondoka Marekani Obama akiwa na miaka 2. Aliishi Kenya akifanya kazi serikalini mpaka mwaka 1982 alipokufa kwa ajali ya gari alilokuwa akiendesha mwenyewe akiwa umri wa miaka 46.

Mwaka 2006 Kabla hajawa Rais, Obama alifanya ziara binafsi kijijini Kogelo wanakoishi ndugu zake wengi upande wa baba.

Chanzo: Aljazeera


0 Response to "HOTUBA YA RAIS BARACK OBAMA KENYA AKIFUNGUA KONGAMANO LA DUNIA LA UJASIRIAMALI"

Post a Comment