KAMA UNATAFUTA MAFANIKIO KUNA SOMO KUBWA LA KUJIFUNZA KWA USHINDI WA TALIBANI AFGHANISTAN NA RAIS HICHILEMA WA ZAMBIA | JIFUNZE UJASIRIAMALI

KAMA UNATAFUTA MAFANIKIO KUNA SOMO KUBWA LA KUJIFUNZA KWA USHINDI WA TALIBANI AFGHANISTAN NA RAIS HICHILEMA WA ZAMBIA

Kundi la Taliban na Rais wa Zambia Hichilema
Mawili Miongoni mwa matukio makubwa duniani yaliyotokea hivi karibuni ni lile la Ushindi wa Kundi la Talibani nchini Afghanistani lililokuwa likipigana na Muungano wa Majeshi ya NATO yaliyokuwa yakiongozwa na Marekani pamoja na tukio jingine la Ushindi wa Rais Hakainde Hichilema wa nchi ya Zambia aliyemshinda hasimu wake mkuu Rais Edgar Lungu anayeondoka madarakani. 

Katika matukio yote haya mawili ingawa hayana uhusiano wa moja kwa moja lakini kuna jambo moja kubwa sana linayoyaunganisha. Yakiwa yametokea kwa nasibu ndani ya mwezi mmoja kuna kitu kikubwa ambacho mtu yeyote yule, (kikundi au taasisi,)mwenye nia au malengo ya kufanikiwa katika jambo lolote lile maishani anaweza akajifunza.

Wanamgambo wa Talibani kwa takribani miaka 20 kwa kutumia silaha duni, bila uwezo mkubwa kifedha na kiuchumi wamekuwa wakipambana na na Majeshi ya NATO yaliyokuwa na nguvu nyingi za kiuchumi, silaha, na hata ushawishi duniani kote. Ni kitu gani hicho hatimaye kilichowasaidia wanamgambo hawa kuiteka nchi nzima ya Afghanistan tena kwa siku 10 tu bila upinzani wowote toka kwa wapinzani wao NATO na majeshi ya serikali ya Rais Ashraf Ghani?

SOMA: Muhammad Ali: uvumilivu, nidhamu, ujasiri, msimamo vilimpa ubingwa Kinshasa Zaire

Mwanasiasa Hakainde Hichilema kwa muda wa miaka zaidi ya 15 amekuwa akiwania urais wa Zambia bila ya mafanikio. Katika safari yake hiyo ya kusaka mafanikio amepitia kukatishwa tamaa kwingi, changamoto za kila namna ikiwemo hata kubambikiwa kesi ya ugaidi ambayo maana yake ni uhaini na adhabu yake kwa mujibu wa sheria ingeliweza kuwa adhabu ya kifo. Lakini licha ya misukosuko yote hiyo aliendelea tu kuwa king’ang’anizi na uvumilivu wa hali ya juu bila ya kukata tamaa mpaka leo hii ambapo amefanikiwa kufikia malengo yake ya kushika uraisi wa Taifa la Zambia.

Ukiwa na MSIMAMO “huwezi kudanganyika hata kwa mbegu za mtama” Wamarekani walijaribu kuwahadaa Watalenani kwa kila njia ikiwemo hata kuahidi kushea madaraka na serikali ya Kabul lakini katu hawakutetereka wala kulegeza msimamo wao. Msimamo ni lazima uambatane na lengo kamili ambalo walikuwa nalo tayari, lengo la kusimamisha utawala au serikali yao inayofutata  Sharia za Kiislamu (Islamic Emirate of Afghanstan). Lengo kamili ni lazima pia liambatane na mipango ya kivitendo itakayotekelezwa kulifikia lengo, na Talibani utaona walikuwa na mikakati kadhaa ikiwemo mapambano na serikali na majeshi ya NATO na propaganda mbalimbali zilizosaidia Jamii ya Waafghanistan kuichukia serikali yao iliyokuwa imejaa vitendo vya rushwa na ufisadi

NATO: Rais Obama kila mtu anatakiwa apewe nafasi ya kurekebisha maisha yake

Ijapokuwa ushindi wa Taliban kwa wengi unaweza usiwe ni jambo la kufurahisha hasa ukizingatia historia na itikadi waliyo nayo dhidi ya haki za binadamu hususani wanawake na watoto, lakini ukweli unabakia palepale kwamba ni kielelezo kizuri cha kuwa na MSIMAMO katika mapambano ya kufikia lengo lolote lile maishani.

Aidha ushindi wa Taliban siyo dalili njema hata kidogo kwa Dunia na hasa Afrika kunakoonekana kuibuka kwa makundi ya kijihadi yaliyo na muelekeo na Itikadi za Al-Qaeda, ISS(Dola la Kiislamu) na makundi mengine ya misimamo mikali kama Boko haram Nigeria, Al-Shaababu kule Somalia na hata hapa jirani Msumbiji.

SOMA: Maziwa na asali vya Gadafi, Mubarak na Sadam Hussein vipo wapi?

Bila shaka makundi haya yatapata motisha, nguvu na ari mpya baada ya kuona kumbe kwa MSIMAMO kila kitu kinawezekana chini ya jua haijalishi ni muda gani utapita. Hili laweza kugeuka janga na silaha moja hatari sana. Ni tishio kubwa linaloinyemelea Dunia hasa Afrika ukanda wa Sahel

Silaha hii ya MSIMAMO hakuna mahali popote imewahi kushindwa. Inapotumiwa kwa usahihi adui utamwona akifunga virago vyake mwenyewe mithili ya NATO na Marekani kule Afghanistani au Edgar Lungu wa Zambia alivyosalimu amri kwa hasimu wake Hichilema pasipo hata kwenda mahakamani kupinga ushindi kama ilivyo kwa Wanasiasa wengi wa Afrika wanaposhindwa chaguzi.

SOMA: Kati ya Obama na Putin ni nani anayeisaidia IS?

Hata katika mapambano ya kawaida ya kusaka mafanikio kiuchumi na kimaisha kwa ujumla, silaha hii inaweza ikatumika na kufanya maajabu! Katika kitabu mashuhuri cha THINK AND GROW RICH silaha ya msimamo imepewa sura nzima ya 9. Unaweza kushangaa sana busara hizi zilizoandikwa miaka mingi huko nyuma lakini leo hii zinafanya kazi utadhani zimeandikwa jana tu.

Ukisoma ndani ya kitabu hiki namna vile MSIMAMO ulivyo na nguvu katika kufanikisha mambo unaweza kujilaumu sana nikwanini hukukisoma kitabu hiki pale tu ulipoanza kujua kusoma na kuandika, leo hii usingekuwa pale ulipo.

Nimeweka nukuu chache tu za baadhi ya aya za sura hiyo ya 9 hapa chini;

 

“MSIMAMO ni kigezo muhimu katika njia ya kugeuza SHAUKU kuwa katika kipimo chake cha fedha. Msingi wa msimamo ni NGUVU YA UTASHI”

 

Wengi wa watu wapo tayari kutupilia mbali nia na malengo yao na kukata tamaa katika dalili za mwanzo za upinzani au mkosi. Wachache huendelea licha ya upinzani wote mpaka wanafikia lengo lao. Wachache ndio kina Ford, kina Carnegie, kina Rockfellers na kina Edson.”

 

“Ikiwa unafuatilia kitabu hiki kwa lengo la kutumia maarifa kinachotoa, jaribio la kwanza la msimamo wako litakuja wakati utakapoanza kufuata hatua sita zilizoelezwa katika sura ya pili. Ikiwa kama wewe siyo mmoja wa wawili kati ya kila watu mia ambaye tayari una “lengo kamili” ambalo unalilenga na mpango kamili kwa ajili ya kulifikia, unaweza kusoma maelekezo na kisha kuendelea na ratiba zako za kila siku, kamwe usifuate maelekezo hayo.”

 

“Jihusishe mwenyewe na Kundi la Kushauriana, na jenga msimamo kupitia juhudi za ushirikiano wa wanachama wa kundi hili. Utapata maelekezo ya ziada ya kujenga msimamo katika sura ya 4 juu ya Kujishauri-binafsi na sura ya 12 juu ya Akili ya ndani.

Fuata maelekezo yaliyotolewa katika hizi Sura mpaka tabia yako ya asili ikabidhi kwa akili yako ya ndani picha halisi ya kitu unachotamani. Kutoka hatua hiyo na kuendelea, hautalemazwa tena na ukosefu wa msimamo.”

 

“Ni nguvu gani ya kimuujiza hutoa kwa watu wenye MSIMAMO uwezo wa kukabiliana na magumu? Ubora wa MSIMAMO hutengeneza katika akili ya mtu aina fulani ya shughuli za kiroho, kiakili, au kikemikali ambazo humpa uwezo wa kuzifikia nguvu za Kiungu? “

 

“Je, Nguvu kuu isiyo na mipaka(MUNGU) kawaida hujitupa yenyewe katika upande wa mtu ambaye bado anaendelea kupambana baada ya kushindwa vita, huku dunia nzima ikiwa kinyume naye?”

 

Katika kitabu hicho cha Think & Grow Rich (FIKIRI NA UTAJIRIKE) tafsiri orijino kwa kiswahili ya mwaka 2021 Sura ya 9 ya MSIMAMO inazungumzia maswala mengi wakiwemo watu mbalimbali mashuhuri Duniani walivyotumia silaha ya MSIMAMO katika kufanikisha malengo yao wakiwemo Mitume, Manabii na viongozi mbalimbali waliowahi kutokea Duniani mfano akina Mtume Muhamad, Yesu Kristo, Mahatma Ghandi, Badhi ya wafalme na Marais wa Taifa la Uingereza, Marekani na wengineo wengi.

SOMA: Je, wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya madogomadogo?

Kitabu cha Think & Grow Rich ni watu wachache sana wanaoujua ukweli kwamba ndio kitabu cha kwanza Duniani kilichoandika kwa ukamilifu zaidi kuhusiana na Elimu ya Fedha na Mafanikio, kinatambulika dunia nzima kwamba ndiyo Baba wa vitabu vingine vyote vya Mafanikio na ushahidi wa jambo hili utakutana nao kwa karibu kila mwandishi au mhamasishaji wa elimu ya mafanikio duniani, wote wanakiri na wanakubaliana na FALSAFA ya NAPOLEON HILL katika kitabu hiki na wengi wao mafundisho yao ni yaleyale yanayopatikana katika kitabu hiki.

Binafsi wakati fulani katika harakati za kusoma vitabu mbalimbali niligundua kwamba karibu kila mwandishi nguli wa Elimu ya mafanikio duniani niliyemsoma anakiri kwa namna moja au nyingine kwamba moja ya vitabu au watu waliomhamasisha zaidi kwenye elimu ya fedha na mafanikio alikuwa ni Napoleon Hill na kitabu chake cha Think & Grow Rich. Sasa nikawa najiuliza hivi:-

“Ikiwa kama kila mwandishi mashuhuri wa mafanikio duniani anakiri kuhamasishwa na kitabu cha Napoleo Hill cha Think & Grow Rich kwanini basi nisianze na kitabu hicho kwanza kukisoma ndipo nisome hivyo vya waandishi wengine?”

Swahi hili ndilo lililosababisha hatimaye mimi kuanza safari ya kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya kiswahili kwani baada tu ya kumaliza kukisoma niligundua hazina kubwa liyokuwa imejificha ndani ya kitabu hiki na ambayo kuna watu wengi walikuwa wakiikosa kwasababu tu ya kushindwa kuelewa kiingereza sawasawa au kuona kazi ngumu kusoma kwa lugha wasiyoizowea.

 

JINSI YA KUKIPATA KITABU CHA THINK AND GROW RICH-SWAHILI EDITION 2021 (FIKIRI & UTAJIRIKE)


KITABU CHA KARATASI / HARD-COPY

(1)        Dukani(Bright Future Books & Stationery): Lipo Mbezi Kimara, Kibanda cha Mkaa karibu na St. Augustino Sekondari TAGASTE, Kituo cha bajaji – KWA MOTA. bei dukani ni tsh. 20,000/=(Elfu ishirini tu)

 

(2)        Kuletewa mpaka ulipo: Kama upo Dar es salaam tunakuletea kwa Tsh. 22.000/=(Elfu 22).

Ukiwa mikoa mingine tunatuma kwa mabasi kwa Tsh. 30,000/= (Elfu 30)

 

KITABU NAKALA-TETE / SOFTY-COPY

1.  Kinapatikana katika mtandao wa GETVALUE kwa anuani(link) ifuatayo ikiwa unatumia Simu ya Smartphone,

FIKIRI NA UTAJIRIKE (THINK & GROW RICH-SWAHILI EDITION 2021)

 

 

VITABU NA HUDUMA NYINGINE  TOKA KWETU

1)  Vitabu vyetu vingine vyote vinapatikana kwa mifumo yote, vya karatasi(hardcopy) lakini pia Softcopy kupitia Email au Watsap.





2)  Vya karatasi unaweza kufika katika duka lililotajwa hapo juu(BRIGHT FUTURE BOOKS & STATIONERY) au ukawasiliana nasisi tukakuletea ulipo.

3)  Kwa Softcopy Lipia kitabu husika kisha tutumie anuani yako ya email au namba ya watsap tutakutumia kitabu/vitabu muda huohu.


Mawasiliano yetu ni:

Simu / Watsap: 0765553030  au  0712202244  jina ni Peter Augustino Tarimo

 

 

KUANDIKIWA MCHANGANUO/MPANGO WA BIASHARA (BUSINESS PLAN)

(1)        Tunatoa huduma ya kuandika mchanganuo / Mpango mzima wa biashara yeyote ile (Full business plan)  kubwa na ndogo kwa gharama nafuu sana. Tunakutumia maswali yanayohusiana na biashara yako unajibu kwa kifupi, na kisha baada ya hapo kazi nyingine unatuachia sisi. Kuona baadhi ya kazi zetu tulizofanya bonyeza hapa

 

(2)        Tunafanya makisio katika Sehemu/Kipengele cha Fedha cha Mchanganuo wa Biashara kwa yule ambaye ameshaandika sehemu nyingine zote lakini kwa kipengele hiki akahitaji usaidizi. Gharama yake ni ndogo kulinganisha na gharama ya kuandika mchanganuo mzima.


KUJIUNGA NA GROUP NA CHANNEL YA MICHANGANUO-ONLINE (MASTERMIND-GROUP)

1)  Kwa shilingi elfu 10 (10,000/=) tu kwa mwaka mzima unajiunga na group la watsap ambalo tunajifunza kila siku Michanganuo ya Biashara mbalimbali zenye ubunifu kwa mtaji mdogo pamoja na Masomo yenye maudhui ya Fedha. Pia tunakuwa na semina za mara kwa mara juu ya uandishi wa Michanganuo ya biashara.

Kujiunga na Group Lipia kiingilio chako kupitia namba 0765553030 au 0712202244 kisha tuma ujumbe; "NIUNGANISHE NA MASTERMIND GROUP LA MICHANGANUO2021"

 

SIMU:       0712202244

WATSAP: 0765553030

 

0 Response to "KAMA UNATAFUTA MAFANIKIO KUNA SOMO KUBWA LA KUJIFUNZA KWA USHINDI WA TALIBANI AFGHANISTAN NA RAIS HICHILEMA WA ZAMBIA"

Post a Comment