MAZIWA NA ASALI VYA GADAFI, MUBARAK, NA SADAM HUSSEIN VIPO WAPI? | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAZIWA NA ASALI VYA GADAFI, MUBARAK, NA SADAM HUSSEIN VIPO WAPI?

Wakati mwingine mimi hawa wazungu huwa wananishangaza sana, kabla ya mapinduzi walikuwa hawaishi kupiga kelele, “demokrasia demokrasia”…..sijui haki za binadamu, uhuru wa kuabudu na mambo chungu nzima yanayofanana na hayo. Hatimaye Sadamu Hussein alingoka tena kama haikutosha wakamtia na kitanzi juu. Vivyo hivyo ikafuatia na kwa Muamar Ghadafi na swahiba yake Mubarak wa masri.

Hayati Muamar Ghadafi
Baada ya Mubarak kungolewa huku wazungu hao hao wakiwa kimya, kila mtu alifikiri sasa Misri itakuwa nchi ya kidemokrasia kama Marekani, wala hakuna mtu aliyejishughulisha kufikiria matokeo yaliyoonekana Iraq na hata Libya. Hali ilikuwa mbaya zaidi kushinda kabla ya mapinduzi, Alqaeda wameigeuza Iraq dimbwi la damu na huko Libya ilikuwa aibu tupu, balozi wa waokozi wa Walibya kugeukwa na kuuwawa mithili ya  paka na wale waliodaiwa kukombolewa.


Hayati Saddam Hussein
Mohamed Mursi alipoingia madarakani nilishuhudia Wazungu hao hao walioshangilia kungonga kwa aliyekuwa kipenzi chao wakati fulani  Hussein Mubarak wakiupokea ujio huo kwa tashwishi ya hali ya juu kwa kuwa hawakutegemea hata kidogo kwamba chama cha kiislamu kingeshinda uchaguzi, walijutia kuondolewa Mubarak. Kipindi kifupi Mursi alichokuwa madarakani tukashuhudia vitimbi kibao, vyombo vya habari nya Magharibi kama kawaida ya vikaanza kuchimb chimba kila kona Misri wakilalama Chama cha Udugu wa kiislamu kilikuwa kinaminya uhuru wa wachache na kilikuwa na njama za kuigeuza Misri kuwa Taifa la Kiislamu kama Iran.

Madai hayo yalilipa jeshi nguvu ya kumngoa Musri, na badala ya kuliunga tena mkono, wamenishangaza tena juzi wakiwalaani wanajeshi. Sasa Wazungu hawa wanachokitaka ni nini? Hawataki moto wala baridi,  lakini pia cha ajabu hata uvuguvugu pia inaonekana hawapendi. Tatizo kubwa kwa nchi za Kimagharibi ni kutaka kushinikiza aina yao ya demokrasia kwa mataifa mengine pasipo kuelewa kuwa Nchi hasa za Kiafrika na zile Za Kiarabu zina tamaduni zao tofauti kabisa na zile za kwao.

Rais wa zamani Misri Hussein Mubarak

Kabla ya mapinduzi nchi za Libya, Irak, Misri, Tunisia na sasa Syria wananchi wake walikuwa wakiishi maisha mazuri na  ya amani, inasadikiwa kama Libya ilikuwa hata mtu ukitaka kuoa serikali  ilikuwa ikikugharamia kila kitu. Sasa hivi kila mtu anashangaa ! , yale maziwa na asali viko wapi tena?


0 Response to "MAZIWA NA ASALI VYA GADAFI, MUBARAK, NA SADAM HUSSEIN VIPO WAPI?"

Post a Comment