Huu ni mfululizo wa masomo yahusuo mfumo wetu wa
bure wa usimamizi wa fedha na wateja kwenye biashara za rejareja, FOREVER
FREE POS & CRM, mfumo ambao ni mkombozi kwa wafanyabiashara na
wajasiriamali wadogo wasiofikia viwango vya kulipia mifumo mikubwa. Mfumo huu
una vipengele (features) zote muhimu
zinazokidhi biashara ndogo na za kati
Katika somo letu la kwanza kabisa tutakwenda kuona
jinsi ya kuanza kuutumia mfumo huu, mtu yeyote awe ana biashara tayari au bado
anapanga tu kuja kuwa nayo hapo baadae anaweza akaanza kuweka mfumo huu katika
simu ama kompyuta yake kwa lengo la kuufanyia mazoezi kabla hajaanza rasmi
kuutumia
Ikiwa kama unayo biashara tayari, ni vizuri ukaanza
moja kwa moja kuutumia bila kusita ukiweka bidhaa kwani hata ukikosea utafanya
marekebisho taratibu kadiri muda unavyokwenda na kwa kuwa utakuwepo darasani na
mwalimu huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani utauliza chochote na kupewa majibu
Ikiwa unapenda kuanza kuufanyia majaribio mfumo
bado huna biashara, napo ni rahisi tu kwani nitakuonyesha kuunda bidhaa za
bandia pamoja na jinsi ya kuziuza huku ukiona namna ripoti zinavyokuwa na stoku
ya bidhaa hizo inavyopungua dukani kama tu inavyokuwa kwenye duka la ukweli
Kutumia mfumo wowote ule hakuna tofauti na
kuendesha gari, ukishafahamu kuendesha gari mfano aina ya Toyota, moja kwa moja
gari nyinginezo hata iwe Ford sijui Mercedez benz hazitakupiga chenga kwani
tayari umeshazijua ABC za udereva
Na hii mifumo ndiyo hivyohivyo ilivyo, ukishafahamu
kutumia mfumo mmoja hata ukija hapo baadae kubadilisha mfumo ukatumia mwingine haitakupa
shida, hivyo mafunzo haya ya bure na mfumo wa bure ni vya thamani kubwa mno kwa
mjasiriamali mwenye ndoto ya kufika mbali kwenye ulimwengu wa kufanya biashara
inayojiendesha yenyewe hata ikiwa haupo pale muda wote
JINSI YA
KUFUNGUA AKAUNTI YA MAJARIBIO YA FOREVERFREE POS & CRM
Forever free POS & CRM
inaruhusu mtu yeyote kufungua akaunti ya majaribio, na hii ndiyo njia bora
zaidi ya kujifunza jinsi mfumo unavyofanya kazi kabla ya kuanza biashara
Hapa kuna mambo unayoweza kufanya kwenye akaunti
hiyo ya majaribio:
Unachoweza kufanya kwa majaribio
(1)
Kuweka bidhaa za bandia: Unaweza
kuongeza jina la bidhaa, bei na kiasi cha stoku mfano "Shati la
Majaribio" - shilingi 10,000/=
(2)
Kufanya mauzo ya bandia/mfano: Unaweza
kubofya bidhaa, kupokea malipo ya bandia taslimu "Cash", na kuona
jinsi mzigo (stoku) unavyopungua
(3)
Kuangalia ripoti: Unaweza kuingia kwenye tovuti (Back Office) kuona grafu na ripoti za
mauzo uliyoyafanya kwa majaribio, kumbuka kuna vitu viwili, APP na TOVUTI, na
ukitaka kuingia kokote ni lazima ujisajili kwa email na nenosiri lako
Jinsi ya kuanza
Pakua app ya kwenye simu au tablet yako
Bofya neno Sign Up na ujaze barua pepe
(email) na neno la siri (password)
Chagua aina yeyote ile ya biashara, yaweza kuwa ni;
Biashara ya duka la rejareja, mkahawa, mama lishe, grocery, kioski, genge, duka
la dawa baridi, biashara ya kuuza nguo za mitumba, dula la nafaka, bucha la
nyama, saluni nk. ili uanze
Baada ya
kumaliza kujifunza, unaweza kufuta bidhaa hizo na kuweka bidhaa halisi
utakapoanzisha duka lako halisi
.........................................................
SOMO
HILI KAMILI NA KWA VITENDO LINAPATIKANA KWENYE GROUP LA TANZANIA RETAILERS
PREMIUM GROUP (TRPG)
Mwanachama ni mtu yeyote
mwenye nakala ya kitabu cha MAFANIKIO YA
BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION 2027
Kupata nakala yako tuma
ujumbe whatsapp usemao “NATAKA
KITABU NA DARASA” kwa namba 0761002125
Au
bofya hapa kupata kitabu na darasa sasa hivi
Ndani
ya group pia kuna;
(1) Machimbo
yote ya bidhaa za bei rahisi Kariakoo na nchi nzima
(2) Ubunifu
wa biashara kwa wajasiriamali wa maudhui mtandaoni (Content creators) - watajifunza jinsi ya kuanza biashara mtandaoni
bila kutumia vifaa vya gharama kubwa
(3) Aidha
washiriki wanaweza kuuliza swali lolote kuhusu mada na mifumo yote iliyopo kitabuni,
ile ya kianalojia (madaftari) na ile ya kidijitali (POS, Accounting Software,
ERP, CRM nk.)
SOMA NA HIZI PIA;
1.
Chuma ulete anavyowatesa wenye maduka na wafanyakazi wao dar
2.
Biashara 7 nzuri za kufanya zitakazokuingizia pesa
hata kama umelala
3.
Siri ya kupata mtaji wa biashara
kirahisi kwa mjasiriamali mdogo asiye na dhamana mjini na kijijini
4.
Njia mpya za kufanya mambo: dunia,
biashara, ajira vinabadilika kwa kasi ya ajabu
5.
Mawazo ya biashara zitakazovuma
miaka ijayo 2018 na kuendelea mpaka 2030
6.
Mfumo mpya wa bure wa kusimamia biashara ya duka la rejareja
(forever free pos & crm)
7.
Duka linalojiuza lenyewe bila mhudumu/muuzaji
8.
Eti ni kweli biashara ya genge la matunda na mbogamboga ina
faida nusu kwa nusu?
9.
Duka la rejareja ukitumia silaha (nyenzo) hizi 2 umetoboa kwa
urahisi sana
10. Biashara ya vinywaji jumla, mtaji milioni moja (1) naomba
ushauri

0 Response to "JINSI YA KUFUNGUA AKAUNTI FOREVERFREE POS & CRM - SOMO LA KWANZA"
Post a Comment