UAMUZI WA KUCHUKUA HATUA HIZI (3) UTARAHISISHA KUFIKIA MAISHA MAZURI UNAYOTAMANI KUISHI DUNIANI NA AKHRERA

MAISHA MAZURI DUNIANI NA AKHERA

Nashindwa kuandika makala hii ya leo bila ya kumhusisha hata kidogo Marehemu Dr. Reginald Abrahamu Mengi. Nikiri tu kwamba mzee huyu watu wengi nikiwemo na mimi binafsi tulivutiwa sana na kuhamasishwa na maisha yake katika nyanja mbalimbali japo sisemi ni katika kila alichokifanya kwani kama binadamu mwingine yeyote yule hawezi kukosa naye kuwa na baadhi ya mapungufu yake.

Kuna mambo makubwa matatu (3) muhimu sana mtu yeyote anayetaka kufanikiwa katika jambo lolote lile maishani anapaswa kuyazingatia. Katika mambo hayo 3 nitakayoyazungumzia kuna moja ambalo ndilo kiini cha mambo mengine mawili na hili si jingine bali ni KUCHUKUA HATUA au UTEKELEZAJI.

SOMA: Mawazo mengi hufa kabla hayajazaliwa, ili kupona yanahitaji mipango na vitendo.

Uchukuaji wa hatua tumewahi kuzungumzia mahali pengi sana na siyo jambo geni hata kidogo masikioni mwa watu wengi. Katika kuyazungumzia mambo hayo matatu, kwa heshima kubwa ya Marehemu Mzee wetu Reginald Mengi ambaye tumemuaga siku ya leo rasmi yeye akitangulia nasi tukisubiri kufuata, nitakuwa nikichomekea vipande kadhaa vinavyohusiana na yale aliyoyafanya na kuyaishi alipokuwa hai.

Hivyo natanguliza kuomba radhi kwako wewe ambaye pengine kwa namna moja ama nyingine usingependezwa na hilo. Najua kuna watu wengine huwa hawapendi kusikia sana habari za mtu hasa sifa baada ya kutangulia mbele za haki, wengine huwa hawapendi kutokana tu na majonzi au sababu zingine zozote zile.
Kama nilivyotangulia kusema, leo nina mambo matatu 3 makubwa na kabla sijaenda kuyaelezea moja baada ya jingine hebu kwanza niyataje yote matatu 3 hapa;

1.  UAMUZI
2.  KUCHUKUA HATUA
3.  MSIMAMO THABITI


2. KUCHUKUA HATUA
Nimetangulia kusema pia kwamba kiini cha mambo hayo 3 makubwa ni KUCHUKUA HATUA au kwa lugha nyingine unaweza ukasema UTEKELEZAJI(Implementation). Kwa kweli kwa yeyote aliyewahi kukisoma kitabu changu kiitwacho; “KANUNI YA KUJIFUNZA ELIMU YA PESA NA MAFANIKIO” atakuwa na ufahamu mkubwa sana juu ya mantiki hii ya Utekelezaji au Uchukuaji wa hatua nitakayoizungumzia leo.

SOMA: Kwanini vitabu na semina za elimu ya pesa na mafanikio haviwasaidii watu wengi?

Unajua Dunia katika karne tunayoishi leo kumejaa kila aina ya taarifa zilizokuwa nzuri na mbaya ambazo mtu unaweza kuzipata muda wowote utakao katika ncha ya vidole vyako. Karibu kila kitu tunachohitaji kukijua kipo karibu kabisa na sisi kupitia mtandao wa Intaneti.

Lakini kuna jambo moja muhimu sana, kila kitu unachosoma mtandaoni au mahali pengine popote pale mfano kutoka kwenye vitabu, majarida nk. kuhusiana na jinsi ya kukuza biashara yako, namna ya kuboresha afya yako, masomo na course aina zote unazoweza kuzitaja hapa hazina maana yeyote ile ikiwa hautachukua hatua ya kuteleza yale uliyojifunza au kuyapanga.

SOMA: Ni kitabu gani hautakisahau maishani?

Hebu hapo ulipo sasa hivi jiulize hivi, katika vitabu vyote ulivyowahi kusoma au katika mipango ya biashara yote uliyowahi kuipanga , ungelikuwa wapi leo hii ikiwa kama ungelichukua mafunzo uliyoyapata kutoka katika kitabu kimoja tu au mpango mmoja tu uliopanga na ukafanyia utekelezaji barabara kwa kila ulichojifunza au kupanga. Sina shaka yeyote ile kwamba leo hii ungelikuwa ni mmoja wa Mabilionea au tuseme matajiri wakubwa Tanzania.

Nataka tu uelewe kwamba, Mpango mmoja utakaotekelezwa vizuri una nguvu kubwa kushinda maarifa lukuki utakayoyapata kwa kusoma vitabu elfu moja(1000) ambayo hautayafanyia utekelezaji wowote ule. Dr. Reginald Mengi alikuwa ni mtu wa kuchukua hatua, mfano ni pale alipokuwa na wazo la kuanzisha viwanda, ijapokuwa kipindi hicho kulikuwa na ukiritimba mkubwa ndani ya mifumo ya nchi, yeye hakusema, “acha tu nisubiri mpaka sera za nchi ziwe nzuri” alianza hivyohivyo.

SOMA: Bilionea Dr. Reginald Mengi hakufa na sirwi yeyote moyoni, unajua siri zote alimwachia nani?

Nadhani kwa waliokuwa wanafunzi enzi hizo mika ya 80 wanaweza kukumbuka vizuri sana kalamu za EPICA jinsi zilivyokuwa zikichuana vikali na kalamu nyinginezo kongwe zilizokuwepo wakati huo kama vile BIC na SIMBA, Kumbe Epica ilikuwa ni bidhaa yake ya kwanza kabisa aliyoiasisi Marehemu Dr. Mengi kama mwanaviwanda aliyekuwa na maono makubwa ya siku moja kuja kuwa miongoni mwa Mabilionea wa Bara la Afrika.

Pia wakati Mengi akianza biashara hakuwa na mtaji, na hilo kamwe halikuweza kumzuia kuchukua hatua, alikwenda kukopa benki akaanza any way. Akiwa na ndoto ya kuingia kwenye biashara Mengi ilimbidi kwanza kuchukua hatua muhimu ya kujiuzulu wadhifa aliokuwa nao kwenye ajira yeke katika kampuni kubwa duniani ya Uhasibu ya Cooper and Lybrand (Prince water house Cooper) 

SOMA: Mzee Reginald Mengi hajafa, ataendelea kuishi katika roho zetu siku zote.

Unapoamua kuchukua hatua, chukua hatua tu katika vitu vile vitakavyokuwa na athari kubwa chanya juu ya maisha yako, (vitakavyoacha alama) mfano chukua hatua kwa jambo litakalokusaidia kupata kazi nzuri, kutengeneza fedha nyingi, kuboresha afya yako zaidi, kuboresha mahusiano yako zaidi na watu wengine au kufikia lengo lolote lile ambalo litakuwa chanzo cha furaha yako na kujitosheleza zaidi wewe na wengine katika maisha yako hapa Duniani na baada ya kufa akhera kama alivyofanya Dr. Reginald Mengi.

    1. MAAMUZI
Sijakosea kuweka namba 1. Kabla ya neno Maamuzi na namba 2 kabla ya neno Kuchukua hatua. Kabla mtu hujachukua hatua ni lazima kwanza ufanye UAMUZI. Lakini kwa kuwa KUCHUKUA HATUA ndio neno lililobeba zaidi mada yetu hii ya leo ndio maana nikaona nianze nalo kwanza kule juu.

SOMA: Uamuzi wa kushangaza uliokuwa chanzo cha uhuru wa Taifa la Marekani.

Hali yeyote ile inaweza ikabadilishwa wakati wowote ule, unaweza ukatatua tatizo lolote lile, kuboresha hali yeyote ile mbaya na kufikia ndoto yeyote ile, lakini ni lazima kwanza mtu ufanye Uamuzi ukifuatiwa na Kuchukua hatua. Ikiwa kwa mfano huipendi kazi unayoifanya unaweza ukafanya uamuzi wa kutafuta kazi nyingine.

Ikiwa una mgogoro na mpenzi/mke/mume wako uamuzi wa busara siyo kuchukua hatua ya kuachana naye ghafla, bali kutafuta kwanza suluhu kwa njia mbalimbali ikiwamo kukaa na kuzungumza kwa uwazi wote wawili. Kuachana litakuwa ni jambo la mwisho kabisa ikitokea kila njia imeshindikana. Ikiwa unakabiliwa na tatizo la kiafya, chukua maamuzi stahiki kama vile kuanza matibabu, mazoezi nk. kuboresha hali hiyo na ikiwa unataka kutimiza lengo fulani lakini huna ujuzi au uzoefu stahiki, uamuzi mzuri ni wa kutafuta ni wapi unaweza ukapata mafunzo hayo na uzoefu.

SOMA: Je wajua siri nyingi za mafanikio zimejificha kwenye mambo haya manne madogomadogo?

Baadhi ya hatua hizi zitakulazimu wakati mwingine utoke nje ya ukanda wako wa faraja(Outside your comfort zone). Wakati mwingine utakutana na vigingi au hata kuanguka kabisa lakini ukumbuke kwamba katika kila hatua itakuwa ikikusogeza karibu zaidi na malengo uliyojiwekea.

Mzee wetu Dr. Reginald Mengi katika moja ya maamuzi yake kulingana na hotuba aliyoitoa rafiki yake kipenzi Mzee Felix Mosha katika Ibada ya mazishi kwenye kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Moshi mjini leo. Mzee Mosha alisema kwamba Mengi aliwahi kuchukua uamuzi mgumu wa kuwataja Mafisadi 5 kati ya 10, jambo lililokuwa ni la hatari mno kwake. Mosha alipomuuliza Dr. Mengi kuwa ni kwanini alifanya vile bila hata ya kutaka ushauri kwake, alimjibu kwamba, angemshirkisha asingekubali, angemshauri kuacha kuwataja.

SOMA: Hakuna mbadala wa msimamo, kila anguko huja likiwa na mbegu yenye faida ndani yake.

Mosha amesimulia pia jinsi Mzee Reginald Mengi alivyokataa kuwekeza katika kiwanda cha sigara licha ya faida nono ambayo angeliweza kuja kuipata kwa sanbabu ya kujali afya za watu ambao wangeathirika na madhara ya sigara hizo. Uwezo wa kufanya maamuzi haraka na kwa wakati ulimfanya Dr. Mengi kuwa mjasiriamali wa kipekee.


    1. MSIMAMO THABITI
Ukishafanya maamuzi na kuchukua hatua stahiki, utahitaji kuwa na msimamo thabiti ili kudumisha yale uliyolenga kuyatimiza. Mzee Mengi anatajwa kuwa ni mtu aliyekuwa na msimamo usioyumbishwa kirahisi licha ya kuwa pia alikuwa ni mtu mwenye unyenyekevu mkubwa. Alichokiamini kamwe hakupenda kwenda kinyume chake ingawa pia aliheshimu sana misimamo na mitazamo ya watu wengine. Hili unaweza hata kuliona katika maisha yake binafsi ambayo kwa kweli si haki wala ruksa kuweza kuyaandika hapa. PUMZIKA KWA AMANI BABA YETU MENGI.

MWISHO

.............................................................................................TAARIFA:
HII NI KWA YULE TU AMBAYE HAJAJIUNGA BADO NA GROUP LA (WASAP MASTERMIND GROUP) LA MICHANGANUO-ONLINE AU KUSOMA VITABU VYA SELF HELP BOOKS

Najua wapo wadau ambao ni mara ya kwanza kuingia katika blogu hii na bado hawajazijua  Programu zetu nyingine kama wale waliotangulia, hivyo naomba kuchukua nafasi hii kidogo kuwajulisha Programu hizo.

PROGRAMU#1
SELF HELP BOOKS TANZANIA tuna vitabu mbalimbali vya ujasiriamali katika lugha ya Kiswahili na miongoni mwavyo ni hivi vitabu vikuu vitatu vifuatavyo;

1.MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI
2.MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA
3. MIFEREJI 7 YA PESA NA SIRI MATAJIRI WASIOPENDA KUITOA.

Vitabu vyote 3 softcopy kwa njia ya email ni sh. Elfu 18 na hardcopy kama upo Dar es salaam unaletewa ulipo kwa sh. Elfu 37. Unaweza kupata kimojakimoja pia. Ukinunua vitabu vyote 3 softcopy unapata pia offa ya kujiunga na MASTERMIND GROUP la wasap bure pamoja na michanganuo kadhaa na vitabu vingine 4 bila malipo yeyote.

PROGRAMU#2
MASTERMIND GROUP LA WATSAP
Tunalo group la masomo na mijadala ya kila siku WASAP ambalo tunajifunza hasa Vitu 2 kwa undani, Jinsi ya kuandaa michanganuo ya biashara mbalimbali zinazolipa haraka pamoja na masomo yenye maudhui ya pesa(MZUNGUKO WA FEDHA KWENYE BIASHARA ZETU). Ada ya kujiunga ni sh. Elfu 10 tu mwaka mzima na punde baada ya malipo tunakutumia kupitia wasap au email vitu vyote hivi vifuatavyo;

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Kitabu kipya cha masomo ya Mzunguko chanya wa fedha 2018 part 1

3.  Kitabu kipya cha Masomo ya fedha 2018 part 2

4.  Kitabu kipya 1 cha jinsi ya kuandika michanganuo ya biashara hatua kwa hatua.

5.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

6.  SEMINA: Masomo 11 ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

7.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

8.  Mchanganuo wa biashara ya mgahawa(JANE RESTAURANT) kwa Kiswahili na kiigereza

9.  Mchanganuo wa biashara ya kilimo cha matikiti maji.

10.              Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

11.              Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENT SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

12.              Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

13.              Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

PROGRAMU#3
PACKAGE NZIMA(kifurushi) cha semina kubwa ya jinsi ya kuandaa hesabu za mpango wa biashara(ADVANCED BUSINESS PLAN FINANCIALS) katika mfumo wa PDF. Bei yake ni sh. 10,000(Bado ipo kwenye offa, baadae itarudia bei yake ya kawaida sh. elfu 20)

UKITAKA PROGRAMU ZOTE 3 KWA PAMOJA KATIKA SIMU, KOMPYUTA AU TABLET YAKO NI SH. ELFU 38 TU.

ASANTE SANA,

PETER A. TARIMO

self help books Tanzania

0 Response to "UAMUZI WA KUCHUKUA HATUA HIZI (3) UTARAHISISHA KUFIKIA MAISHA MAZURI UNAYOTAMANI KUISHI DUNIANI NA AKHRERA"

Post a Comment