MAWAZO MENGI HUFA KABLA HAYAJAZALIWA, KUPONA YANAHITAJI MIPAGO NA VITENDO | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MAWAZO MENGI HUFA KABLA HAYAJAZALIWA, KUPONA YANAHITAJI MIPAGO NA VITENDO


SURA YA 9 THINK AND GROW RICH, FIKIRI UTAJIRIKE
Baadae katika maisha nilipokuja kuwa nimewachunguza maelfu ya watu niligundua kwamba, MAWAZO MENGI HUFA KABLA HAYAJAZALIWA NA HUHITAJI PUMZI YA UHAI KUPULIZIWA NDANI YAKE KUPITIA MIPAGO KAMILI YA VITENDO VYA HARAKA: Muda wa kulilea wazo upo wakati ule wazo hilo linapozaliwa. Kila dakika linayoishi lipatie fursa nzuri ya kupona. Hofu ya lawama ipo chini ya maangamizi ya mawazo mengi ambayo kamwe hayawezi kufikia hatua ya mipango na vitendo.

Watu wengi wanaamini kwamba mafanikio ya mali ni matokeo ya bahati. Kuna dalili ya msingi kwa imani hii, lakini wale wanaotegemea moja kwa moja kwenye bahati karibu mara zote hukatishwa tamaa kwasababu hawatilii maanani kigezo kingine muhimu ambacho ni lazima kiwepo kabla mtu hajawa na uhakika wa mafanikio. Ni ujuzi ambao kupitia huo ndipo bahati inaweza kupatikana.

Chunguza watu 100 utakaokutana nao, waulize ni kitu gani wanachopendelea zaidi katika maisha na 98 kati yao hawataweza kukuambia. Ikiwa utawabana wakupe jibu, baadhi yao watasema, ulinzi, wengi watasema ni pesa, wachache watasema furaha, na wengine watasema umaarufu na nguvu na bado wengine watasema kukubalika kijamii, urahisi wa maisha, uwezo wa kuimba, kucheza au kuandika, lakini hakuna hata mmoja kati yao  atakayeweza kuelezea vitu hivi au hata ishara kidogo ya mpango ambao wanategemea kufikia haya matamanio yasiyokuwa wazi.

Matajiri hawashawishiwi na matamanio, wanashawishika tu na mipango kamili inayosaidiwa na shauku kamili, kupitia msimamo thabiti.

Jinsi ya Kukuza Msimamo.
Kuna hatua rahisi nne zinazosababisha tabia ya uvumilivu. Hazihitaji kiasi kikubwa cha akili, wala kiwango fulani cha elimu na lakini huhitaji muda au nguvu kidogo. Hatua hizo muhimu ni;
1.  LENGO DHAHIRI LIKISAIDIWA NA SHAUKU KUBWA KWA AJILI YA KULITIMIZA

2.  MPANGO KAMILI ULIOELEZWA KATIKA WAKATI ULIOPO

3.  AKILI ILIYOFUNGWA KABISA DHIDI YA VISHAWISHI VYOTE HASI NA VYENYE KUKATISHA TAMAA, ukiwemo ushauri hasi wa ndugu, marafiki na jamaa.

4.  USHIRIKIANO WA KIRAFIKI NA MTU MMOJA AU ZAIDI AMBAYE ATAKUTIA MOYO KUFUATA MPAKA MWISHO VITU VYOTE VIWILI MPANGO NA LENGO
Hatua hizi nne ni muhimu kwa mafanikio katika nyanja zote za maisha. Lengo zima la kanuni 13 za falsafa hii ni kukuwezesha kuchukua hatua hizi nne kama suala la tabia.

Ni hatua ambazo waweza kudhibiti hatima yako kiuchumi.

Ni hatua zinazoleta uhuru na kujitegemea kifikra.

Ni hatua zinazoleta utajiri katika kiasi kikubwa au kidogo

Ni hatua zinazoongoza njia ya kuelekea madaraka, umaarufu na kutambulika kidunia.

Ni hatua zinazohakikisha  bahati.

Ni hatua zinazobadilisha ndoto kuwa katika kitu halisi.

Ni hatua ambazo husababisha pia katika kuishinda hofu, kukata tamaa na kutokujali.

Kuna malipo mazuri kabisa kwa wale wote wanaochukua hizi hatua nne. Ni upendeleo wa kuandika tiketi yako mwenyewe na ya kufanya maisha kutoa zawadi yeyote inayoombwa. Ni nguvu gani ya siri hutoa kwa watu wenye msimamo, uwezo wa kukabiliana na magumu?

Ubora wa msimamo hutengeneza katika akili yako aina fulani ya shughuli za kiroho, kiakili, au kikemikali ambazo hukupa uwezo wa kuzifikia nguvu za kiungu? Uwezo usiokuwa wa kawaida hujitupa wenyewe katika upande wa mtu ambaye bado anapambana baada ya kushindwa vita, huku dunia nzima ikiwa kinyume naye?

Maswali haya na mengine yanayofanana nayo yanaibuka katika akili yangu kama nilivyowachunguza watu kama kina Henry Ford, ambao walianza tokea mwanzoni na kujenga himaya kubwa ya kiviwanda wakiwa hawana chochote kingine njiani walipoanza zaidi ya msimamo. Au Thomas A. Edison  ambaye kwa elimu ya chini ya miezi 3 alikuwa mgunduzi aliyeongoza duniani na kubadilisha msimamo kuwa mashine inayozungumza, mashine ya picha zinazotembea pamoja na taa ya balbu, achilia mbali mamia mengine ya uvumbuzi ulio na manufaa alioufanya.

Nilikuwa na upendeleo wenye furaha wa kuwachunguza wote awili, Bwana Edison na Bwana Ford mwaka hadi mwaka kwa kipindi kirefu, na fursa ya kuwachunguza kwa karibu. Kwahiyo nazugumza kutokana na uzoefu halisi wakati ninaposema kwamba sikupata sifa mbadala ya msimamo kati yao wote wawili ambayo hata kwa mbali ilichangia chanzo kikubwa cha mafanikio yao ya kushangaza.


Kama mtu anafanya uchunguzi usiokuwa na upendeleo juu ya watu hawa waliofanikiwa ataishia katika hitimiisho lisiloepukika kwamba, msimamo, msisitizo wa juhudi na ukamilifu wa lengo ndio vyanzo vikubwa vya mafanikio yao. 

MWISHO WA SURA YA 9 


 SOMA SURA NA SEHEMU ZOTE HAPA


0 Response to "MAWAZO MENGI HUFA KABLA HAYAJAZALIWA, KUPONA YANAHITAJI MIPAGO NA VITENDO "

Post a Comment