HAKUNA MBADALA WA MSIMAMO, KILA ANGUKO HUJA LIKIWA NA MBEGU YENYE FAIDA NDANI YAKE | JIFUNZE UJASIRIAMALI

HAKUNA MBADALA WA MSIMAMO, KILA ANGUKO HUJA LIKIWA NA MBEGU YENYE FAIDA NDANI YAKE



Napole Hill katika sura hii anazungumzia jinsi ambavyo msimamo unaweza hata kuhamisha milima, amesimulia kisa kimoja ambacho hata wewe ndugu msomaji sina shaka kama hujawahi kukutana nacho siku moja, JINAMIZI LA USIKU.

Ameelezea vizuri sana namna ambavyo binadamu bila ya kujijua unavyoweza ukatumia nguvu kubwa ya Msimamo katika kukabiliana na jambo la kuogofya kabisa kama jinamizi linalokuja wakati wa usiku umelala kwa sura ya kutishia ya kutaka kukukaba roho na kuondoka na uhai wako.

SOMA: Waota ndoto kivitendo huwa hawakati tamaa.

Anasema ni tekniki ya msimamo ndiyo inayomuokoa binadamu kutokana na majinamizi ya usiku na wala siyo kitu kingine. Ikiwa umewahi kupatwa na jinamizi la usiku habari hii utaifurahia sana kwani utaona kama vile Hill anakuzungumzia wewe.

Sasa nguvu hiyo hiyo ya MSIMAMO, Napoleon Hill anatuonyesha jinsi tunavyoweza kuitumia katika mazingira ya kawaida ya maisha yetu ya kila siku hususani haya ya kutafuta pesa au mafanikio ya kimaisha. Tunaweza kabisa kujiondoa nje ya utepetevu wa akili zetu kwa kutumia tekniki hii muhimu.

SOMA: Imani mapenzi na ngono ndio vitu vyenye nguvu kuliko mihemko mingine yote mikubwa.

Kukosa msimamo wakati mwingine kunatufanya tuhisi labda kuna mtu aliyejificha mahala fulani ambaye hutuongoza kwa siri bila ya sisi kutambua akitumia mazingira na njia zote za kukatisha tamaa iki tufeli. Lakini ukweli wa mambo ni kwamba mtu huyo wala hayupo na kama yupo basi si mwingine bali ni akili zetu wenyewe.

Ungana na Napoleon Hill katika simulizi hii ya kusisimua akufundishe namna binadamu tunavyoweza kuzifundisha akili zetu badala ya akili hizo kutufundisha sisi, kumbuka sisi ndio tunaopaswa kuongoza kila kitu zikiwemo na akili zetu.

SOMA: Wasomi na watu waliofanikiwa hawaachi kujifunza maarifa mapya.

Mpendwa msomaji wetu, safu hii mwanzoni tulikuwa tukiichapisha katika blogu hii, na tangu sura ya kwanza mpaka hii ya 9 sehemu ya 1 unaweza ukaisoma hapa, lakini kuanzia Sehemu ya pili ya sura hii ya 9 mpaka sura ya mwisho ya 16, tumelazimika kuzichapisha kwenye GROUP LA MICHANGANUO ONLINE kupitia whatsapp na Email kwa lengo la wasomaji kuchangia kidogo ili na sisi tupate angalao motisha kidogo ya kuendelea kufanya shughuli hizi, kumbuka kazi ya blogging hugharimu muda na fedha kama zilivyo shughuli nyingine zozote zile, kwa hiyo wakati mwingine ili huduma ziweze kuwa endelevu hatuna budi kuwaombeni wasomaji wetu wapendwa kutuchangia nguvu kidogo.

SOMA: Makosa makubwa 10 ya viongozi na aina mpya ya uongozi unaotakiwa.

Ukilipia kujiunga na GROUP LA MICHANGANUO ONLINE kwa shilingi elfu 10, faida utakazopata ni nyingi, Tunakutumia masomo mengi, ikiwemo kozi nzima ya jinsi unavyoweza kuandaa Mpango wa biashara yeyote mwenyewe bila kuhitaji mtaalamu, vitabu na vitu vingine mbalimbali kama vilivyoorodheshwa hapa chini;

1.  Kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI kwa lugha ya Kiswahili.

2.  Masomo 11 ya semina kamili ya jinsi ya kuandika mpango wa biashara.

3.  Kifurushi maarufu cha michanganuo 3 ya ufugaji wa kuku(MKOMBOZI CHICKS PLAN 3PACKS)

4.  Kitabu mashuhuri zaidi duniani, HOW TO WRITTE A BUSINESS PLAN kwa lugha ya kiingereza, ndio kinachotumika vyuo vikuu vingi duniani.

5.  Mfululizo wa Tafsiri ya kitabu mashuhuri cha THINK & GROW RICH kwa Kiswahili.

6.  Kuunganishwa na blogu ya kulipia ya michanganuo bure.

7.  Vielezo(Templates) za michanganuo ya biashara inayokuwezesha kuandika michanganuo kwa muda mfupi.

8.  Masomo yote yaliyopita katika group la whatsapp la MICHANGANUO NA MZUNGUKO WA FEDHA.

9.  Mfumo mpya wa usimamizi wa duka la rejareja(2 IN ONE STORE MANAGEMENTA SYSTEM) unaomwezesha mmiliki wa duka dogo la rejareja au la kati kuthibiti mapato yake pasipo msaidizi kudokoa hata senti 5

10.      Somo muhimu sana la mzunguko wa fedha.

11.      Ukurasa mmoja wa mchanganuo.

Kujiunga na group hili unaweza kulipa ada moja kwa moja sh. Elfu 10  kupitia namba zetu, 0712202244 au 0765553030 jina ni Peter Augustino Tarimo na kisha kutuma ujumbe wa “NIUNGANISHE GROUP LA MICHAGANUOONLINE” kwa njia ya meseji au watsap 0765553030, AU pia unaweza kuwasiliana na sisi kwa namba hizo kupata maelezo zaidi.


 SOMA SURA NA SEHEMU ZILIZOKWISHAWEKWA

0 Response to "HAKUNA MBADALA WA MSIMAMO, KILA ANGUKO HUJA LIKIWA NA MBEGU YENYE FAIDA NDANI YAKE"

Post a Comment