JINSI YA KUFUTA BIDHAA ZA MAJARIBIO NA KUSAFISHA MFUMO ILI UANZE UPYA KUFANYA MAUZO HALISI – SOMO LA 20 | Jifunzeujasiriamali

JINSI YA KUFUTA BIDHAA ZA MAJARIBIO NA KUSAFISHA MFUMO ILI UANZE UPYA KUFANYA MAUZO HALISI – SOMO LA 20

Mkufunzi Peter Tarimo akifundisha jinsi ya kufuta bidhaa za majaribio na kuanza upya kwenye mfumo wa Forever Free POS & CRM

SOMO LA ISHIRINI

kunaweza kufanyika kwa njia mbili rahisi kulingana na kile unachotaka kukifuta:

Njia ya 1: Kufuta bidhaa moja baada ya nyingine (Kupitia App ya Simu)

Kama uliingiza bidhaa chache tu za majaribio, unaweza kuzifuta moja kwa moja ndani ya app ya Forever Free POS:

·      Fungua app yako na uende kwenye Menu (mistari mitatu juu kushoto)

·      Chagua Bidhaa kisha gusa tena Bidhaa (Items)

·      Bonyeza na ushikilie (Press and hold) jina la bidhaa unayotaka kuifuta

·      Alama ya kopo la takat (au neno Futa/Delete) itatokea juu kulia. Gusa hapo ili kuifuta

Njia ya 2: Kufuta bidhaa zote kwa mkupuo (Kupitia kwenye Kivinjari)

Kama uliingiza bidhaa nyingi na unataka kuzisafisha zote kwa mara moja ili usipoteze muda:

·      Ingia kwenye mfumo wako wa Forever Free ⁠ kupitia kivinjari cha simu au kompyuta

·      Kwenye menyu ya kushoto gusa alama ya kikapu chekundu cha Bidhaa / Items kisha chagua Orodha ya bidhaa

·      Juu kabisa ya orodha ya bidhaa zako, gusa kiboksi kidogo cha uteuzi (Checkbox) kilichopo upande wa kushoto wa neno Jina ili kuzichagua bidhaa zote kwa mara moja

·      Baada ya kuzichagua zote, gusa kitufe cha Futa / Delete kilichopo juu kabisa ya jedwali hilo na uthibitishe kwa kugusa OK

Jambo la Muhimu kulijua kuhusu "Mauzo ya Majaribio"

Hata ukifuta bidhaa, yale mauzo ya majaribio uliyoyafanya mwanzo bado yataendelea kuonekana kwenye ripoti zako za nyuma (kwa sababu mfumo hauruhusu kufuta risiti moja kwa moja)

Ili kusafisha hesabu za fedha zirejee kuwa sifuri (0) na zisianze kuchanganya hesabu zako mpya, unapaswa Kuzifuta Risiti za Majaribio (Cancel Receipts);

·      Ukiwa kule kule kwenye Kivinjari, nenda kwenye menyu ya Ripoti kisha chagua Risiti

·      Gusa ile risiti ya majaribio uliyofanya mwanzo ili ifunguke

·      Gusa alama ya vitone vitatu (•••) juu upande wa kulia na uchague Futa Risiti (Cancel receipt)

·      Thibitisha kwa kugusa Ndiyo

Ukifanya hivi mfumo utatoa hesabu hiyo kwenye ripoti na duka lako litakuwa safi kabisa tayari kwa kuanza biashara rasmi

 

KURUDISOMO LA 19 BOFYA HAPA

 

..............................................

 

SOMO HILI KAMILI NA KWA VITENDO LINAPATIKANA KWENYE GROUP LA TANZANIA RETAILERS PREMIUM GROUP (TRPG)

Mwanachama ni mtu yeyote mwenye nakala ya kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION 2027

Kupata nakala yako tuma ujumbe whatsapp usemao “NATAKA KITABU NA COURSE” kwa namba 0761002125 kisha nitakutumia link na coupon ya kupata kitabu chako

Au bofya hapa kupata kitabu na course sasa hivi

Ndani ya group pia utapata;

               (1)     Machimbo yote ya bidhaa za bei rahisi Kariakoo na nchi nzima

               (2)     Ubunifu wa biashara kwa wajasiriamali wadogo wa rejareja wa maudhui mtandaoni (Content creators) - watajifunza jinsi ya kuanza biashara mtandaoni bila kutumia vifaa vya gharama kubwa

               (3)     Aidha washiriki wanaweza kuuliza swali lolote kuhusu mada na mifumo yote iliyopo kitabuni, ile ya kianalojia (madaftari) na ile ya kidijitali (POS, Accounting Software, ERP, CRM nk.)

               (4)     Course ya VIP kwenye group hili inatoa mafunzo ya kina ya mfumo huu wa FOREVER FREE POS & CRM kwa mtu anayeanzia sifuri kabisa. Ina sehemu kuu 8 na mwisho kuna mtihani na cheti cha kuhitimu course 

 


RUDI SOMO LA 19 HAPA

 

 

 

 

SOMA NA HIZI HAPA;

1.    Biashara ya kutembeza bidhaa za jumla madukani, mbinu 7

2.    Weka tarehe kamili ni lini unakusudia kumiliki pesa unazotamani

3.    Hakuna biashara isiyokuwa na faida

4.    Biashara ya kuuza vocha za simu za mkononi: ulikuwa unalijua hili?

5.    Pipi ya kijiti ni hatari kwa mwanao: chukua tahadhari!

6.    KKKK

0 Response to "JINSI YA KUFUTA BIDHAA ZA MAJARIBIO NA KUSAFISHA MFUMO ILI UANZE UPYA KUFANYA MAUZO HALISI – SOMO LA 20"

Post a Comment