SOMO LA KUMI NA TISA
Ili mfanyakazi wako afanye kazi kwa ufanisi na
kuzuia visingizio kama "simu iliisha chaji" au "sikuiona
skrini vizuri", hapa kuna vifaa vya bei rahisi na vya lazima
unavyoweza kuweka duka la rejareja:
1. Stendi ya Simu/Tablet ya Mezani
Kazi yake:
Huu ni msaada mkubwa wa kumfanya mhudumu asishike
simu mkononi saa zote jambo linaloweza kumfanya adondoshe simu au kuchoka. Simu
inakaa salama juu ya kaunta kama skrini ya kompyuta ya duka kubwa
Faida ya ulinzi:
Wateja wanakuwa wanaona skrini wakati bidhaa zao
zikibonyezwa, hivyo mfanyakazi hawezi kufanya ujanja wa kufuta bidhaa kirahisi
Gharama:
Ni kati ya shilingi 5,000/= hadi shilingi 15,000/=
(Inapatikana maduka mengi ya vifaa vya simu)
2. Power Benki au Waya mrefu wa chaji
Kazi yake:
Hii inahakikisha simu ya kazi inakuwa na umeme kwa
asilimia 100% kuanzia duka linapofunguliwa asubuhi mpaka linafungwa jioni
Faida ya ulinzi:
Inafuta kabisa kisingizio cha "bosi simu
ilizimika chaji ndio maana sikuingiza mauzo ya jioni kwenye Mfumo
Gharama:
Kuanzia shilingi 25,000/= hadi shilingi 40,000/=
kwa Power Benki nzuri ya ujazo wa 10,000mAh au 20,000mAh
3. Droo ya Pesa ya Mbao au Chuma (Cash Drawer/Box)
Kazi yake:
Sehemu maalumu ya kupanga noti kulingana na thamani
zake (mfano, sehemu ya elfu tano, elfu kumi, n.k.)
Faida ya ulinzi:
Inasaidia wakati wa kufanya Miamala ya pesa (Pay
In / Pay Out) na wakati wa kuhesabu pesa jioni (Kufunga Zamu) kwa sababu
fedha hazitakuwa zimechanganyikana au kutupwa ovyo chini ya kaunta
Gharama:
Unaweza kumtuma fundi seremala akutengenezee droo
rahisi ya mbao yenye sehemu tofauti za kuweka pesa kwa chini ya shilingi 20,000/=
4. Router ndogo ya Wi-Fi au laini maalumu ya
Intaneti
Kazi yake:
Kutoa intaneti ya uhakika dukani, ni kwa ajili ya
simu inayotumia mfumo wa Forever Free POS
Faida ya ulinzi:
Ingawa mfumo wa Forever Free POS unaweza kufanya
kazi hata bila ya intaneti (offline), uwepo wa intaneti ya uhakika unakusaidia
wewe kama mmiliki kupokea taarifa za mauzo kwenye kivinjari cha simu yako
kwa sekunde ile ile mauzo yanapofanyika, hata ukiwa mbali
Gharama:
Ni kuanzia shilingi 35,000/=
hadi shilingi 50,000/= kununua kifaa cha MiFi (cha kubebeka), au unaweza kuweka
laini ya kawaida kwenye simu na kuiunganisha kifurushi cha mwezi cha sh. 10,000/=
hadi 15,000/=
Kwa kuanzia, ukiwa na Stendi ya simu na Waya
mrefu wa chaji unaochomekwa ukutani, duka lako litakuwa limekamilika na
mfumo utafanya kazi vizuri sana bila kuathiri mzunguko wako wa mtaji
..................................................
SOMO HILI KAMILI NA KWA
VITENDO LINAPATIKANA KWENYE GROUP LA TANZANIA RETAILERS PREMIUM GROUP (TRPG)
Mwanachama ni mtu yeyote
mwenye nakala ya kitabu cha MAFANIKIO YA
BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION 2027
Kupata nakala yako tuma
ujumbe whatsapp usemao “NATAKA
KITABU NA COURSE” kwa namba 0761002125 kisha nitakutumia link na coupon ya kupata kitabu chako
Au
bofya
hapa kupata kitabu na course sasa hivi
Ndani
ya group pia kuna;
(1) Machimbo
yote ya bidhaa za bei rahisi Kariakoo na nchi nzima
(2) Ubunifu
wa biashara kwa wajasiriamali wadogo wa rejareja wa maudhui mtandaoni (Content creators) - watajifunza jinsi
ya kuanza biashara mtandaoni bila kutumia vifaa vya gharama kubwa
(3) Aidha
washiriki wanaweza kuuliza swali lolote kuhusu mada na mifumo yote iliyopo
kitabuni, ile ya kianalojia (madaftari) na ile ya kidijitali (POS, Accounting
Software, ERP, CRM nk.)
(4) Course
ya VIP kwenye group hili inatoa mafunzo ya kina ya mfumo huu wa FOREVER FREE
POS & CRM kwa mtu anayeanzia sifuri kabisa. Ina sehemu kuu 8 na mwisho kuna
mtihani na cheti cha kuhitimu masomo haya
SOMA
NA HIZI HAPA
1.
Hatua 10 za kuanzisha biashara ya
rejareja (duka)
2.
Ni mwaka wa kujirudishia ukuu wako
tena(make yourself great again)
3.
Biashara ndogondogo za kufanya dar
es salaam kwa mtaji kidogo bila kulipia pango la nyumba
4.
Biashara ya soda maji juisi na
sigara: tumia siri hii kuongeza mauzo × 2
5.
Unajua biashara yenye faida kubwa na
ya haraka mara 2 ya mtaji utakaowekeza?

0 Response to "VIFAA VYA BEI RAHISI KAMA VILE STENDI YA SIMU, POWERBANK, DROO YA FEDHA NA ROUTER YA WIFI UNAVYOWEZA KUWEKA DUKANI ILI MHUDUMU AFANYE KAZI KWA URAHISI BILA VISINGIZIO - SOMO LA 19"
Post a Comment