MICHEZO SABA (7) WAFANYAKAZI WANAWEZA KUFANYA ILI KUKUIBIA NA JINSI YA KUIZUIA MAPEMA KUPITIA MFUMO WA FOREVER FREE POS – SOMO LA 18 | Jifunzeujasiriamali

MICHEZO SABA (7) WAFANYAKAZI WANAWEZA KUFANYA ILI KUKUIBIA NA JINSI YA KUIZUIA MAPEMA KUPITIA MFUMO WA FOREVER FREE POS – SOMO LA 18

Peter Tarimo akifundisha michezo ya wizi kwa wafanyakazi  kwenye mfumo wa Forever Free POS & CRM

SOMO LA KUMI NA NANE

Katika maduka au biashara za rejareja kuna michezo saba (7) ambayo ni maarufu sana inayotumiwa na wafanyakazi wajanja kufanya udokozi kwenye biashara

Uzuri ni kwamba Mfumo wa Forever Free POS & CRM unakupa uwezo mkubwa wa kuigundua na kuizuia mapema kabla haijakuletea hasara kubwa. Iangalie hii kwa makini:

1. Mchezo wa kufuta bidhaa kabla ya kuzisajili kwenye mauzo

Je, mfanyakazi akifuta bidhaa kabla ya kuuza kuna athari yeyote kwenye hesabu?

Hapana, hakuna athari yoyote kwenye hesabu ya fedha wala stoku lakini inategemea amefuta kwa lengo gani

Kufuta bidhaa kwenye kikapu (cart) kabla ya kugusa kitufe cha Toza / Charge maana yake ni kwamba mauzo hayo hayajakamilika na hayajaingia rasmi kwenye mfumo

Hata hivyo, kuna mambo mawili tofauti unayopaswa kuyafahamu kulingana na jinsi anavyofanya mchezo huo:

(1) Inapokuwa siyo mchezo wa wizi (Hali ya kawaida)

Hii hutokea mara nyingi na haina shida:

·      Mfano: Mteja anasema anataka soda na biskuti. Mfanyakazi anazibonyeza kwenye app. Kabla ya kulipa, mteja anagundua hana pesa ya kutosha, anasema: "Hapana, niondolee hii biskuti nitachukua soda tu."

·      Mfanyakazi anaifuta biskuti kwenye kikapu kisha anauza soda peke yake

·      Athari: Hakuna athari yeyote. Stoku ya biskuti haipungui na pesa ya biskuti haitafutwa jioni kwa sababu haijatolewa dukani

(2) Inapokuwa ni mchezo wa WIZI (Mfanyakzi mjanja)

Hapa ndipo unapopaswa kuwa makini, mfanyakazi anaweza kutumia mwanya huu kukuibia kama wewe huna utaratibu wa kutoa risiti za karatasi au wateja wako hawaangalii skrini ya simu:

Mchezo unavyofanya kazi:

·      Mteja anakuja kununua bidhaa za sh. 10,000/= Mfanyakazi anazibonyeza zote kwenye App ili mteja aone jumla ya bei kwenye skrini. Mteja anampa pesa taslimu (Cash) sh. 10,000/= na kuondoka bila kudai risiti

·      Mfanyakazi badala ya kugusa Toza / Charge, anazifuta bidhaa zote kwenye kikapu na kuacha skrini ikiwa safi, kisha anachukua ile sh. 10,000/= na kuitumbukiza mfukoni kwake

·      Athari kwenye hesabu: Jioni hesabu ya mfumo na ya droo italingana vizuri (Tofauti itakuwa 0) kwa sababu mauzo hayo hayakusajiliwa kwenye mfumo. Lakini utakuwa umepoteza mzigo (stoku) na umepoteza pesa bila mfumo kujua

Jinsi ya kuzuia ujanja huu kwa asilimia 100%:

·      Kagua ripoti ya Bidhaa zilizofutwa "Deleted Items": Kama nilivyokwambia mwanzo, ingia mara kwa mara kwenye Mfumo -> Ripoti -> Bidhaa zilizofutwa. Ukiona mfanyakazi anafuta bidhaa nyingi kwenye kikapu mara kwa mara jua kuna mchezo mchafu anafanya

·      Sisitiza wateja kudai risiti: Weka bango dogo mbele ya kaunta lililoandikwa: "Kama usipopewa risiti, bidhaa hiyo ni bure" au "Tafadhali dai risiti yako". Hii inamlazimu mhudumu kugusa kitufe cha Toza / Charge ili kutoa risiti

·      Fanya "Stock Take" (Kuhesabu Mzigo): Mara moja kwa wiki, hesabu bidhaa zilizopo kwenye shelfu kwa mikono na ulinganishe na idadi inayosoma kwenye app ya Forever Free POS. Ikiwa kwenye mashelfu kuna sabuni 5 lakini kwenye app inasema zipo 8, maana yake kuna sabuni 3 zimeuzwa kwa ujanja huo wa kufuta kikapu

2. Mchezo wa "Kununua kwa jumla na kuuza Rejareja" (Kuingiza bidhaa zao kwa siri)

Huu ni mchezo hatari sana ambapo mfanyakazi analeta mzigo wake kinyemela kutoka nyumbani kwake na kuuweka dukani kwako

Mchezo unavyofanya kazi:

·      Mfanyakazi ananunua katoni ya soda kwa fedha zake (mfano: kwa sh. 12,000/=) na kuileta dukani kwako Mteja akija kununua soda badala ya kumpa soda yako na kuiandika kwenye mfumo, anampa soda yake ya siri na kuchukua sh. 1,000/= taslimu na kuiweka mfukoni kwake

·      Athari: Hesabu ya mfumo na pesa ya droo jioni zitakuwa sahihi kabisa (Tofauti itakuwa 0). Pia stoku yako haitapungua. Lakini duka lako litakuwa linatumia umeme wa friji lako na nafasi yako kutengeneza faida ya mfanyakazi, huku bidhaa zako zikikaa bila kuuzika

Jinsi ya kuzuia: Fanya ukaguzi wa ghafla (Surprise Stock Count). Ukikuta duka lina chupa 50 za soda lakini kwenye app ya Forever Free (Bidhaa) inasema unapaswa kuwa na chupa 30 tu, jua kuna mzigo wa siri umeingizwa

 

3. Mchezo wa "Kutumia punguzo la bei la uwongo" (Fake Discounts)

Mfanyakazi anaweza kutumia kipengele cha kutoa punguzo (Discount) kukuibia pesa kama hukumzuia kwenye mfumo

Mchezo unavyofanya kazi:

·      Mteja ananunua bidhaa ya sh. 10,000/= na kumpa mfanyakazi sh. 10,000/= kamili. Mteja akishaondoka, mfanyakazi anaweka punguzo (Discount) la 20% kwenye app ya Forever Free POS, hivyo mfumo unasoma mauzo ni sh. 8,000/=  Mfanyakazi anaweka sh. 8,000/= kwenye droo na kuchukua sh. 2,000/= zilizobaki na kuweka mfukoni

Jinsi ya kuzuia:

Hii ndiyo sababu mwanzoni tuliondoa alama ya vema (untick) kwenye Kuweka Punguzo / Apply discounts katika vyeo vya wafanyakazi (Access Rights), hakikisha mfanyakazi hana ruhusa ya kutoa punguzo kabisa bila PIN yako wewe bosi

 

4. Mchezo wa "Kuuza nje ya mfumo" (Kutumia kikokotoo/Calculator ya kawaida)

Wafanyakazi wajanja hupenda kusema "Simu ilikuwa haina chaji" au "App ilikuwa inasumbua" ili watumie kikokotoo cha kawaida cha simu kupigia wateja hesabu

Mchezo unavyofanya kazi:

·      Wakati wateja wanapokuwa wengi, anazima app au anaiacha tu na kuanza kupiga hesabu kwa calculator au kichwani. Anapokea pesa na kuziweka kwenye droo, kisha jioni anakuambia "Bosi, nilisahau kuingiza baadhi ya mauzo kwa sababu duka lilikuwa na watu wengi sana." Hapa anakuwa ameshatenga fungu lake la wizi pembeni

Jinsi ya kuzuia:

·      Weka sheria ngumu kuwa mauzo yote lazima yapitie kwenye mfumo wa Forever Free POS. Hakuna kutumia calculator ya simu. Kama simu haina chaji, hakikisha unanunua Powerbank duka liwe na umeme wa akiba masaa 24

 

5. Mchezo wa "Kutouza bidhaa zinazofanana kwa thamani"

Huu ni mchezo wa siri sana ambao hauathiri hesabu ya pesa jioni, lakini unaharibu stoku yako ya bidhaa na kukuibia faida

Mchezo unavyofanya kazi:

·      Mteja anakuja kununua bidhaa ya bei ghali (mfano: Sabuni ya unga ya sh. 5,000/=) Mfanyakazi kwenye app anagusa bidhaa tofauti kabisa lakini ya bei ya chini (mfano: Sabuni ya kipande ya sh. 2,000/=). Mteja anampa sh. 5,000/= taslimu. Mfanyakazi anaweka sh. 2,000/= kwenye droo (kama mfumo unavyotaka) na kuchukua sh. 3,000/= zilizobaki na kuweka mfukoni

Athari:

·      Hesabu ya jioni italingana vizuri (Tofauti itakuwa 0) Lakini mwisho wa wiki ukikagua stoku ya bidhaa, utakuta sabuni za unga zimepungua kimyakimya huku faida yake ikiwa haipo

Jinsi ya kuzuia:

·      Weka Picha halisi kwenye kila bidhaa ndani ya Mfumo wako wa Forever Free POS. Pia ukiwa mbali kagua ripoti ya Mauzo ya Bidhaa kwenye Mfumo wako. Ukiona bidhaa za bei rahisi zinauzwa kwa kasi isiyo ya kawaida kuliko zile za bei ghali, fanya ukaguzi wa stoku ya ghafla mara moja

 

6. Mchezo wa "Kurejesha bidhaa kifisadi" (Fake Returns / Refund)

Kama ulimpa mfanyakazi wako ruhusa ya kushughulikia bidhaa zinazorudishwa na wateja (Refunds), anaweza kutumia mwanya huu kukuibia kirahisi

Mchezo unavyofanya kazi:

·      Mteja ananunua bidhaa, analipa na kuondoka zake kwa amani na risiti yake. Mteja akishaondoka, mfanyakazi anafungua ile risiti ya nyuma na kubonyeza kitufe cha Kurudisha bidhaa (Refund) kana kwamba mteja amerudi kulalamika na kurudisha mzigo. Mfumo unarudisha bidhaa hiyo kwenye stoku na mfanyakazi anachukua fedha hizo kwenye droo na kuweka mfukoni kwake

Jinsi ya kuzuia:

·      Huu ni mwanya mkubwa! kwenye ruhusa ya ufikiaji kwenye mfumo (Access Rights), ondoa kabisa ruhusa ya kufanya "Refund" kwa wafanyakazi . Sheria iwe: Kama mteja anataka kurudisha bidhaa na kupewa pesa yake, lazima amsubiri mmiliki (wewe) au mfanyakazi akupigie simu uingize PIN yako ya (Bosi) ili uidhinishe

 

7. Mchezo wa "Kukopesha marafiki kwa Siri"

Mhudumu anaweza kutumia duka lako kama “shirika” la misaada kwa ndugu, jamaa na marafiki zake bila wewe kujua

Mchezo unavyofanya kazi:

·        Rafiki wa mfanyakazi anakuja dukani, anachukua bidhaa za sh. 20,000/= na kuondoka nazo bila kulipa. Mfanyakazi ili asionekane amekubali deni, anachukua ile risiti na kuiweka kama Deni kwenye mfumo. Anapanga kuwa rafiki yake akimrudishia pesa hiyo wiki ijayo ndipo ataifunga ile risiti

Athari:

·        Stoku yako inakuwa imetoka, lakini pesa huioni kwa wiki nzima jambo linalofubaza mzunguko wako wa mtaji (Cash Flow)

Jinsi ya kuzuia:

·        Kagua sehemu ya Madeni kwenye mfumo wako kila siku jioni ukiwa nyumbani. Ukiona kuna madeni yamekaa kwa zaidi ya masaa 24 bila kulipwa au kufungwa, mhoji mfanyakazi hapo hapo kujua kwa nini mauzo hayo hayajakamilika

Muhtasari wa kinga ya kudumu (Mbinu ya Dhahabu):

Mifumo yote ya POS duniani (ikiwemo Forever Free POS & CRM) inafanya kazi kwa usahihi ikiwa tu binadamu anayeitumia anajua anasimamiwa;

·        Fanya Stock Take (kuhesabu bidhaa zilizopo kwenye mashelfu) mara kwa mara na kwa kushtukiza

·        Mfanyakazi akijua kuwa kila Jumamosi asubuhi unahesabu idadi ya sabuni, mafuta na soda vilivyobaki na kuvilinganisha na namba zilizopo kwenye Mfumo, hatajaribu mchezo wowote ule kwa sababu anajua atakamatwa mara moja

 


KURUDI SOMO LA 17 BOFYA HAPA

KWENDA SOMO LA 19 BOFYA HAPA

 


..................................................

 


SOMO HILI KAMILI NA KWA VITENDO LINAPATIKANA KWENYE GROUP LA TANZANIA RETAILERS PREMIUM GROUP (TRPG)

Mwanachama ni mtu yeyote mwenye nakala ya kitabu cha MAFANIKIO YA BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION 2027

Kupata nakala yako tuma ujumbe whatsapp usemao “NATAKA KITABU NA COURSE” kwa namba 0761002125 kisha nitakutumia link na coupon ya kupata kitabu chako

Au bofya hapa kupata kitabu na course sasa hivi

Ndani ya group pia kuna;

               (1)     Machimbo yote ya bidhaa za bei rahisi Kariakoo na nchi nzima

               (2)     Ubunifu wa biashara kwa wajasiriamali wadogo wa rejareja wa maudhui mtandaoni (Content creators) - watajifunza jinsi ya kuanza biashara mtandaoni bila kutumia vifaa vya gharama kubwa

               (3)     Aidha washiriki wanaweza kuuliza swali lolote kuhusu mada na mifumo yote iliyopo kitabuni, ile ya kianalojia (madaftari) na ile ya kidijitali (POS, Accounting Software, ERP, CRM nk.)

               (4)     Course ya VIP kwenye group hili inatoa mafunzo ya kina ya mfumo huu wa FOREVER FREE POS & CRM kwa mtu anayeanzia sifuri kabisa. Ina sehemu kuu 8 na mwisho kuna mtihani na cheti cha kuhitimu 

 

RUDI SOMO LA 17 HAPA

NENDA SOMO LA 19 HAPA

 



SOMA NA HIZI HAPA

1.    Biashara ya duka inavyoweza kukutoa kimaisha ukiwa mjanja

2.    Mbinu hizi 2 za uendeshaji duka la rejareja kwa mafanikio hazipo mahali pengine popote

3.    Biashara 1 nzuri inayolipa tanzania unayoweza kufanya kipindi hiki kigumu cha fedha 2017

4.    Mchanganuo wa biashara ya duka la kuuza vinywaji baridi mchanganyiko na maji

5.    Somo la 5: maelezo ya biashara au kampuni


0 Response to "MICHEZO SABA (7) WAFANYAKAZI WANAWEZA KUFANYA ILI KUKUIBIA NA JINSI YA KUIZUIA MAPEMA KUPITIA MFUMO WA FOREVER FREE POS – SOMO LA 18"

Post a Comment