SOMO LA KUMI NA SABA
Hapana, hawezi kabisa, ilimradi tu uwe umefuata
hatua za usalama:
Forever Free POS imetengenezwa kwa mifumo imara
sana ya ulinzi inayomzuia mfanyakazi mjanja kufanya ujanja wowote wa kufuta
bidhaa au kufuta risiti, kwa sababu mambo hayo mawili hayawezi kufanyika
ndani ya app ya kawaida ya POS ya mfanyakazi dukani
Hapa kuna sababu tatu kwa nini uko salama kwa
asilimia 100%:
1. Hakuna kitufe cha kufuta risiti "Cancel"
kwenye App ya Forever Free POS
Kwenye app anayotumia mfanyakazi dukani, hakuna
kabisa kipengele au kitufe cha kufuta (Cancel) risiti ya nyuma, kufuta
risiti kunaweza kufanyika tu kupitia Kivinjari cha mtandaoni anachotumia
mmiliki, na kama ulivyomzuia mwanzoni, yeye hana neno la siri la kuingilia huko
2. Hawezi kufuta au kubadilisha bei ya bidhaa
Kama uliondoa alama ya vema (untick) kwenye sehemu
ya Kusimamia bidhaa katika mipangilio yake (Access Rights), mfanyakazi
wako akijaribu kwenda kwenye sehemu ya bidhaa (Items):
·
App itamgomea kabisa na kumwambia hana ruhusa
(Permission Denied)
·
Hawezi kufuta bidhaa ili apoteze stoku na hawezi
kupunguza bei ya bidhaa ili amuuzie rafiki yake kwa bei ya chini
3. Hata akijaribu "Kusafisha" kikapu
kabla ya kuuza
Kama mteja akija na mfanyakazi akabonyeza bidhaa
kwenye simu (mfano. Sabuni na Mafuta), halafu akabadili mawazo na kuzifuta
kwenye kikapu kabla ya kugusa Toza / Charge:
·
Unaweza kuona mchezo huo! kupitia kivinjari chako
kwenye simu au kompyuta kwani, kuna ripoti inayoitwa, Bidhaa
zilizofutwa / "Deleted items "
·
Ripoti hii itakuonyesha kuwa mfanyakazi wako
alifuta bidhaa fulani kwenye kikapu kabla ya kukamilisha mauzo na itakuambia
alifanya hivyo saa ngapi
Ushauri wa kitaalamu:
Kitu pekee unachotakiwa kuwa makini nacho sana ni Neno
lako la siri (Password/PIN) la mmiliki
· Hakikisha
mfanyakazi wako haoni namba yako ya siri unapoingia kwenye mfumo
· Usiache
kamwe akaunti yako ya kwenye mfumo ikiwa wazi (logged in) kwenye kompyuta au
simu ambayo mfanyakazi anaweza kuifikia
Mbali na hayo, unaweza kulala usingizi mnono ukijua
kuwa mfumo wa Forever Free unalinda kila senti na kila bidhaa iliyopo dukani
kwako
...............................................
SOMO HILI KAMILI NA KWA
VITENDO LINAPATIKANA KWENYE GROUP LA TANZANIA RETAILERS PREMIUM GROUP (TRPG)
Mwanachama ni mtu yeyote
mwenye nakala ya kitabu cha MAFANIKIO YA
BIASHARA YA DUKA LA REJAREJA NEW TECH EDITION 2027
Kupata nakala yako tuma
ujumbe whatsapp usemao “NATAKA
KITABU NA COURSE” kwa namba 0761002125 kisha nitakutumia link na coupon ya kupata kitabu chako
Au
bofya
hapa kupata kitabu na course sasa hivi
Ndani
ya group pia utapata;
(1) Machimbo
yote ya bidhaa za bei rahisi Kariakoo na nchi nzima
(2) Ubunifu
wa biashara kwa wajasiriamali wadogo wa rejareja wa maudhui mtandaoni (Content creators) - watajifunza jinsi
ya kuanza biashara mtandaoni bila kutumia vifaa vya gharama kubwa
(3) Aidha
washiriki wanaweza kuuliza swali lolote kuhusu mada na mifumo yote iliyopo
kitabuni, ile ya kianalojia (madaftari) na ile ya kidijitali (POS, Accounting
Software, ERP, CRM nk.)
(4) Course
ya VIP kwenye group hili inatoa mafunzo ya kina ya mfumo huu wa FOREVER FREE
POS & CRM kwa mtu anayeanzia sifuri kabisa. Ina sehemu kuu 8 na mwisho kuna
mtihani
SOMA NA HIZI HAPA:
1.
Biashara ndogo rahisi kwa
wajasiriamali zinazoenda na wakati tulio nao
2.
Aina za bidhaa za duka zenye faida
ndogo lakini hutoka haraka haraka
3.
Jinsi ya kuuza wazo lako la biashara
au ubunifu kwa wawekezaji na watu wengine
4.
Somo:mamilionea vijana 10 wakisimulia siri za utajiri wao
walivyofanikiwa
5.
Mafunzo matano (5) ya jinsi ya
kuanzisha biashara toka mwanzo mpaka mafanikio

0 Response to "JE, MFANYAKAZI MJANJA HAWEZI KUFUTA BIDHAA NA RISITI NISIPOKUWA MAKINI? – SOMO LA 17"
Post a Comment