MCHANGANUO WA BIASHARA YA DUKA LA KUUZA VINYWAJI BARIDI MCHANGANYIKO NA MAJI | JIFUNZE UJASIRIAMALI

MCHANGANUO WA BIASHARA YA DUKA LA KUUZA VINYWAJI BARIDI MCHANGANYIKO NA MAJI

Biashara ya jumla hapa Tanzania ni biashara yenye fursa kubwa ukizingatia kwamba maduka na biashara nyingi za rejareja, hutegemea kununua bidhaa kutoka kwayo kwa ajili ya kuuza. Maduka ya jumla yamegawanyika makundi mawili, yale yanayouza bidhaa za aina moja tu na yale yanayouza bidhaa mchanganyiko.


Vinywaji baridi maana yake ni vinywaji visivyokuwa na kileo. Maduka ya jumla mengi yanayouza vinywaji baridi utakuta ni maduka yenye mchanganyiko wa bidhaa mbalimbali kama vile utakuta yakiuza soda mchanganyiko na vinywaji vingine kama maji, juisi, maziwa ya paketi, vinywaji vya kuongeza nguvu mwilini(energy drinks) nk.

Ukitaka kuanzisha duka la jumla hasa la vinywaji baridi na uone mafanikio yake haraka itakubidi uwe na mtaji wa kutosha kuhakikisha vinywaji vyote muhimu wateja wanapofika dukani hawavikosi. Kiasi cha mtaji kitategemea ni skock ya bidhaa kiasi gani utakachoamua kuwa nacho dukani kwako. Ikiwa hautapenda kuagiza vinywaji kiwandani mara kwa mara basi itakupasa uweke stoku ya kutosha.


Uendeshaji wa duka la jumla ni kama zilivyokuwa biashara zingine tu kwani utahitaji mtaji, mtu wa kuuza, mtu wa kutoa na kuweka mizigo stoo, mtu wa kufungia wateja mizigo pamoja na mtu wa kufuatilia wateja mitaani. Lakini kama bado mtaji wako ni kidogo unaweza ukawa na msaidizi mmoja tu halafu shughuli zote mkafanya watu wawili tu na pengine mtu mmoja tena wa muda(partime) kama vile mbebaji mizigo ambaye hulipwa na wateja wanaokuja kununua bidhaa.

Katika kitabu cha MICHANGANUO YA BIASHARA NA UJASIRIAMALI, miongoni mwa michanganuo ya biashara iliyokuwepo, upo mchanganuo wa biashara ya duka la jumla la vinywaji baridi, biashara iliyopo Malapa jijini Dar es salaam. MCD Provision Store linamilikiwa na bwana Chacha Mwita na husambaza vinywaji baridi maeneo mengi ya Buguruni Malapa na baadhi ya maeneo ya Temeke.


Ufuatao ni muhtasari wa mchanganuo huo ambao kwa yule mwenye kitabu hicho anaweza akausoma mchanganuo huo mzima pamoja na michanganuo mingine mbalimbali ya biashara za Kitanzania zinazolipa. 



DUKA LA JUMLA.
MCD Provision Store.

Duka la jumla la vinywaji  baridi Malapa Cold Drinks  Provision Store, MCD  ni duka litakalouza  vinywaji vya aina mbalimbali visivyo na kileo. Litaanzishwa katika eneo  la Buguruni Malapa na kuhudumia maeneo yote ya jirani pamoja na  wateja wanaotoka maeneo nje ya hapo. MCD Provision  mwaka 2013 imeweka  lengo la kuingiza  mapato yanayofikia shilingi milioni 450.

MCD imepanga kufikisha huduma zake za usambazaji wa vinywaji visivyokuwa na kileo katika manispaa nzima ya Ilala pamoja na baadhi ya maeneo  ya  Temeke. Mmiliki wa duka hili ni bwana Onesmo Chacha ambaye baada ya kuuza sehemu ya shamba kubwa alilorithi kutoka kwa babu yake kijijini kiasi cha shilingi milioni 70 aliamua kuja kuanzisha duka hilo.

MDC litauza bidhaa zifuatazo.
·        Soda  aina zote.
·        Maji aina zote.
·        Juice aina zote.
·        Malta.
·        Redbull na
·        Bavaria

Maeneo ya Buguruni, kuna maduka mengi ya reja reja pamoja na Bar/Groceries, vyote hivi huhitaji vinywaji kwa ajili ya kuwauzia  wateja rejareja.Makadirio  ya mauzo katika miaka mitatu yamekisiwa kutokana na utafiti uliofanyika kuhusiana na soko la vinywaji baridi lililopo katika eneo la Buguruni sokoni, Malapa pamoja na  yale maeneo MDC inayopanga kufikisha huduma zake.

1.1.    Dhamira  kuu.
MCD  Provision Store imedhamiria  kutoa huduma  bora za usambazaji   wa vinywaji  visivyokuwa na kileo katika  maduka, mabaa na sehemu yeyote  yenye shughuli  kwa bei nzuri pamoja na usafiri wa uhakika.

1.2.    Malengo.
·        Kusambaza vinywaji katika kata zote  za Ilala na baadhi ya maeneeo ya  Temeke ifikapo mwaka 2014.
·        Kuongeza pikipiki za matairi  matatu kutoka 1 mpaka kufikia 3 ifikapo mwaka wa 2015.
·        Kufikisha  mauzo yapatayo milioni 560  ifikapo mwaka 2015.


2.0 Maelezo kuhusu biashara
MCD Provision chini ya mmiliki wake bwana Onesmo Chacha Mwita itajijengea umaarufu wa kipekee kwa wateja wake kutokana na kuwafikishia vinywaji mpaka mlangoni mwa biashara zao. Mtaji wa kuanzishia biashara hii aliupata baada ya kuuza sehemu ya shamba kubwa alilorithi kutoka kwa marehemu babu yake huko kijijini Migori.


2.2   Historia ya Biashara.
Miaka  kabla  ya 2012 katika eneo zima la Buguruni Malapa  kulikuwa na maduka machache sana yaliyokuwa  yakiuza vinywaji vya jumla visivyokuwa na kilevi, hata maduka  machache yaliyokuwepo mteja ilimbidi aende na usafiri wake au  mtu maalumu wa kumbebea  mzigo. Onesmo kwa kuliona hilo mwaka huo huo  mwezi Septemba aliamua kuanzisha mipango ya kufungua  duka katika eneo hilo baada ya kuacha kazi  katika kiwanda cha soda.

Mwanzoni MCD itatoa huduma katika maeneo machache tu lakini baadaye  itafika hata maeneo  mengine ya mbali kama vile; Buguruni kwa Mnyamani, Buguruni  Madenge na Ilala Shariff Shamba. Itaanza na mfanyakazi mmoja na baada ya miezi michache itaongeza kufikia watatu.

2.3 Kianzio.
Gharama mbalimbali zitahitajika wakati wa kuanza, nazo zimekisiwa kama ifutavyo; usajili, uwekaji wa bango pamoja na ukarabati wa chumba cha biashara jumla Sh. 500,000/=.Vile vile kutahitajika rasilimali mbalimbali zikiwemo, fedha taslimu, bidhaa za kuanzia, mali nyinginezo na mali za kudumu kama vile pikipiki ya bajaji na makreti ya soda jumla shilingi 52,000,000/= Chati na majedwali yafuatayo  vinaelezea kwa ufupi makisio hayo. Jumla ya fedha zote za mahitaji ni Sh.52,500,000/=. Na zitatokana na mauzo ya shamba la urithi Shilingi milioni 70.





0 Response to "MCHANGANUO WA BIASHARA YA DUKA LA KUUZA VINYWAJI BARIDI MCHANGANYIKO NA MAJI"

Post a Comment