Vigezo vinavyotumika katika kuorodhesha vitabu vya
mafanikio katika blogu hii ya jifunzeujasiriamali siyo kigezo kimoja, kuna
vigezo zaidi ya kimoja kama vile, umaarufu wa kitabu, ukongwe au muda kitabu
kilipotungwa, idadi ya nakala za kitabu zilizochapishwa ama kuuzwa, umaarufu wa
mwandishi na maudhui ya kitabu kwa ujumla. Unaweza kudhani labda kitabu fulani hakikustahili
kuwa kwenye namba kilipo kulingana na kigezo kimoja lakini kumbe kigezo
kilichofanya kitabu kiwe pale ni kingine.
Kitabu
cha leo, The Science of Getting Rich, Sayansi ya kupata Utajiri.
Hiki ni kitabu cha rika la vitabu kama kina Think &Grow Rich(Fikiri Utajirike) naThe Master Key System, tena ni kikongwe hata kuvishinda hivyo
vingine viwili kwani kilitungwa mwaka 1910 wakati Master Key System 1912 na
Think and Grow Rich mwaka 1937.
Mwandishi wa kitabu akiwa ni Wallace D. Wattle chini ya
kampuni ya Elizabeth Towneni miaka zaidi ya 100 sasa imepita lakini bado kitabu
kinaendelea kutolewa nakala ijapokuwa na kampuni nyingine tofauti kama vile
kampuni ya Rhonda Byrne’s mwaka 2006
Kitabu cha Sayansi ya kupata utajiri kwa kifupi
kinazungumzia jinsi ya kuondokana na vikwazo vya kifikra na namna ambayo
ubunifu unavyoweza kuwa chanzo cha mafanikio ya kiuchumi maishani tofauti na
ushindani. Wattle anaamini kwamba ipo namna fulani ya kufikiri(sayansi) ambayo
inaweza kunfanya mtu kuwa tajiri na njia au sayansi hiyo mtu yeyote anaweza
kujifunza.
Anasema utajiri wa pesa na mali huja baada ya mtu kutenda
mambo kwa njia hiyo na wale wanaofanya mambo kwa njia hiyo iwe ni kwa kukusudia
au hata wanafanya tu kwa bahati mbaya bila ya kujua wanachotumia ni njia(sayansi)
hiyo, basi hujikuta wametajirika. Na kwa wale ambao hufanya mambo kinyume na
njia hiyo, pasipokujali ni juhudi kubwa kiasi gani wataonyesha wataendelea
kubakia kuwa masikini vilevile walivyokuwa.
Ni sheria ya asili ambayo mtu yeyote yule atakayeamua
kujifunza na kuitumia, bila shaka yeyote ile hubadilika na kuwa tajiri. Kwa
upande mwingine maudhui ya kitabu hiki yanaegemea katika maudhui ya dini ya
Kihindu lakini hata hivyo mwandishi amejitahidi kukifanya kionekani ni cha
kisekula zaidi.
................................................................................................
TUNAKARIBISHA PIA WASHIRIKI KATIKA SEMINA YA KUANDIKA MPANGO WA BIASHARA
0 Response to "KITABU CHA SAYANSI YA KUWA TAJIRI (THE SCIENCE OF GETTING RICH) CHA WALLACE D. WATTLE"
Post a Comment